MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Wapiganaji wa Wagner waelekea Moscow kuuondoa utawala wa kijeshi unaoongozwa na SERGEI SHOIGRU. Kiongozi wa Wagner anadai kwamba majeshi ya urusi yamekuwa yakishambulia kambi zao nchini UKRAINE.

Huu Uzi nitatoa update ya kila kinachoendelea.

=====
Update: Maafisa wa Ukraine wasema watatumia 'mapinduzi ya kijeshi' nchini Urusi kurejesha eneo lililochukuliwa

Katika tishio moja kwa moja kwa mamlaka ya Putin, Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa Wagner, aliishutumu jeshi la Moscow kwa kupiga bomu askari wake na kudhibiti jiji muhimu la Urusi mapema asubuhi.

Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali wa jeshi binafsi maarufu zaidi ulimwenguni aliahidi kwenda kwenye mji mkuu kwa kulipiza kisasi.

Katika hotuba isiyokuwa ya kawaida, Bwana Putin alilitaja tukio hilo kuwa "uhaini" na akasema wale wanaounga mkono vitisho na njia za kigaidi watapata adhabu isiyoweza kuepukika.

Rais wa Ukraine, Zelensky, alivunja ukimya na kusema kuwa hii ni mfano mwingine wa "udhaifu kamili wa Urusi".

=====

Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi waagiza watu kubaki nyumbani

Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi walitoa wito kwa watu kubaki ndani ya nyumba zao kwa sababu za usalama.

Walitoa onyo hilo kutokana na ripoti kuwa wapiganaji wa Wagner walikuwa wakitumia eneo hilo wakati wa safari yao kuelekea Moscow.

=====

Wagner wateka makao makuu ya jeshi la Urusi ukanda wa Kusini
Gavana wa Voronezh, nchini Urusi alisema Jumamosi kuwa huduma za dharura zilikuwa zikijaribu kuzima tanki la mafuta linalowaka katika kituo cha mafuta.

Zaidi ya askari zimamoto 100 na vifaa 30 vya kuzimia moto walikuwa wakifanyia kazi katika eneo hilo, alisema Gavana Alexander Gusev kupitia Telegram.

Awali Jumamosi, chanzo cha usalama nchini Urusi kiliiambia Reuters kuwa wapiganaji wa Wagner walidhibiti vituo vya kijeshi katika jiji la Voronezh, umbali wa kilomita 500 (maili 310) kusini mwa Moscow. Reuters hawakuweza kuthibitisha madai hayo.
=====

NDEGE YA RAIS YADAIWA KUONDOKA MOSCOW, WAGNER WAKIDAIWA KUKARIBIA MJI

Inadaiwa Wapiganaji wa Wagner wameendelea na mapambano na sasa wamefika katika Mkoa wa #Lipetsk, takriban Kilometa 450 kutoka Moscow

Aidha, inaelezwa kuwa Ndege za Kivita za Urusi zimeshambulia misafara ya Wapiganaji wa #Wagner na tayari Wanajeshi wameshajipanga katika nafasi za kuulinda Mji Mkuu, Moscow

Kiongozi wa Wagner, Yevgeny #Prigozhin amedai kuwa Wapiganaji wake wamepokelewa kama 'Wakombozi' na kuwa waliweza kuchukua Makao Makuu ya Kijeshi huko #Rostov bila mapigano

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Ndege ya Rais imeonekana kuondoka #Moscow, hata hivyo Ikulu imedai kuwa Rais #Putin bado yupo katika Mji Mkuu huo

Wagner wasitisha kwenda Moscow wakidai hawawezi kumwaga damu ya Warusi

Kiongozi wa kundi la Wagner amesema kwenye chanel yake ya Telegram kwamba wamekubaliana kuacha kupeleka vikosi vyake Moscow.

Prigozhin amesema wapiganaji wanarejea kwenye kambi za Ukraine na hawataki kumwaga damu za warusi.

Makubaliano ya ghafla ya kuondoa hali ya sintofahamu yanakuja baada ya kiongozi wa Beralus, Alexander Lukashenko kufanya maongezi na Prigozhin kulingana na channel ya Kirusi ya Rossiya 24
 
Back
Top Bottom