johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,107
Prigozhin ahofiwa kufariki katika Ajali ya Ndege

Watu 10 wameripotiwa kufariki kwenye ajali hiyo ya ndege

Watanzania tumuombee apumzike kwa amani!

Source: Al jazeera

====

Kwa mujibu wa Idara ya Habari ya Urusi (TASS), abiria 10 waliokuwa kwenye Ndege Binafsi wamefariki ambapo inaaminika Kiongozi wa Jeshi Binafsi la Wagner Group, Yevgeny Prigozhin naye alikuwepo kwenye Ndege hiyo

Taarifa za awali zilizoripotiwa na akaunti ya Grey Zone inayodaiwa kuwa na uhusiano na #WagnerGroup zimeeleza kuwa Ndege hiyo ilishambuliwa na Walinzi wa Anga katika Mkoa wa Tver, Kaskazini mwa Moscow

Juni 2023, Prigozhin aliongoza kilichoelezwa kuwa ni Uasi wa muda mfupi dhidi ya Wakuu wa Kijeshi wa Urusi ambapo Rais Vladimir Putin alimtaja Kiongozi huyo kama Msaliti.

russia-768x512.jpg
Yevgeny Prigozhin was passenger on crashed plane, Russian officials say Ten died when aircraft came down on flight from Moscow to St Petersburg, according to emergency ministry

Wagner boss Yevgeny Prigozhin was on the passenger list of a plane which crashed in Russia, killing all 10 on board. He was believed to be on board the plane. Earlier, a Wagner-linked Telegram channel Grey Zone reported that the jet was shot down by air defences in Tver region, north of Moscow.
 
Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin amefariki katika ajali ya ndege nchini Urusi, pamoja na watu wengine tisa waliokuwemo ndani pia wamefariki.

************************************************

Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin alikuwa kwenye orodha ya abiria wa kwenye ndege iliyoanguka nchini Urusi na kuwaua watu wote 10 waliokuwa ndani.

Inaaminika kuwa alikuwa ndani ya ndege hiyo.

Hapo awali, chaneli ya Telegram yenye mahusiano na Wagner, Gray Zone iliripoti kwamba ndege hiyo ilidunguliwa na walinzi wa anga katika mkoa wa Tver, kaskazini mwa Moscow.

Prigozhin aliongoza uasi wa mapinduzi yaliyoshindwa dhidi ya vikosi vya jeshi la Urusi mnamo Juni.

View attachment 2726574
BBC.
 
Kifo chake kilishatarajiwa wakati wowote ule baada ya ile Mutiny, lilikuwa ni swala la muda tu. Halafu huyu Boss Prigozhin anazingua, jana kapost video anatuambia yuko Africa tena akisema (we are working, the temperature is 50°C plus) leo wamemuulia huko Urusi. Ukute hapa tunachengeshwa tu, maana wanasema eti "he was on the passenger list" na vipi kama list haikutimia on board 😁
 
Case Closed.

Nimesema humu JF kuwa mazee (Putin, Lukashenko & Co) si watu wa kuwachezea weye fanya mambo yako, wao hukulia "timing" tu ikifika muda muafaka hutekeleza.

 
Back
Top Bottom