Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Hiyo stori hapo mwisho mbona kama ya kizushi Mkuu! Miaka hiyo ndio zilikuwa pande zangu hizo na kulikuwa na Baa inaitwa "Igongwe" hapo Mwenge kwa wachonga vinyago ikitazamana na uwanja wa mpira hapo.
Nilichanganya jina; baa hiyo ni Igongwe ndiyo iliyoleta. Mmiliki wake zamani alikuwa mama fulani wa Iringa; alikuwa na binti wawili ambapo mmoja wao alikuwa kibindoni mwangu! Sijui kama tulikuwa tunashea.

Wakati Mayaula analetwa baa iyo ilikuwa imekodishwa na jamaa anaitwa Sharifu, nadhani alikuwa mme wa Balozi Majaar ambaye mdogo wake alichukua taji la Miss Tanzania enzi hizo.
 
Ni wimbo wa "The Beat Masters" na unaitwa "Warm Love"

Hizi ngoma za zamani ngumu sana kuzipata hasa kwa kuwa nyingi hazijawahi pandishwa mitandaoni. Ninazo nyingi sana nilizorekodi na kujaribu ku_shazam bila mafanikio.

Bahati mbaya nyingine ni wale ma_Dj wanaogonga hizi nyimbo hawataji majina,ni wachache sana wanaofanya hivyo. Huu baada ya kuutafuta muda mrefu sana, siku moja kwenye "Mtaa wa Mangoma" na "Dj JD" aliutaja jina lake. Tangu hapo sijawahi kuusahau.
Mkuu UMETISHAA

Yaani nimeutafuta huu wimbo mwaka wa 4 sasa kila nikiusikia radioni niki Shazam holaaaa
Pale mtaa wa Magoma Dj Titna hatajagi kabisa majina anatwanga tu

Hilo songi linanikumbusha enzi za ujana wangu pale Tanga kuna ukumbi ulikua unaitwa LIMBACHIA tulikua tunatoroka maskani na washkaji tunaenda kujiarusha

Thanks 🙏
Nimeupakua Mjini Youtube
 
Mkuu UMETISHAA

Yaani nimeutafuta huu wimbo mwaka wa 4 sasa kila nikiusikia radioni niki Shazam holaaaa
Pale mtaa wa Magoma Dj Titna hatajagi kabisa majina anatwanga tu

Hilo songi linanikumbusha enzi za ujana wangu pale Tanga kuna ukumbi ulikua unaitwa LIMBACHIA tulikua tunatoroka maskani na washkaji tunaenda kujiarusha

Thanks 🙏
Nimeupakua Mjini Youtube
Safi sana. Hizi ngoma licha ya kuburudisha pia zinakumbusha mbali sana. Basi hata mimi nina vipande vya nyimbo kwenye memory yangu miaka sasa nahangaika kutafuta majina.
 
Mwanzoni mwa miaka ya sabini, Verckys Kiamangwana Mateta alitunga wimbho uliojulikana kama "Nakomitunaka" uliopata umaarafu sana lakini ukpingwa sana na kani katoliki kwa vile ulikuwa unauliza kwa nini sanamu za yesu, malaika na mitume zilikuwa za watu weupe lakini sanamu za shetani zilikuwa za watu weusi. Wimbo huo original uliimbwa na Pepe Kalle wakati angali Ochestra Veve ni huu hapa

View: https://www.youtube.com/watch?v=DcW40E-rRxQ

Jamaa hawa wamejitahidi kutafsri msitali mmoja mmoja kwenye wimbo huo


View: https://www.youtube.com/watch?v=HnoGOdpWFRE

Wanamuziki wa zamani walikuwa wanajua sana kuangalia mambo ya kijamii kwa ndani sana kuliko hawa wa leo
 
Kuna Mnigeria huyu kwa jina la Onyeka Onwenu ambaye amefariki mwaka jana. Alivuma kwa muda mrefu sana ila kwenye miaka ya themanini alitoa wimbo wa "Ekwe" uliotawala la anga la Afrika. Wewe uliusikia wimbo huo kwa mara ya kwanza ukiwa wapi?


View: https://www.youtube.com/watch?v=9_Vu19wiDC0
Mkuu nimesuuzika roho pakubwa sana kwa wimbo huu. nimeutafuta sana wimbo huu. ubarikiwe sana.
 
Uzi mzuri sana, nimesikia baadhi ya nyimbo za watu wa zamani..

Kweli ni old days, wengine hatukuwepo, tumekua tunazikuta tu.
 
Kumbe humu tupo na wazee hivi aisee kama ndo hivyo basi mi najitoa JF
Hapana; usijitoe, bali uwe unajadili mambo kwa heshima ukitumia lugha za kistaarabu. Usifanye hapa Instagram au facebook
 
Haddaway yeye alihit na nyimbo moja tuu. "What's Love" akapotea.
Nakuwekeeni mashairi hapa chini.
 

Attachments

  • Haddaway - What is Love -with lyrics-.mp4
    6.2 MB
Back
Top Bottom