Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Ulisikia muziki huu kwa mara ya kwanza Ukiwa wapi?

Hizi za kale ndio zilikuwa nyimbo na si haya matakataka ya siku hizi kama Dr nipime homa au UTI MA

mara sijui panauma panaessha
 
Franklin Boukaka alinyongwa mwaka 1972; alitoa wimbo huo mwaka 1970 ukampa umaarufu sana na kusababisha apendwe sana na wanamapinduzi wa wakati huo waliochukia wakoloni weupe kuondoka na kupata wakaloni weusi; jambo hilo lililomfanya achukiwe na viongozi wa Congo wakati huo na kusababisha anyongwe.
duhh
 
Ni kweli, Nzinzi wa Kester Emeneya ulitoka nadhani mwaka 1986 au 1987 hivi, na ulitawala sana anga wakati huo.


View: https://www.youtube.com/watch?v=sVPx2sLCO48

Mayaula Mayoni alikuwa na vipaji sana. Alisoma chuo kikuu cha Dar es salaam akapata digrii ya Methametics; wakati akiwa mwanafunzi wa Dar alikuwa mcheza mpira akiichezea timu Yanga (jangwani). Baada ya kupata digrii na kurudi kwao Zaire, hakupenda kuwa mwalimu ndipo akajiunga na bendi ya TP OK Jazz kama muimbaji.

Wimbo huo wa Mbongo ulivuma sana mwanazi mwa miaka ya tisini. Pale Mwenge kulikuwa na baa inaitwa Mbogwe, ilimwalika mwaka 1995 apiga wimbo huo wa Mbongwe mfululizo na watu wakacheza mpaka saa kumi alfajiri.


View: https://www.youtube.com/watch?v=Zf6kBV1NNvs

Hiyo stori hapo mwisho mbona kama ya kizushi Mkuu! Miaka hiyo ndio zilikuwa pande zangu hizo na kulikuwa na Baa inaitwa "Igongwe" hapo Mwenge kwa wachonga vinyago ikitazamana na uwanja wa mpira hapo.
 
Alafu kulikua na dansa anaitwa Black Moses sijui alipotelea wapi.yule jamaa alipewa kipaji aisee sidhani km kuna dansa atamfikia yule
Musa Simba aka "Black Moses" marehemu huyu jamaa hivi sasa. Ni kweli alikuwa super talented.
 
Wakuu hivi hili song linaitwaje?

Nililisikia Radio One mtaa wa magoma nika Shazam lakini haikunipa majibu

Mwenye kuujua unaitwaje na umeimbwa na nani?

Kichuguu
Ni wimbo wa "The Beat Masters" na unaitwa "Warm Love"

Hizi ngoma za zamani ngumu sana kuzipata hasa kwa kuwa nyingi hazijawahi pandishwa mitandaoni. Ninazo nyingi sana nilizorekodi na kujaribu ku_shazam bila mafanikio.

Bahati mbaya nyingine ni wale ma_Dj wanaogonga hizi nyimbo hawataji majina,ni wachache sana wanaofanya hivyo. Huu baada ya kuutafuta muda mrefu sana, siku moja kwenye "Mtaa wa Mangoma" na "Dj JD" aliutaja jina lake. Tangu hapo sijawahi kuusahau.
 
Kundi la Boney M lilianzishwa na mjerumani mmoja akiitwa Frank Farian. Baada ya Boney M kuvunjika, Frank alianzisha kundi jingine lililoitwa Milli Vanilli. Wimbo uliowapa sifa sana Milli Vanilli ni huu hapa ambao ulihusisha waimbaji wawili ambao hawakuwa waimbaji ila waigizaji tu: Fab Morvan and Rob Pilatus. Kwenye wimbo huu, Rob Pilatus anaonekana kama mwimbaji lakini siyo kweli kwani anaigiza midomo ya uimbaji tu, yaani lip-syncing. Mimi niliusikia mara ya kwanza mwaka 1990 baada ya kununua cassete tapes zake pale Kariakoo siku moja baada ya Papa Pulo wa sita kuendesha ibada yake pale Jangwani. Jje wewe uliusikia ukiwa wapi? Ni Wimbo uliovuma sana miaka ya tisini


View: https://www.youtube.com/watch?v=ZbUENJ5FjBk

Hii casette Dingi aliinunua mwaka 1991 kama sijakosea. Halafu ikatokea mtoto wa baba Mkubwa alikuja home akawaka nayo kichizi akaichukua. Mzee baada ya kugundua haipo, alinipa kazi ya kwenda kuifata nyumbani kwao na kuirudisha haraka sana. Ina ngoma kali sana. Wonderful enough mpaka leo hiyo cassete na nyinginezo zipo tu ingawa ndio hakuna mashine ya kuzi_play.
 
Back
Top Bottom