Mradi Ufugaji wa Kuku wa Mayai

Mfugaji123

New Member
Apr 3, 2020
3
41
Leo napenda kujadili mradi mkubwa wa ufugaji wa kuku wa mayai 30,000. Kama ilivyo kwa biashara nyingi za uzalishaji uzalishaji mkubwa hupunguza gharama za uzalishaji kwa bidhaa moja ( Unit cost) na hivyo kuweza kufaidika na soko kwa kuuza kwa bei shindani na pia kufaidika na economic of scales ( kufaidika kwa kuuza bidhaa nyingi kwa bei shindani).
Kabla ya Kuangalia mradi huu kwanza tuone hali ya uzalishaji na mahitaji ya mayai. Kwa sasa uzalishaji wa mayai nchini ni takribani bilioni 5.5 wakati mahitaji halisi ni bilioni 8.1. Kwa hiyo kuna deficit ya mayai takribani bilioni 2.6 kwa mwaka. Dar es Salaam ni mlaji mkubwa wa mayai, inakadiriwa Dar Es Salaam pekee hutumia mayai milioni 500 kwa mwaka wakati mahitaji halisi ni mayai bilioni moja. Inakadiriwa kufikia mwaka 2050, Dar Es Salaam itahitaji mayai ya kuku bilioni 2.5
Mchanganuo wa Mradi
Shamba lenye kuku wa mayai 30,000

Kwa kuku 30,000;
(1)Jenga mabanda 2 yenye uwezo wa kubeba kuku 15,000. Vipimo vya banda: Urefu mita 80 , upana mita 13 na kimo mita 3.5
(2)Nunua Cage zenyeUkubwa: 2.2m*2.4m*1.95m, Uwezo wa kubeba kuku: 160,Idadi ya cage ziwe: 192.Kila Banda liwe na cage 96. Katika banda kutakuwa na safu 3 za cage. Kila safu iwe na cage 32
(3) Unaweza kununua mashini ya kulisha automatically au ukatumia watu kulisha. Hiiinategemea kama bajeti ipo vzr
(4) Nunua maghala ya kisasa ya kuhifadhia raw material za chakula (silo) kama bajeti ipo vzr
(5)Unaweza kununua mashini Maalum ya kukusanya mayai. Kibongobongo kazi hii inafanyika na wafanyakazi
(6)Unaweza kununua mashini ya kuondoa kinyesi cha kuku. Bado kazi hii inaweza kufanywa na wafanyakazi
(7) Nunua feni ya kuongeza Mzunguko wa hewa na pazia la unyevu ili kudhibiti unyevu ndani ya Banda. Hii inafanyika Kama unataka kuku watage mayai kwa wingi. Ni lazima mazingira ya bandani yawe rafiki kwa kuku kutaga vinginevyo Uzalishaji utakuwa chini ya kiwango. Feni ziwe 12 kila Banda na pazia liwe eneo la mita za mraba 84 kwa kila banda
(8)Mashine ya kuzalisha chakula yenye uwezo wa kuzalisha tani 1-2 kwa saa. Kutengeneza chakula kutaokoa gharama za ulishaji
(9) Kama hakuna umeme unapaswa kuweka umeme wa solar
10) Weka miundombinu ya Maji kama kuchimba kisima au matanki ya maji
11: Gari ni muhimu kwa shughuli za Shamba

Matokeo ya Mradi

1:Gharama za chini za uwekezaji zinaweza kufika TSh million 350

2:Gharama za chakula kwa kipindi cha wiki 70-80 zinaweza kufikia Tsh bilioni 1.5

3:Uzalishaji wa mayai kama hali iko vzr unaweza kufikia milioni 10 kwa Ufugaji wa kipindi cha wiki 70-80

4:Mapato yote kwa kipindi cha wiki 70-80 yanaweza kufikia Tsh bilioni 2.7-3

5: Na faida bila kodi inaweza fikiaTsh milioni 700 hadi bilioni 1

Uchambuzi wa Kiuchumi

IRR=45%
Annualized ROI: 15.9%
Payback period: 1.8 years
Discounted payback period (18%): 2.4 years

Kwa Mahitaji ya Business plan ya mradi huu na zingine za uwekezaji mkubwa kwenye Ufugaji tutafute.

Simu: 0621106923
 

Attachments

  • unnamed.jpg
    unnamed.jpg
    88.3 KB · Views: 25
Back
Top Bottom