Mkuu vip nikioa mwanamke wa rwanda, kuna process gan nitatakiwa kuzifanya ili aje aishi tz bila bugudha?
tukianzia pale mpakan anapitaje au hadi akatiwe visa?
Tracy Chapman
Kama kuna kitu rahisi duniani, ni process ya uhamiaji Rwanda.
Kutoka, analazimika kuwa na hati ya kusafiri. Zipo za aina tatu:
Ipo ya EAC, gharama yake ni kama Tshs 22,000.
Ipo Passport ya miaka 5, gharama yake ni Tshs 155,000
Ipo passport ya miaka 10, gharama yake ni Tshs 205,000
Zote hizi hupatikana Maximum 3 days kama mhusika hana tataizo lolote. Kama anadaiwa, lazima alipe kwanza.
Kama unataka kumuolea Tanzania, process ni wewe na uongozi wako, ila nachokijua ubalozini lazima, itahitajika Criminal record certificate. Hii huweza kuchukua hata week, maana screening inapita sehemu tofauti tofauti.
Na kama unataka kumuolea Rwanda na kwenda nae Tanzania, ndoa ya kiserikali ikiisha, unakuwa na cheti chako, ambacho utatumia kumuombea Residence permit. Kwa mwanamke wa kinyarwanda alieolewa na mtanzania, nijuavyo mimi, hakuna usumbufu kama wewe ni mtanzania harisi.. Issue tu ipo kwa wanaume.