Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,151
Nimekulia mitaa hiyo enzi mzee mpemba yuko hai alikua na hoteli hpo jirani na sokoni
Nimekulia mitaa hiyo hiyo kwa mzee Khalifan (RIP masikini)
Nimekulia mitaa hiyo enzi mzee mpemba yuko hai alikua na hoteli hpo jirani na sokoni
na Mazigo wapi?
Nimekulia mitaa hiyo hiyo kwa mzee Khalifan (RIP masikini)
Mzee kanyau alikuwa mlevi sana wa gongo, halafu meno ya chini alikuwa KANG'OA.
Huyu mzee niliskia aligongwa na Bus La mwatex ndio ikawa sababu ya kifo chake.
Nani anamkumbuka yule mgambo pale Feri ya kwenda Kamanga?
Alikuwa ana tumbo kubwa sana km Ngoma, anatembea na Rungu lake ameliandika" PIGA LKN USIUWE" na picha ya Kipepe!
Ha ha ha ha ha!
Hii ilikuwa inaitwa Dakik au DikDik? Hii nilikuwa napanda kutoka Kayenze kuja mjini miaka hiyo! Kayenze tunapandishwa saa 8 usiku, nilikuwa nachoka kabisa, njia nzima umesinzia tu mpaka unafika mjini. Siku moja nikashushwa home pale Nyakato saa 11 alfajiri almanusura niangukie mikononi mwa vibaka, shukrani kwa mzee Mathias mzee wa Kikurya jirani yetu aliyekuwa askari pale Mwatex!Hahaha nimekumbuka mbali dakik bus service
Aisee! Kumbe ugaidi huwa hauishi hata kama utazeeka yaani unazeeka nao, hili jamaa mika hiyo lilikuwa gaidi sana lakini naona mpaka leo linaendelea kuwa gaidi!Enzi hizo ukienda na demu mkali lazima Matata akupore,sasa hivi ni Mheshimiwa Diwani.
Shukran mkuu nimekuelewa.Mkuu enzi hizo mtu kuwa na Kamera ilikuwa issue kupita kiasi. Picha tulikuwa tunapiga studio tu. Halafu pale stendi mjini kulikuwa na kituo cha Polisi na mkuu wa kituo alikuwa anaitwa Kalori, Mzee mmoja mweupe amejaza halafu kapanda juu. Huyu alikuwa anawajua vibaka/vijana wa pick pocket wote. Akimwona mmoja akimwangalia jicho tu inabidi huyo kibaka akimbie kama hana akili nzuri. Mwanza enzi hixo. Mimi nilisoma Mwanza Secondari.
Tiba
Mzee khalifan yule wa kiarabu au mana mi nimekulia ile nyumba ilikua na hospital hpo jirani n moonlight
Hapo palikuwa na hospitali ya ndelingo.
Mazigo, Pius na Sadoti Jr...
Mzee khalifan yule wa kiarabu au mana mi nimekulia ile nyumba ilikua na hospital hpo jirani n moonlight
Hapana alikuwa mswahili yaani alikuwa anaishi nyumba ya pili kutoka kwa Sadoti (nyumba kubwa ila ilikuwa haijaisha vizuri na walikuwa wanauza bia za jumla.. nyumba imetizamana na shimo la taka.. Moonlight niliwahi kufanya kazi hapo wakati nasubiri matokea miaka hiyo.....
Enzi zile Express za Mkuyuni mwisho ilikuwa kona ya Butimba! Ha ha ha! Kwenda nyegezi jeshini lazima ukanyage!