Utani wa Rais Samia na Ruto kuhusu lugha ya Kiswahili na Kingereza

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Wakiwa kwenye Mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), Rais Samia wa Tanzania na Rais William Ruto wa Kenya walitaniana kuhusu Matumizi Sahihi ya Lugha za Kiswahili na Kingereza

Swali la Utani: Kati ya Kenya na Tanzania, wapi Kingereza kinazungumzwa kwa ufasaha?

Sa mbona jibu unalo mkuu. Ngel ya kenya iko juu kwa ufasaha. Sie tunapuyanga si kiswahili chenyewe wala hicho kikristu
 
Sisi hatukukipa kiingereza kipaumbele kama lugha ya taifa. Kiswahili kilikuzwa na kufanywa lugha ya taifa ikiunganisha makabila yote. Kama kiingereza kingefanywa lugha ya taifa kama kenya tungekuwa tunaongea kwa ufasaha tu. Mpaka vijijini watu wangekuwa wanaongea kiingereza kama kiswahili kilivyochukua nafasi kubwa kiasi cha lugha za makabila kusahaulika
 
Nyerere Kiingereza chake kizuri. Aliiva alipokuwa Tabora au Makerere au Edinburg?
 
Nilikaa Kenya miezi 3 Nairobi Cty maenei ya Gymkhana sikuwahi kuona watu wakizungumza kiingereza mtaani.kinachowasaidia Kenya tokea chekecheka watoto wanasoma kwa English
 
Sisi hatukukipa kiingereza kipaumbele kama lugha ya taifa. Kiswahili kilikuzwa na kufanywa lugha ya taifa ikiunganisha makabila yote. Kama kiingereza kingefanywa lugha ya taifa kama kenya tungekuwa tunaongea kwa ufasaha tu. Mpaka vijijini watu wangekuwa wanaongea kiingereza kama kiswahili kilivyochukua nafasi kubwa kiasi cha lugha za makabila kusahaulika
Kwani lini Kingereza kilifutwa kutumika Tanzania?
 
Hizi ni hulka za ubaguzi tu zinatusumbua!
Kwa uzoefu wangu Kiswahili kinazungumzwa ukanda wote wa East Africa. Ukiwa Nairobi au Busia kwa mfano; Kiswahili kinatumika sana! Si askari, si kwenye matatu, si boda boda, si vendors, makanisani, misikitini, n.k! Kiswahili kinazungumzwa hasa! Na lahaja zinafuraisha kama midundo ya mzuki mzuri.
Lugha yoyote ile ikizungumzwa na watu wa jamii tofauti tofauti waliotenganishwa na mipaka ya asili lazima matamshi na lahaja ziwe tofauti! Mfano: Kiingereza cha mmarekani, mkanada, muingereza, muaustria, mfaransa, mdachi, mwarabu n.k ni tofauti! Muhimu ni kuwa watu wanawasiliana na deals zinakamilika!
Sasa tunapoteza muda kuanza kujadili wapi wapo vizuri wapi hawako vizuri! waTanzania tunajinasibu kuwa tunakiongea Kiswahili kwa ufasaha sana Lakini walioshikilia fursa za kukifundisha na kukiendeleza kwenye vyuo nje ya nchi ni waKenya.

Tutafute vinavotuunganisha!
 
Kiswahili chenyewe kuna watu wansema kaRamu badala ya kaLamu au Linda sehemu ya Rinda, tafrani tupu.
Umeona eeh. Badala kujikita kwenye maendeleo sisi tunajikita kubaguana!
Sikutegemea viongozi waanze utani wa kijinga!
 
Sisi hatukukipa kiingereza kipaumbele kama lugha ya taifa. Kiswahili kilikuzwa na kufanywa lugha ya taifa ikiunganisha makabila yote. Kama kiingereza kingefanywa lugha ya taifa kama kenya tungekuwa tunaongea kwa ufasaha tu. Mpaka vijijini watu wangekuwa wanaongea kiingereza kama kiswahili kilivyochukua nafasi kubwa kiasi cha lugha za makabila kusahaulika
Hoja ya msingi hapa ni kuwa hatujui english hayo mengine ni kujipooza na kujifariji.
 
Kasome kuhusu "establishing rapport" kwenye "mass communication" mada ya "presentation".

Binadam hautakiwi uwe "serious" muda wote, hutosikilizwa. Waongeaji wazuri wote lazima watie utani kidogo.
Sawa... but utani kwenye high level presentations zinakoleza mijadala ya kibaguzi huku kwa common wananchi!
 
Sio amani, sema uoga na uzombie.
Kenya hakuna uongo na Uzombie kwa kuwa wanajua Kiingereza? katika kosa ambalo naweza kumlaumu Nyerere ni kuwanyima exposure wa Tanzania kama Wewe maana unaona kila kitu cha nje ya Nchi yako ni kizuri na kila kilichofanywa Nchini ni kibaya
 
Back
Top Bottom