Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 532
- 1,089
Ni kweli naelewa unatakiwa uchanganye kwa mashine, unaweza nunua kila kitu na vikorokoro vingine ukaongezewa kwenye mashine zinazosaga wakakusagia ukapaki mifuko yako, saizi ya punje itakuwa ngumu kama unatumia kinu na sio mashine. Namsoma amesema alinunua kinu.... alternatively kuna maduka ya vyakula huwa yanauza mahindi yaliyoparazwa na vikorokoro vingine vingi, vifaranga wanahitaji vitu vyote muhimu kwani wanakua haraka. Kuna formula zinataja damu, mabaki ya samaki, majani yaliokaushwa, premix, kwa v iwango tofauti sasa kama vikizidi au kupungua.... mimi nina vifaranga chotara hapa wiki 2 nawalisha starter bado ila watakaototolewa na hawa najiandaa kuchanganya mwenyewe nitaleta feedback hapa
Mama Joe vifaranga walishatotolewa tayari? Yaani kujitengenezea chakula cha vifaranga hiki ni kitendawili tunatakiwa tukitegue tuweze kupata faida kubwa, tunakusikilizia Mkuu.