Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni jambo linalowezekana

Manchid

JF-Expert Member
May 29, 2016
218
462
Kumekuwa na kasumba juu ya swala Zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji kuonekana kama ni swala lisilowezekana yaani kufuga kuku wa kienyeji mpaka kufikia idadi kubwa yani 1000, 2000 au hata 3000

Baada ya majaribio kadhaa ya kufuga hawa kuku sasa rasmi nmeingia kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mazingatio ya hali ya juu na mpaka kufikia mwezi December nataka kuwa na kuku si chini ya 1000.

Nimeanza na makoo 35 na majogoo 6. Mpaka sasa nina vifaranga zaidi ya 50 ambao nawalea kwa kutumia joto la taa na mkaa na makoo zaidi ya 7 yanayolalia mayai yasiyopungua 15 kwa kila moja

Rafiki njoo tubadilishane mawazo juu ya mradi wa kuku wa kienyeji pure.

20230902_141107.jpg
20230902_141104.jpg
20230901_171019.jpg
 
Inawezekana....nakutia🙂....moyo
Kuna rafiki yangu kafikisha kuku 10,000 na zaidi...ila hafanyi shughuli nyingine...yupo mwenyewe 24/7...
Siku namtembelea alikuwa anauza majogoo 15,000x500=7,500 000
Na nikiangalia wale kuku wala sioni tofauti kama wamepungua.....Sasa fikiri haupo ni umeweka mfanyakazi.....lazima akutie👆
 
Siyo kirahisi hivyo, gharama za chakula zitakutoa jasho.... miezi sita mpaka anunuliwe, amekula chakula kiasi gani?
 
Kama una eneo kubwa, waweke wawe free range wajitaftie chakula. What you do, asubuh unawawekea kidogo af unawaacha watafute, jioni wakikaribia kurudi unawawekea tena chakula kidogo af wanaenda kulala.
Same thing kwa vifaranga, wakimaliza mwezi unawaachia. Kwa kias fulani itapunguza gharama ya chakula.
Muhim uwe na fence na uhakikishe hawali mavi. Pia vicheche ni hatari.
All in all kila.la kheri mkuu
 
chakula kitakutoa josho maana wanakula sana na hawakui haraka mpaka miezi 6 or so! hutaweza !
#Be positive mkuu, kila mwanadam anahtaj zaid faraja pas na kukatshwa tamaa. Ndugu yetu amejaribu yapaswa kumpa moyo il apge hatua zaid.

Kama ulijua tatzo n chakula kwann usimpe suluhu ya nn kfanyke il kutatua changamoto, neno #HUTAWEZA kweny uzi huu sio mahala pake.
 
Inawezekana....nakutia....moyo
Kuna rafiki yangu kafikisha kuku 10,000 na zaidi...ila hafanyi shughuli nyingine...yupo mwenyewe 24/7...
Siku namtembelea alikuwa anauza majogoo 15,000x500=7,500 000
Na nikiangalia wale kuku wala sioni tofauti kama wamepungua.....Sasa fikiri haupo ni umeweka mfanyakazi.....lazima akutie
#Fact
 
Kama eneo ni kubwa na salama wanajiokotea wenyewe.....unaongeza matakataka kidogo toka ma dampo ya sokoni..migahawani

.
Practicality yake ndiyo ngumu. Ninafuga hao wa kienyeji kama 40 hivi. Chakula kinanitoa jasho. Kilo Moja ya mchanganyiko wa pumba, mashudu alizeti/ pamba, mahindi, lukina, dagaa ni elfu moja. Wakila kilo 5 a day for six months....na unauza unapata Nini?

Nina eneo kubwa kama nusu eka, lkn hakuna chakula maana ni jua hakuna wadudu wa kuokoteza. Mahotelini labda lkn na wenyewe watakuchoka unless unalipia matakataka hayo. Dampo huko siwezi...

Kibaya soko lake ni kama hakuna. Hapa kwetu mjini ni elfu kama sh 15-35...nani uswazi atoe Hela hiyo!

Nami nilivutiwa na story kama hizi, lkn Kuna shida kidogo Kwenye chakula. Magonjwa siyo kihivyo ukiwa makini na chanjo, vitamins, minerals etc etc
 
#Be positive mkuu, kila mwanadam anahtaj zaid faraja pas na kukatshwa tamaa. Ndugu yetu amejaribu yapaswa kumpa moyo il apge hatua zaid.

Kama ulijua tatzo n chakula kwann usimpe suluhu ya nn kfanyke il kutatua changamoto, neno #HUTAWEZA kweny uzi huu sio mahala pake.
Mimi ni objective, scientific, sina longo longo. Kwenye science hakuna wengi Wape na kupeana moyo.
Nimesema shida ni chakula, kama anaweza pata chakula Cha bei nafuu kwa miezi kama 6 ( mpaka kukomaa kuuzwa) then let him go on!

Nawafuga and I have 40 or so, therefore I am talking from experience. Akiweza chakula Cha bei nafuu, then ni mradi mzuri maana Hauna risk ya magonjwa kama wa kisasa.
Soko unaweza kutafuta taratibu maana Kwa bei yake kubwa wateja wanakuwa kidogo.
All in all, ni vema kujaribu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom