Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Studio iliyokuwa pale miti mirefu kwaona Shyrose Bhanji ilikuwa inaitwa Lucky Photo Studio. Pale kulikuwa na bro mmoja mweupe mchaga akichana nywele zake staili ya afro hivi. Wito Studio yenyewe ilikuwa maeneo ilipo stand ya daladala za kwenda Mwaloni. Ukishuka ngazi za kutokea kituo cha polisi pale Tanganyika bus na kulipokuwa na restaurant ya Mwadeco kisha ukatize barabara studio ilikuwa kushoto mwa hiyo stand ya Mwaloni.

Sawa ni lucky studio hiyo ingine ilikua mitaa ya bamboo club
 
Kulikuwa na mashine kule sokoni kirumba but tulikuwa hatuendi huko, ilikuwepo mashine hapa karibu na Monarch hotel, hii barabara kama unaenda CCM kirumba

Hizo mashine za kirumba ni zipi? zile za barabara ya kwenda mwaloni au?
 
Kulikuwa na mashine kule sokoni kirumba but tulikuwa hatuendi huko, ilikuwepo mashine hapa karibu na Monarch hotel, hii barabara kama unaenda CCM kirumba

Hapo sawa sawa, na uko sawa kabisa, nimeikumbuka, ila mashine hiyo wakati ule ni kama vile tulikuwa tunasema iko Mbugani au?
 
  • Thanks
Reactions: ram
ahahahahahhhh... yaani nimechekaje kwa sauti, duh! kadogori, mie mwenyewe kitambo sana sijazikia hapa town

Hahahaha
Kuna nyimbo moja ilikuwa inaimbwa na lile kundi la kutoka kigoto inaitwa shida haina adabu,Jamaa alikuwa anamalasta, zikianza na zile filimbi hahaha mabinti walikuwa wanakatikaje!!!! LOL.
 
  • Thanks
Reactions: ram
kadogori ilikuwa si mchezo, zile filimimbi na zile ngoma automatic tu unajikuta unatikisika, kulikuwa na kundi la kigoto, ibanda na shede. Shede nako ilikuwa balaa, kuanzia kadori, lelemama,vikojozi wanaotembezwa mitaani, ghasi zote zilikuwa zinapatikana shede

Hahahaha
Kuna nyimbo moja ilikuwa inaimbwa na lile kundi la kutoka kigoto inaitwa shida haina adabu,Jamaa alikuwa anamalasta, zikianza na zile filimbi hahaha mabinti walikuwa wanakatikaje!!!! LOL.
 
Kuna magari yao na yule dada wa Kona ya Bwiru, Zainabu Kichaa, Yalikuwa yanaitwaje ram? na mengine yalikuwa pale kwa Bora Kufa, unayakumbuka?
 
Mkuu QSS hawajawahi kuwa jirani na Mwanza Hotel. Labda kama unazungumzia Jyoti Art Studio ndiyo waliokuwa pale jirani na ofisi za RFA lakini siku hizi nao wamehamia karibu na lilipokuwa duka la FM studio (wauzaji maarufu wa audio cassettes miaka hiyo). QSS miaka mingi wako pale Nyerere road jirani na Furniture Centre.

Basi Mkuu QSS utakuwa umewafahamu hivi karibuni. Mwanzoni kabisa walikuwa maeneo ya mwanza hotel. Jyoti walihama baada ya jengo lao kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya.
 
Basi Mkuu QSS utakuwa umewafahamu hivi karibuni. Mwanzoni kabisa walikuwa maeneo ya mwanza hotel. Jyoti walihama baada ya jengo lao kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya.
Mkuu kwa kiasi fulani Mwanza mimi ni mwenyeji. Ngoja nikukumbushe kitu. Waliokuwa jirani na Mwanza Hotel ni Jyoti Art Studio. Hawa QSS mwanzo kabisa 1984 na kurudi nyuma yule mzee na vijana wake wawili walikuwa wakifanya biashara tofauti na walikuwa pale Nyerere road jirani kabisa na zilipo traffic lights. Yaani kama unatokea kule Mwanza Hotel ukifika pale kwenye mataa na kuvuka barabara wao walikuwa jengo la kwanza au la pili kushoto kabla ya kupita kichochoro cha kuelekea Salma cone. Kulia kabla ya kuanza uchochoro kukiwa (hadi leo) na mzee mmoja hivi wa kihindi akiuza juice kwa sana na kadi mbalimbali. Wakiwa pale yule mzee na hao watoto wake walikuwa wakipokea mikanda na negative za picha za rangi kutoka kwa wateja na wao kuwapatia madereva wa magari ya kwenda Kenya kisha kurudi nazo baada ya kusafisha kwa ajili ya watej wao. Kumbuka wakati huo kulikuwa hakujawa na mitambo ya kusafisha picha za rangi kwa Mwanza. Baadae kidogo wakiwa palepale karibu na hizo traffic lights ndipo mwaka 1985 wakaweza kununua na kufunga mitambo ya kusafisha picha za rangi. Hii ilikuwa ni mitambo ya kwanza kabisa ya picha za rangi kuingia mjini Mwanza. Nakumbuka vizuri kijana wake wa pili yule mzee wa QSS (Shakeel?) aliacha masomo kabla hata ya kumaliza form one pale Mwanza Secondary ili aweze kuungana na baba yake katika kusimamia hiyo biashara ya photo printing. Walikaa hapo miezi michache tu kisha wakahamia mtaa wa Uhuru. Hapo Uhuru street ndipo jina la QSS lilipokua kwa kasi na pia mikanda ya Tudor, Konica na Fuji colour kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa wapiga picha. Baada ya miaka michache wakahamia walipo sasa hivi Nyerere road kwenye jengo lao jirani na Furniture Centre, Chakula Barafu, mnara wa Nyerere au NBC. Kwa waliokuwepo miaka hiyo na wenye kumbukumbu nzuri palipo hilo jengo la QSS kabla ya jengo la awali kuvunjwa na kujengwa ghorofa la sasa palikuwa na duka la National Pharmaceuticals Company Ltd (NAPCO). NAPCO baadae wakahamia Kenyatta/ Rwegasore. Kuna jamaa alikuwa hapo QSS miaka mingi akiitwa Morgan namkumbuka sana. Sijui kama bado yupo au la. Baadae kidogo kuna studio nyingine ikiitwa Shelui nao waliweka mitambo yao kwenye jengo ilipokuwa Urshers club maeneo ya Liberty kabla ya studio zingine zaidi za picha za rangi kuibuka.
 
Last edited:
Wadau wa rock city enzi zile mnakumbuka Mwanza hapakuwa na usafiri wa vipanya kama leo. Vipanya vilikuwa Mabatini na Kirumba tu lakini Igombe kulikuwa na min bus zikiitwa Toto Tundu, Mayeji na Jalijalalam, Igoma kulikuwa na Last Boy na Mkuyuni air Jordan.
Jay ambe na geza ulole
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom