Mapigano kati ya Wagner group na Jeshi la Urusi yaripotiwa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,268
Mapigano yameripotiwa kati ya mamluki wa Wagner group na Jeshi rasmi la Urusi, wapiganaji kadhaa wa Wagner wanaripotiwa kuuawa katika shambulizi liliofanywa na Jeshi la Urusi.

Baadhi ya vyanzo vya taarifa vinadai Wagner wanafanya jaribio la mapinduzi na wanataka kuanza kwa kuuondoa uongozi wa Jeshi la Urusi. Prighozin ametoa kauli kwamba viongozi wa vyombo vya usalama na jeshi la Urusi walimdanganya Putin kuivamia Ukraine na kwamba vita hiyo haikuwa na ulazima, ilikuwa inaepukika!

Rais wa Putin ametoa kauli kwamba anaelewa kinachoendelea katika kundi la Wagner group.

Taarifa zaidi kwa kina zitaendelea kuletwa kadri zinavyopatikana.
 
Counter-offensive
Screenshot_20230624-011847.jpg
 
Kama wanataka kujiweka juu ya serikali ni razima wadhibitiwe.
Tatizo huyu kiongozi wa wargener bifu zake na Shoigu anarazimisha ziwe za nchi nzima.
 
Kama wanataka kujiweka juu ya serikali ni razima wadhibitiwe.
Tatizo huyu kiongozi wa wargener bifu zake na Shoigu anarazimisha ziwe za nchi nzima.

Well shoigu ni top military asset. Hiyo si bifu za mitaani
 
Back
Top Bottom