Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Kwa kuanza tuu napenda niwafahamishe kuwa namfahamu BINAFSI huyu NEHEMIA hivyo sina kinyongo wala matatizo naye if anything nilimfahamisha what to expect alipopewa taarifa ya uteuzi huu miez kadhaa iliyopita.

By definition UFISADI pamoja na kuibia serikali ..tunaweza kusema ni kurudisha maendeleo nyuma na kuwa na upendeleo wa dhahiri kwenye ajira serikalini including NHC!

Nadhani mnakumbuka takriban miezi sita iliyopita nilileta thread ya uteuzi wa DG mpya wa NHC na nikaelezea jinsi uhuni ulivyokuwa umefanywa ili kukidhi profile ya baadhi ya watu. Uhuni huu haukufanywa na mwingine bali IKULU ambako walitoa maagizo kuwa tangazo la awali la nafasi hii iliyotolewa gazetini ibadilishwe...in short tangazo la nafasi ya hii la mwanzo lilitaka mtu mwenye qualifications kem kem baadae tangazo la pili lililotoka likawa limepunzuza sifa za anayetakiwa ...bila maelezo yoyote ile.

Ukweli wa uteuzi huu wa nehemia ni kama ufuatavyo:

1.Nehemia HAKUOMBA kazi hii kama ambayo sheria ilitaka afanye

2. Nehemia hakuitwa kwenye USAILI kama ambavyo sheria ilitaka ifuatwe

3. Nehemia kapata kwa sababu ya presha na ufisadi wa hali ya juu uliyofanywa na Katibu Mkuu wa Ikulu bwana LUHANJO

4. Ambao waliomba na wakaitwa kwenye usaili hawajaandikiwa barua ni sababu zipi walikosa halafu kazi akapewa ambaye hakuomba hiyo kazi in the first place.

Sasa in the wake of haya ya kumsifia Nehemia na mengineyo tusisahau kuwa kuna uteuzi kama huu unaweza kuja kufanywa na rais na nadhani ni muhimu watu wasilalamike kuhusu FAIRNESS kama ambavyo hawalalamiki kuhusu procedures zilizotumika kumpata huyu Bwana NEHEMIA....isije ikawa Mkuki Kwa Nguruwe...

If anything hata kama Luhanjo alikuwa anamtaka kijana wake what was so difficult or worong UTARATIBU ukafuatwa?
 
mi ndio maana nikiona matangazo ya kazi magazetini ya serikali sito kaa niombe kazi...ushenzi mtupu

kama mnakumbuka nilileta mada moja kuhusu ufisadi uliotaka kufanywa kwenye nafasi ya director ambayo lilipelekwa jina la mmoja wa director anaengoza kampuni moja ya ndege ya serikali lilipofika watu wakataka atangazwe kabla ya wahuni kumfwata luhanjo na kumwambia atuonyeshe sehemu huuyu jamaa aliomba kazi kama directo,..yeye aliomba kama bod member na mwenyekiti wa bodi ikaonekana vikubwa sana kwakwe wakampirtisha kwenye udirector nashukuru nafasi ile awajatoa majibu mpaka leo kudhirisha upumbavu na unafiki wa ajira serikalini unaofanywa na luhanjo na kampuni zake

dem gov
 
Mmmmmm!!!!!!!!!!!! Maumivu ya kichwa huanza polepole!!!!!!!!!!!!!!
 
Hili limekuwa likfanyika mara nyingi si mara zote anayeteuliwa kuongoza mashirika ya umma huwa ni yule aliyeshinda katika mchakato wa usaili.Wakati mwingine huwa ni discretion ya Rais na yeye ndiye wa kuulizwa vigezo alivyotumia na si mwingine.
 
Mmh hii kali sasa, kweli we dare to talk openly.,ngoja wanahabari waikamate hii na kuishikia bango tuone kitakachoendelea.
 
Wakati mwingine head hunting hufanyika pia... for a good reason na siyo lazima ufisadi...

I have participated in recruitment processes... wakati mwingine kazi inatangazwa.. wanaoomba unakuta ni watu wa viwango vya chini mno... hata ukiwashindanisha wenyewe kwa wenyewe utaishia kupata mtu asiye stahili.In such circumstance u may be forced to resort to head hunting.

Nehemia as I know him is a material for the position.... tunaweza kulaumu na kusema mengi lakini anabakia THE CEO FOR NHC for the time being..tukubali na tumpe nafasi jamani. It could have been you or me..ila haikuwa.
 
Afadhali GT umeleta uwanja mpya wa kujadili hii issue, nimejaribu kupost kwenye thread ile ya kumpongeza naona hakuna response au ndio double standard kuna post hapa nime 'iba kule' kuna watu waliuliza lakini hawakupata majibu

wakati kikwete anateuliwa kuwa mgombea urais, mlio wengi mlidhani mmepata kijana mwenzenu kama nehemia, kumbe baadaye mkagundua kuwa nehemia kikwete alikuwa backed na bandits like rostam azizi, and lowasa sasa mnajuta, wengi hamjui historia ya nehemia, mnatumia tu uzoefu wa kuambiwa au alama zake za darasani pale udsm, hamjui kuwa kama ni mwadilifu na mpenda nchi yake kama tulivyo wengine na napenda muaminini hivyo asingeweza kufurukuta na kuteuliwa nafasi hiyo.

NHC ndo source kubwa ya pesa za uchaguzi za mwaka huu, vyanzo vingine kama ppf , nssf viko hoi kwa kuwa vinateketeza mabilioni kwa mradi wa udom wa dodoma, hivyo Jk akilamba pale tena hayo mashirika yataanguka kifo che mende, mtu pekee anayeweza kuwasaidia pale NHC wakachota hayo mapesa si mwingine bali huyo nehemia, aliweza kuwasaidia yale mapesa ya EPA yakapita pale CBA baada ya kwingine kushindikana, sasa yuko jikoni atawapakulia ya NHC. for the past ten years NHC hakuna cha maana zaidi ya kwenda kujenga nyumba za kupanga kijijini kwa kikwete pale chalinze, na chato kwa maghufuli!

Raia mwema walishatoka na data za mchakato wa kumpata CEO wa NHC na jinsi waziri usika alivyoingia kwenye kashfa.Bahati mbaya jina la mlengwa RAIA MWEMA walilitia kapuni. Ebu tujikumbushe kwa kudokoa link hapo chini.
http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1809

Asante mkuu, ndio maana nilitaka maelezo ya kujiridhisha kutoka kwa Mwikimba na Kapinga.Kumbe hii titile ni kubwa sana na kabla ya hapo ilikuwa na mizengwe mingi.

Kwa hali ilivyo Tanzania lolote laweza kutokea kwa haraka haraka napata maswali haya

1. Je huyu bosi mpya anahusika na fedha za EPA?
2. Je jina lake ndilo lililoingizwa kisiri na Chiligati baada ya ile kampuni kufanya usaili wao
3. Je kuna uhusiano wa position hii na CCM? AU how CCM may benefti from this new guy?
4. Je kuna mtu anajua lolote kama ushauri wa Enerst Young ulifuatwa?

Pamoja na Raia Mwema kugundua hii issue

5. Je kuna uhakika gani kuwa hii position imepatikana kwa merit? maana mamlaka yote anayo Chiligati.

6, Je baada ya Chiligati kukataa mapendekezo ya E&Y je kampuni gani nyingine ilifanya mchakato huu? maana hizi issue zilikuwa za november tu na sasa ni february!

maswali yanaweza kuendelea tena na tena

Haya mahojiano yana question mark nyingi pia

RAIA MWEMA: "Mheshimiwa Waziri, tueleze ni sababu gani zilikushawishi kupuuza mapendekezo ya Ernst & Young kampuni inayoheshimika, na kisha kuteua kampuni nyingine kufanya kazi hiyo iliyokwishafanywa?

CHILIGATI: "Nani kakueleza mambo hayo?

RAIA MWEMA: Tumepata taarifa za uhakika kupitia njia zetu za utendaji kazi wa kawaida.

CHILIGATI: "Sasa nenda kaandike kuwa mchakato wa kumpata mkurugenzi (wa NHC) unaendelea."

RAIA MWEMA: "Bado swali la msingi linalohusu matumizi ya fedha za wananchi pamoja na mapendekezo ya kampuni ya awali kupuuzwa na kuteuliwa kampuni mpya kwa kazi hiyo hiyo, hujajibu Mheshimiwa Waziri…naomba majibu ili wananchi waelewe kinachoendelea kwenye shirika lao la taifa."

CHILIGATI: "Nakwambia…sikiliza bwana…watu hawana shida ya kujua hayo yote, wewe nenda kaandike kwamba mchakato unaendelea na hivi karibuni na hasa mwanzoni mwa mwezi Novemba, mkurugenzi mkuu atatangazwa…nitamtangaza mkurugenzi mkuu…sawa?"

This is just questions no offence please

EPA, Kukataliwa mapendekezo ya consultant, kupenyezwa jina la siri,........

I asked those questions kama kuna mtu ajibu, ila aidha watu hawajaona, au hawataki kujibu!

WanaJF habarini za asubuhi/machana/jioni

nimesoma maoni mengi humu ila out of curiosity nina maswali kuhusu huu uteuzi

  • Wajumbe wa Bodi ya NHC kazi yao ni nini?
  • Nehemia Mchechu ana any work/academic experience kwenye mambo ya building/contruction, estate management or construction/planning project management?

He has to be real estate manager, he has to be professional in that sector, this is not minister's positions. japo nazo tunaona kabisa tunahitaji wataalamu husika wa hilo eneo. He still fit on the company but on the financial issues, au kuwa msaidizi wa director mkuu. I believe Ernst and Young walishauri hivyo

The guy may be clean, ila kawekwa pale kwa kazi maalum, we have been living in this agony for 47 years! why are we forgeting these so easily?
 
Kwenye bodi mpya ya wakurugenzi kuna mbunge, ambaye hatakiwi kabisa kuwamo kwenye hiyo bodi!
 
This is confusing. Kwenye thread ile tuliyommwagia hongera 'kijana', kama sikosei iliandikwa mahala na Maane kwamba Mchechu alishauriwa apeleke CV ya kwa ajili ya hiyo kazi na hatimaye akaipata.

Nakushukuru sana Nehemiah ulikubali maombi yaliyoletwa mezania kwako na ukakubali kupeleka CV yako!!!!

Ina maana ilienda CV peke yake bila application? Hata kama hivyo ndivyo na ameipata kazi hiyo bila kufuata utaratibu lakini anao uwezo wa kuimudu hiyo kazi what is all the fuss about? Wapo wangapi wanaoteuliwa na Rais na hawakidhi matakwa ama hawana uwezo unaotakikana?
 
Duh huwa tanzania nachokea hilo tu. Jana katika viti virefu nilikuwa naongea na mshkaji leo naona JF kuna muungwana kaposti. Kuna jamaa wa Standard Chart alikuwa ananigaia information ya ndani akanambia jamaa amepelekwa pale kimalengo na ikulu. Nasikia kuna swala la kujenga nyumba za bei nafuu. Pesa zilitolewa since december mwaka jana. Sasa kuna kamchezo mchafu kanataka kuchezwa kwani anayetakiwa kupewa hiyo project ni NHC.

Binafsi nilimuona kama ni majungu kwani nakumbuka Nehemia alikuwapo StanChart but naendelea kukusanya information ndipo niamini mwenye data zaidi atudondoshee maana kabla hatujaamini lazimia tujiridhishe kwanza
 
sina hakika: kuna mdau anasema inawezekana fedha za uchaguzi zikatokea huko, huyu bwana kuna wasiwasi alihusika na kuoitisha fedha za EPA CBA wakati kote zilikataliwa?

If this is another plan of CCM to plunder our wealth is not good!

kwa nini waliukataa mchakato wa E&Y??
 
Game Theory said:
Nadhani mnakumbuka takriban miezi sita iliyopita nilileta thread ya uteuzi wa DG mpya wa NHC na nikaelezea jinsi uhuni ulivyokuwa umefanywa ili kukidhi profile ya baadhi ya watu. Uhuni huu haukufanywa na mwingine bali IKULU ambako walitoa maagizo kuwa tangazo la awali la nafasi hii iliyotolewa gazetini ibadilishwe...in short tangazo la nafasi ya hii la mwanzo lilitaka mtu mwenye qualifications kem kem baadae tangazo la pili lililotoka likawa limepunzuza sifa za anayetakiwa ...bila maelezo yoyote ile.
Hapa sasa ndipo mtu wakawaida kabisa unapoanza kutilia shaka uwezo wa viongozi wetu wa Ngazi za juu wanavyoyatazama haya mambo, kweli inashangaza sana.

Hii Serikali ni KIZIWI, pamoja na matatizo yooote ambayo inapata lakini bado haijifunzi, mimi inanikera sana.

Kila kitu kuvunja taratibu, kila jambo kwenda nje ya taratibu tulizojiwekea....inakera
.
 
nehemiah ni kada wa chama kwa taarifa yenu. sasa mlitegemea hiyo nafasi apewe kijana wa CUF?
 
Wakati mwingine head hunting hufanyika pia... for a good reason na siyo lazima ufisadi...

I have participated in recruitment processes... wakati mwingine kazi inatangazwa.. wanaoomba unakuta ni watu wa viwango vya chini mno... hata ukiwashindanisha wenyewe kwa wenyewe utaishia kupata mtu asiye stahili.In such circumstance u may be forced to resort to head hunting.

Nehemia as I know him is a material for the position.... tunaweza kulaumu na kusema mengi lakini anabakia THE CEO FOR NHC for the time being..tukubali na tumpe nafasi jamani. It could have been you or me..ila haikuwa.

Leave this head hunting to private sectors not government sectors please!
 
sina hakika: kuna mdau anasema inawezekana fedha za uchaguzi zikatokea huko, huyu bwana kuna wasiwasi alihusika na kuoitisha fedha za EPA CBA wakati kote zilikataliwa?

If this is another plan of CCM to plunder our wealth is not good!

kwa nini waliukataa mchakato wa E&Y??

Kama Nehemia ana uwezo na amefanikiwa huko ni big up kwake

Kama uteuzi walicheza hizo rafu kwa kutumia mwanya wa uzoefu wake huko alikopita kwa ajili ya malengo la kulihujumu taifa,napinga kwa nguvu zote huo uteuzi

Huu mwaka inabidi tuwe makini sana,kimsingi hatukustahili hata kuibembeleza hii serikali iliyoingia madarakani kwa njia ya KAGODA.
 
Back
Top Bottom