Uliza chochote kuhusu Rwanda

Uliza chochote kuhusu Rwanda

Una chochote unachojiuliza kuhusu Rwanda?

Una chochote unachotaka kujua kiundani zaidi?

Una chochote ulichokisikia na bado umebaki njia panda!!

Iwe jambo la maana, iwe utani, iwe siasa, chochote, uliza utajibiwa hapa hapa.

Rwanda ndo nchi pekee barani Afrika, ukiingia huulizwi utakaa siku ngapi na unaenda kufanya nini. Kama unataka, funga mizigo yako hamia, kama una biashara yako, fanya, kama una ujuzi wako, omba ajira, ukipewa hakuna wa kuja kuuliza mbona huyu si mnyarwanda, kasoro serikalini tu. Ila na penyewe ikiwa una ujuzi ambao wanyarwanda hawana, kupata ajira ni simple.

Sehemu nzuri za kufanya utalii na kutembelea? Gharama zake roughly zikoje?
 
Sehemu nzuri za kufanya utalii na kutembelea? Gharama zake roughly zikoje?
Mbuga ya wanyama ya kutembelea, moja nzuri ni Akagera. Gharama za kuingia, kwa raia wa EAC, ni dola 16 za kimarekani. Hukokuna wanyama kama Serengeti(siyo Boy lakini).

Sehemu nyingine, ni Gorilla trecking, kwenye milima(Volcano) ya Musanze. Kuna pia Nyungwe Forest.

Gharama ni affordable(mi sijawahi kwenda, kiukweli siyo Hobby yangu), ntakuangalizia mtandaoni kama una interest.
 
Haya weweee
 
So unaachivu nini kama watu wanakaa na kisasi si ni suala la muda tu yatatokea yale yale. Yaan kundi kubwa la watu wakae nje ya maamuzi halafu ujione uko salama. Unatengeneza aman bandia kwa kuwatisha watu. Ikotany ikiongozwa na kaberebe imeua wahutu milion 4 lakin kwasababu kwasasa ulaya na marekan iko upande wenu watu wanawaangalia tu. Lakin pia chanzo cha genocide nani asiyejua aliyesababisha kifo cha rais marehem
Marehem huyu huyu inaesadikiwa kuwa serikali ya sasa ililikuta deni la mapanga ya kuwachinjia au? Kuna documents za ICTR hii habari iliandikwa kama sikosei
 
Hao wahutu Milioni 4 walitoka wapi? Acheni mihemko.
Rudia hesabu zako vizuri,tafuta rekodi za sensa ya mwisho kabla ya 1994.

Basi,kama wauaji wa wautu wameungwa mkono na nchi hizozisizotambua uhalali wa maisha ya watu, ni vyema.
 
Marehem huyu huyu inaesadikiwa kuwa serikali ya sasa ililikuta deni la mapanga ya kuwachinjia au? Kuna documents za ICTR hii habari iliandikwa kama sikosei
Serikali ni serikali tu. Deni utalipa hata kama hujui lilitoka wapi, kikubwa ushahidi uwepo. Unalipa tu.
Kuna mzee mmoja anaitwa Mironko, alisupply vifaa vya jeshi, kabla ya 1994. Aliifungulia kesi serikali ya RPF, ilimlipa.
 
1.Kwanini mr.p.
Anaomba kuhifadhi wageni wapya tena wa rangi nyeupe kutokea nchi za mbaali saana,
Japo kua rwanda ni nchi ndogo saana tena ilojawa na wakimbizi mipakani mwa nchi jirani kama Tanzania.
2. Kwanini asiwakusanye wenye asilia makambini na kuwaleta pamoja kuijenga Rwanda moja?
 
jibu no.2 nitakupinga kidogo, uzoefu wa vita wa jwtz ni mkubwa kuliko hata wa rwanda, nisiingie sana ndani ila ukweli huo unaujua ww mwenyew..hilo jeshi la rwanda limepigana vita gani zaidi ya hayo makundi ya uasi?? toa mfano jeshi la rwanda limeshinda vita gani
Ngoja na mimi nichangie kidogo "Betason" , Tanzania mara ya mwisho imepigana vita 1978, Hii ni zaidi ya miaka 40 iliyopita. Askari aliekuwa na miaka 20-30 ameshastaafu. Kwa ufupi ni kwamba askari wote wa sasa wa jwtz hawajapigana vita yoyote. Jeshi la Rwanda halijawahi kutulia liko vitani tangia mwaka 1994 mpaka leo hii.
 
Kariakoo haina kifani mkuu, hakuna sehemu ya kuifananisha nayo. Kigali mjini kuna kaeneo kadogo sana. Ukitembea,ndani ya nusu saa mitaa yote umeimaliza, kanaitwa Matheus. Ndo hapo vitu vinavyopatikanaga.
Asante boss
 
Ntakujibu mimi kama mimi sijibu kwa niaba ya serikali:

1. Wanajeshi ni ibinadamu kama wengine. Jeshini,kosa vyote, siyo nidhamu. Rwanda bila kujali una cheo gani, ukilalamikiwa, hasa na raia, na kweli ukakutwa na hatia, ndo imeisha hiyo. Kwa hiyo, wanajeshi kufukuzwa kazi ni jambo la kawaida.

Jeshi la Rwanda kusupport M23 ndo sijui. Kilichopo labda kama kuna mwanajeshi, inasemekana waliweka mbinu za kiusalama(Security measures) kulinda mipaka ya nchi. Inasemekana zinaweza kuwa ndani au nje ya mipaka.

Lakini pia, kumbuka M23 ni wanyarwanda wa Congo, ambao uraia wa Congo waliupata kutokana na mipaka ya wakoloni. Hivyo,kuoana na kuzaliana na kutembeleana, kulibaki pale pale.

N nadhani mpaka sasa kinachowachanganya wengi, ni kutofautisha wanajeshi wa Rwanda na wa M23 ukiacha uniform. M23 wanaongea kinyarwanda. Sawa na masai wa Kenya na Tanzania. Ukiambiwa tofautisha, sidhani kama unaweza.

M23 ni watu waliokimbia mauaji dhidi ya watutsi huko miaka ya 1995 na kuendelea. Wapo wanaume, na watoto wao.
Kwa sababu wengine walikuwa ndani ya jeshi la serikali, baada ya kuona serikali imekalia kimya mauaji hayo, waliamua kusaliti jeshi lao na kujiunga.

M23 ya leo ni muungano wa makundi tofauti tofauti, yaliyokuwa na nia ya kupigania haki za watu wao waliokuwa wakiuliwa huko mashariki mwa DRC.

Kwenye swala la kudumisha amani, bado sijakubaliana na wewe kwa kauli hiyo:

Nianze na Uganda: Katika vita vya pili vya Congo, Rwanda na Uganda walikiwasha, na inasemekana Uganda ilipoteza sana, ikahapa kulipiza kisasi kwa kuivvamia Rwanda. Rwanda haikuwa na namna, lazima ijilinde

Kuhusu Congo: Machafuko yote unayoyaona, yameanza baada ya interahamwe kukimbilia Congo. Walipokuwa huko, walijipanga na kuivamia Rwanda, mara kadhaa, na walifanikiwa,na kila mara,waliua. Serikali ya Rwanda ilikuwa ikiomba DRC iwachukulie hatua, ilishindikana. Na ndo kikawa chanzo cha wahutu hao, kuyavamia makazi ya watutsi huko DRC, na kuanza kuwaua na kuchoma nyumba zao. Mpaka leo hii, wakimbizi wa mambo hayo, wapo Rwanda na Burundi, na nahisi Tanzania wanaweza wakawepo.

Kuhusu Burundi, mzozo ulianzia hapa: 1994 wakati wa mauaji dhidi ya watutsi, kuna wakimbizi wa kihutu walikuwa nchini Rwanda. hawa walisaidia Interahamwe za Rwanda kuua watusti. Badae serikali ya Rwanda ikatoa list ya watu hao, wakamatwe na washitakiwe, serikali ya Burundi ikauchuna. Ambapo utasikia kuna watu walihusika na kutaka kupindua serikali mwaka 2015, wakakimbilia Rwanda, na yenyewe ikakumbushia. Sasa mtihani ukawa hapo. Burundi tuliokuomba uwashughulikie, ulikataa. Leo hii, unataka tukupe unaowataka wewe. Haikuwezekana na kuanzia hapo, mahusiano yakaharibika.
Pia, kwa sasa, FDLR inasaidiwa na serikali ya Congo. Hivyo yeyote anayesaidia jeshi la Congo, ni mshirika kuisaidia FDLR.
Burundi ikiwa mstari wa mbele. Hapo hayo mahusiano mazuri yatatoka wapi?

Lakini pia, kumbuka, Burundi ndo ilifunga mipaka, siyo Rwanda.

Navyosikia, vitu vinavyoendelea huko kijeshi, si mchezo. Ukifuatilia, FDLR mafunzo ni polii la Kibila upande wa Burundi. kwa maana, inawaunga mkono. Mahusiano mazuri yatatoka wapi!
Navyosikia, iwe hao wa Kibila au waliopo DRC, wanapata dose ya uhakika, na hakika kila mtu anajua aliefanya hivi atakuwa ni furani.

Kwa sasa, Burundi imeomba poo. Viongozi wa kidiplomasia wana vikao, ngoja tuone kitatokea kitu gani. Hapa M23 ndo inaenda kupakana na Burundi, ambayo ndo wanajeshi wake walikuwa wanaua ndugu zao. M23 na Burundi ujirani utakuwa wa style gani?
Asante sana boss, Swali jingine,
Inasemekana Rwanda Kuna soko kubwa sana la Pumba za alzet pamoja mafuta ya kupikia ya alzet?
 
Asante sana boss, Swali jingine,
Inasemekana Rwanda Kuna soko kubwa sana la Pumba za alzet pamoja mafuta ya kupikia ya alzet?
Hata alizeti yenyewe ina soko. Kuna kiwanda cha kukamua mafuta,alizeti na soya, japo huko alizeti hailimwi. Pumba hizo hutumika pia kutengeneza sabuni za miche.
 
Una chochote unachojiuliza kuhusu Rwanda?

Una chochote unachotaka kujua kiundani zaidi?

Una chochote ulichokisikia na bado umebaki njia panda!!

Iwe jambo la maana, iwe utani, iwe siasa, chochote, uliza utajibiwa hapa hapa.

Rwanda ndo nchi pekee barani Afrika, ukiingia huulizwi utakaa siku ngapi na unaenda kufanya nini. Kama unataka, funga mizigo yako hamia, kama una biashara yako, fanya, kama una ujuzi wako, omba ajira, ukipewa hakuna wa kuja kuuliza mbona huyu si mnyarwanda, kasoro serikalini tu. Ila na penyewe ikiwa una ujuzi ambao wanyarwanda hawana, kupata ajira ni simple.
Naomba kujua madhebu ya paul kagame,maana wengine wanasema msabato,wengine mkatoliki
 
Vipi kuhusu bidhaa za electronics kama simu, Tv, Laptop, printer na photocopy machine nasikia vina bei rahisi ukilinganisha na Tanzania?
 
Back
Top Bottom