Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

NKM anavuta sana uliza mmiliki wa zile appartemnt za pale OASIS mbezi beach ni nani kama hujaambiwa ni huyo huyo Mchechu?

Kaangalie zile nyumba za NHC kigamboni contractors ni kina nani? Na kama utaona sticker za CRB kwenye ule ubao wa mradi?
pale kigamboni wakandarasi wapo watatu na wamepatikana kwa taratibu zote za procurement nimetoka huko juzi nilienda katika shughuli za kutafuta maeneo. Wakandarasi wa pale ni Shibat, Pioneer na Sevacom Africa. Kuhusu hayo ya Oasis hayo ni yako.
 
Wanoatakiwa kujiuzulu ni wale wenye mkono wetu wananchi juu ya kupata kwao nafasi husika. Sio kila mtu anaweza kujiuzulu. Mtu wa kujiuzulu kama kujiuzulu ni dawa kwenye hili ni waziri wa ardhi na nyumba mijini na sio Nehemia kama mtoa uzi ulivyopendekeza. Waziri Prof. Tibaijuka ndiyo anatakiwa kuwajibika hapa. Basically mwenye macho haambiwi tazama, Nehemia has managed it.
 
Jamani, mimi nasimamia ukweli na hapa lazima tulonge ki ukweli kabisa!

Mchechu angekuwa sawa basi asingeogopa kivuli chake pale NHC, mfano kuna dada mmoja alikuwa mwajiriwa wa NHC tena katika ngazi za juu tu na lipata kufanya kazi hapa Dar na Baadaye mmoja wa mikoa ya kusini na ndiko dhahama ya Mchechu ilipompata.

Ni kwamba huyo mdada ambaye mimi namwita ni jembe alikuwa akiandika makala mbalimbali zinazomhusu DG wa NHC na aliziandika kikwelikweli kwakuwa alikuwa jikoni alikuwa anazifahamu na kwa ufupi tuazo zote kwa mlipuo wa mwisho.

Kilichotokea na kwamba Mchechu alizipata kupitia vyanzo vyake kwa maana email na kompyuta alizotumia yule dada zilikuwa hijacked na Mchechu amini usiamini alituma timu nzito ya polisi kwa kukodi helikopta kwa fedha ya NHC ili wamlete yule dada hapa Dar.

Alipofika hapa Mchechu alimwita ofisini na kumtolea bastola eti aeleze ukweli kwa nini anamfuatafuata kiasi hicho la sivyo atamlipua na bunduki, na akamlazimisha aandike barua ya kukiri ku violate kanuni za NHC na akiri na kuandika barua ya kuomba asamehewe ili uwe ushahidi wa Mchechu baadae kumfukuza kazi.

Yule dada kwakuwa hakuwahi kuonyweshwa bunduki alitii yote aliyoambiwa na Mchechu na kafanya kama alivyoelekezwa, walikuwa wawili tu kipindi hicho pale ofisini kwake na alikuwa akitamba kuwa yeye katumwa kazi na ikulu na yeye dada anataka kumwaribia na baadae Mchechu akawaita timu yake inayo shughulika na nidhamu kwa wafanya kazi na kuanza process za kmwajibisha dada wa watu na hadi leo wamemtupa nje na bado anahangaika katika vyombo vya sheria kueleza ukweli na apate haki yake.

Nauliza hivi huyu Mchechu angekuwa mtu safi ni kwanini atumie nguvu kupita kiasi kulinda maslahi yake kufikia kutishia wasema ukweli kwa bunduki?

Je, yule dada leo aki uawa akafa je Mchechu atajiweka katika staili ipi?

Je, na yeye awekwe katika orodha ya watekaji nyara na kutishia masha ya wasema kweli hapa nchini?

NKM hayupo sawa na mnao mtetea hamjui wala kutambua undani wake:shut-mouth:
 
Wanoatakiwa kujiuzulu ni wale wenye mkono wetu wananchi juu ya kupata kwao nafasi husika. Sio kila mtu anaweza kujiuzulu. Mtu wa kujiuzulu kama kujiuzulu ni dawa kwenye hili ni waziri wa ardhi na nyumba mijini na sio Nehemia kama mtoa uzi ulivyopendekeza. Waziri Prof. Tibaijuka ndiyo anatakiwa kuwajibika hapa. Basically mwenye macho haambiwi tazama, Nehemia has managed it.

Nehemiah Mchechu has to go.
 
Wakati taifa lipo katika kuombeleza janga la kuanguka kwa jengo la ghorofa kati kati ya jiji, kuna mambo kadhaa yamejitokeza kuhusiana na mkasa huu.

Shirika la Umma kama NHC kuingia ubia wa kimagumashi magumashi na wafanyabishara wababaishaji kumepelekea kupotea kwa maisha ya ndugu zetu takriban 20+. Inakuwaje uwekezaji mkubwa kama huu NHC wanaacha kila kitu kiendeshwe kienyeji enyeji tu? kibaya zaidi sasa wanaibuka na kusema wanapitia upya sera yao ubia ili washirikishwe zaidi!.

Kwa mshangao mkubwa juhudi zote za uokoaji zinazo endelea si Mchechu au kiongozi yeyote mwandamizi wa NHC alie thubutu walau kufika site kujionea hali halisi. Rais pamoja na majukumu yake mengi ameshatembelea eneo husika mara mbili.

Imefika wakati mkurugenzi mkuu wa NHC akamatwe na awajibishwe na mamlaka za uteuzi. Taifa haliwezi kuingia katika janga kubwa kama hili wakati wahusika wala hawana habari.

Mchechu has to go....

==========
Majibu ya Nehemiah Kyando Mchechu:
Rafiki yangu Joshi bado una hasira zile zile za wakati ule ndugu yangu, let's be fair kaka mambo yale ya kodi kaka yamepita. Nakumbuka ni wewe na wenzako mliopinga saana uteuzi wa huyu bwana, sasa naona mnachekea chooni baada ya hili ghoroffa kuanguka mwatafuta kila sababu ili mpate pa kutokea. Mbane yule Mmiliki Razahussein uhuni kaufanya yeye. Vinginevyo kumwandama mchechu ni kazi bure. Nawasilisha mkuu kanji.
 
...defence kama hizi ndizo zitakazo mfanya Mchechu aonekane liable....I'm afraid.......Mdondoaji...siamini haya maandishi yanatoka kwako!.........

Ogah,

Mkuu kama unakumbuka Jamiiforum ya zamani niliandika I am against unfairness. I neither want to see someone accuse another person nor want to accuse someone based on baseless attacks. However, there is something which made me a bit wary about the NHC module operandi especially the 75%-25% deal that they entered with the investor in the construction of a building. Just read this story here courtesy of Tanzania Daima:-

NHC yatoa msimamo jengo lililoporomoka


na Mwandishi wetu

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limefafanua kuwa jengo linalojengwa kwenye kiwanja namba 2032/73 Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam lilianguka jana kutokana na sababu ambazo bado hazijathibitishwa kitaalamu na mamlaka husika.

Taarifa ya shirika hilo kwa vyombo vya habari jana jioni ilisema kuwa limesikitishwa na tukio hilo la kuanguka kwa jengo pamoja na maafa yaliyotokana na tukio hilo la kusikitisha.

Pia shirika lilitoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba uliotokana na ajali hiyo.

"Mradi huu wa ubia kati ya NHC na M/s Ladha Construction Limited ya jijini Dar es Salaam ulianza kutekelezwa Februari 4, 2008 ambapo Shirika la Nyumba litakuwa na hisa asilimia 25 na mbia ana asilimia 75 mara baada ya mradi kukamilika," alisema.

Kwa mujibu wa sera ya ubia iliyoanza kutumika mwaka 1993 na kuhuishwa mwaka 1995 na 2005, Shirika la Nyumba la Taifa lilikuwa likitoa ardhi ambayo ilikuwa ikihesabika kama asilimia 25 ya mtaji wake kwenye jengo husika na mbia alikuwa akipata asilimia 75.

Kwa mujibu wa mkataba huo, mbia mwendelezaji M/s Ladha Construction Limited kama walivyo wabia wengine, anapaswa kabla ya kuanza ujenzi kupata vibali kutoka kwenye mamlaka husika na kuwa na wataalamu wa ujenzi na washauri waliokubalika na kuthibitishwa na mamlaka husika.

Aidha, mbia huyu akishapata wataalamu hao ndiye anayehusika kuingia nao mikataba ya kazi ya kujenga na kusimamia ubora wa jengo husika kwa mujibu wa sheria.

"Katika mradi huu mbia mwendelezaji aliajiri wataalamu wote waliosajiliwa na mamlaka husika ambazo ni CRB, ERB, AQRB na mansipaa husika na mamlaka nyinginezo," ilisema taarifa hiyo.

Kwamba kwa kuwa ujenzi ulikuwa bado haujakamilika, shirika lilikuwa bado halijapata asilimia 25 ya umiliki wake.

"Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Shirika la Nyumba la Taifa lilisimamisha utoaji wa miradi mipya ya ubia mwaka 2010 ili kuweza kutathimini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa miradi ya ubia na hivyo kuwezesha kutengeneza sera mpya," ilisema taarifa hiyo.

Katika sera mpya ambayo utekelezaji wake utaanza hivi karibuni shirika litahusika moja kwa moja katika kuteua mjenzi mtaalamu (contractor), msimamizi mtaalamu wa mradi husika (consultant) na kusimamia kikamilifu shughuli zote za ujenzi.

Jengo hilo la ghorofa 16 lililokuwa likiendelea kujengwa liliporomoka jana asubuhi na kusababisha vifo vya watu watano na wengine 15 kujeruhiwa.

==================

Maswali ya Kujuiliza sana ni kama ifuatavyo:-

a. Hapo kwenye nyekundu wamefikia katika hesabu zipi hadi ikahesabika mchango wa NHC katika hiyo project ni just 25% mwekezaji ni 75%. Nitatoa mfano bei ya ardhi ya kariakoo sasa unaweza kukuta inafika hata 500,000 per square meter. Hivyo eneo la square meter 2,000 linauzwa hadi Tshs Billioni 1. Sasa kama bei ya ardhi kariakoo ni billioni 1 na bei ya ardhi pugu ni milioni 5 per square meter 2000 huo mchango wa 75-25 vp uwe sawa???

b. Mbona katika maelezo ya NHC hawatuambii huyo muwekezaji anakaa muda gani akivuta hiyo 75-25. Kama ni indefinite life au 99 years au 30 years. If it exceeds more than 20 years then huo mkataba ni wa kinyonyaji kwasababu Jengo mfano wa Viva Towers pale Serena Hotel limegharimu sio zaidi ya bilioni 30. Sasa kama kila flat wakipangisha $2000 per month jengo zima hawakosi $100,000 per month from rental fees. Kama wanatapangisha for a year ni kama $1.2 million for 10 years ni sawa $12 million ambapo ni sawa Billion 19.2 after 20 years ni sawa na Billion 38.4. Sasa utaona mwekezaji atakuwa kesharudisha hela yake in 20 years or less kwani rent mjini sasa hivi inafika $4,000.

Ikiwa mkataba ni wa kudumu utaona huo mkataba ni kinyonyaji maana anawekeza halafu anavuna faida ya mara 400 zaidi ya gharama alizojengea na kwangu mie huo ni ufisadi wa hali ya juu.

Mkuu mie nipo makini ila sipendi mtu aonewe kwa sababu zisizo na msingi. Mchechu ametuambia ataitisha press conference I am anxious to hear what he is going to report during that press conference.
 
Mkuu,

Kama una chuki binafsi na mchechu sema but hoja yako haina mashiko. Mchechu ameingia after 2007 na ameinadilisha shirika lililokuwa mbioni kufa sasa wanatembelea hilux kwenye kazi zao. Pia hoja yako haina mashiko kwasababu mkataba wa kujenga lile jengo ulifungwa mwaka 2006, sasa Nehemiah Mchechu anahusikaje? Mie namtetea labda ulete sababu zenye mashiko but hii sio mkuu.

Point of correction mkataba wa NHC na Ladha ulikubaliwa February 4, 2008 na Mchechu ameingia NHC 2010 . Just noted it while reading this article of Tanzania Daima
 
Joshi Kanji, Ogah na Mdondoaji:

1. Kumbukeni scandal ya kesi ya Radar ilifumuka wakati wa Kikwete wakati mambo yote yalifanyika wakati wa Mkapa. Nehemia vile vile amerithi huu mkataba.

2. Nehemia hanunuliki ndio maana yeye mwenyewe anasema haja saini mkataba wowote wa ubia tangu aingie.

3. Nehemia hanunuliki kwa hiyo maadui ni wengi na huu ndio wakati muafaka wa hao maadui kutumia fursa hii kumtoa Nehemia kwenye hiyo nafasi ile weweze kula kama zamani.

4. Nehema apewe uhuru wa kufanya maamuzi zaidi bila kuingiliwa au kupewa pressure yoyote na atumie fursa hii kusafisha uozo wowote uliobakia NHC, alete vijana safi watakao msaidia kufuatilia miradi itekelezwe kwa umakini.

5. Tuweke siasa pembeni, the fact is, Nehemia ameweza kuleta maendeleo makubwa NHC sababu hanunuliki na anataka kuwa mfano wa taasis za serikali kiutendaji.

6. Huyo Ladha aseme alihusika na nani kufanya ubidhilifu wake, au alipataje pataje hiyo fursa kupitia kwa aliyekuwa NHC DG wakati wa mkataba.

Are you joking? Sisi tunazungumzia vifo vya watu zaidi ya 30 wewe unatuletea mambo gani hapa. Pamoja na uchapa kazi wake na kutonunuluka kwake ilikuwaje jengo litoke ghorofa 10 mpaka 16 bila yeye (mchapakazi asiyenunulika) kuwa na taarifa? Kuna mwenzako kwenye post iliyotangulia( Mdondoaji )anahaha kupita kiasi kuonyesha mkataba ulisainiwa na mtu mwingine lakini kila anavyofurukuta ndivyo anazidi kumpaka huyu mtu wake kinyesi
 
Are you joking? Sisi tunazungumzia vifo vya watu zaidi ya 30 wewe unatuletea mambo gani hapa. Pamoja na uchapa kazi wake na kutonunuluka kwake ilikuwaje jengo litoke ghorofa 10 mpaka 16 bila yeye (mchapakazi asiyenunulika) kuwa na taarifa? Kuna mwenzako kwenye post iliyotangulia( Mdondoaji )anahaha kupita kiasi kuonyesha mkataba ulisainiwa na mtu mwingine lakini kila anavyofurukuta ndivyo anazidi kumpaka huyu mtu wake kinyesi

Macho mbadiliko hebu nisome vizuri mkuu,

Mie sina upande wowote ila najaribu kuonyesha tusimuonee Mchechu kwa kulalama aondoke bila ya kuwa sababu za msingi za kwanini aondolewe na wala tusimchukulie yeye ni malaika hana makosa. Nimeainisha mfano tu hiyo 75-25 ratio ina walakini kama haijatolewa ufafanuzi kwasababu zifuatazo:-
a. Bei za ardhi zinatofautiana na hivyo basi kwenye ardhi nyengine unaweza kuta muwekezaji akatoa hela chache kuliko mtoaji ardhi sasa iweje wagawane 75-25????

b. Muda wa mkataba. Muda wa mkataba ukiwa mrefu ni ufisadi kwani mwekezaji mara nyingi baada ya miaka 20 anakuwa asharudisha hela yake. Sasa akizidi kuendelea kukaa anachokifanya ni ufisadi na unyonyaji ni muhimu Mchechu atueleze kunaendelea kitu gani hapa.

Naomba unielewe mie sina interest na mtu napenda tu kudondoa mambo ya muhimu kuleta usawa na haki.

Nilikuwapo!
 
Joshi, NKM stands for Nehemiah Kyando Mchechu, and in future when you see such an ID just know that it's Mchechu responding on issues or commenting! I am not a person who will hide is ID since I believe in truth and transparent! Neither do you have so many people at my level in Public Sector and non political who stands by their ID's.

Just to prove you wrong I am now at the accident scene as I am writing to you and we are not more than 70 people, and I was hear yesterday up until 01:30am! I am following through all the comments in different threads, actually I have always been a good follower of JamiiForums but I was never a contributor! I think the series of threads which most are misleading without facts have pushed me to consider responding to all these issues. However, by obviously fact I do not expect to become an active member on contributions!

For now I have opted to focus on the task at hand here at the accident scene, and I will try to respond on these few in a very brief in the coming two days either by posting a thread or by calling a press conference where you can come and ask as many questions as you want and we will respond to all of them and I hope it Will be at your satisfactory level and to others as well! There is nothing to hide here, no politics, no partisans side and no blax2! I am sure the press conference has always enough participants who are members of JamiiForums and they gone through all the posted comments and certainly they will be looking for answers by asking the same sort of questions!

Thanks and stay relaxed till then!

Ila mkurugenzi sio jambo jema kuwa eneo hilo ukiwa umelewa kwa sababu unaweza kutoa uamuzi wenye madhara kwa sababu ya pombe.
Nasema hivi kwa sababu kama wewe ni mswahili mwenzetu, confidence ya kuporomosha umombo, huku ukijua kabisa kiingereza chako ni kibovu kama cha kwangu lazima itakuwa imechangiwa na the power of kiroba...
Huwa tunavisikia sana hivi viingereza baa...

How in the world did I miss this gem? Shukrani kwa kui out hii mkuu Tuko.

Huyu jamaa anayesifiwa sana ndo airhead hivi ashindwe hata kujua kwamba Kiingereza hajui na aachane nacho asijiaibishe?

Au ni wapinzani wake tu wanamuumbua? Hivi kweli tumeshindwa kuweka watu ambao wanaweza angalau mawasiliano?

Sasa mtu anayeshindwa ku post JF post iliyonyooka anaweza kusimamia mighorofa yote hii iende straight?
 
Mkuu,

Kama una chuki binafsi na mchechu sema but hoja yako haina mashiko. Mchechu ameingia after 2007 na ameinadilisha shirika lililokuwa mbioni kufa sasa wanatembelea hilux kwenye kazi zao. Pia hoja yako haina mashiko kwasababu mkataba wa kujenga lile jengo ulifungwa mwaka 2006, sasa Nehemiah Mchechu anahusikaje? Mie namtetea labda ulete sababu zenye mashiko but hii sio mkuu.
Mdondoaji wewe sasa ni kama unatatea ndugu yangu vitu ambavyo havina msingi....sijui huyu Mchecu ni ndugu yako ama la!!! haiwezekani mkataba uingiwe na mtu fulani katika kipindi ambacho Mchechu hayupo, then Mchechu aingie madarakanani, (kwa miaka saba sasa) usipitie mikataba iliyoingiwa kabla yake...TENA MIKATABA AMBAYO UTEKELEZAJI WAKE HAUJAKAMILIKA...Simtuhumu Mchechu ila unatatea mambo yasiyo na msingi. Kiongozi bora kwa level yake anatakiwa angekuwa anajua kinachoendelea, na istoshe kipindi anaingia, mradi huu ulikuwa haujaanza kutekelezwa (ingawa sina uhakika, ila kulingana na hali ya jengo lilipokuwa limefikia).

Mkataba unasemekana ni wa ghorofa 14 (nirekebishwe kama nimekosea) lakini ngoma imeenda mpaka 16, bado unasema mbia (Mchechu) hawajaibiki??? Acha hizi kaka/dada
 
Last edited by a moderator:
Mdondoaji wewe sasa ni kama unatatea ndugu yangu vitu ambavyo havina msingi....sijui huyu Mchecu ni ndugu yako ama la!!! haiwezekani mkataba uingiwe na mtu fulani katika kipindi ambacho Mchechu hayupo, then Mchechu aingie madarakanani, (kwa miaka saba sasa) usipitie mikataba iliyoingiwa kabla yake...TENA MIKATABA AMBAYO UTEKELEZAJI WAKE HAUJAKAMILIKA...Simtuhumu Mchechu ila unatatea mambo yasiyo na msingi. Kiongozi bora kwa level yake anatakiwa angekuwa anajua kinachoendelea, na istoshe kipindi anaingia, mradi huu ulikuwa haujaanza kutekelezwa (ingawa sina uhakika, ila kulingana na hali ya jengo lilipokuwa limefikia).

Mkataba unasemekana ni wa ghorofa 14 (nirekebishwe kama nimekosea) lakini ngoma imeenda mpaka 16, bado unasema mbia (Mchechu) hawajaibiki??? Acha hizi kaka/dada

@ Kiherehere
Wewe ni jembe ktk uchambuzi wa hili swala na ni mtu unayesimama katikati kujadili maswala yanayolihusu taifa letu. Watu kama Mdondoaji ni aina ya watu wanaopandikizwa na watu au viongozi wanaotuhumiwa jambo fulani ktk sehemu zao za kazi ili wawatetee. Huu ni mtindo mpya wa ufisadi ktk nchi yetu. Kwa taarifa yako @ Kiherehere jengo lilikuwa lijengwe ghorofa 10 wao wakazidisha 60% ya kibali cha mwanzo yaani waliongeza floor 6 zaidi tena chini ya kiwango. Haya ni wauaji kabisa walitakiwa wafunguliwe kesi ya mauaji. Unapojenga jengo lefu namna hile tena chini wa viwango unategemea nini baada muda fulani? Just imagine lingekuwa tayari lina wapangaji kama banks, ofisi za kawaida ambako kuna idadi kubwa ya watu ingekuwaje @ Kiherehere? NKM lazima awajibike tu. He has got his share in this terrible sagga. Tafakari.
 
Last edited by a moderator:
Macho mbadiliko hebu nisome vizuri mkuu,

Mie sina upande wowote ila najaribu kuonyesha tusimuonee Mchechu kwa kulalama aondoke bila ya kuwa sababu za msingi za kwanini aondolewe na wala tusimchukulie yeye ni malaika hana makosa. Nimeainisha mfano tu hiyo 75-25 ratio ina walakini kama haijatolewa ufafanuzi kwasababu zifuatazo:-
a. Bei za ardhi zinatofautiana na hivyo basi kwenye ardhi nyengine unaweza kuta muwekezaji akatoa hela chache kuliko mtoaji ardhi sasa iweje wagawane 75-25????

b. Muda wa mkataba. Muda wa mkataba ukiwa mrefu ni ufisadi kwani mwekezaji mara nyingi baada ya miaka 20 anakuwa asharudisha hela yake. Sasa akizidi kuendelea kukaa anachokifanya ni ufisadi na unyonyaji ni muhimu Mchechu atueleze kunaendelea kitu gani hapa.

Naomba unielewe mie sina interest na mtu napenda tu kudondoa mambo ya muhimu kuleta usawa na haki.

Nilikuwapo!
Kaka mdondoaji nami nakubali pia kwamba mikataba hii haikutenda haki si kwa Shirika tu bali hata kwa Taifa, sababu ikumbukwe pia kwamba nyumba hizi Shirika hilo lilikabidhiwa na Serikali baada ya aidha kuzitaifisha na au kujenga wenyewe Shirika la Nyumba, ardhi ya CBD ina bei mbaya saana na ilitakiwa kiuhalisia hilo Shirika kwa niaba ya serikali limiliki asilimia 50-50 right from the begining. halafu baadaye baada ya miaka kadhaa wabia wangeweza kuzungumza modalities za kununua hisa kwa bei ya soko.
Kwa nilivyofuatilia miye na ninavyofahamu hisa hizi asilimia 25 zingedumu miaka mitano na baada ya kufika miaka mitano Shirika lingeweza kununua hisa zingine asilimia 25 kwa bei ya soko, suala ambalo ni unyonyaji mwingine, nadhani ndiyo maana kama wanavyosema mikataba hiyo wanaipitia, tunachoombea tu mikataba hiyo iwe na faida kwetu na ninaamimi itakuwa hivyo. Nawasilisha
 
Ndugu yangu Mchechu aka NKM,

Shukran kwa majibu yako ijapokuwa hayajakata kiu yangu.

Nitakujibu maswali yako kama ulivyoomba, lakini kama hautaridhika basi nakukaribisha NHC kuonana na mtu yeyote na kila mwana NHC ataweza kukujibu kwa ufasaha! Kwa baadhi yetu tunapata tabu sana kumjibu mtu usiyemjua na kuendelea kubishana, and therefore remaining silence is our best option!

Nashukuru kwa mwaliko wako wa kutembelea ofisi zenu lakini napata taabu kidogo kuelewa unaposema kama sijaridhika wanikaribisha "kuonana na mtu yeyote na kila mwana NHC ataweza kunijibu kwa ufasaha!" sidhani kama ni sahihi mimi kuja hapo na kumkuta dereva, mesenja, au mpika chai na kuanza kumuuliza iweje mkataba wa kujenga ghorofa kumi uwe wa kujenga ghorofa 16. Naomba unielekeze wahusika/wasemaji wa kuwaona ili wajibu maswali yangu.

Kuhusu 'kubishana' na mtu usiemjua, kwanza hatubishani tuna elimishana kwa mustakabal mwema wa shirika na nchi kwa ujumla. Pili usikhofu hapa JF kanuni zetu zipo wazi wengi ni anonymous wengine wapo kwa majina yao halisi kama wewe.





NHC wana mikataba ya aina tofauti ambayo imekuwa ikiboreshwa kila inapobidi. Uboreshaji wa mikataba unakuwa kwaajili ya mikataba mipya na hiigusi mikataba ya zamani automatically, mpaka kunapokuwa na specific negotiations kama inavyoendelea kwasasa kwa baadhi ya mikataba. Mpaka sasa kuna version nne za mikataba inayoendelea ambayo iilisainiwa katika vipindi tofauti, na kwa kutambua hilo, ndio maana SERIKALI walitoa maagizo mwaka 2010 wakati waikizindua Bodi mpya na Menejimenti mpya ya kuwa NHC wasitishe kutoa mikataba mipya ili waipitie upya sera yao ya ubia.
Katika mikataba hiyo, kuna mojawapo ambayo NHC wanapata asilimia 25% mara mradi ukukamilika na asilimia nyingine 25% baada ya miaka kumi na mbili na kufanya kuwa asilimia 50% kila upande! Katika hii ya mwanzo NHC walikuwa wanamwachia muwekezaji wajibu wote wa kutafuta wataalamu waliosajiliwa na pia wajibu wa kupata vibali vyote, pamoja na kutafuta pesa ya ujenzi na kusimamia mradi mpaka ukamilike. Mkataba wa Ladha ni mmoja wapo wa mikataba hiyo.

Kuna maboresho yaliyofanyika baadae kuanzia mwishoni mwa mwaka 2007 ambapo NHC walichukua jukumu la kushiriki katika hatua za kuchagua wataalamu, pamoja na kusimamia miradi na hii ni katika miradi mingine inayoendelea kwa sasa.

Wajibu wa kupata kibali ulikuwa ni kwa mbia mwendelezaji kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa 04/02/2007. Na hata kama kuna ongezeko la mahitaji ilikuwa ni wajibu wa mwekezaji.

Mkuu hapa umejichanganya sana. (msisitizo kwenye blue) Unadai mmekuwa na mikataba tofauti na imekuwa ikiboreshwa kila inapobidi. Halafu unadai maboresho hayo ni kwa mikataba mipya tu lakini mwishoni mwa post yako umesema kwa uhakika kabisa hujawahi kusaini mkataba mpya hata mmoja!. Swali je hayo maboresho ya mikataba mipya ni yepi wakati kimsingi hakuna mkataba mpya?

Jingine linalotisha zaidi ni unadai kama kutakuwa na ongezeko la mahitaji ( kwa maana kuongeza ghorofa) ni wajibu wa mwekezaji!. Kwa kifupi mnampa blank cheque afanye atakavyo kama mkataba wa kujenga ghorofa 5 hata zikifika 50 haliwahusu!

Swali kama baada ya kusaini mkataba yanayofuata hayawahusu iweje leo mnshinda site uongozi wote, mmechukua jukumu la kugharamia mazishi na matibabu ya waathirika? si mngemuachia Ladha agharamie nyie hisa zenu ni 25%



Hisa za 25% ni katika makubaliano yaliyoko kwenye mkataba na kama kuna ongezeko
automatically inaongezeka lakini hii inafanyika mara mradi unapokwisha. Hakuna flat inayoweza kufichwa kwahiyo NHC lazima wapate haki yao inayoonekana.


Duh! hii hatari Kaka! hiyo automatically ni clause ya kwenye mkataba au assumption tu? kama ni clause ina maana the reverse is true. Kama mkataba kujenga ghorofa 20 anaweza kujenga 2 tu! kwa kuwa kuna clause inaitwa automatically inaji adjust!

Rejea number 1 hapo juu, mwenye wajibu wa kuomba vibali kutoka mamlaka husika ni mbia mwendelezaji. Na lazima tujifunze kuheshimu mikataba na kama haufai kabisa unajadili na mbia mwenzako kwa ajili ya marekebisho au unajifunza kutokana na makosa na kutenegenza mikataba mizuri kwa siku za usoni. Kwa kukubali kuchukua wajibu Fulani unakuwa responsible katika hilo! Na kama umesaini kuendesha mradi kamili ni lazima uheshimu sheria za nchi na pia kutimiza wajibu wako wa kimkataba.

Hapo kwenye blue, huo ni mkanganyiko na sintofahamu ya hali ya juu kutoka kwenye majibu yako (flip flopping). Mwanzo umedai mkataba ya zamani haibadilishwi, baadae inaweza kuboreshwa na unaweza kujadili na mbia mwezako kwa ajili ya marekebisho, now which is which? Je huu ulio tuulia watu 30+ kwanini msiujadili na kuurekebisha?

Genge si lugha ya kistaarabu, lakini nitakujibu hilo unaloliita genge hawajawahi kusaini mkataba wowote wa ubia, na serikali ililiagiza hilo genge kuipitia upya sera ya ubia iliiweze kukidhi mahitaji ya sasa kwa kuyafanyia kazi makosa yaliyokuwepo katika sera ya mwanzo bila kupoteza yale yaliyo mazuri.

BUT PUT SIMPLE, NKM HAS NEVER SIGNED ANY JV CONTRACT SO FAR. Lakini hiyo haifanyi sera ya ubia kuwa ni mbaya na kwamba hatutarejea kwenye sera hii, kimsingi tumeishafanyia marekebisho makubwa sana na kwasasa ina mazao (Products) matatu kwa kufuata sera ya PPP ambayo kwasasa ipo. Na the growing upcoming middle class wananafasi kwasasa kuchangamkia nafasi hizi za uwekezaji ambazo uwazi wake umeongezeka kwa kiwango kikubwa.


Naomba radhi kwa ku kengeuka hapo, niruhusu nibadilishe neno "genge" na kuweka timu ya wataalam wako.

tukirudi kwenye mada hapa unatu hakikishia hujawahi kusaini mkataba mpya, hii inapingana na maelezo ya juu kabla.


Kiuchumi, huwezi ukawa na kiwanja cha bilioni tano na ndani yake ukawa una nyumba ya thamani ya milioni mia, na sehemu inayoweza kuwa na watanzania mia ukawa na familia mbili. Kwanini utake watanzania wengine wateseke kusafiri kutoka Kimara na Tegeta kwa masaa manne kila siku iendayo kwa Mungu wakati wangeweze kwenda ofisini kwa dakika kumi kutoka Upanga na maeneo ya karibu ya jiji kama wewe ufanyavyo. Kwanini unapenda kufikiri kuwa watanzania wote hawaujui uchumi rahisi huo?! Huoni ya kuwa hii itasaidia kupunguza hata foleni kama baadhi ya wakazi wetu watahamia mjini kati kutoka pembezoni mwa Dar!


Sipingi sera yenu ya uwekezaji kwa ujumla wake. Taizo langu lipo kwenye mikataba ya ujanja ujanja na ulaghai inayo hatarisha maisha ya watu na pato la shirika kw ujumla, naomba nieleweke hivyo.

Rejea namba moja na namba tano, inawezekana ni kwasasababu ya huo usomi na kuwa na jopo zuri la wataalamu wa real Estate hapo NHC ndo maana hakuna mkataba uliosainiwa tokea mwaka 2010 na hii inamaanisha kuwa wameniongoza vizuri. Lakini hii haimanishi ya kuwa Ubia ni kitu kibaya lahasha! Ubia unafanyika Dunia kote na kitu cha muhimu ni kuwa na mikataba yenye tija!

Hapo kwenye blue ndio msisitizo wangu ulipo.


Na ndiyo maana marekebisho kwenye sera ya ubia yamefanyika, angalia kwenye website utaona baadhi ya Products, na pia Road show zimeshafanyika, na kama unafikiri kuna haja ya maboresho kwenye Products hizo, tafadhali tunaomba utupe maoni yako moja kwa moja kwenye website yetu, kwenye email yangu, au karibu NHC tuweze kukusikia mawazo yako mazuri na tuweze kuboresha products zetu kwa manufaa ya nchi na wananchi.

Hilo nitalifanya
 
rudini nyuma mtusome wengine tulisema nini wakati ule wa uteuzi wake. Mimi ni miongoni mwa watu ambao ninaamini nhc ilipaswa ivunjwe na kurudishwa katika kazi yake ya kwanza kabisa siyo sasa hivi walivyoligeuza kuwa ni shirika la kibiashara.
sikutegemea mtu kama wewe ungetoa comment hii...kipindi shirika halipo kibiashara ni watanzania wangapi walikuwa wanafaidi hizo huduma za shirika? Na ni watu maskini ama?
 
sikutegemea mtu kama wewe ungetoa comment hii...kipindi shirika halipo kibiashara ni watanzania wangapi walikuwa wanafaidi hizo huduma za shirika? Na ni watu maskini ama?

Mbebs unafanya nini huku?
 
........Jingine linalotisha zaidi ni unadai kama kutakuwa na ongezeko la mahitaji ( kwa maana kuongeza ghorofa) ni wajibu wa mwekezaji!. Kwa kifupi mnampa blank cheque afanye atakavyo kama mkataba wa kujenga ghorofa 5 hata zikifika 50 haliwahusu!.........
......hii ndio moja ya concern niliyonayo Mkuu.....wewe umeiweka vizuri........
........Duh! hii hatari Kaka! hiyo automatically ni clause ya kwenye mkataba au assumption tu? kama ni clause ina maana the reverse is true. Kama mkataba kujenga ghorofa 20 anaweza kujenga 2 tu! kwa kuwa kuna clause inaitwa automatically inaji adjust!......
......hahaha...kuna sehemu alisema "Uchumi rahisi".....pengine hiyo new principle ina-apply hapo......yaani jamaa anasema mwekezaji akijenga zaidi kitu kitaonekana na wao NHC watapata haki yao accordingly.........yaani kwa kauli hii tu......nikawa na maswali mengi zaidi juu ya Mchechu na malengo yake binafsi Vs Wananchi.......
 
......hii ndio moja ya concern niliyonayo Mkuu.....wewe umeiweka vizuri........ ......hahaha...kuna sehemu alisema "Uchumi rahisi".....pengine hiyo new principle ina-apply hapo......yaani jamaa anasema mwekezaji akijenga zaidi kitu kitaonekana na wao NHC watapata haki yao accordingly.........yaani kwa kauli hii tu......nikawa na maswali mengi zaidi juu ya Mchechu na malengo yake binafsi Vs Wananchi.......
NYIE MNA chuki na huyo mkurugenzi wa nhc .....shida mnaiona kwake tu?.....
 
Back
Top Bottom