Uliza chochote kuhusu Rwanda

Uliza chochote kuhusu Rwanda

Swali kumaliza ukabila Rwanda ili yasijirudie ya Genocide Rwanda imechukua hatua zipi kuhakikisha ukabila hauna nafasi Rwanda?
Haujaisha kivile,

Kinachofanyika ni kuendelea kuelimisha watu. Kwa sababu katika kila kabila, vigezo vyote vipo pande zote. Na maisha ya kila siku, watu wanahitaji wenzao.
Tatizo lipo hasa upande wa watu ambao wana amini uongozi lazima wakabe,
 
Umejibu vizuri

Kwa nini Rwanda kuepuka hilo tatizo kwa nini haikuongea na nchi jirani zake wawachukue hao wakimbizi wa Rwanda wawape uraia kama ilivyofanya Burundi kuongea na Tanzania na Tanzania ikakubali kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi 250,000 na kuwapa vitambulisho vya taifa ili wawe raia wa Tanzania?
Bado tunarudi pale mwanzoni.

Mtutsi alisadikika kuwa ni mtu mbaya na hastahili kuishi. Ndio maana akaitwa nyoka, mende na majina mengine. Waliolishwa sumuhiyo, kwa sasa ni watu wazima, na bado wapo ambao wana imani hiyo. Hivyo, usipokuwa makini kama kiongozi, watauliwa tu. Na isitoshe, mpaka sasa hizo kesi zipo.

Serikali ya Rwanda ya kipindi hicho, haikutaka kusikia neno hilo au kujihusisha na jambo lolote linalowahusu, ilikuwa kama si wanyarwanda.
Ndo maana utasikia chanzo cha kuwatupia mto Kagera kipindi kile cha mauaji ya kimbali, ni kwamba asili yao ni Ethiopia, hivyo maji ya mito na ziwa yawarudishe kwao.

Kama labda umeongelea issue ya kufukuzwa kwao juzi, mnyarwanda aliezaliwa tanzania na sasa ana miaka 50, Rwanda itamtambuaje? Ila, akienda atapokelewa. Na kwa vitu kama hivi, utakuta mtu anaishi nchi furani, kwa sababu ndo anapoona fursa za kimaisha, mwingine atakana uraia wake, kwa sababu anajua akirudishwa, maisha yanarudi zero
 
1. Ni nani ambaye pengine anaandaliwa kumrithi Mr. Tall, akiondoka madarakani?

2. Mfumo wa elimu ya Rwanda ukoje? Kuanzia msingi mpaka vyuo.

3. Mfumo wa matibabu ukoje, huduma za afya zinapatikana kwa urahisi?
Watu wengi wanatumia bima ya afya?
Je serikali inagharamia matibabu kwa baadhi ya makundi ya watu?

4. Rwanda mnachimba madini gani hasa?

5. Kwa nini unasema Rwanda ni masikini wakati mmewekeza mpaka kwenye baadhi ya vilabu vya mpira ulaya (Arsenal, PSG nk..)?

6. Vipi huko Rwanda umeme ni tatizo kubwa? Kuna mgao wa umeme? Vijiji vyote vina umeme?

7. Je huko pia kuna machawa? 😂

Ahsante sana!
1. Sijui

2. Rwanda shule ya msingi ni miaka 6, sekondali miaka 6(O level miaka 3 na A level miaka 3) Kwa sasa kuna kitu kinaitwa 9 years Basic Education. Unasoma shule ya msingi miaka 6, na 3 ya O level sehemu moja.
Kwingine ni 12 years Basic Education. Yaani miaka yote 12 unasomea sehemu moja.

Elimu kwa ujumla imekumbwa na changamoto ya mfumo. Zamani, kulikuwa na mfumo wa kifaransa, badae ukageuzwa kuwa wa kiingeleza. Hivyo, waliokuwa wakisoma mfumo wa kifaransa, walipata changamoto ya kuadapt lugha.
Mbali na hilo, uongozi wa Wizara unaokuja, unakuja na mapya yake. Labda vyuo vikuu, na kwenyewe badhi ya sections furani, kama sheria, nursing,ICT, ndo unakuta wameiva sana.

Ila wasomi wengi, wapo chini ya kiwango

3. Mfumo wa matibabu, wanywarwanda wamegawanywa katika makundi 4 kulingana na uwezo wao. Kundi la kwanza, linasaidiwa na serikali kulipiwa.
Kundi la pili na la tatu, kila kichwa cha familia ni Faranga elfu 3(karibia elfu 6 ya Tanzania). Kundi la 4 ambalo ni la watu wenye uwezo wa juu, kila kichwa cha familia ni elfu 7(Karibia 14 ya kitanzania).

Kwa ujumnla, upatikanaji ni rahisi, kwa sababu kila raia ana access kwa daktari. Na kabla hujafika huko, nchi nzima kuna wahudumu wa afya, kila kitongoji, ukijisikia vibaya unamuona. Huduma za kwanza wanatoa, na dose kama za malaria na magomnjwa madogo madogo unapata hapo hapo. Ikiwa ni kesi iliyo nje ya uwezo wao, kuna zahanati za kata. Hapo wakiferi, unaenda kituo cha afya. Kesi yako ikiwa kubwa, unapewa referal kuelekea Hospitali ya wilaya.
Kwa hiyo kuna bima ya afya ya Pamoja(CBHI Community Based Health Insurance), na bima za mashirika. So, ukienda kwa ajili ya matibabu, unalipia 10% ya gharama zote, hata ulazwe miaka 10.

uongozi wa wilaya ukibainisha mtu hana uwezo, serikali inaghalamia 100%

4. Rwanda, madini yapo. Kuhusu labda tetesi za wanaossema ya DRC. Hilo sitoliingilia, lakini inawezekanaje mashariki ya Congo yote iwe na hizo ressources, then zisivuke mpaka! Sema tu kwa kuwa ni nchi ndogo, na technologia labda isiwe kubwa kama ya migodi ya kifahari, na uchimbaji wake ni wa masharti, lakini madini yote yapo. Labda nitafute majina.

5. Umasikini naouongelea, ni hatua ya maendeleo ukilinganisha na nchi jilani zilizotangulia, au na maisha kwa ujumla. Uwekezaji kwa timu za nje, ni kwa ajili ya kuhamasisha watu kuja kuwekeza ndani na kutengeneza ajira. Jambo hilo linasaidia kupunguza ukosefu wa ajira. Pia, ukilinganisha na nchi jirani,fursa za kimaisha ni tofauti na za nchi hizo. Hivyo,niseme ni nchi ambayo inajijenga, miaka 30 ni muda mfupi sana kuweza kufikia hatua za waliokutangulia.

6. Rwanda mgao wa umeme hakuna. Inaweza tokea labda kama kuna marekebisho. Vijini umeme unasambazwa, nadhani kwa sasa wanyarwanda 70% au zaidi kidogo wana umeme. Kukatika ni kama 5%

7. Nahisi uchawa unamaanisha kujipendekeza: Rwanda unalipwa kwa kile ulichokifanya na chenye manufaa kwa jamii.
Ukizingatia, ni nchi cganga,chama tawala cha RPF ndo kimekuwepo kuhakikisha kila jambo linatekelezwa. Vyama vya upinzani, vingi vilionekana kutaka kurudisha mfumo wa kikabila,havikupewa nafasi.
Hata vilivyopo, ni kwa misingi ya chama tawala. Upinzani utakuwepo kuhakikisha wanaikosoa serikali kwa yale yasiyokuwa sahihi, na sera zenye mashiko. Sasa, wenye sera hizo, utakuta ni mtu anaehitaji kujenga jina kisiasa au kujipatia chochote tu.

Kama sijajibu vizuri uliza
 
Hizo picha sidhani kama sina cha kufanya, kwa sababu wanyarwanda wanachokiangalia ni umhimu wa fulani kwenye nafasi aliyo nayo.
Mtutsi anayesimamia haki, na mhutu anaesimamia wazo la kuua watutsi. Bora nani?

Hao inkotanyi, wawalipe tabasamu wauwaji?
So unaachivu nini kama watu wanakaa na kisasi si ni suala la muda tu yatatokea yale yale. Yaan kundi kubwa la watu wakae nje ya maamuzi halafu ujione uko salama. Unatengeneza aman bandia kwa kuwatisha watu. Ikotany ikiongozwa na kaberebe imeua wahutu milion 4 lakin kwasababu kwasasa ulaya na marekan iko upande wenu watu wanawaangalia tu. Lakin pia chanzo cha genocide nani asiyejua aliyesababisha kifo cha rais marehem
 
Una kila haki ya kuumia kwa sababu marehemu raisi alitaka kutengeneza kizazi kisicho na chimbuko. Alichokitoa, ndo alichokipata.

Kisasi hicho lazima watu wawe nacho, na ndo maana serikali inalazimika kuwa karibu na kutoacha mianya ya kulipiza visasi hivyo, bali kuendelea na safari ya kuelimisha watu kuuhusu madhara ya visasi hivyo
 
Maoni yao ni kwamba hizo ni ndoto, na mwenye wazo hilo ni mjinga.
Sio ndoto na nina imani wananchi mtafurahia uhuru mlioukosa.
Mtapanda boti na kwenda Zanzibar bila kuulizwa, mtakuja Kilimanjaro mtaoa na kuolewa nk.... Hili ni jambo zuri hebu lifikirieni.
Rais wenu wa sasa atakua moja ya mawaziri wa Tanzania au atakua jeshini kutusaidia mbinu mbalimbali
 
1. Sijui

2. Rwanda shule ya msingi ni miaka 6, sekondali miaka 6(O level miaka 3 na A level miaka 3) Kwa sasa kuna kitu kinaitwa 9 years Basic Education. Unasoma shule ya msingi miaka 6, na 3 ya O level sehemu moja.
Kwingine ni 12 years Basic Education. Yaani miaka yote 12 unasomea sehemu moja.

Elimu kwa ujumla imekumbwa na changamoto ya mfumo. Zamani, kulikuwa na mfumo wa kifaransa, badae ukageuzwa kuwa wa kiingeleza. Hivyo, waliokuwa wakisoma mfumo wa kifaransa, walipata changamoto ya kuadapt lugha.
Mbali na hilo, uongozi wa Wizara unaokuja, unakuja na mapya yake. Labda vyuo vikuu, na kwenyewe badhi ya sections furani, kama sheria, nursing,ICT, ndo unakuta wameiva sana.

Ila wasomi wengi, wapo chini ya kiwango

3. Mfumo wa matibabu, wanywarwanda wamegawanywa katika makundi 4 kulingana na uwezo wao. Kundi la kwanza, linasaidiwa na serikali kulipiwa.
Kundi la pili na la tatu, kila kichwa cha familia ni Faranga elfu 3(karibia elfu 6 ya Tanzania). Kundi la 4 ambalo ni la watu wenye uwezo wa juu, kila kichwa cha familia ni elfu 7(Karibia 14 ya kitanzania).

Kwa ujumnla, upatikanaji ni rahisi, kwa sababu kila raia ana access kwa daktari. Na kabla hujafika huko, nchi nzima kuna wahudumu wa afya, kila kitongoji, ukijisikia vibaya unamuona. Huduma za kwanza wanatoa, na dose kama za malaria na magomnjwa madogo madogo unapata hapo hapo. Ikiwa ni kesi iliyo nje ya uwezo wao, kuna zahanati za kata. Hapo wakiferi, unaenda kituo cha afya. Kesi yako ikiwa kubwa, unapewa referal kuelekea Hospitali ya wilaya.
Kwa hiyo kuna bima ya afya ya Pamoja(CBHI Community Based Health Insurance), na bima za mashirika. So, ukienda kwa ajili ya matibabu, unalipia 10% ya gharama zote, hata ulazwe miaka 10.

uongozi wa wilaya ukibainisha mtu hana uwezo, serikali inaghalamia 100%

4. Rwanda, madini yapo. Kuhusu labda tetesi za wanaossema ya DRC. Hilo sitoliingilia, lakini inawezekanaje mashariki ya Congo yote iwe na hizo ressources, then zisivuke mpaka! Sema tu kwa kuwa ni nchi ndogo, na technologia labda isiwe kubwa kama ya migodi ya kifahari, na uchimbaji wake ni wa masharti, lakini madini yote yapo. Labda nitafute majina.

5. Umasikini naouongelea, ni hatua ya maendeleo ukilinganisha na nchi jilani zilizotangulia, au na maisha kwa ujumla. Uwekezaji kwa timu za nje, ni kwa ajili ya kuhamasisha watu kuja kuwekeza ndani na kutengeneza ajira. Jambo hilo linasaidia kupunguza ukosefu wa ajira. Pia, ukilinganisha na nchi jirani,fursa za kimaisha ni tofauti na za nchi hizo. Hivyo,niseme ni nchi ambayo inajijenga, miaka 30 ni muda mfupi sana kuweza kufikia hatua za waliokutangulia.

6. Rwanda mgao wa umeme hakuna. Inaweza tokea labda kama kuna marekebisho. Vijini umeme unasambazwa, nadhani kwa sasa wanyarwanda 70% au zaidi kidogo wana umeme. Kukatika ni kama 5%

7. Nahisi uchawa unamaanisha kujipendekeza: Rwanda unalipwa kwa kile ulichokifanya na chenye manufaa kwa jamii.
Ukizingatia, ni nchi cganga,chama tawala cha RPF ndo kimekuwepo kuhakikisha kila jambo linatekelezwa. Vyama vya upinzani, vingi vilionekana kutaka kurudisha mfumo wa kikabila,havikupewa nafasi.
Hata vilivyopo, ni kwa misingi ya chama tawala. Upinzani utakuwepo kuhakikisha wanaikosoa serikali kwa yale yasiyokuwa sahihi, na sera zenye mashiko. Sasa, wenye sera hizo, utakuta ni mtu anaehitaji kujenga jina kisiasa au kujipatia chochote tu.

Kama sijajibu vizuri uliza

Umejibu vizuri mkuu., ahsante.

-Je Kiswahili ni mojawapo ya masomo yanayofundishwa shuleni?

-Makala yako (nyuzi zako) nyingi humu JF huwa unaandika kwa Kinyarwanda, kwa nini usiwe unaandika kwa Kiswahili au Wanyarandwa Kiswahili kwao sio kipaumbele?

-Vyakula maarufu huko Rwanda ni vipi?
 
Una kila haki ya kuumia kwa sababu marehemu raisi alitaka kutengeneza kizazi kisicho na chimbuko. Alichokitoa, ndo alichokipata.

Kisasi hicho lazima watu wawe nacho, na ndo maana serikali inalazimika kuwa karibu na kutoacha mianya ya kulipiza visasi hivyo, bali kuendelea na safari ya kuelimisha watu kuuhusu madhara ya visasi hivyo
Tukiachana na mengine kama hayo vp kuhusu suala la PK kuogopeka hasa ndani ya Rwanda kuwa ni rahisi kumtukana Mungu (kwa wenye iman na mambo ya uwepo wake) ila ikawa ni kawaida ila sio kumsema kwa mabaya PK pia kuwa mkosoaji wa utawala wake,

Ninyi kama watu wa taifa hilo mnazungumziaje suala la PK kuwaua na kuwapoteza watu wanaokitaka kiti chake mfano yule binti aliyeuawa miaka ya hivi karibuni je, mambo kama hayo yanawafurahisha ama ndio hamna pa kusemea???

Pia unazungumziaje suala la PK kufungia makanisa je, kwenu Raia linawafurahisha na adhma yake ni kupambana na watu ambao huenda wana plans na agenda zao tofauti na mambo ya uinjilisiti ama movement za kisasi kwa jamii zinaupinga utawala wa PK na wanyarwanda zinaweza kuanzia huko ndio maana anazuia makanisa kuwepo kwa wingi???
 
Dah!
Mkuu, mi nianze kwa kukupa pole. kwa sababu, haya matango ya kulishwa kwenye media na vyombo vya habari, ndo yanaonekana yana nguvu kuliko uhalisia.
Nianze na huyo binti:
Binti unaemsema, anatokea familia ya tajiri mkubwa miongoni mwa wengine nchini Rwanda.
Dada yake ndo aliejitokeza kugombea urais.
Vitu vingine, tusiwe na ushabiki wa kijinga.
Vigezo vya kugombea, kila nchi inavyo vya kwake.
Rwanda, kosa la kugushi, adhabu yake ni miaka 7 jera. Nadhani alikutwa na saini za watu ambao ni marehemu. Hajawahi kuhukumiwa, jina lake ni Diane Rwigara.
Aliefaliki, ni mdogo wake, anaitwa Anne Rwigara. Sasa, wewe hapa unaemzungumzia, ni mdogo mtu, ambae hakuhusika na mambo ya uchaguzi. Usikalilishwe, ukiwa na interets na kitu, fanya tafiti za kutosha.

Kuogopeka, ukiachana na kuwa ni rais, na maadili, mzazi wako kama huwezi kumkosea heshima, iweje umkosee heshima mzazi wa mtu mwingine?
Rais Samia, aliwahi kusema kwamba anaweza akakusamehe na akapotezea, lakini wasaidizi wake wakakushughulikia.
Je, kila mtu akimchukulia na kumsema anavyotaka rais, hiyo itakuwa nchi au sehemu tu ya wahuni?
Je, hao wanaokitaka kiti alichokalia, wanakitaka kwa lipi walilofanyia taifa labda? mtu hata alikozaliwa, hajulikani,hata shamba hana, from nowhere anataka kiti cha rais!

Linakuingia akilini kweli? Rwanda haiendeshwi kimasihara,
Rwanda ni nchi ambayo raia wake wengi walikufa wakafufuka, Rwanda ni nchi inayojua kila aina ya huzuni na chozi, hivyo si sehemu ya kuchezea danadana.
 
Umejibu vizuri mkuu., ahsante.

-Je Kiswahili ni mojawapo ya masomo yanayofundishwa shuleni?

-Makala yako (nyuzi zako) nyingi humu JF huwa unaandika kwa Kinyarwanda, kwa nini usiwe unaandika kwa Kiswahili au Wanyarandwa Kiswahili kwao sio kipaumbele?

-Vyakula maarufu huko Rwanda ni vipi?
-Kiswahili si moja wapo wa masomo yanayofundishwa, kwa sababu walimu wa kiswahili si wengi, au hawapo.
Kiswahili wanafundishwa wanaosoma option ya Lugha huko sekondari. Kiswahili cha darasani, ni tofauti sana na cha kuongea. Hivyo, mwalimu wa kiswahili Rwanda, akifika Tanzania anaweza akapotea na asiweze kupata huduma yoyote.

-Nyuzi zangu za kinyarwanda, ukiangalia, utakuzikuta kwenye jukwaa la Rwanda. ni jukwaa ambalo lipo kwa ajili ya lugha ya kinyarwanda. Hii, ni kwa sababu JF ni mtandao wa kimataifa, na hasa kwa nchi jirani. Kinyarwanda, rwanda na Burundi wanaelewa.
Lakini, issue yoyte inayohusu Rwanda, mfano wa hii hapa, utazikuta International forum. Kwa yeyote anaetaka kujua chochote, anaweza kuuliza na atajibiwa.

Kiswahili cha wanyarwanda, asilimia kubwa sana ni kama cha DRC, utakuta kinajumuisha zaidi ya lugha moja. Kwa ujumla, wengi wanaweza kusom na wasielewe.
Kwa sasa ndo serikali inasisitiza watu wajifunze, ili waweze kuwa na ujuzi wa ziada kimawasiliano.

-Vyakula vya Rwanda, kuna ndizi, wali, viazi,mbatata na vitamu,maharage, mihogo, ugali wa mahindi(Sembe), dona huwezi kupata labda usage mwenyewe, ugali wa mhogo, vitu kama hivyo. Nakorokolo mengi yaliopo TZ, Rwanda hayapo.
 
Back
Top Bottom