Uliza chochote kuhusu Rwanda

Uliza chochote kuhusu Rwanda

Lakini kwa nini uzi kama huu nyakati kama hizi?, je ni kujisafisha?, ni propaganda? au ni nini haswa, na mtoa mada uanonekana mi mtu uliyepo humu JF intentionally kabisa kwa kazi fulani, but nachowakubali Wanyarwanda mpo patriotic sana na nchi yenu, ukianzia Rais wenu huo ukatili unaosemwa ni just because ya maslahi ya nchi yake, heko kwenu, nina mengi ila ngoja niachie hapo
 
“Visit Rwanda 🇷🇼” ktk jersey za PSG ya France 🇫🇷 na ile Arsenal pale England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 inamatokeo chanya hasa ktk kuvutia watalii, kipi kimeongezeka ktk tasnia yenu ya utalii baada ya kuwepo kwa visit hizo ktk club kubwa za ulaya???
Sasa kama unajua ni chanya, nikujibu nini?

Ila, ingekuwa haina matokeo mazuri, usingekuwa unaiona mpaka sasa.
 
Mimi ni Dereva wa Truck, knowledge yangu kuhusu Rwanda inatokana na mimi kwenda Rwanda Burundi DRC Uganda Kenya Malawi Zambia nk. mara kwa mara, wewe ulijifungia Wilayani kwenu usiwe rahisi ku judge
Kwan ukikubal kwenu Rwanda tutakufukuza?
 
Rwanda ipi wanainjoi mkuu mbona unatufanya kama ni wageni Rwanda.
Unachokiita kuenjoy ni nini labda? Kama huna unachokipenda, uunapenda ulicho nacho.
Wenyeji wako unategemea na utembeleako. Na mtu kuwa na kidogo kuliko ulicho nacho wewe,hakuwezi kumfanya aonekane mnyonge.
Mbona Tanzania wapo wenye hali ngumu zaidi ya hao wanyarwanda? hawaenjoy maisha yao?
 
Ni kweli FDLR Bado ni tishio kwa usalama wa rwanda.mbona hao migambo hawafiki hata 5000 ni wachache ila tu idealogy Yao ndo mbaya..ila nguvu hawana..ni kweli wanapewa sapoti na majeshi ya DRC?
 
Cha kwanza kabisa kuna certificate of import, inapatikana kwa fedha ya Rwanda laki mbili(200,000 Frws), ushuru, kilo moja mara ya mwisho ilikuwa 500 kwa kilo, hapo uhakika wa 100% unapata kwa watu wa forodha mpakani.
Kilo moja ya mchele huko Rwanda ni bei gani?
 
Una chochote unachojiuliza kuhusu Rwanda?

Una chochote unachotaka kujua kiundani zaidi?

Una chochote ulichokisikia na bado umebaki njia panda!!

Iwe jambo la maana, iwe utani, iwe siasa, chochote, uliza utajibiwa hapa hapa.



Rwanda ndo nchi pekee barani Afrika, ukiingia huulizwi utakaa siku ngapi na unaenda kufanya nini. Kama unataka, funga mizigo yako hamia, kama una biashara yako, fanya, kama una ujuzi wako, omba ajira, ukipewa hakuna wa kuja kuuliza mbona huyu si mnyarwanda, kasoro serikalini tu. Ila na penyewe ikiwa una ujuzi ambao wanyarwanda hawana, kupata ajira ni simple.
Eti ni kweli alipiga marufuku makanisa na misikiti kuwepo nchini kwake ?ina maana hakuna kanis lolote au msikiti mnaishi tuu kama wachina?
 
Ni kweli FDLR Bado ni tishio kwa usalama wa rwanda.mbona hao migambo hawafiki hata 5000 ni wachache ila tu idealogy Yao ndo mbaya..ila nguvu hawana..ni kweli wanapewa sapoti na majeshi ya DRC?
Sasa mkuu, unajua kilichopelekea watutsi wa DRC kuanza kuuliwa si idadi, bali hiyo ideology?
Jiulize, mtu ambae ndugu yake yupo huko,atamtelekeza?
Unajua kuna wanawake ambao,waume zao ndo wapo huko, na kudinywa lazima waende huko?

Kuhusu kupewa support, si jeshi la DRC, bali serikali. Mpaka sasa, kwenye ngazi za jeshi hadi walinzi wa rais, wamo.
Unapowaita mgambo, huku wengi,hasa watu wazima ni wanajeshi, na waliojiunga wamepewa mafunzo ya kijeshi, idadi hiyo unaiona ndogo?
Harafu, pia ujue, media ina nguvu sana kuliko nguvu ya mtutu wa bunduki.
 
Kilo moja ya mchele huko Rwanda ni bei gani?
Kwa mchele wa Tanzania, ni kati ya 2500 hadi 3200. Hizi ni Grade II na III, Grade I yenyewe haipo.

Kama ni mfanya biashara, cgangamkia fursa hii: Rwanda hapo mpakani kuna soko la kisasa. Mazungumzo baina ya uongozi wa wilaya za mpakani, wameamua kupeleka bidhaa za kitanzania sokoni humo, ila mfanyabiashara awe anafahamika kuepusha hali ya ujanja ujanja na kuweza kufatiliwa inapokuwa lazima. Hivyo, ukiwa na stock huko au mpakani upande wa Tanzania, uhakika wa kuuza upo.
 
Unachokiita kuenjoy ni nini labda? Kama huna unachokipenda, uunapenda ulicho nacho.
Wenyeji wako unategemea na utembeleako. Na mtu kuwa na kidogo kuliko ulicho nacho wewe,hakuwezi kumfanya aonekane mnyonge.
Mbona Tanzania wapo wenye hali ngumu zaidi ya hao wanyarwanda? hawaenjoy maisha yao?
Rwanda ni gereza kubwa. Kwa ambao wameenda pale ni mashahid hawana tofauti na Korean kaskazin
 
Eti ni kweli alipiga marufuku makanisa na misikiti kuwepo nchini kwake ?ina maana hakuna kanis lolote au msikiti mnaishi tuu kama wachina?
Hahahahahahah


Story za kijiweni hizo.

Iko hivi, kila mtu alikuwa akijisikia kuanzisha kanisa, anaanzisha.
Ilitokea sasa yakaanza makanisa ya watutsi tupu, ya wahutu tupu.
Wenye makanisa wakawa kama matapeli, wanachukua tu hela kwa waumini, ikaonekana ni biashara sasa.
Kila sehemu unajenga, wengine majumbani.

Serikali ikaona malalamiko yamekuwa mengi, ndo wakaanza ukaguzi wa kuangalia vigezo vya kanisa(vilivyoidhinishwa na serikali). kama hujakidhi, unafungiwa. Ukirekebisha, wanakagua, ukikidhi, kanisa linafunguliwa. Ikiwa hakuna, ndo hakuna kufunguliwa.

Badhi ilikuwa kama jengo kutoruhusu sauti za ndani kutoka nje, kutokuwa kwenye makazi ya watu, kutokuwa na eneo kubwa kwa ajiri ya mkusanyiko wa dharura na parking, vyoo safi na salama, upatikanaji wa maji, walimu waliosoma masono ya dini, na vitu kama hivyo. Kwa hiyo, waliokidhi vigezo, wanaoperate.

Kingine, ni kuweza kucontrol pesa zinazotumika zinatoka wapi na matumizi yake yakoje
 
Kwanini Kagame amemitumua Karusisi na kumuweka Gashugi ambaye hana uzoefu mkubwa ???

Kwanini Rwanda, nchi ambayo ni tajiri inaogopa kuwekewa vikwazo vya misaada (Aids and Grants) kutoka EU na G7 ???

Hivi kima cha kipato cha kila raia wa Rwanda (GDP Per Capita) ni kikubwa kiasi gani ???
 
Kwanini Kagame amemitumua Karusisi na kumuweka Gashugi ambaye hana uzoefu mkubwa ???

Kwanini Rwanda, nchi ambayo ni tajiri inaogopa kuwekewa vikwazo vya misaada (Aids and Grants) kutoka EU na G7 ???

Hivi kima cha kipato cha kila raia wa Rwanda (GDP Per Capita) ni kikubwa kiasi gani ???
. Karusisi: Hakuna mnyarwanda kwenye cheo chake ni mungu-mtu. Amekuwepo, ametekeleza majukumu yake, na wengine wanahitaji kupata uzoefu.
Sijui kitu gani unachokiita kutimua: Je, kama anakopelekwa kunahitaji mwenye uzoefu alio nao, au anatakiwa pia na yeye ajifunze mengine, atakuwaje ametimuliwa!!! Gashugi nae ana haki ya kuwa na madaraka kwenye nchi yake, kama amekidhi vigezo. Katoka sehemu moja, kahamishiwa kwingine, na baada ya muda atakabidhiwa mwingine.


Rwanda haiogopi kuwekewa vikwazo. Ni kweli msaada kama upo, ni msaada. Ila usipokuwepo, maisha yataendelea.
Mwaka 1994 Rwanda iliishi kwa msaada wa nani? Mara mia Tanzania iliyopokea wakimbizi, ikawapa hifadhi na mahitaji mhimu,itaheshimika miaka mia kuliko hao wa mbali, ambao misaada yao ina masharti.

Hivi, hao mnawaona wajinga,ndo wana hela za kuchezea kutoa misaada? Kodi za raia ndo ziende kuchezewa?
Marekani imeisaidia Ukraine kwenye vita vyake. Kilichofuata ni mfano hai wa hiyo misaada.




Missada hiyo unayoisema, chunguza imekaeje kwanza.
Shilika likija na hela, na kukuelekeza namna ya kuzitumia, na wanaozitumia wametoka nao kwao, ndo wanunulie magari, ndo walipwe mishahara, ndo matumizi yao kila siku, kwenye milioni 100, msaada kwako ni kiasi gani?

Nchi tajiri labda unaipima kwa vigezo gani!! Rwanda ni nchi inayojitafuta, siyo nchi tajiri. Japo pia si masikini kihivyo.

GDP ipo kwenye Dola elfu moja na kitu
 
Mkuu una uhakika wewe ni mnyarwanda? Mbona unachalaza Kiswahili kama mzalamo wa manzese kabisa.
Teh teh teh teh teh teh teh !!! Kwa hiyo, mtanzania aliezaliwa Rwanda akija kwenu na kuongea Kinyarwanda, ataonekana mnyarwanda!

Japokuwa tukiachilia mbali mihemuko na roho mbaya, rwanda na Tanzania ni majirani, hivyo ...................................
 
Ndoto yangu ni kuzaa Na mnyarwanda uzuri naongea kishubi cha ngara najua tunasikilizana vizuri.
 
Back
Top Bottom