Uliza chochote kuhusu Rwanda

Uliza chochote kuhusu Rwanda

Teh teh teh teh teh teh teh !!! Kwa hiyo, mtanzania aliezaliwa Rwanda akija kwenu na kuongea Kinyarwanda, ataonekana mnyarwanda!

Japokuwa tukiachilia mbali mihemuko na roho mbaya, rwanda na Tanzania ni majirani, hivyo ...................................
Kumbe umezaliwa bongoland ndio maana. Vp mkuu huko mnasikiliza mziki wa bongo? Kama kweli ni wasanii gani wa bongo wanatamba sana huko?
 
. Karusisi: Hakuna mnyarwanda kwenye cheo chake ni mungu-mtu. Amekuwepo, ametekeleza majukumu yake, na wengine wanahitaji kupata uzoefu.
Sijui kitu gani unachokiita kutimua: Je, kama anakopelekwa kunahitaji mwenye uzoefu alio nao, au anatakiwa pia na yeye ajifunze mengine, atakuwaje ametimuliwa!!! Gashugi nae ana haki ya kuwa na madaraka kwenye nchi yake, kama amekidhi vigezo. Katoka sehemu moja, kahamishiwa kwingine, na baada ya muda atakabidhiwa mwingine.
Umejibu hili swali kisiasa.

Mwanajeshi huondolewa kwenye nafasi, aidha kwa kupandishwa cheo, ambapo tulitegemea Karusisi angepelekwa kuwa Leuitenant General au kupewa cheo cha kiraia kama ambavyo Paul Kagame amekuwa akifanya kwa zaidi ya miaka 20.

Hata hivyo, RDF ina Major Generals wasiopungua 18 ambao wangeweza kuongoza SOF, lakini kwanini kaamua kumpa nafasi hiyo Brigedier General ambaye ametokea kwenye Ukanali tu, tena mtu wa Military Intelligence???
Rwanda haiogopi kuwekewa vikwazo. Ni kweli msaada kama upo, ni msaada. Ila usipokuwepo, maisha yataendelea.
Mwaka 1994 Rwanda iliishi kwa msaada wa nani? Mara mia Tanzania iliyopokea wakimbizi, ikawapa hifadhi na mahitaji mhimu,itaheshimika miaka mia kuliko hao wa mbali, ambao misaada yao ina masharti.
Siyo rahisi kama unavyosema hapa. Asilimia zaidi ya 40% ya bajeti ya Rwanda inatokana na misaada ya nje. Mbadala wa misaada ya nje, siku zote ni FDI na International Trade. Ukilinganisha na majirani zake Rwanda wa EAC, Rwanda iko chini sana kwenye FDI ambapo ni asilimia 2.5% tu ya GDP, ambapo mataifa mengine masikini FDI imefika asilimia 3.8% ya GDP. Hizi ni takwimu za The Institute of Security Studies, kwenye ripoti yao ya mwaka 2023.

Leo mchana nimesikiliza hotuba ya Paul Kagame, ambapo kawaambia Wanyarwanda kile ambacho Mzee Nyerere aliwaambia watanzania mwaka 1980, kwamba "WAFUNGE MKANDA". Tena Paul Kagame naye kaongea kwa Kiswahili kabisa. Sasa kama misaada haina umuhimu hivyo kwanini kufunga mkanda ???
Nchi tajiri labda unaipima kwa vigezo gani!! Rwanda ni nchi inayojitafuta, siyo nchi tajiri. Japo pia si masikini kihivyo.
Rwanda ni nchi masikini. Unaposema siyo masikini kihivyo ilhali raia wake zaidi ya asilimia 50% wanaishi chini ya dola 1.1 moja kwa siku unamaanisha nini ???
GDP ipo kwenye Dola elfu moja na kitu
Rwanda bado haijafika kwenye Per Capita ya $ 1 kwa mtu.
 
Kumbe umezaliwa bongoland ndio maana. Vp mkuu huko mnasikiliza mziki wa bongo? Kama kweli ni wasanii gani wa bongo wanatamba sana huko?
Hahahahahahah

Miziki ya kibongo siyo kihivo, kwa sababu ya lugha, ni kusikiliza midundo.

Kwa wasanii wanaotamba, mara nyingi ni wale wa zamani, kina kuku kapanda baisikeli(Mr. Nice). Diamond yupo. Professor J, na Mbosso.

Binafsi, ananikosha RAIS wa KITAA. Mwamba nampa maua yake
 
Asante sana kwa majibu yako
Kwa mchele wa Tanzania, ni kati ya 2500 hadi 3200. Hizi ni Grade II na III, Grade I yenyewe haipo.

Kama ni mfanya biashara, cgangamkia fursa hii: Rwanda hapo mpakani kuna soko la kisasa. Mazungumzo baina ya uongozi wa wilaya za mpakani, wameamua kupeleka bidhaa za kitanzania sokoni humo, ila mfanyabiashara awe anafahamika kuepusha hali ya ujanja ujanja na kuweza kufatiliwa inapokuwa lazima. Hivyo, ukiwa na stock huko au mpakani upande wa Tanzania, uhakika wa kuuza upo.
 
Back
Top Bottom