Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,354
- 23,760
Ndugu zangu Watanzania,
Mpaka sasa kila mmoja wetu anafahamu ya Kuwa Mheshimiwa Balozi Daktari Emmanueli Nchimbi Ndiye Mgombea Mwenza Wa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Lakini pia Ni ukweli ulio wazi kuwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Ndiye anayekwenda Kuwa Makamu Wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sasa kwa kuwa kwa sasa ndiye mtendaji mkuu wa CCM Taifa . Na kwa kuwa nafasi hii ni ya kiutendaji Zaidi. Hivyo umuhimu wake ni Mkubwa sana na hivyo haiwezi kukaa au kuchukua muda mrefu ikiwa wazi bila kujazwa mtu Rasmi wa kuhudumu katika nafasi hiyo. Ili majukumu ya chama yaendelea kama kawaida hususani kipindi na wakati wa kampeni na baada ya kampeni.
Swali nawaulizeni watanzania wenzangu ambao mnaitazama CCM Yetu kwa jicho la Matumaini. Mngependa Jina gani lipewe nafasi ya kuchukua nafasi ya Mwamba Mwenyewe Balozi Daktari Emmanueli Nchimbi? Nani ataendana na siasa za kisasa za wakati huu? Nani ataendana na kizazi cha wakati huu na kuleta matumaini na kuvuta wanachama wengine wengi zaidi wapya?
Nani unafikiri ataweza kuvivaa vyema viatu vya Mheshimiwa Balozi? Nani unafikiri ataendeleza Umoja , mshikamano,upendo na Nguvu na ushawishi wa CCM? Nani unafikiri ataweza kuendana na kasi ya Jemedari wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan?
Ikumbukwe ya kuwa mtu na kiongozi huyo itapaswa kuwa yule mwenye uzoefu wa kutosha ndani ya CCM na pengine hata serikalini, mwenye kuijua vyema historia ya CCM,mwenye ushawishi ndani na nje ya CCM,mwenye uwezo wa kuzungumza na akasikilizwa na watu wote, mwenye uwezo wa kujenga hoja,kukitetea chama ,Mwana mikakati na atakaye hakikisha CCM inaongeza wanachama kila uchao pamoja na kuendelea kuwa mdomoni Mwa Watanzania.
Ni lazima awe mtu mwenye Haiba ya uongozi, Ushawishi kwa watu, uwezo wakujenga hoja ,kupangua hoja na kutetea hoja kwa uharaka ,wepesi na kwa lugha yenye kueleweka vyema na kwa urahisi kwa watu wa rika zote na wenye Elimu za viwango tofauti tofauti. Ni lazima awe ni mtu mnyenyekevu, mzalendo, mchapakazi,muadilifu lakini mwenye misimamo katika kukisimamia chama na wanachama.
Ni lazima awe ni mtu wa haki ,mtu safi na mwenye historia safi isiyo na makando kando na matope . Asiwe mtu mwenye tuhuma chafu na mbaya. Kwa kuwa CCM inaheshimika sana hivyo ni lazima ilete mtu mwenye tabia njema na mwenye taswira njema na kuheshimika machoni pa Umma wa watanzania.
Ni lazima awe mtu ambaye anakuja kukijenga na kukiimarisha zaidi chama badala ya kuja kumjenga na kumuimarisha mtu kwa ajili ya mbio za Urais wa 2030. Ni lazima mtu huyo aepuke na asiwe mtu mwenye kupenda na kuendekeza makundi , migogoro,visasi ,chuki,hasira ,jazba na Mihemuko. Ni lazima awe mtulivu wa akili na maamuzi Makini yenye kuzingatia misingi ya katiba na miongozo na kanuni za CCM. Azungumze baada ya kufikiria badala ya kufikiria baada ya kuzungumza jambo.
Asiwe na Papara katika mambo mazito na yenye kushika na kuteka hisia za watu. Azungumze mambo mazito yenye kugusa hisia za watu baada ya kufikiria kwa kina na kwa utafiti na ushahidi. Awe mwenye ndimi moja,. Ajiheshimu yeye binafsi popote awapo ndani na nje ya Tanzania kwa kutambua uzito wa nafasi aliyonayo na historia nzuri na yenye kuheshimika ya CCM.
Je Mtu huyo ni Nani? Na ikumbukwe mtu huyo ni lazima atakuwa mtanzania Mwana CCM ambaye siyo malaika.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.