Uliza chochote kuhusu Rwanda

Uliza chochote kuhusu Rwanda

Nikiwa mtanzania naweza kufanya kazi au kuajiriwa na serikali ya Rwanda? vip kama sifaham kinyarwanda ntawezaje kuwa na marafiki huko Rwanda? Je, kama anaitaji Shori wa kudate naye huko Rwanda on line nampataje? Je Rwanda nako kuna wauwaji wasiojulikana kama Tanzania?Vip swala la usalama wa raia na mali zao upo wa kutosha? Nikiwa kama mgeni huko Rwanda ni sehemu gani salama ya kufikia? vip swala la dini, dini ipi inaongoza? Ni sehemu ip kwa Rwanda sio salama kwa Raia kwamaana vibaka,wezi na majambazi ndo kambi zao? Vip Wanyarwanda ni wabaguzi kwa raia wa nchi nyingine? Biashara gani ambayo inatoka kwa wingi huko Rwanda? Sehem gani ya Rwanda unaweza pata huduma ya sex chap kwa haraka ukaendelea na mishe zako? vip usalama wa barabarani?
jibu haya maswali mtoa mada.
 
Ntakujibu kwa ninavyoelewa mimi( si precision ya 100%):

1. Si kweli. kwa sababu mifano ya taasisi zenye wasomi wa mfumo wa Kifaransa, ambao walio wengi ni wale wajulikanao kama wahutu, zipo. Mfano wa Rwanda Revenue Authority, na sehemu nyingine zinazohusika na pesa. Hawa, wana nidhamu ya hali ya juu. Si watu wa kukaa na kusubiri mshahara.

2. Si kweli kwa sababu ukifatilia, utagundua vigezo vinavyotumika kuweka watu kwenye makundi hayo ya ukabila, kila upande vipo. Utampata mtutsi mfupi, kiujumla zile sifa za watutsi hana. Na mhutu, utakuta ana kila sifa ya mtutsi. Na mbali na hilo, kwa sasa hivi ni ngumu, kwa sababu watu wanazaliana.

mfano mwingine, wanawake waliobakwa na Interahamwe mwaka 1994, ni watutsi, lakini wamezaa wahutu(kwa tunavoelewa kwamba mtoto ni kabila la baba'ke). Hawa, mbona wapo kwenye hizo ngazi?

3. Hata nyumbani kwako, huwezi kumuamini sana mjakazi kuliko mke wa ndoa. Hivyo,kutokana na historia ya nchi yenyewe, kuna watu wanaujua uchungu wa maisha kuliko wengine.
Hii comment imetosha kuniambia wewe ni mtutsi unayeipigia promo/debe Rwanda kwa uovu inaoufanya DRC.
 
Mimi kama mgeni nataka kuja kutembelea rwanda.
Niandae kiasi gani kuanzia kula,guest na bata.

Na vipi kuhusu usalama,siwezi kufananishwa na mhutu au tutsi nikachinjwa?
 
Binafsi nawapenda sana wanyarwanda kwa sababu ya wanamshikamo sana kuliko hata watanzania, japo napenda sana Wanyarwanda kwa sababu ya ukalimu wao na vile walivyo wazalendo wa nchi yao. Sijawahi kuona mnyarwanda asopenda nchi yake . Hongereni sana .Fauka ya hayo nina vimaswali kidogo hivi,
1. Mapema mwaka 2017 tulisikia katika vyombo vya habari wanajeshi zaidi Ya 800 waliachishwa na August 2024 tukasikia maafisaa 216 wamefukuzwa Kutoka RDF bila kutolewa sababu za kufukuzwa baada muda mfupi tukasikia Tena M23 imeanzisha mapambao dhidi ya Jeshi la Congo huko Goma . Kutokana na hali hiyo;
Je, ni kweli kwamba Jeshi la Rwanda linatoa support kwa M23?
Je, wanajeshi waliofukuzwa Huko Rwanda ndio hao M 23?
Ili nchi ipate Maendeleo ni muhimu sana kudumisha amani na majirani zake ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kufanya biashara , je, kwa nini Rwanda hawapendi kudumisha amani na usalama dhidi ya Congo, Rwanda, Burundi, Uganda?
 
Nikiwa mtanzania naweza kufanya kazi au kuajiriwa na serikali ya Rwanda? vip kama sifaham kinyarwanda ntawezaje kuwa na marafiki huko Rwanda? Je, kama anaitaji Shori wa kudate naye huko Rwanda on line nampataje? Je Rwanda nako kuna wauwaji wasiojulikana kama Tanzania?Vip swala la usalama wa raia na mali zao upo wa kutosha? Nikiwa kama mgeni huko Rwanda ni sehemu gani salama ya kufikia? vip swala la dini, dini ipi inaongoza? Ni sehemu ip kwa Rwanda sio salama kwa Raia kwamaana vibaka,wezi na majambazi ndo kambi zao? Vip Wanyarwanda ni wabaguzi kwa raia wa nchi nyingine? Biashara gani ambayo inatoka kwa wingi huko Rwanda? Sehem gani ya Rwanda unaweza pata huduma ya sex chap kwa haraka ukaendelea na mishe zako? vip usalama wa barabarani?
Ukiwa Mtanzania, kama una ujuzi flani ambao kwa Rwanda una soko la ajira, utaajiliwa.
Kuhusu serikalini, itategemea na kitengo gani. Ila kwa sasa, kuhusu hilo sioni likiwa rahisi, kwa sababu Rwanda inasomesha watu kila nyanja,ili kuziba pengo la uhitaji wa watu kutoka nje.

Wanyarwanda hata kama kitu hawakijui, ila ukiwa mgeni wa lugha hata wao wanajitahidi kibubu bubu mnaenda tu.
Swala la kudate online hapo sielewi,ila kama nchi nyingine, hakika mtandaoni wapo, ila sasa, jiandae. Hao wenye uwezo huo, walishachangamka. Hao utawakoma.

Usalama wa watu na mali zao ni zaidi ya kitu kingine chochote nchini. Wanyarwanda, sawa vibaka wapo, ila ukipoteza kitu, ukiripoti kwa muda kinarudi. Pesa labda. kama ni ya mawazo,labda alieiba ametumia, hapo ni ngumu. Ila vitu vingine tangible, havipotei.
Rwanda hakuna sehemu isiyo salama, hasa kwa mgeni. kuhusu dini, wengi sana ni wakatoliki. Kigali mjini,maeneo ya uswahilini ndo kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na vibaka. Majambazi hakuna. Wanyarwanda si wabaguzi. Biashara ya vyakula ndo inaongoza. Sex kila semu utapa,kukiwa na lodge karibu ni uhakika.
Usalama wa barabarani ni wa uhakika. Ukijichanganya, hasa speed, camera zipo za kutosha, kama mgeni, deni lako utalikuta mpakani ukitoka. Kama unaendesha gari lililosajiliwa Rwanda, hapo hapo unapata sms ya kosa lako na faini yake.
 
Mimi ningependa kuuliza Rwanda kama naweza kupata mshirika wa kilimo biashara Rwanda hasa kwa mazao muhimu ila adimu Rwanda.Asante.
Ardhi Rwanda ni issue. Kilimo cha biashara, uhakika wa ardhi sidhani. Kupata heka nzima kwa pamoja si kazi ndogo, na ukiipata wakati mwingine ni maeneo ya marisho ya mifugo, na ni jimbo ambalo mvua si za kuaminika.

Ila, ukitafuta soko, unalima huku unawauzia,au wanakuja kuchukua wenyewe kama una mzigo.
Nyanya, nyingi hutoka Shinyanga, tikiti maji hutoka TZ, maembe,.....

Ila, unaweza pia fanya utafiti kuhusu uuzaji wa matunda na mbogamboga nje. Najua kuna certificates za exports, watu wanauza parachichi, asali, tikiti,mboga mboga huko Ulaya. na wanakusanya toka kwa wakulima.

Hakuna kitu kisicho adimu, kwa sababu uhitaji wa vitu bado mkubwa. Changamoto inakuja tu pale ambapo huwezi jipangia bei wewe, vitu vingi vina bei elekezi.
Na jiandae kutumia mashine ya risiti hata kama unauza mgahawa.
 
Mimi kama mgeni nataka kuja kutembelea rwanda.
Niandae kiasi gani kuanzia kula,guest na bata.

Na vipi kuhusu usalama,siwezi kufananishwa na mhutu au tutsi nikachinjwa?
Hhahahahahaha niangue kicheko kwanza.

Upuuzi wa wahutu na watutsi utauona mtandaoni tu. Watu nchini hawana hayo mambo. Na mgeni ana thamani kuliko raia sasa,ulijue hilo. Police na vyombo vingine vya usalama vipo makini zaidi ya sana,

Itategemea na utakaa muda gani. Lodge za kibongo kama ya elfu 20, kule ni Hoteli ya kifahari huiwezi. Inayojitahidi kule, utapata kama elu 20 au 15 ya kitanzania, lakini ni kama gesti bubu. Maji mnayonunua Dar kwa sh 700, ukiwa Rwanda ni kama Sh 2000. Kwa hiyo, gharama za vitu zimechangamka tofauti na Tanzania.
 
Binafsi nawapenda sana wanyarwanda kwa sababu ya wanamshikamo sana kuliko hata watanzania, japo napenda sana Wanyarwanda kwa sababu ya ukalimu wao na vile walivyo wazalendo wa nchi yao. Sijawahi kuona mnyarwanda asopenda nchi yake . Hongereni sana .Fauka ya hayo nina vimaswali kidogo hivi,
1. Mapema mwaka 2017 tulisikia katika vyombo vya habari wanajeshi zaidi Ya 800 waliachishwa na August 2024 tukasikia maafisaa 216 wamefukuzwa Kutoka RDF bila kutolewa sababu za kufukuzwa baada muda mfupi tukasikia Tena M23 imeanzisha mapambao dhidi ya Jeshi la Congo huko Goma . Kutokana na hali hiyo;
Je, ni kweli kwamba Jeshi la Rwanda linatoa support kwa M23?
Je, wanajeshi waliofukuzwa Huko Rwanda ndio hao M 23?
Ili nchi ipate Maendeleo ni muhimu sana kudumisha amani na majirani zake ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kufanya biashara , je, kwa nini Rwanda hawapendi kudumisha amani na usalama dhidi ya Congo, Rwanda, Burundi, Uganda?
Ntakujibu mimi kama mimi sijibu kwa niaba ya serikali:

1. Wanajeshi ni ibinadamu kama wengine. Jeshini,kosa vyote, siyo nidhamu. Rwanda bila kujali una cheo gani, ukilalamikiwa, hasa na raia, na kweli ukakutwa na hatia, ndo imeisha hiyo. Kwa hiyo, wanajeshi kufukuzwa kazi ni jambo la kawaida.

Jeshi la Rwanda kusupport M23 ndo sijui. Kilichopo labda kama kuna mwanajeshi, inasemekana waliweka mbinu za kiusalama(Security measures) kulinda mipaka ya nchi. Inasemekana zinaweza kuwa ndani au nje ya mipaka.

Lakini pia, kumbuka M23 ni wanyarwanda wa Congo, ambao uraia wa Congo waliupata kutokana na mipaka ya wakoloni. Hivyo,kuoana na kuzaliana na kutembeleana, kulibaki pale pale.

N nadhani mpaka sasa kinachowachanganya wengi, ni kutofautisha wanajeshi wa Rwanda na wa M23 ukiacha uniform. M23 wanaongea kinyarwanda. Sawa na masai wa Kenya na Tanzania. Ukiambiwa tofautisha, sidhani kama unaweza.

M23 ni watu waliokimbia mauaji dhidi ya watutsi huko miaka ya 1995 na kuendelea. Wapo wanaume, na watoto wao.
Kwa sababu wengine walikuwa ndani ya jeshi la serikali, baada ya kuona serikali imekalia kimya mauaji hayo, waliamua kusaliti jeshi lao na kujiunga.

M23 ya leo ni muungano wa makundi tofauti tofauti, yaliyokuwa na nia ya kupigania haki za watu wao waliokuwa wakiuliwa huko mashariki mwa DRC.

Kwenye swala la kudumisha amani, bado sijakubaliana na wewe kwa kauli hiyo:

Nianze na Uganda: Katika vita vya pili vya Congo, Rwanda na Uganda walikiwasha, na inasemekana Uganda ilipoteza sana, ikahapa kulipiza kisasi kwa kuivvamia Rwanda. Rwanda haikuwa na namna, lazima ijilinde

Kuhusu Congo: Machafuko yote unayoyaona, yameanza baada ya interahamwe kukimbilia Congo. Walipokuwa huko, walijipanga na kuivamia Rwanda, mara kadhaa, na walifanikiwa,na kila mara,waliua. Serikali ya Rwanda ilikuwa ikiomba DRC iwachukulie hatua, ilishindikana. Na ndo kikawa chanzo cha wahutu hao, kuyavamia makazi ya watutsi huko DRC, na kuanza kuwaua na kuchoma nyumba zao. Mpaka leo hii, wakimbizi wa mambo hayo, wapo Rwanda na Burundi, na nahisi Tanzania wanaweza wakawepo.

Kuhusu Burundi, mzozo ulianzia hapa: 1994 wakati wa mauaji dhidi ya watutsi, kuna wakimbizi wa kihutu walikuwa nchini Rwanda. hawa walisaidia Interahamwe za Rwanda kuua watusti. Badae serikali ya Rwanda ikatoa list ya watu hao, wakamatwe na washitakiwe, serikali ya Burundi ikauchuna. Ambapo utasikia kuna watu walihusika na kutaka kupindua serikali mwaka 2015, wakakimbilia Rwanda, na yenyewe ikakumbushia. Sasa mtihani ukawa hapo. Burundi tuliokuomba uwashughulikie, ulikataa. Leo hii, unataka tukupe unaowataka wewe. Haikuwezekana na kuanzia hapo, mahusiano yakaharibika.
Pia, kwa sasa, FDLR inasaidiwa na serikali ya Congo. Hivyo yeyote anayesaidia jeshi la Congo, ni mshirika kuisaidia FDLR.
Burundi ikiwa mstari wa mbele. Hapo hayo mahusiano mazuri yatatoka wapi?

Lakini pia, kumbuka, Burundi ndo ilifunga mipaka, siyo Rwanda.

Navyosikia, vitu vinavyoendelea huko kijeshi, si mchezo. Ukifuatilia, FDLR mafunzo ni polii la Kibila upande wa Burundi. kwa maana, inawaunga mkono. Mahusiano mazuri yatatoka wapi!
Navyosikia, iwe hao wa Kibila au waliopo DRC, wanapata dose ya uhakika, na hakika kila mtu anajua aliefanya hivi atakuwa ni furani.

Kwa sasa, Burundi imeomba poo. Viongozi wa kidiplomasia wana vikao, ngoja tuone kitatokea kitu gani. Hapa M23 ndo inaenda kupakana na Burundi, ambayo ndo wanajeshi wake walikuwa wanaua ndugu zao. M23 na Burundi ujirani utakuwa wa style gani?
 
Back
Top Bottom