Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Watu wanavyocheza na media basi woote mnadanganyika, hivi wewe uliweza kununua apartment pale shekilango? if yes basi unaweza kuwa na majengi kadhaa hapa mjini. Mchechu anawaburuza nanyi basi mnaingia, vijana wetu mfanoi graduates watakuja kupanga wapi? au ndo wakapange sinza kodi laki saba wakati mshahara laki nne. baada ya muda NHC itakuwa inamiliki nini? au ndo yaleyale mawaziri wanakaa quarter za pale kijitonyama wenzao wajanja wameporomosha majengo kwenye nyumba za masaki walizouziwa, talk to NHC employees wenye vision wakwambie, Mchechu yuko njiani he wants to reach somewhere as fast as possible. Sasa ndo ndo nini unaingia joint venture na wale wahindi wanalipualipua majengo wakati we ndo majority shareholder usiwe na kitengo mathubuti cha kusimamia quality ya majengo. Kaingia NHC taaluma za ujenzi kaziignore na kuwaajiri watu wa masoko na benki ili wauze nyumba na nyie mnaavyoamishwa na kila msikiacho mnakubali na kutoa misifa, Mungu atupe uhai utakuja kuelewa.

wewe hujui biashara kabisa sio kila kitu lazima ukariri..soma biashara ya real estate...kati ya business ya kujenga nyumba na kuuza na kujenga nyumba na kurent ipi profitable ndo uje uandike ----- wako hapa! watu wanatumia akili , nehemia ni jembe muacheni miaka elfu..lala huko
 
Kusema kwamba NHC/Mchechu na viongozi wengine wa shirika hilo hawahusiki ni kijidangaya wenyewe. NHC kama miliki wa kiwanja halitakiwa wajue nini kinachoendelea kwenye plot yake. Inakuaje mkataba ya kujenga ghorofa 10 na liendelee mpaka ngorofa 16 bila wao kutia neno? Je NHC wakaguzi wa plots na majengo yao? pili ukiangalia ilo jengo lilivyosambaratika utafikiri limepigwa na bomu, hata foundation haijabakia-means ujenzi wake ulikua duni sana sana sana. Maana yake hata kama lingekamilika mwisho wa mkataba kama ni miaka 20-30 mbia wa pili angerudisha jengo kwa NHC likiwa sio salama kwa watumiaji. Je hapo sio kwamba NHC wanahatarisha usalama wa wapangaji wao? Je kwanini NHC ya leo inashindwa kusimamia ujenzi wa nyumba imara kama hizo zilizojengwa na mkoloni/wahindi wa miaka 1960s.

Mwisho nikisema kwamba NHC inachangia kuvuruga Master plan ya mji mkongwe wa DSM nitakua nakosea?, kwani pembeni mwa jengo lililoanguka kuna jengo lingine la ghorofa 15 linaendelea kujengwa ndani ya plot nyingine ya NHC. Hao maeneo yalikua murua kama yakiendelea na nyumba zisizozidi 5 storey block (check pic:source Michuzi). NHC kama shirika la serikali lililo jaa wasomi kibao wa real estate lilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa wa kufuata taratibu za mipango miji. Mchechu hatabakia hapo kwa sababu ni mtoto wa "ikulu" na hatuna culture ya kuwajibika, kama ana akili timamu anatakiwa kuachia ngazi kuonyesha uwajibikaji.
 
Attachments

  • GOPR2834.jpg
    GOPR2834.jpg
    213.1 KB · Views: 126
Hivi ni nani anatakiwa kuwajibishwa au kuwajibika? Naona wengi wanaingia mtego wa chuki ambazo hazina mbele wala nyuma. Je ni nani anatoa kibali cha ujenzi? Je ni nani anaridhia ramani hadi jengo kuanza kujengwa? Ni nani anasimamia ujenzi kuona kwamba viwango vilivyowekwa vinafuatwa? Je wizara inayohusika au kitengo kinachohusika kimeshaweka mkakati wa uchunguzi yakinifu kuangalia hasa ni nini kilichofanya jengo hilo kuporomoka? Je, wizara husika imechukua hatua gani kusitisha ujenzi wowote ule wa majengo marefu bandarini salama au kufanya ukaguzi wa hali ya juu kuokoa maisha ambayo yanaweza kupotea kwenye baadhi ya majengo yanayoendelea?

Maswali ni mengi, Je tume iliyochunguza kuporomoka kwa ghorofa miaka michache hapa Dar ilitoa ripoti gani na je hiyo ripoti ilifanyiwa kazi? Je hawa makandarasi wana wafanyakazi wenye viwango vinavyokubalika kimataifa kwenye fani zao? Nani inaangalia kwamba hatuna wafanyakazi ambao ujuzi wao ni sawa na wanaomaliza shule za kata?
 
Mkuu with due respect wewe hoja zako ndio hazina mashiko!

1. Unadai mkataba ulifungwa 2006 na kwa kuwa Mchechu aliingia 2007 hahusiki! wot a joke! Jengo limeanguka jana 2013 kwa taarifa yako. Kibaya zaidi mkataba ulikuwa wa kujenga ghorofa 10 tu ngoma imeendelea mpaka ghorofa ya 16! under watchfull of Mchechu!

2. Eti "sasa wanatembelea Hilux!" kichekesho mkuu, kutembelea Hilux ndio justification ya kuua watu 20+?

Huu utetezi ulioleta hapa ni mwembamba sana, sidhani hata kama unafahamu dhana ya kuwajibika ilivyo. Likibuma chini ya uongozi wako ndio lako hilo, kaingia toka 2007 kwanini ali review mikataba ya kimagumashi?

Mchechu has to go....

Kanji,
Kukimbilia kuhukumu bila kulielewa tatizo unaweza usitatue chochote. Hapa tatizo sio mkataba, bali ni ujenzi mbovu, material dhaifu, design mbovu au mchanganyiko wa hivyo nilivyotaja. Kwa hiyo watu wanaotakiwa kuwa wa kwanza kuminywa ni Mjengaji (Contractor), Msimamiaji wa ujenzi (Project/Resident Engineer/Consultant), Archtect, Structural Engineer, idara ya ujenzi NHC, City Engineer na wengine wengi wanaohusika moja kwa moja na ubora wa jengo kitaaluma.

Mchechu na wengine wasiohusika na ujenzi moja kwa moja kitaaluma, wao zamu yao itakuja baada ya uchunguzi wa nini kilichoangusha jengo kujulikana. Ushirikiano kwenye uwekezaji wa miradi ya NHC sio ulioangusha jengo. Lakini kama ujenzi na usimamizi ungekuwa ni huu huu, basi hili lingetokea hata kama pesa ya ujenzi ingekuwa ya NHC peke yake.
 
mchechu anahusika sana km hahusiki basi ladha wanamuonea yeye anahusikaje?

watu kama nyie ndio mnauwa nchi. Ndio maana Mawaziri washenzi hawawajibiki maana wenye akili za panzi kama ninyi mnawatetea.Aibu kila mahali. Ungesoma media za nje ndio ungejua hata presida alipaswa kuwajibika kwa kuteua vilaza.Giv me a break alaaah
 
Kanji,
Kukimbilia kuhukumu bila kulielewa tatizo unaweza usitatue chochote. Hapa tatizo sio mkataba, bali ni ujenzi mbovu, material dhaifu, design mbovu au mchanganyiko wa hivyo nilivyotaja. Kwa hiyo watu wanaotakiwa kuwa wa kwanza kuminywa ni Mjengaji (Contractor), Msimamiaji wa ujenzi (Project/Resident Engineer/Consultant), Archtect, Structural Engineer, idara ya ujenzi NHC, City Engineer na wengine wengi wanaohusika moja kwa moja na ubora wa jengo kitaaluma.

Mchechu na wengine wasiohusika na ujenzi moja kwa moja kitaaluma, wao zamu yao itakuja baada ya uchunguzi wa nini kilichoangusha jengo kujulikana. Ushirikiano kwenye uwekezaji wa miradi ya NHC sio ulioangusha jengo. Lakini kama ujenzi na usimamizi ungekuwa ni huu huu, basi hili lingetokea hata kama pesa ya ujenzi ingekuwa ya NHC peke yake.

Kama hujui dhana ya uajibikaji piga domo kufuli mkuu. Unabwabaja tu.
 
Tukiacha rushwa tutakuwa na guts za kufanya maamuzi magumu
 
Joshi, NKM stands for Nehemiah Kyando Mchechu, and in future when you see such an ID just know that it's Mchechu responding on issues or commenting! I am not a person who will hide is ID since I believe in truth and transparent! Neither do you have so many people at my level in Public Sector and non political who stands by their ID's.

Just to prove you wrong I am now at the accident scene as I am writing to you and we are not more than 70 people, and I was hear yesterday up until 01:30am! I am following through all the comments in different threads, actually I have always been a good follower of JamiiForums but I was never a contributor! I think the series of threads which most are misleading without facts have pushed me to consider responding to all these issues. However, by obviously fact I do not expect to become an active member on contributions!

For now I have opted to focus on the task at hand here at the accident scene, and I will try to respond on these few in a very brief in the coming two days either by posting a thread or by calling a press conference where you can come and ask as many questions as you want and we will respond to all of them and I hope it Will be at your satisfactory level and to others as well! There is nothing to hide here, no politics, no partisans side and no blax2! I am sure the press conference has always enough participants who are members of JamiiForums and they gone through all the posted comments and certainly they will be looking for answers by asking the same sort of questions!

Thanks and stay relaxed till then!
 
Hivi ni nani anatakiwa kuwajibishwa au kuwajibika? Naona wengi wanaingia mtego wa chuki ambazo hazina mbele wala nyuma. Je ni nani anatoa kibali cha ujenzi? Je ni nani anaridhia ramani hadi jengo kuanza kujengwa? Ni nani anasimamia ujenzi kuona kwamba viwango vilivyowekwa vinafuatwa? Je wizara inayohusika au kitengo kinachohusika kimeshaweka mkakati wa uchunguzi yakinifu kuangalia hasa ni nini kilichofanya jengo hilo kuporomoka? Je, wizara husika imechukua hatua gani kusitisha ujenzi wowote ule wa majengo marefu bandarini salama au kufanya ukaguzi wa hali ya juu kuokoa maisha ambayo yanaweza kupotea kwenye baadhi ya majengo yanayoendelea?

Maswali ni mengi, Je tume iliyochunguza kuporomoka kwa ghorofa miaka michache hapa Dar ilitoa ripoti gani na je hiyo ripoti ilifanyiwa kazi? Je hawa makandarasi wana wafanyakazi wenye viwango vinavyokubalika kimataifa kwenye fani zao? Nani inaangalia kwamba hatuna wafanyakazi ambao ujuzi wao ni sawa na wanaomaliza shule za kata?

Hujui sheria. Mmliki wa kwanza ni NHC. Jifanye ni wewe halafu tuone kama mmliki utatetewa kipuuzi hivi. Wengine wote ni wahusika baki.Fahamu tu kuanzia leo.Uliza pia ukiona shida kabla ya kupost.
 
Joshi, NKM stands for Nehemiah Kyando Mchechu, and in future when you see such an ID just know that it's Mchechu responding on issues or commenting! I am not a person who will hide is ID since I believe in truth and transparent! Neither do you have so many people at my level in Public Sector and non political who stands by their ID's.

Just to prove you wrong I am now at the accident scene as I am writing to you and we are not more than 70 people, and I was hear yesterday up until 01:30am! I am following through all the comments in different threads, actually I have always been a good follower of JamiiForums but I was never a contributor! I think the series of threads which most are misleading without facts have pushed me to consider responding to all these issues. However, by obviously fact I do not expect to become an active member on contributions!

For now I have opted to focus on the task at hand here at the accident scene, and I will try to respond on these few in a very brief in the coming two days either by posting a thread or by calling a press conference where you can come and ask as many questions as you want and we will respond to all of them and I hope it Will be at your satisfactory level and to others as well! There is nothing to hide here, no politics, no partisans side and no blax2! I am sure the press conference has always enough participants who are members of JamiiForums and they gone through all the posted comments and certainly they will be looking for answers by asking the same sort of questions!

Thanks and stay relaxed till then!
Mkuu tunaomba utakapojibu utujulishe ubia wenu ulikuwa ni wa gorofa ngapi? Na ilikuwa mbia akaenda mpaka gorofa 16 bila nyie kujua?

Umiliki wetu wa 25% ni wa gorofa ngapi? Nini mnachomiliki? Na mngekuta sicho, utaratibu ni upi? Mkataba wa jengo pacha unasemaje? Hilo lililosimamishwa kujengwa?
 
Mkuu with due respect wewe hoja zako ndio hazina mashiko!

1. Unadai mkataba ulifungwa 2006 na kwa kuwa Mchechu aliingia 2007 hahusiki! wot a joke! Jengo limeanguka jana 2013 kwa taarifa yako. Kibaya zaidi mkataba ulikuwa wa kujenga ghorofa 10 tu ngoma imeendelea mpaka ghorofa ya 16! under watchfull of Mchechu!

2. Eti "sasa wanatembelea Hilux!" kichekesho mkuu, kutembelea Hilux ndio justification ya kuua watu 20+?

Huu utetezi ulioleta hapa ni mwembamba sana, sidhani hata kama unafahamu dhana ya kuwajibika ilivyo. Likibuma chini ya uongozi wako ndio lako hilo, kaingia toka 2007 kwanini ali review mikataba ya kimagumashi?

Mchechu has to go....

Ndugu mleta mada naona unakurupuka sana, hoja yako labda ni nzuri lakini tatizo linalokusibu ni namna ya kuwasilisha hoja yako kwa ma-GT, vilevile nimegundua hujui mambo mengi sana kuhusu NHC wala sakata zima la tukio la kuporomoka kwa jengo.

Siku nyingine ukitaka kuleta mada hakikisha huwe full equipped, lakini hata hujui bwana Mchechu kaingia lini NHC (naona hapo umeandika heti kaingia 2007, what a shame), hujui NHC ina kesi ngapi mahakamani za kutengua mikataba ambayo ilikuwa haina manufaa kwa shirika na umma kwa ujumla, ambayo ilisainiwa na menejimenti ya kabla yake bwana Mchechu.

NHC ana ubia wa asilimia 25 tu kwenye hilo jengo, kwa maana ya kwamba wao ndio wenye kiwanja ila mwendelezaji ana miliki asilimia 75, zinamfanya yeye hawe na majority share, na katika maamuzi mwendelezaji huyu (ambae sio NHC) ana nguvu na mamlaka zaidi. Hapa unaweza kuona jukumu la kutafuta vibali na wataalamu lote analo mmiliki.

Katika kutafuta mtu wa kuwajibishwa hapa, NHC haihusiki hata kidogo, lakini mmiliki kwa kuwa amefanya negligance that had lead to death toll, yeye ndio awajibike kwa 100%, baadae wafatie hao wataalamu.
 
Tatizo la wabongo ni ushabiki na urafiki wa kubebana ktk mambo ya msingi. Hata kama NHC ana 25% share ktk jengo hili hata kama ni minority bado huwezi kuja na hoja nyepesi eti Mchechu Nehemia hausiki. Ni ajabu kweli kweli. Lingekuwa ni jambo la sifa ungekuwa wa kwanza kuropoka kwamba kwa kutetea huyo mchechu wako! Hata ukitetea namna gani NHC hawawezi kupona hapa.
 
Mkuu,

Kama una chuki binafsi na mchechu sema but hoja yako haina mashiko. Mchechu ameingia after 2007 na ameinadilisha shirika lililokuwa mbioni kufa sasa wanatembelea hilux kwenye kazi zao. Pia hoja yako haina mashiko kwasababu mkataba wa kujenga lile jengo ulifungwa mwaka 2006, sasa Nehemiah Mchechu anahusikaje? Mie namtetea labda ulete sababu zenye mashiko but hii sio mkuu.

Umejitahidi lakini kwa bahati mbaya hakwepi kuhusishwa. Mimi sijui ameingia lini lakini tuseme ameingia 2008. Kama ni hivyo ni miaka zaidi ya mitano ambapo ameshika usukani. Moja ya jukumu lake lingekuwa kupitia mikataba yote ya ubia na kuangalia "exposure" ya shirika lake. Alitakiwa ajue kuwa kama mbia atavuna mabaya na mazuri yanayotokana na joint venture hizo. Alitakiwa kuhakikisha kuwa jengo lolote linalojengwa kwa ubia na shirika lake linajengwa kwa viwango vinavyotakiwa na ubora unaostahili. Hawezi kusema kuwa yeye kama mbia hakujua kuwa ingawa jengo liliongezwa ghorofa zaidi ya zile walizokubaliana mwanzo. Ukweli ni kuwa washitiri wa mradi huu, yaani Ladha Construction na NHC ndio wawajibikaji wa kwanza. Kwa vile Msechu ndie anayeiongoza NHC kwa wakati huu basi na yeye anatakiwa awajibike. Lakini usiwe na hofu, haitatokea katika nchi yetu. Watashikwa vidagaa, itaundwa tume halafu tutasahau mpaka litakapoanguka jengo lingine.

Amandla......
 
Wakati taifa lipo katika kuombeleza janga la kuanguka kwa jengo la ghorofa kati kati ya jiji, kuna mambo kadhaa yamejitokeza kuhusiana na mkasa huu.

Shirika la Umma kama NHC kuingia ubia wa kimagumashi magumashi na wafanyabishara wababaishaji kumepelekea kupotea kwa maisha ya ndugu zetu takriban 20+. Inakuwaje uwekezaji mkubwa kama huu NHC wanaacha kila kitu kiendeshwe kienyeji enyeji tu? kibaya zaidi sasa wanaibuka na kusema wanapitia upya sera yao ubia ili washirikishwe zaidi!.

Kwa mshangao mkubwa juhudi zote za uokoaji zinazo endelea si Mchechu au kiongozi yeyote mwandamizi wa NHC alie thubutu walau kufika site kujionea hali halisi. Rais pamoja na majukumu yake mengi ameshatembelea eneo husika mara mbili.

Imefika wakati mkurugenzi mkuu wa NHC akamatwe na awajibishwe na mamlaka za uteuzi. Taifa haliwezi kuingia katika janga kubwa kama hili wakati wahusika wala hawana habari.

Mchechu has to go....
Kwani wewe haujui huu ni wakati wa sikukuu, Mchechu na management yake wako likizo wanakula sikuku
 
Mleta mada una wivu na chuki kwa nehemia mchechu,kwa mfano unavosema tangu jengo lidondoke hajafika eneo la ajali unadhihirisha uongo wa hali ya juu!kwa taarifa tu bodi ya wakurugenzi ya NHC imekuwa site hadi saa 7 usiku siku ya ajali hata jana pia.lakini pia katika partnership kati ya mwenye jengo na NHC ni kwamba shirika linatoa kiwanja tu ambacho ni 25% ya hisa na km una ujuzi kdg kuhusu hisa haitakupa tabu kugundua nani ana maamuzi makubwa katka huo ubia
 
Ndugu mleta mada naona unakurupuka sana, hoja yako labda ni nzuri lakini tatizo linalokusibu ni namna ya kuwasilisha hoja yako kwa ma-GT, vilevile nimegundua hujui mambo mengi sana kuhusu NHC wala sakata zima la tukio la kuporomoka kwa jengo.

Siku nyingine ukitaka kuleta mada hakikisha huwe full equipped, lakini hata hujui bwana Mchechu kaingia lini NHC (naona hapo umeandika heti kaingia 2007, what a shame), hujui NHC ina kesi ngapi mahakamani za kutengua mikataba ambayo ilikuwa haina manufaa kwa shirika na umma kwa ujumla, ambayo ilisainiwa na menejimenti ya kabla yake bwana Mchechu.

NHC ana ubia wa asilimia 25 tu kwenye hilo jengo, kwa maana ya kwamba wao ndio wenye kiwanja ila mwendelezaji ana miliki asilimia 75, zinamfanya yeye hawe na majority share, na katika maamuzi mwendelezaji huyu (ambae sio NHC) ana nguvu na mamlaka zaidi. Hapa unaweza kuona jukumu la kutafuta vibali na wataalamu lote analo mmiliki.

Katika kutafuta mtu wa kuwajibishwa hapa, NHC haihusiki hata kidogo, lakini mmiliki kwa kuwa amefanya negligance that had lead to death toll, yeye ndio awajibike kwa 100%, baadae wafatie hao wataalamu.

Are you serious? Walipoingia makubaliano yalikuwa ya kujenga jengo la aina gani, ukubwa gani na ghorofa ngapi? Unataka kuniambia hawakupewa hata michoro, bills of quantities, mkataba wa ujenzi n.k.? Sasa kama hawakupewa vyote hivyo wangejuwaje thamani ya hiyo asimilia 25? Au na yenyewe walingojea Ladha awaambie? Yote haya ni maswali ya kujiuliza.

Kama NHC, ambaye alikuwa na asilimia 25 ya hisa katika jengo alimuachia mwenzake afanye atakavyo basi alikuwa mzembe wa kutupwa. Kuwa na asilimia ndogo hakukuzuii kuwa na mikutano na mbia mwenzako na kuhoji utendaji wake. Hili lilifanyika? NHC ina wataalamu wa ujenzi (tusisahau kuwa ni washauri na makandarasi pia), je walikuwa wanahudhuria mikutano ya sait? Je walikuwa wanapewa ripoti ya maendeleo ya mradi? Kama walikuwa hawapewi, waliwahi kudai? Waliwahi kutuma wataalamu wao sait wakafukuzwa kwa sababu wana hisa kiduchu?

Na hili ni fundisho kwa wale wote wanaoingia ubia wa kupatiwa viji-apartment Upanga. Janga likitokea utahusishwa moja kwa moja kwa hiyo ni bora udai kushirikishwa kikamilifu katika ujenzi wa jengo lenu ama sivyo ujitoe katika ubia, chukua kiwanja chako umuachie jengo.

Amandla........
 
Sasa comment kama hii huyu jamaa hata sijui nitamwelimishaje ili aelewe maana ya uwajibikaji. Ndio wasomi wa bongo hawa. Utafikiria ni vile vipindi vyaa akina pwagu na pwaguzi
@ macho muelimishe mpaka aelewe.Tatizo n vimaneni vya kashfa mnavyoviweka.
Mara pwagu mara low thinking level, hapo mtachafua hali ya hewa.
Tuellewesheni taratibu kwa mifano rahisi bila maneno ya kashfa.Endeleeni sasa.
 
Mkuu tunaomba utakapojibu utujulishe ubia wenu ulikuwa ni wa gorofa ngapi? Na ilikuwa mbia akaenda mpaka gorofa 16 bila nyie kujua?

Umiliki wetu wa 25% ni wa gorofa ngapi? Nini mnachomiliki? Na mngekuta sicho, utaratibu ni upi? Mkataba wa jengo pacha unasemaje? Hilo lililosimamishwa kujengwa?
@ Vikwaxo take his word"in few days to come briefly he will tell the public thru media what happened.
Anaweza kujiuzulu if he will b in wrong do.
 
Back
Top Bottom