Wakubwa huko mijini mliko je hii Easter soko la kuku wetu hawa wa kienyeji lilikuwaje? Je Kuku walidoda? Kwa mtu aliekuwa amesubiria kuuza wakati huu wa sikukuu anaweza kuwa amepiga bao?

Naomba ukarimu wenu tushee taarifa hiyo kwa kila aliebahatika kushuhudia harakati za manunuzi ya hawa ndege. Je inahitaji kupiga debe sana ili kuweza kuuza kuku wakati wa siku kuu? Maana nimewahi kushuhudia baadhi ya mazao kama nyanya kukiwa na demand kubwa wanunuzi hufikia hadi kutoa rushwa ili kuweka ORDER!
 
Habari za Easter wadau, tumerudi tena sasa huko wengine tulikuwa hakuna network. Hongera LiverpoolFC kwa kuongeza vinyoya, kweli umejitahidi sana kaza buti, mimi wangu wanaendelea vizuri.

Kuhusu soko Kubota, mimi sikuwa na wa kuuza labda wadau wengine waje watatuelezea. Kila la heri.
 
habari za Easter wadau, tumerudi tena sasa huko wengine tulikuwa hakuna network. Hongera LiverpoolFC kwa kuongeza vinyoya, kweli umejitahidi sana kaza buti, mimi wangu wanaendelea vizuri.

Kuhusu soko Kubota, mimi sikuwa na wa kuuza labda wadau wengine waje watatuelezea. Kila la heri.

Asante Mama Joe nimefurahi kukusikia tena.
 
Asante sana wadau kwa michango yenu. mimi nimeanza na kuku 3 jogoo 1, mitetea 2, mafundi ndio wanamalizia banda, nina mpango wa kuongeza mitetea 2. so far changamoto nilizopata ni kuku kukataa kutaga kwenye makalai niliyowaandalia.
 
Maisha ni jinsi unavyoyatengeneza kama wazazi wako walikupeleka shule na ukakubali kusoma, elimu uliyo ipata ukaitumia kwenye maisha ya kila siku, hakika lazima ufanikiwe.
 
Maisha ni jinsi unavyoyatengeneza kama wazazi wako walikupeleka shule na ukakubali kusoma,elimu uliyo ipata ukaitumia kwenye maisha ya kila siku,hakika lazima ufanikiwe.
Karibu sana JF, Mkuu Mbugazetu! Hapa ndiyo Forum ya ujasiriamali na hii umeingia ni thread ya ufugaji wa kuku wa kienyeji. Karibu sana mgeni wetu!
 
mkuu Kubota tunaendelea kukusikilizia kwenye darasa lako!

Poa Mkuu betlehem, darasa litaendelea usikae mbali. Nilipause kidogo maana unajua wachangiaji ndiyo wanaoamsha masuala ya kujadili na wachangiaji wangu nadhani hizi mvua zimewakeep bize kulima, hawaingii jukwaani. Mimi hizi mvua kwenye matanuru yangu ya mkaa mbona ni baraka, bwana miti anavyoogopa mvua, tunajimegea tu miti. Halafu na kamshahara kake bado hajakamaliza hadi aishiwe atakuta nimeshapakuwa huyooo mjini.
 
Mkuu muda si ni kama wa kuku siku 21? haiana tofauti na kuku, Mkuu China kampuni ziko nyingi mno zinazo tenegneza Incubators na bei zao ziko Chini kabisa ingawa kuna zingine ni ghali, Ila ya Mayi 1500 mpaka kuifikisha Babdari ya Dar ni kama Milioni Moja na Lakini Mbili tatu, Ya mayai Buku ni kama laki 9 hivi,

Mkuu ina maana bei za incubator ndio zimeshuka hivi aisee? Maana juzi kati niliona ya mayai kama 500 hivi ilikua zaidii ya Million 4 Au umekosea ku-type mkuu?

Kama bei ni hii basi na mie nikaagize fasta maana kutotoa kwa kutegemea kuku wenyewe ni mateso sana aisee....
 
Kubota bado najifunza kuhusu ulinzi, aina ya mbwa: lazima nipate waliofunzwa au ninunue mdogo nimfundishe mwenyewe? Je mbwa yeyote anafaa?
 
Ndugu wanajf mimi ni mgeni humu ndan lakin nimeona mwanga tulivu kwani nafuga kuku wa kienyej kupitia uzi huu nimejifunza jins ya kuboresha mradi wangu,soon ntakuwa na mashine ya kutotoleshea vifaranga,naomba ushaur zaid ili nijikwamue kimaisha..thanx an God bless u all!
 
Karibu sana mkuu na hongera kwa kuwa na mawazo ya kijasiriamali...

Mashine za kutotoleshea mara nyingi watu wanaagiza CHINA maana ndii nafuu kulinganisha na za MAREKANI na UROPE na zinapiga mzigo kwa efficiency kubwa kulinnganisha na za BONGO zinazotengenezwa mitaani. Bei zake zina tofautiana sana ila juzi kuna kwenye uzi mmoja mkuu Chasha aliongelea kuwa zipo za mayai 1500 kwa million 1.2 na sikuamini nikamuuliza maswali mawili matatu lakini hakunijibu mpaka leo

Nafikiri ni wakati mzuri sana kwa mkuu Chasha kutueleza vizuri sasa kama kweli kwa hiyo bei unaweza kupata incubator nzuri kutoka China maana za hapa BONGO ni pasua kichwa sana...
 
Last edited by a moderator:
Poa Mkuu betlehem, darasa litaendelea usikae mbali. Nilipause kidogo maana unajua wachangiaji ndiyo wanaoamsha masuala ya kujadili na wachangiaji wangu nadhani hizi mvua zimewakeep bize kulima, hawaingii jukwaani. Mimi hizi mvua kwenye matanuru yangu ya mkaa mbona ni baraka, bwana miti anavyoogopa mvua, tunajimegea tu miti. Halafu na kamshahara kake bado hajakamaliza hadi aishiwe atakuta nimeshapakuwa huyooo mjini.

Mkuu Kubota katika pita pita zangu nimekutana na hii kitu au maarifa kutoka kwa moja ya wafugaji wanaofuga kuku wa kienyeji kibiashara..

Wanadai ukitaka kuku atage na kutotoa vifaranga wengi na wakue na afya nzuri na kwa speed nzuri (good growth rate) inabidi uhakikishe kuku wenye uhusiano wa damu hawapandani. Yaani kama ni jogoo basi lisiwe na undugu wowote na mitetea, kama ni baba asiwapande watoto wake, majogoo nayo yasiwapande mama zao, lakini pia kaka na dada wasipandane...

Wanadai ukifanikiwa kwa hilo utaangua vifaranga wengi kwa muatamio mmoja na vifaranga vitakua kwa speed kali mno na havidhuriwi sana na magonjwa...Sijui kama mlikua mnaijua hii kitu...

Kitu ambacho nimekua nikifuatilia sijapata jibu ni suala la vyakula gani umlishe kuku wa kienyeji ili atage mayai kwa wingi, maana katika kuku wa kisasa hii kitu ipo. Watengenezaji wa vyakula vya kuku huchanganya baadhi ya vyakula vinavyomp kuku stimu za kutaga (anakua na stimu za kudondosha mayai kama mtu aliye na tumbo la kuhara anavyokuwa na stimu za kudodondosha zigo lake kwa choo)..

Nikifanikiwa kupata hili nitamwaga jamvini hapa ila kama kuna wakuu wengine wana ideas wanaweza kutumwagia hapa...
 
Ndugu wanajf mimi ni mgeni humu ndan lakin nimeona mwanga tulivu kwani nafuga kuku wa kienyej kupitia uzi huu nimejifunza jins ya kuboresha mradi wangu,soon ntakuwa na mashine ya kutotoleshea vifaranga,naomba ushaur zaid ili nijikwamue kimaisha..thanx an God bless u all!

Poa Mkuu wewe funguka tu juu ya unachotaka ushauriwe.
 
Mkuu Kubota katika pita pita zangu nimekutana na hii kitu au maarifa kutoka kwa moja ya wafugaji wanaofuga kuku wa kienyeji kibiashara..

Wanadai ukitaka kuku atage na kutotoa vifaranga wengi na wakue na afya nzuri na kwa speed nzuri (good growth rate) inabidi uhakikishe kuku wenye uhusiano wa damu hawapandani. Yaani kama ni jogoo basi lisiwe na undugu wowote na mitetea, kama ni baba asiwapande watoto wake, majogoo nayo yasiwapande mama zao, lakini pia kaka na dada wasipandane...

Wanadai ukifanikiwa kwa hilo utaangua vifaranga wengi kwa muatamio mmoja na vifaranga vitakua kwa speed kali mno na havidhuriwi sana na magonjwa...Sijui kama mlikua mnaijua hii kitu...

Kitu ambacho nimekua nikifuatilia sijapata jibu ni suala la vyakula gani umlishe kuku wa kienyeji ili atage mayai kwa wingi, maana katika kuku wa kisasa hii kitu ipo. Watengenezaji wa vyakula vya kuku huchanganya baadhi ya vyakula vinavyomp kuku stimu za kutaga (anakua na stimu za kudondosha mayai kama mtu aliye na tumbo la kuhara anavyokuwa na stimu za kudodondosha zigo lake kwa choo)..

Nikifanikiwa kupata hili nitamwaga jamvini hapa ila kama kuna wakuu wengine wana ideas wanaweza kutumwagia hapa...

Asigwa umedisturb mbavu zangu kuhusu ishu ya hizo stimu za utagaji wa kuku. Nashukuru umenifanya nicheke leo!! Hilo ulilolisema ni kweli Mkuu. Kuna baadhi ya viumbe wanaathirika sana wanapozaliana ndugu (inbreeding). Moja ya viumbe hao ni kuku. Inbreeding husababisha udhaifu uitwao kitaalamu inbreeding depression, udhaifu huu huendana na kupungua uzalishaji kwa namna zote, iwe utagaji, kukua (growth rate), zaidi ya hapo husababisha kuku rahisi kushambuliwa na magonjwa. Kuku wanapozaliana wa damu moja husababisha madhaifu yale ambayo yalikuwa yamejificha kujitokeza zaidi.

Ili kuepuka tatizo hilo kiutaalamu unashauriwa kubadili jogoo kila mwaka. Hata kama jogoo lako unalipenda vipi hapa hakuna jinsi! Matatizo mengine mengi tunayoyaona ya udhaifu wa kuku ni shauri ya udhaifu wa kuzaliana ndugu. Kwa hiyo ama ununue jogoo jingine au ubadilishane na mfugaji mwingine. Kuna baadhi ya nchi zimewahi kuwa na mpango unaitwa cock exchange programme, yaani wakulima wa eneo moja wanakuwa wanabadilishana majogoo na wakulima wa eneo tofauti kila mwaka.

Mkuu Asigwa hili swali umeuliza ni la muhimu sana nakupongeza Mkuu.

Kuhusu kutengeneza chakula ili kuku wa kienyeji atage kwa wingi kama nitakuwa nimekuelewa vema ni kwamba kuku wa kienyeji anaukomo wake wa kutaga mayai. Kuku wa kienyeji akilishwa vizuri anaweza kutaga mayai mengi lakini hawezi kupita uwezo wake wa asili! Kama lengo lako ni kumlisha ili aweze kutaga mfululizo kama kuku wa mayai hilo haliwezekani! Kuku wa kienyeji hataumlishe chakula cha broiler hawezi kukua kwa spidi kama broiler! Kuku wa kienyeji ni mbegu tu kama ilivyo mbegu za binadamu! Mtoto atokae ukoo wa watu wafupi hata umlishe chakula wanachokula Masai hawezi kurefuka kama Masai! Ni mambo ya genes! Yale madawa wanayopatiwa kuku wa mayai na kuwafanya watage kwa fujo hiyo inawaongezea uwezo ambao tayari wanao, lakini ukifanya hivyo kwa kuku wa kienyeji unaweza usipate matokeo hayo. Kwa kifupi ni hivyo vinginevyo kama vipi si ufuge tu kuku wa mayai ili ufurahie hiyo stimu ya kumwaga mayai, ha hahaaaa. Asigwa wewe ni nooma !!!
 
Mkuu ina maana bei za incubator ndio zimeshuka hivi aisee??? Maana juzi kati niliona ya mayai kama 500 hivi ilikua zaidii ya Million 4...Au umekosea ku-type mkuu??

Kama bei ni hii basi na mie nikaagize fasta maana kutotoa kwa kutegemea kuku wenyewe ni mateso sana aisee....[/QUOTE

Mkuu Asigwa, usishangae, Chasha hajakosea kutype !!! Ukibahatika kuona bei ya vitu vya China kwenye mtandao, utashangaa sana na unaweza kulia na wahindi wanaoagiza vitu huko na kutubamiza mibei ya kutisha kwenye maduka yao ya uhindini. Ukiingia kwenye mtandao ukaangalia bei za mashine mbali mbali na vifaa vya kilimo hata mashine za kukamulia alizeti huwezi kuamini bei zilivyo!! Kwa mfano kuna powertiller (horse power 15) inajembe la kuchavanga kwenye mpunga, ina trailer ya tani 1, ina mashine ya kupandia, ina jembe la kulimia plow inauzwa USD 2000. Ukibadili USD kwenda T sh ni kama shillingi 3,300,000/= ukijumlisha na gharama za kukomboa bandarini hata zikifika millioni 5 bado ni bei poa sana ukilinganisha na bei za uhindini ambazo si chini ya 9 millioni.

Kwa hili Chasha anamaanisha alichokiandika, na mwenyewe ataongezea. Ingia ucheze uone utamu wa ngoma mkuu Asigwa.
 
Mkuu Asigwa halafu jamaa wana respond haraka sana cheki hii chini nilikudokezea hapo juu:

Dear ,

how are you!

our bigest horse power is 15hp our engine is kubota engin ,so stronger for now i am very glad to sent you best price as follows:
15hp kubota engine power tiller cif dares salaam port
1set usd1400/set

implements:
double-plough usd120/pc
rotary tiller with seat usd150/pc
seeder usd150/pc
grass cutter usd190/pc
trailer usd290/pc
payment:t/t
delivery:within25days after order
also please find the pictures for our machinery for your reference.

wait for your reply!

Best regards,

Jane wang
 
Ufugaji huria wa kuku, ambapo kuku huchunga wenyewe, ufugaji huu unapunguza gharama za chakula cha kuku na kufanya ufugaji kuwa wenye faida kubwa sana. Tanzania tuna ardhi ya kutosha ya nini kubanana sehemu moja, kwa nini tusitumie fursa hii ya kujimwaga mbugani tutafute pesa?
WhatsFresh_Chicken3.jpg

3217378769_225cfc6646.jpg

Similar Discussions

Back
Top Bottom