Nini kilikuvunja moyo ulipofika Dar es Salaam kwa Mara ya kwanza?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,855
NINI KILIKU- DISAPPOINT ULIPOFIKA DSM KWA MARA YA KWANZA?

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Huenda uligugumia kimoyomoyo na hukumwambia yeyote. Ulijakaza kisabuni ili mwenyeji wako asigundue hila ya moyo wako. Jinsi matarajio yalivyoangusha shukrani zako. Najua. Na kama utanibishia shauri yako.

Mdogo wangu kanifurahisha sana. Alikuja DSM kunitembelea na hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kuja Dar. Na mimi ndiye Kakaake. Hadithi yake ikanikumbusha miaka 15 iliyopita wakati nami ndio nakuja Dsm.
Wala sitaki kumuona dogo anatabia mbaya kwa sababu hali hiyo hata mimi ilinikuta miaka hiyo nilipofika Dar kwa mara ya kwanza.

Ile picha ambayo wachungaji wanawaambia waumini wao kuhusu mbinguni basi ndio picha ambayo sisi watoto wa miaka hiyo tulikuwa nayo tukiambiwa habari za Dasalama. Ile picha ambayo tunayo kuhusu Ulaya ndio ilikuwa ipo katika vichwa vyetu kuhusu Dasalama.

Dasalama! Katoka Dasalama huyo! Dasalama! Kaenda Dasalama huyo! Mambo yalikuwa hivyo.
Mimi kwa umri huo Dasalama ya akili yangu ilikuwa Dasalama ya mabishoo, matozi nyangema wanaonyuka bringbring shalopers, Dasalama ya Watoto wakali, warembo wenye sura za mvuto kama Majini, Dasalama ya Maghorofa, misosi ya maana, watoto mashombe shombe! Dasalama yangu hiyo mtu asiiguse!

Sijui wewe ambaye umetoka mkoani ulikuwa na Dasalama ya namna gani? Lakini naamini hata wewe ulikuwa na Dasalama yako. Nami siigusi.

Taikon Master siku ya kuja Dasalama ikafika. Pakufikia nikapata. Alikuwa Kakaangu kwa Mama Mkubwa.
Safari ya Dasalama inachelewa kama pesa za mkopo. Lakini siku ikafika. Huyo mpaka majira ya saa kumi na moja hivi nilikuwa nipo Stendi ya Ubungo.

Mji umechangamka balaa! Pirikapirika kibao! Yaani taikon hatulii. Makundi ya Watu sikujua yanaelekea wapi na wala wao hakuwajua natokea wapi. Kila mtu na hamsini zake. Situlii! Sikuwahi kuona maelfu elfu ya Watu wakitembeatembea kama sisimizi.

"Karibu Dasalama" Nikajisemea kimoyomoyo nikijikaribisha kabla mwenyeji wangu hajafika. Nikawa nimetulia zangu, nafikiri hamu ilizidi uzuri wa Dasalama. Hivyo mpaka muda ule sikuona ubaya wowote wa Dasalama.
Na hiyo ikanifanya nijiambie "Hongera Taikon kwa kutimiza ndoto yako" hapo nikachukua kichupa cha juisi kwa muuzaji nikachamba koo. Huku macho yangu yakiendelea kusoma mabango makubwa yaliyokuwa yakielea angani kwa shani ya kupendeza. Ningeonea wapi mambo haya? Acha nifurahi mimi. Nikasema.

Kile kilichonileta nilianza kuonjeshwa onjeshwa. Mara huku naona mdada amevaa kisketi kifupi mapaja yako wazi. Mara kule naona mwingine kavaa suruali iliyomshika huku mapaja na makalio yake manene yakiniomba msaada kwa kujaribu kutikisika kama yanataka kujitoa kwenye ile suruali. Huenda ningeona huruma lakini niliishia kutekewa nisijue kama nafurahi au nimeshangaa. Akili yangu ikaniambia" bado hujaona, hii ni rasharasha, bado Elinino inakuja" nikaachia tabasamu kama mshindi huku nikinywa juisi yangu ambayo sikuisoma hata jina lake.

Licha ya kuwa ile midada iliyokuwa pale stendi ilikuwa iko busy na mambo yao bila kujali uwepo wangu lakini nilijiona nami ni sehemu ya washika dau katika sehemu ya maisha yao. Nilichukizwa Kaka alipofika, alinikuta nikiwa katika kina kirefu cha maji ambacho nilikuwa sihitaji kuokolewa. Bro akacheka sana aliponiona nilishangaa wale warembo ambao wengi wao walikuja kupokea ndugu zao waliotoka mkoani.

Ati yeye alijifanya kama anaona kitu cha kawaida na keshazoea na wala hababaishwi. Nilichukizwa sana lakini nami nikajigomboa niwe kama mtu wa mjini.

Huyo tukatoka pale akili yangu ikiwa imekaribishwa kwa namna ambayo nimefurahishwa na ukaribu wa awali. Mpaka kwenye kituo cha Daladala huko magari nilikuta ni mengi ajabu. Yanayoenda nisikokujua na yanayorudi nisikokujua. Sikujali yaliandikwa nini. Kwani niliyaona kama Majina ya Dawa za hospitalini zinazotibu magonjwa yanayoambukiza.

Kwa mara ya kwanza nikawa Disappointed. Tulipanda Daladala limejaa hilo. Shingo juujuu kama beberu. Hii sio Dasalama yangu. Nikajisemea. Lakini nikajikaza kisabuni huku mara kwa mara Bro akinipa Onyo kama Onyo la mwisho la Polisi wanaopambana na majambazi yaloyojificha kwenye jengo. "Kuwa makini, angalia usijeukaibiwa" hapo moyo unapiga paaah! Sasa kila mtu aliyekaribu yangu ambaye amechokachoka au anayefanana au kufananishwa na mwizi nilikuwa namhofia.

Mpaka tunashuka shingo ilikuwa inauma. Mara ya mwisho kuumwa shingo kama vile ilikuwa kipindi tumeenda kukata Kuni. Nilibeba mzigo mzito wa kuni ambao angepaswa kubeba Mnyamwezi. Sasa leo sijabeba chochote kichwani lakini shingo inauma kama nini. Ningefanyaje zaidi ya kumeza fumba la mate Kwa hasira kusafisha koo.

Tukaanza kukatiza mitaa, ilikuwa saa kumi na mbili inaenda saa moja hivi, bado giza halijaingia vizuri. Tukasonga nakusonga kila tulipokuwa tunapunguza mwendo alafu mbele kuna geti nilikuwa nafikiri tumefika lakini Walaa! Tukavuka mageti na mageti ya rangi na kila rangi. Nilibeti nikachoka.

Dasalama yangu niliamini kuwa ndugu yangu angekuwa anaishi ndani ya Geti kwenye nyumba nzuri hata kama isipokuwa nyumba kubwa ya kifahari lakini angalau ingelingana na ile nyumba iliyopo kwenye akili yangu. Thubutu! Tukafika nikiwa nimechoka mwili lakini akili bado ilikuwa na nguvu. Lakini makazi ya kaka yalinimalizia nguvu zangu za akili nilizokuwa nimebakiwa nazo.

Nyumba mbaya! Mazingira ya nje mabaya! Hii sio Dasalama yangu. Nikajisemea nikiwa nakaribishwa na wapangaji wenzake na kaka ambao walikuwa wamekaa vibarazani wanapika huku wengine wakipembua mchele. Walikuwa Wakarimu kweli lakini mimi mwenzao nilikuwa Disappointed. Nikawa najitabasamisha kuwalipa hisani wasijeniona namna gani vipi. Disappointed.

Tukaingia ndani, kilikuwa chumba na sebule. Hapo nikamkuta shemeji yaani mke wa kaka ameketi sebuleni anaangalia luningq sikumbuki kama lilikuwa igizo au muziki. Baada ya kusalimiana basi mara moja nikaambiwa niingie chumbani nikabadilishe ngúo niende bafuni nikaoge. Bafu halina mlango, bafu hapohapo choo! Ni bafu choo! Haya bafu choo halina paa. Yaani sio Pouwa! Hii sio Dasalama yangu. Nikasema huku nikiwa naoga. Disappointed.

Nikarudi, chakula kwenye kalenda kasufuria jamani. Wali ulikuwa sijui ni robo sijui ni nusu mimi sijui. Ila maswali nikawa najiuliza, huu wali ni wa mtu mmoja au wawili au watatu kama tulivyo. Mara zokaletwa sahani tatu. Nikasema basi. Nikashusha pumzi fuuuu! Kama Bata dume. Kwa kuchoka na kukata tamaa. Shemeji akanipa pole na safari wakati Mimi niko- Disappointed.

Dasalama yangu uko wapi?
Uko wapi Dasalama yangu?
Nikawa najiuliza.
Unajua akili za kimkoani ile kujua Dasalama hakuna shida au ile akili ya kiafrika kujua Ulaya hakuna shida. Au ile akili ya Walimwengu kujua mbinguni hakuna shida hivyo ndivyo nilivyokuwa.

Sasa mdogo wangu alipofika kwangu nikamuuliza swali hili; Hii ndio Dasalama yako au umekuwa Disappointed?
Akacheka kisha aliponijibu ndipo nikakumbuka miaka kumi na tano iliyopita.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kitu pekee ambacho kilinidisappoint ni kuwa Dasalama bei kitonga. Hela kidogo tu, unapata nguo nyingi sana.

Mama wee, naenda nilipoelekezwa badala ya kukuta nguo napewa matambala. Eti ndizo nguo za bei chee.

Nikiuliza za aina niliyobeba kichwani, nasisimkwa kwa ughali wake.
 
Hatari Sana.
 
Uchafu,uswazi,foleni na joto.

Nilichopendelea Dar ni warembo wa Kila sampuli maana wakati Fulani nilikuwa na mademu 13.

Si ajabu nikirudi Mkoani Kwa nauli ya Msaada kutoka Kwa School mate baada ya kufulia mbaya.
 
... wenyeji, watani zangu, washamba kuliko mimi ninaetoka MANG'WANZA!
1700574052424.png
... sasa hivi wanapanga kwenye vibanda vyangu!
 
Kukutana na watu waongo sijawahi kuona! Sikuwahi kufikiri watu wanaweza kuishi namna hii.
Kila wasemacho, wanavyoishi ni mashaka matupu.

Sasa hivi nimezoea, mpaka nina mpenzi mdaslam na namwamini.
Nilipokuwa huko mikoani km wanavyosema vijana wa dar, nilihisi watu wa dar ni matapeli si ke wala me, sasa nilipoenda najiuliza na mie ni tapeli au😂
 
Nilishangaa watu wanakula utumbo wa kuku , kichwa na miguu !! wakati mkoani hivi vitu vinatupwa !! Hiyo hiyo siku nafika jirani kulikua na Arobaini nikasema ngoja nikaoshe macho kidogo !! hicho kisingeli kinavyochezwa na kina dada aseee !!!
ila tuseme ukweli hii bongo hakuna mkoa unaoifikia Dar hata nusu ya kwa kila kitu kuanzia maovu na mishemishe na uchafu hadi bata linalolika DSM.
 
Kukutana na watu waongo sijawahi kuona! Sikuwahi kufikiri watu wanaweza kuishi namna hii.
Kila wasemacho, wanavyoishi ni mashaka matupu.

Sasa hivi nimezoea, mpaka nina mpenzi mdaslam na namwamini.

😆😆😆
Uongo ndio maisha ya mjini. Bila uongo mjini utakwama.
Sema inategemea uongo unamfanyia nani
 
Back
Top Bottom