Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Mkuu Pasco,

Unachosema hapa ni kuwa kwa kuwa MV Bukoba hakuwajibika mtu basi tuendelee hivyo hivyo watu wanakufa hakuna wa kuwajibika kwa sababu eti uwajibika ulizikwa to enzi za Nyerere! Naaa Naaah!

Mwingine anadai Loawassa kawajibika imesaidia nini? makubwa haya! basi wale wahandisi na Halmashauri, contarctor na Mr Ladha watolewe kizuizini wanaonewa.

Nianze kwa kuunga mkono anachosema Pasco. Ukweli ni kwamba nchi hii hakuna narudia tena hakuna kabisa utamauni wa kuwajibika wala kuwajibishwa. Utamaduni huo ulikufa tangu Mwl. Nyerere alipong'atuka katika uongozi. Yapo mambo yanayotokea ndani ya serikali ambayo katika hali ya kawaida usingetarajia wahusika wakuu kutowajibika lakini utashangaa maisha yanasonga mbele tena basi wahusika wakuu wanapandishwa hata vyeo. Kwa hili sihitaji hata kutoa mifano. Leo hii, tunapomsakama Mchechu eti awajibishwe tunakuwa kama wageni wa nchi hii na hata wananchi wa kawaida watatushangaa kulikoni Mchechu!

Niseme kwa ufupi tu mtazamo wangu kwamba utamaduni huu wa watu kutowajibika au mamlaka zilizo juu kutowawajibisha wahusika unaweza kubadilishwa na mtu mmoja tu ambaye ni kiongozi mkuu wa nchi. Mkuu wa nchi anaposhindwa kuwawajibisha anaowateua wanaposhindwa waziwazi kusimamia maeneo yao, walio chini yake wanawezaje kuwawajibisha watu wao wa chini!!! Kwa hali ilivyo sasa katika nchi yetu kiuwajibikaji, Mchechu asiwe na wasiwasi kabisa. Hana kosa na ajisikie kutohusika kabisa.
 
yaleyale ya mtu kuchora Zombi kwenye mtihani halafu kapata zero mnataka waziri ajiuzulu.
aduwilly
Sio kosa lako umekulia ktk jamii isiyowajibika na isiyotambua kuwa cheo ni dhamana! Kwa jamii makini na zinazoheshimu raia kuliko watawala viongozi wote wanaohusika na janga hili wangelishakabidhi resignation letters kwa wakubwa wao wa kazi kwa kukili kutowajibika na kutambua kuwa wapo watz kama wao wenye uwezo zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Kama una chuki binafsi na mchechu sema but hoja yako haina mashiko. Mchechu ameingia after 2007 na ameinadilisha shirika lililokuwa mbioni kufa sasa wanatembelea hilux kwenye kazi zao. Pia hoja yako haina mashiko kwasababu mkataba wa kujenga lile jengo ulifungwa mwaka 2006, sasa Nehemiah Mchechu anahusikaje? Mie namtetea labda ulete sababu zenye mashiko but hii sio mkuu.

...defence kama hizi ndizo zitakazo mfanya Mchechu aonekane liable....I'm afraid.......Mdondoaji...siamini haya maandishi yanatoka kwako!.........
 
Heshima mbele wakuu Joshi Kanji na Mkuu macho_mdiliko .........naomba mtambue kuna watu wengi sana wanafaidika na upuuzi unaoendelea katika nchi hii......umeona Pasco anavyompigia "chepuo" Mchechu kuwa CS!.....daahh sisi wabongo aisee.....halafu antoa mifano akihalalisha uzembe.....tena anazidi kuuhalalisha eti ulianzia kwa JKN (RIP)......duuhh
 
Last edited by a moderator:
Mkuu haihitaji kuwa rocket scientist kujua kama kuna rushwa kubwa kwenye mkataba huu. Kwa maelezo ya NHC wenyewe pamoja na kutoa kiwanja ( kati kati ya jiji ) wao umiliki wao ni 25% tu ya jengo. Kabla ya hapo kulikuwa na jengo la ghorofa saba likimilikiwa na NHC exclusively. Limebomolewa kupisha "ubia" wa kimagumashi.

Hata mkimpaka rangi vipi Mchechu has to go....

....wow...wow...I did not know this!!......duuhh.....sasa naanza kuelewa mambo fulani...naendelea kuunganisha dots......damn! when you need Mzee Mwanakijiji .....uko wapi mkuu?.....this time around we have Mchechu....wakati ule tulikuwa naye Dr. Dau......
 
Heshima mbele wakuu Joshi Kanji na Mkuu macho_mdiliko .........naomba mtambue kuna watu wengi sana wanafaidika na upuuzi unaoendelea katika nchi hii......umeona Pasco anavyompigia "chepuo" Mchechu kuwa CS!.....daahh sisi wabongo aisee.....halafu antoa mifano akihalalisha uzembe.....tena anazidi kuuhalalisha eti ulianzia kwa JKN (RIP)......duuhh
Pasco huyu ni mchumia tumbo siku nyingi. Alikuwa Jeshi la Wananchi kukamshinda ndio akaibukia Radio Tanzania. Ni mmoja ya watu wanaomtetea sana huyu MD wa NHC. Halafu nasikia jamaa ametembeza bahasha iliyoendana na press release ili kina Manyenyre Jackton wamsafishe na waandishi wengine wamsafishe
 
Unajua huyu bwana a Mchechu kaingia NHC kimagumashi, tunajua fika kwamba hata katika usahili uliofanywa na wale jamaa wa Delloitte n touch nadhani hapa sijapatia jina lao haswa, ni kwamba Mchechu alifeli kwa mbali katika usaili na ilitumika tikitaka kuwakataa wasomi wa Ardhi na wengineo ili wachukue nafasi. Sasa Mchechu alipoingia kalazimisha kufanya mambo makubwa yanayomzidi uwezo na hatimaye yale mazuri waliyofanya uongozi uliopita yeye kayazika na kuanzisha yake na ndio maana Ghorofa lilikuwa na kibali cha ghorofa chache yeye kaziongeza ili aonekane tofauti na watangulizi wake. Sasa hii ni moja mengine makubwa yanafuata na kwa ufupi nadharia ya Kibenki sio kivitendo vya shirika kubwa la nyumba la Taifa ambalo Baba wa Taifa hili alianzisha kwa minajili ya wanyonge waweze kumudu kulipia kodi lakini yeye kapandisha kodi ili wenye nazo kama fisadi yeye waweze kuishi. Yetu masikio na tutayaona ya Mchechu ni mengi na yanatisha, ni fisadi kuliko wale wanaotajwa hasa katika masuala ya NHC na ubia, jamaa anatisha halingani na umri wake, je umechunguza ni kwanini ameanzisha ajira ya wakurugenzi zaidi ya 12? ili hali yeye akipata mshahara wa kufa mtu? sasa twende kwenye sifa za hao wakurugenzi wake wapya, yupo mmoja hana sifa huko alikokuwa yaani kampuni moja inayojihusisha na upangishaji wa majumba, huyo anashutumwa huko kwa maosa ya uwizi. Jamaa hafai.:shut-mouth:
 
NKM....mkuu jitihada zako za kufufua maiti(NHC) zinaonekana na sasa inapiga chafya..haya ni maajabu makubwa tunakupongeza

Swali langu moja..ni vipi pale Shekilango muwaongezee adha wapangaji wenu kwa kuwajengea ghorofa kati ya ghorofa?

Wapaki wp magari?watoto wao wacheze wapi? Nguo waanike wapi? Na majanga kama moto yakitokea hali itakuwaje maana hata gari ya Fire & rescue haitaweza kuingia

Je hamna viwanja vipya au vya zamani venye nafasi hata nje ya jiji mkaviendeleza kuliko kuchafua jiji namna ile? Kumiliki vile viwanja sio maana yake lazima uvijenge!!!

kwa ahadi yako kuwa utajibu ukiwa na wasaa naomba hili pia lijibu katika press conference kwa ufasaha


whaaaat?....eti nini?.........kuna ujenzi unaendelea pale?............dah....basi huyu jamaa hafai kabisa.......duuhh! hivi kweli tuna Town Planning Committee kweli?....... au wamepigwa vibahasha.........nimechukia sana kusikia hili jambo.....
 
whaaaat?....eti nini?.........kuna ujenzi unaendelea pale?............dah....basi huyu jamaa hafai kabisa.......duuhh! hivi kweli tuna Town Planning Committee kweli?....... au wamepigwa vibahasha.........nimechukia sana kusikia hili jambo.....
Mkuu ukipaona utadhani ni eneo la biasharakumbe ni makazi ya watu,hata hewa itakuwa ya mgao na sijui siku sewerage zikiziba itakuwa kasheshe
yaani utadhani tupo tokyo kwenye uhaba wa ardhi
 
Mchechu aka NKM,

Shukran kwa kuja kwenye jukwaa hili na karibu JF.

Nianze kwa kukutaka radhi kwa kauli yangu kuwa hujafika eneo la tukio ilhali umeshafika mara mbili, hii inatokana uwepo wako kutoripotiwa na vyombo vyetu vya habari ambavyo wengi ndio tunategemea kuhabarishwa navyo.

Tuingie kwenye somo husika sasa, kwa kuwa umedai kwa sasa unashughulika na zoezi la uokoaji na utatoa majibu ya kadhia yote ndani ya siku 2, ama kuanzisha thread hapa au kuitisha mkutano na waandishi wa habari. Ombi langu kwako ni wengine hapa sio waandishi wa habari na wala hatuna press card za kuingia katika mikutano hiyo, jukwaa letu ni JF na kwa kuwa umeamua kujisajiri hapa naomba majibu ya maswali yangu hapa hapa JF. Nina maswali yafuatayo;

1. Mkataba wenu na Ndugu Ladha ni kujenga ghorofa 10 na kibali kilichotolewa na Manispaa ya Ilala ni ujenzi wa ghorofa kumi. Je imekuwaje zikajengwa ghorofa 16? Je hamkulijua hilo?

2. Hisa zenu ni 25% na Mr Ladha 75% je hii hesabu 25% yenu imekokotolewa kutoka kwenye ghorofa 10 au 16?

3. Ikiwa (namba 2 hapo juu ) jibu ni hesabu imekokotolewa kutoka kwenye ghorofa 10 ina maana mmedhulumiwa ghorofa 6 kwenye mapato hence kwa nini tusiite mikataba yako na Mr Ladha ni sawa na ile ya Sultan Mangungu wa Msovero na Karl Peters?

4. Ikiwa ( namba 2 hapo juu ) jibu ni hesabu imekokotolewa kutoka kwenye ghorofa 16 ina maana umeshiriki katika kupindisha sheria na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20 kwa nini usiwajibike na kufunguliwa mashtaka ya kuuwa bila kukusudia?

5. Inakuwaje nyumba ambazo Marehemu Mwalimu Nyerere alizitaifisha kutoka kwa wahindi ili watu wakipato cha chini wapate makazi wewe na genge lako mnaziuza kwa bei chee (throw away price) kwa wahindi hao hao kwa kwa jina la "ubia" wa 25%?

6. Hivi pamoja na usomi wako wote na jopo la wataalam wa real estate hapo NHC, role yenu kwenye so called "ubia" inaishia kutoa kiwanja tu halafu mnaacha mtu afanye atakavyo hata akijenga ghorofa ni mitete na matope haliwahusu?

7. Pale kariakoo kuna nyumba nyingi za watu binafsi zinajengwa kwa "ubia" mikataba yao si ya ki Karl Peters kama ya kwako, kuna wengine wanatoa kiwanja "mwekezaji" anajenga na kulitumia jengo say kwa miaka 10 au 15 baadae linarudi kwa mwenye kiwanja, wakati huo huo ndani ya kipindi hicho anapewa frame za maduka 2 au 3 na floor kadhaa. Je kwa nini usiende kujifunza kutoka huko? (assuming utaendelea kuwepo kwani kama alivyosema Fundi Mchundo usiwe na khofu watatolewa kafara vidagaa ninyi mpapa mtaachwa)

8. Based on the above, kwa nini usijiuzulu na kufunguliwa mashtaka?

Nitashangaa sana kwa mtu mkweli na muwazi NKM atakapokuja hapa akiwa Defensive kujibu maswali hayo ya Joshi Kanji ......

maswali mazuri sana hayo mkuu
 
Kuna watu humu hawajui hata wanaongea nini?msikurupuke kuongea vitu ambavyo huvijui,ushabiki usiokuwa na tija haujengi,mtu kama unachuki binafsi na mtu humu si mahali pake,mtafute na umueleze na sio kuongea pumba ambazo hazina mantiki.message sent

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
mjenga ghorofa ni diwani(ccm)!mmiliki ni mchechu (Luhanjo) dah dhaifu ana kazi apa...alafu pia naskia :shut-mouth:
 
Wakati taifa lipo katika kuombeleza janga la kuanguka kwa jengo la ghorofa kati kati ya jiji, kuna mambo kadhaa yamejitokeza kuhusiana na mkasa huu.

Shirika la Umma kama NHC kuingia ubia wa kimagumashi magumashi na wafanyabishara wababaishaji kumepelekea kupotea kwa maisha ya ndugu zetu takriban 20+. Inakuwaje uwekezaji mkubwa kama huu NHC wanaacha kila kitu kiendeshwe kienyeji enyeji tu? kibaya zaidi sasa wanaibuka na kusema wanapitia upya sera yao ubia ili washirikishwe zaidi!.

Kwa mshangao mkubwa juhudi zote za uokoaji zinazo endelea si Mchechu au kiongozi yeyote mwandamizi wa NHC alie thubutu walau kufika site kujionea hali halisi. Rais pamoja na majukumu yake mengi ameshatembelea eneo husika mara mbili.

Imefika wakati mkurugenzi mkuu wa NHC akamatwe na awajibishwe na mamlaka za uteuzi. Taifa haliwezi kuingia katika janga kubwa kama hili wakati wahusika wala hawana habari.

Mchechu has to go....

==========
Majibu ya Nehemiah Kyando Mchechu:
Msechu hawezi kujiuzulu kwakuwa yeye siyo mhandisi wa ujenzi wa jengo hilo Msechu kwa niaba ya NHC alitoa ardhi kwa yule mtu lakini yeye hana jukumu lakufuatilia ubora wa ujenzi bali zipo mamlaka zinazohusika na jukumu hilo na ndizo zinapaswa kuwajibishwa lakini kwa ushamba na ulimbukeni wa Msechu akiamini kuongea kiingereza ndiyo kusoma sana nina mashaka hata na upeo wake wa kupambanua mambo. Hivi nyie wabongo malimbukeni kama msechu mnadhani kuongea lugha ya mwingine ndiyo uonekane umekwenda shule kuliko mchina anayetumia lugha yake kuitawala africa? Badilika acha ushamba na utumwa wa kufikiri.
 
Mkuu with due respect wewe hoja zako ndio hazina mashiko!

1. Unadai mkataba ulifungwa 2006 na kwa kuwa Mchechu aliingia 2007 hahusiki! wot a joke! Jengo limeanguka jana 2013 kwa taarifa yako. Kibaya zaidi mkataba ulikuwa wa kujenga ghorofa 10 tu ngoma imeendelea mpaka ghorofa ya 16! under watchfull of Mchechu!

2. Eti "sasa wanatembelea Hilux!" kichekesho mkuu, kutembelea Hilux ndio justification ya kuua watu 20+?

Huu utetezi ulioleta hapa ni mwembamba sana, sidhani hata kama unafahamu dhana ya kuwajibika ilivyo. Likibuma chini ya uongozi wako ndio lako hilo, kaingia toka 2007 kwanini ali review mikataba ya kimagumashi?

Mchechu has to go....

Mimi pia nasema Msechu hahusiki kwa sababu yeye siyo mrasimu ramani wala injia amehusika pale kama Mkurugenzi wa NHC TU. JENGO LINA UBORA GANI ZIPO MAMLAKA ZA KUHAKIKI MAJENGO NA UKIJUA DIVISION OF LABOR HUTAMLAUMU MSECHU, KAMA JENGO LILIKUWA LA GHOROFA KUMI MHANDISI WA UJENZI WILAYA YA ILALA ALIKUWA WAPI MPAKA ZIKAFIKA 16? HUYO NDIYO ANATAKIWA KUNYONGWA BILA HATA KUPELEKWA MAHAKAMANI NA WENZAKE NA SI BISHOO MSECHU ANAYE AMINI KIINGEREZA NDIYO SHULE
 
Mkuu ukipaona utadhani ni eneo la biasharakumbe ni makazi ya watu,hata hewa itakuwa ya mgao na sijui siku sewerage zikiziba itakuwa kasheshe
yaani utadhani tupo tokyo kwenye uhaba wa ardhi
watu wetu siku hizi hawajali kwasababu wanapopanga miradi ya wananchi hawajioni na kudhani hata wao wanaweza wakaishi ama kupata huduma hiyo!! wanaviona hivyo viota ni kwa ajili ya masikini,siyo kwa hadhi yao! ni matatizo yanayozikabili karibu sekta zote muhimu ambazo ni elimu,afya na makazi!
 
Joshi,

Nitakujibu maswali yako kama ulivyoomba, lakini kama hautaridhika basi nakukaribisha NHC kuonana na mtu yeyote na kila mwana NHC ataweza kukujibu kwa ufasaha! Kwa baadhi yetu tunapata tabu sana kumjibu mtu usiyemjua na kuendelea kubishana, and therefore remaining silence is our best option!

1. Mkataba wenu na Ndugu Ladha ni kujenga ghorofa 10 na kibali kilichotolewa na Manispaa ya Ilala ni ujenzi wa ghorofa kumi. Je imekuwaje zikajengwa ghorofa 16? Je hamkulijua hilo?

NHC wana mikataba ya aina tofauti ambayo imekuwa ikiboreshwa kila inapobidi. Uboreshaji wa mikataba unakuwa kwaajili ya mikataba mipya na hiigusi mikataba ya zamani automatically, mpaka kunapokuwa na specific negotiations kama inavyoendelea kwasasa kwa baadhi ya mikataba. Mpaka sasa kuna version nne za mikataba inayoendelea ambayo iilisainiwa katika vipindi tofauti, na kwa kutambua hilo, ndio maana SERIKALI walitoa maagizo mwaka 2010 wakati waikizindua Bodi mpya na Menejimenti mpya ya kuwa NHC wasitishe kutoa mikataba mipya ili waipitie upya sera yao ya ubia.

Katika mikataba hiyo, kuna mojawapo ambayo NHC wanapata asilimia 25% mara mradi ukukamilika na asilimia nyingine 25% baada ya miaka kumi na mbili na kufanya kuwa asilimia 50% kila upande! Katika hii ya mwanzo NHC walikuwa wanamwachia muwekezaji wajibu wote wa kutafuta wataalamu waliosajiliwa na pia wajibu wa kupata vibali vyote, pamoja na kutafuta pesa ya ujenzi na kusimamia mradi mpaka ukamilike. Mkataba wa Ladha ni mmoja wapo wa mikataba hiyo.

Kuna maboresho yaliyofanyika baadae kuanzia mwishoni mwa mwaka 2007 ambapo NHC walichukua jukumu la kushiriki katika hatua za kuchagua wataalamu, pamoja na kusimamia miradi na hii ni katika miradi mingine inayoendelea kwa sasa.

Wajibu wa kupata kibali ulikuwa ni kwa mbia mwendelezaji kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa 04/02/2007. Na hata kama kuna ongezeko la mahitaji ilikuwa ni wajibu wa mwekezaji.

2. Hisa zenu ni 25% na Mr Ladha 75% je hii hesabu 25% yenu imekokotolewa kutoka kwenye ghorofa 10 au 16?

Hisa za 25% ni katika makubaliano yaliyoko kwenye mkataba na kama kuna ongezeko automatically inaongezeka lakini hii inafanyika mara mradi unapokwisha. Hakuna flat inayoweza kufichwa kwahiyo NHC lazima wapate haki yao inayoonekana.

3. Ikiwa (namba 2 hapo juu ) jibu ni hesabu imekokotolewa kutoka kwenye ghorofa 10 ina maana mmedhulumiwa ghorofa 6 kwenye mapato hence kwa nini tusiite mikataba yako na Mr Ladha ni sawa na ile ya Sultan Mangungu wa Msovero na Karl Peters?
Refer to No.2.
4. Ikiwa ( namba 2 hapo juu ) jibu ni hesabu imekokotolewa kutoka kwenye ghorofa 16 ina maana umeshiriki katika kupindisha sheria na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20 kwa nini usiwajibike na kufunguliwa mashtaka ya kuuwa bila kukusudia?
Rejea number 1 hapo juu, mwenye wajibu wa kuomba vibali kutoka mamlaka husika ni mbia mwendelezaji. Na lazima tujifunze kuheshimu mikataba na kama haufai kabisa unajadili na mbia mwenzako kwa ajili ya marekebisho au unajifunza kutokana na makosa na kutenegenza mikataba mizuri kwa siku za usoni. Kwa kukubali kuchukua wajibu Fulani unakuwa responsible katika hilo! Na kama umesaini kuendesha mradi kamili ni lazima uheshimu sheria za nchi na pia kutimiza wajibu wako wa kimkataba.

5. Inakuwaje nyumba ambazo Marehemu Mwalimu Nyerere alizitaifisha kutoka kwa wahindi ili watu wakipato cha chini wapate makazi wewe na genge lako mnaziuza kwa bei chee (throw away price) kwa wahindi hao hao kwa kwa jina la "ubia" wa 25%?
Genge si lugha ya kistaarabu, lakini nitakujibu hilo unaloliita genge hawajawahi kusaini mkataba wowote wa ubia, na serikali ililiagiza hilo genge kuipitia upya sera ya ubia iliiweze kukidhi mahitaji ya sasa kwa kuyafanyia kazi makosa yaliyokuwepo katika sera ya mwanzo bila kupoteza yale yaliyo mazuri.

By the way si vema kuwahukumu watu kwa rangi zao, na ni upuuzi kuzungumzia neno Wahindi kwasasa, wakati dunia inazidi kujichanganya na makundi mengi zaidi ya mataifa mbalimbali. Suluhisho la matatizo yako linaanzia kwako mwenyewe na sikulaumu matabaka mengine na hususani kwa mtu anayeonekana kuwa na weredi kama wewe!


BUT PUT SIMPLE, NKM HAS NEVER SIGNED ANY JV CONTRACT SO FAR. Lakini hiyo haifanyi sera ya ubia kuwa ni mbaya na kwamba hatutarejea kwenye sera hii, kimsingi tumeishafanyia marekebisho makubwa sana na kwasasa ina mazao (Products) matatu kwa kufuata sera ya PPP ambayo kwasasa ipo. Na the growing upcoming middle class wananafasi kwasasa kuchangamkia nafasi hizi za uwekezaji ambazo uwazi wake umeongezeka kwa kiwango kikubwa.

Kiuchumi, huwezi ukawa na kiwanja cha bilioni tano na ndani yake ukawa una nyumba ya thamani ya milioni mia, na sehemu inayoweza kuwa na watanzania mia ukawa na familia mbili. Kwanini utake watanzania wengine wateseke kusafiri kutoka Kimara na Tegeta kwa masaa manne kila siku iendayo kwa Mungu wakati wangeweze kwenda ofisini kwa dakika kumi kutoka Upanga na maeneo ya karibu ya jiji kama wewe ufanyavyo. Kwanini unapenda kufikiri kuwa watanzania wote hawaujui uchumi rahisi huo?! Huoni ya kuwa hii itasaidia kupunguza hata foleni kama baadhi ya wakazi wetu watahamia mjini kati kutoka pembezoni mwa Dar!
6. Hivi pamoja na usomi wako wote na jopo la wataalam wa real estate hapo NHC, role yenu kwenye so called "ubia" inaishia kutoa kiwanja tu halafu mnaacha mtu afanye atakavyo hata akijenga ghorofa ni mitete na matope haliwahusu?

Rejea namba moja na namba tano, inawezekana ni kwasasababu ya huo usomi na kuwa na jopo zuri la wataalamu wa real Estate hapo NHC ndo maana hakuna mkataba uliosainiwa tokea mwaka 2010 na hii inamaanisha kuwa wameniongoza vizuri. Lakini hii haimanishi ya kuwa Ubia ni kitu kibaya lahasha! Ubia unafanyika Dunia kote na kitu cha muhimu ni kuwa na mikataba yenye tija!

Na ndiyo maana marekebisho kwenye sera ya ubia yamefanyika, angalia kwenye website utaona baadhi ya Products, na pia Road show zimeshafanyika, na kama unafikiri kuna haja ya maboresho kwenye Products hizo, tafadhali tunaomba utupe maoni yako moja kwa moja kwenye website yetu, kwenye email yangu, au karibu NHC tuweze kukusikia mawazo yako mazuri na tuweze kuboresha products zetu kwa manufaa ya nchi na wananchi.

Narejea ya kuwa Ubia si kitu kibaya, ni kitu kizuri na kinchohitajika ni kuwa na mikataba yenye masilahi na kuwa na uwezo wa kuisimamia vyema katika utekelezaji wake. Na sera yetu mpya iliyoanza kazi imeyafanyia kazi madhaifu yaliyokuwepo kwenye sera zetu za awali.

7. Pale kariakoo kuna nyumba nyingi za watu binafsi zinajengwa kwa "ubia" mikataba yao si ya ki Karl Peters kama ya kwako, kuna wengine wanatoa kiwanja "mwekezaji" anajenga na kulitumia jengo say kwa miaka 10 au 15 baadae linarudi kwa mwenye kiwanja, wakati huo huo ndani ya kipindi hicho anapewa frame za maduka 2 au 3 na floor kadhaa. Je kwa nini usiende kujifunza kutoka huko? (assuming utaendelea kuwepo kwani kama alivyosema Fundi Mchundo usiwe na khofu watatolewa kafara vidagaa ninyi mpapa mtaachwa)
Mimi Binafsi ninajifunza kwa watu wengi sana bila kujali rika zao, nafasi zao katika jamii, na rangi zao! Huko kariakoo kuna watu wengi sana ambao hawajafika hata Chuo Kikuu lakini wanaendesha vizuri maisha yao, na hawa siwatu wa kubeza! Huwa natamani tungekuwa na watanzania wengi wenye bidii kama watu wa Kariakoo na hususani kutoka kwenye kundi la wasomi wetu. Hao watu wa Kariakoo uliowalenga katika point yako hii, hawaijui ajira ya kuajiriwa lakini ni nadra kuwasikia wakilalamika kuwa hakuna ajira na mengine, kimsingi ni wapiganaji! Kwahiyo nawaheshimu sana. Na pia najifunza kutoka kwa watu wa mataifa mengine mengi na ninaamini katika imani ya kujifunza daima, nafikiri kwa spirit hiyo, bado nina maisha yenye matumaini hata baada ya NHC, na nitachapa kazi mpaka dakika ya mwisho kama nilivyofanya katika taasisi zingine nilizofanya kazi, tembea na ulizia!
8. Based on the above, kwa nini usijiuzulu na kufunguliwa mashtaka? Need say more based on the above! I am not going to comment on this one, but your voice may have been heard.
However if you never knew NHC is my fifth employer in my career, and this should be enough to remind you that there is no permanence to most people in our current generation, and we are all a labor commodities and we all walk with our price tags! And it is the deliverables that sets your price either in the Government or in private sector! And for me, I am happy with what I have achieved in NHC in the less than three years of my stay of less than there so far.

Feel free kuwasiliana moja kwa moja na NHC au mimi mwenyewe kwa email au simu, na nitasikiliza mawazo yako na kuyafanyia kazi yaliyo mazuri. Ni vyema kupata undani wa mambo kabla ya kukimbilia kutoa shutuma, ingawa bado mawazo mazuri tunayachukua hata pale yanapokuja kwa lugha mbaya!
 
Dahhh hili ni dongo kwa Haruna Masebu.........NKM....tunashukuru kwa kutumia muda wako kutoa ufafanuzi........

majibu yako however yameonyesha kuwa NHC ina tamaa kubwa ya maendeleo kuliko kuangalia obvious risks in short, median and long term......unaposema eneo lina thamani ya Billioni 5 na investiment ni ya milioni mia.....ni kweli kama ulivyosema.....huo ni "uchumi rahisi" ambao unatuingiza katika challenges......kama ifuatavyo

1. Mazingira
2. Health and safety
3. Miundo mbinu (Utility Services and associated maintenances)

Swali la kwanza umelikwepa kwa kutupia mzigo kwa mwekezaji na Mkataba as if NHC hamkuwa na interest......sasa kwa "uchumi rahisi" uliouzungumzia.........what if mwekezaji hawekezi kulingana na thamani za uchumi rahisi uliozungumzia.....umeona MATOKEO YAKE SASA!!........well its very simple "uchumi rahisi"


Jibu lako la swali la nne....bado unaendelea kukwepa......yaani kwa kifupi NHC mlikuwa mnakubali Jengo kukamilika without quality........ambalo lets say watu wangehamia na baada ya muda lote linaanguka.....bado ungesema unaheshimu mkataba.........huku ukiwaweka Wazalendo uliodai upcoming Middle Class kwenye Risk ya kupoteza maisha......vipi gharama za kupoteza maisha ya hizo resources kwa serikali na kwa familia zao husika.......bado unajivika mwamvuli wa Mkataba!........

Tunakubali wewe ni bidhaa yenye price tag.....na kuwa soko lako kubwa....lakini unasahau jambo moja kuwa umekosa uzalendo wa kutojali maisha ya Watanzania nakujali unachopata wewe na mwajiri wako bila kuangalia madhara mbeleni in a bigger picture..........

Jibu lako la pili.....pia linaonyesha wewe uko kwenye ku-receive immediate kipato kwa NHC bila kuangalia madhara makubwa kwa serikali na wananchi wake.......
 
....wow...wow...I did not know this!!......duuhh.....sasa naanza kuelewa mambo fulani...naendelea kuunganisha dots......damn! when you need Mzee Mwanakijiji .....uko wapi mkuu?.....this time around we have Mchechu....wakati ule tulikuwa naye Dr. Dau......
Rudini nyuma mtusome wengine tulisema nini wakati ule wa uteuzi wake. Mimi ni miongoni mwa watu ambao ninaamini NHC ilipaswa ivunjwe na kurudishwa katika kazi yake ya kwanza kabisa siyo sasa hivi walivyoligeuza kuwa ni shirika la kibiashara.
 
Jamani It is common sense, NHC haiwezi kuepuka katika sakata hili, sema kwa kuwa serikali yetu ni ya kishikaji ni sawa tu, pamoja na kuwa na 30% bado interms of responsibility na authority katika ku protect national interest NHC inajukumu na majority shareholder na kama hili wakina Mchechu na mshikaji wake JK hawakulijua basi ni kichekesho.

Mimi ni mmoja kati ya watu wachache sana waliokwisha sema hii habari ya roadshow media management ya wakina Mchechu ni time bomb na kashfa yake itazidi hata zile za EPA na Dowans, sasa ndugu yangu angalia hata hicho kiingereza chenyewe ni cha kikurungezi kweli (I am hear?) nakubaliana kabisa na Joshi Kanji tabia za wakina Pasco za upambe hazitusaidii, jengo la vioo la samora ndio litakalovunja rekodi zote ulimwenguni siku ya siku.

Swali la msingi inamaana responsibility ya NHC kwenye joint venture hiyo ni kupata revenue tu mwisho wa siku? where were they wakati linaongezwa gorofa kwa 60% if the original BOQ? rubbish hatawapeani vyeo gani na kulindana vipi, siku ya siku kila aliyeua kwa 10% kama hoja zinajenwa kwa wakina Tony Blair na George Bush itakua hawa wa huku kwetu?
 
Last edited by a moderator:
NKM anavuta sana uliza mmiliki wa zile appartemnt za pale OASIS mbezi beach ni nani kama hujaambiwa ni huyo huyo Mchechu?

Kaangalie zile nyumba za NHC kigamboni contractors ni kina nani? Na kama utaona sticker za CRB kwenye ule ubao wa mradi?

Mcheshu mwenyewe kapata hio Kazi Kimizenge.....!!! Msitegemee Maajabu!!!

Zilikuja Post kibao hapa za Kusupport nomination yake km vile ilivyosasa baadhi tunavyotetea Uozo!!!

Watu wanatoa Mifano MFU ili tu kutetea Tumbo au Ushikaji....!!! Eti Uwajibikaji Ulizikwa na Nyerere?
Wakati Juzi Juzi tu hapa wakati wa kuzama kwa meli ZNZ kuna mmoja Kawajibika!!!

Tonge tamu....the guy na waliomuweka hawatapenda "Dogo" aachie Ngazi!!!!
 
Back
Top Bottom