Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Igombe hadi leo zile bus za DIGIDIGI zinapiga mzigo, chezea waarabu wewe
 
Wadau wa rock city enzi zile mnakumbuka Mwanza hapakuwa na usafiri wa vipanya kama leo. Vipanya vilikuwa Mabatini na Kirumba tu lakini Igombe kulikuwa na min bus zikiitwa Toto Tundu, Mayeji na Jalijalalam, Igoma kulikuwa na Last Boy na Mkuyuni air Jordan.

MIAKA HIYO STEND ilikuwa mtaa wa miti mirefu kwa Kishimba,
Gari maarufu miaka hiyo Igoma ilikuwa ni Patrick kluivet ,(tim mtoto yule)

Mecco ilikuwa ni kilunguja na kilugwe

pale Buzuluga palipo na kituo cha mafuta cha GBP palikuwa garage ya mabasi ya Lake Transport, ulienda mbele kituo kilikuwa ni maziwa kabla ya nyehunge , ustawi ,Mayala garage, Pamba quick, sinai , Idara ya maji, Mziray , Kokoto, esso, california (mabatini) , geti, lango, natta. mitaa ya natta hotel.
 
N:B Mzee Kalori kwa sasa ni marehemu alifariki na kuzikwa kijijini Ruhunga Bukoba vijijini alikokuwa amenunua shamba.

Tiba
mmutaje basi hata na kinshuri, au marwa lucas pembeni yake alikuwepo mafuru.
 
Nakumbuka kila kitu ndugu yangu wakati huo Mkuu wa shule alikuwa ni muha fulani akiitwa Mwitila alikuwa anakuja shule akiendesha pikipiki. Mwalimu Mwombeki Mama wa kujisikia utafikiri dunia yote yeye ndiye alikuwa mwanamke peke yake bila kumsahau Mwl. Malaya aliyekuwa anafundisha muziki, Mkuburo akifundisha biology, Mdashas akifundisha Geography na wengineo. Usije kuta wewe tulikuwa darasa moja!!!!!!

Tiba
wale mabaunsa wa miaka hiyo hukumbuki hata mmoja, na wale masista duu wavaa nguo za kuhamasisha?
 
Wadau wa rock city enzi zile mnakumbuka Mwanza hapakuwa na usafiri wa vipanya kama leo. Vipanya vilikuwa Mabatini na Kirumba tu lakini Igombe kulikuwa na min bus zikiitwa Toto Tundu, Mayeji na Jalijalalam, Igoma kulikuwa na Last Boy na Mkuyuni air Jordan.

Vp na zile za akina Lema,monica lewinski,digididi halafu kulikuwa na gari fulani kichwa lori nyuma basi.
 
Hahahahaaaa...... mtoa uzi umenikumbusha mbali tulikuwa tunapanda sh. 500 kutoka Nassa Ginnery mpaka Mwanza mjini, lami iliyokuwepo na uafadhali ni kutoka Musoma mpaka Nyanguge na baada ya hapo ni vumbi mpaka unaingia mjini.
 
Chale sugu kesasa yuko sengerema,ni mganga wa jadi.
Daah Chale Sugu nilisoma na mdogo wake darasa moja usagara s/m.Jamaa namkubwa alikua master wangu mambo ya kun-fu,gymnastics na acrobat,Chale alikua mkali sana wa haya mambo.
 
Vp na zile za akina Lema,monica lewinski,digididi halafu kulikuwa na gari fulani kichwa lori nyuma basi.
Mbona unaogopa kutaja jina la hilo gari? Tulikuwa tunaliita "FISI".

Tiba
 
Wadau wa rock city enzi zile mnakumbuka Mwanza hapakuwa na usafiri wa vipanya kama leo. Vipanya vilikuwa Mabatini na Kirumba tu lakini Igombe kulikuwa na min bus zikiitwa Toto Tundu, Mayeji na Jalijalalam, Igoma kulikuwa na Last Boy na Mkuyuni air Jordan.

Umesahau digidigi la kayenze, weee
 
Kumbe nyie wote mliotoa comment mpaka sasa hivi ni wa juzi tu. Miaka ile ilikuwa hakuna cha minibus wala nini. Tulikuwa tunapanda zile peugeot za kizamani mnarundikwa kama ndizi humu. Station wagon moja ilikuwa inaweza kubeba hadi abiria 8. Zilipotoka hizo ndio zikaja express. I love Mwanza mji niliokulia.

Tiba

Hahaha
 
Vipi kuna anaekumbuka jina la video library moja iliyokuwa mwanzoni mkono wa kulia kama unatoka kwenye round about ya mnara wa Nyerere kuelekea kule Natta Hotel? Na pia jina la music centre iliyokuwa maeneo ya mtaa/barabara ya Msikiti wa Ijumaa jirani na/au kwenye nyumba lilipokuwa duka la spea za magari na matairi la Lema. Pia naikumbuka Monroe Music Studio (mtaa wa Posta, mwanzoni tu kulia kama unatokea traffic lights kuelekea Mwanza Hotel) ya bro Machemba ambaye kama sikosei alifariki 1990 au 1991. Studio hizo zilinisaidia sana kujua miziki mbalimbali ikiwa ni pamoja na orodha ndefu ya wanamuziki wa Marekani na Ulaya kwa ujumla. Hii ilikiwa ni kabla ya ujio wa FM studio (1992?). Nakumbuka mtangazaji Gadner G. Habash nae alipata kufanya kazi FM studio hapo Mwanza kabla hajahamia duka la jirani la Bw. Mushi lililokuwa likiuza vifaa vya electronics e.g. TV n.k (1997). Pia nawakumbuka mtangazaji Paul James Sweya (P. J.) akipiga disco pale Pamba Roof na kijana mmoja hivi ambaye kwa wakati huo alikuwa anasoma Lake High School akiitwa Deo Mutagonda (Kool Dior). Hii ya P.J. na Deo Mutagonda ilikuwa ni kwenye late 1980s (to be specific it was in 1989). Aisee tunakumbuka mbali!
 
Wadau wa rock city enzi zile mnakumbuka Mwanza hapakuwa na usafiri wa vipanya kama leo. Vipanya vilikuwa Mabatini na Kirumba tu lakini Igombe kulikuwa na min bus zikiitwa Toto Tundu, Mayeji na Jalijalalam, Igoma kulikuwa na Last Boy na Mkuyuni air Jordan.
wasukuma mtaacha lini ushamba sijui.mpaka leo daladala halina muziki hawapandi
 
Nawakumbuka pia wachezaji wa break dance akina Bob Sado, Matondo na watoto wa mzee mmoja maarufu akiitwa Mzee Jumbe (mtaa wa Rufiji?). Hii ilikuwa ni kwenye mid 1980s. Wakati huo DJ maarufu kwa Mwanza akiwa ni DJ Yusuph na wadogo zake. Baadae nikaja kusikia Bob Sado alikuwa ni "aunt". Nikabaki kustaajabu tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom