Aliye anzisha jina la soko la Kariakoo ni mme wa mama yangu mkubwa, kwasasa ni marehemu alijulikana kwa jina la baba Chale, nahuyo mwanae alikuwa chautundu hakuna mfano, sarakasi yumo,ngumi usiseme,hataungekuwa na ndevu utaliatu. ikabidi aitwe Chale sugu. hata shule aliishia darasa la nne shule ya Makongoro ,alikuwa anajificha mlima kwasasa panaitwa mjimwema .hiloeneo la mjimwema tulikuwa tunagombanishia Mbwa kila j.mosi tukitoka josho KAUMA ya zamani, ilikuwa kama mbwa wako unamuamini kwa ukali unamuleta mlimani,mbwa wa Chale sugu walikuwa wakali baraa ila ikitokea mbwa wake akapigwa basi mbwa aliyeshinda atapigwa mawe na wewe ukileta za kuleta unapigwa, mimi nilikuwa natumia kule kuwa ndugu na Chale sugu nami naonekana mtemi mkwala wangu ilikuwa sarakasi na mabreka dansi,Enzi za Kabibi Hotel