technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,960
48,759
Ijapokuwa Ole Sabaya anatuhumiwa kufanya uovu mkubwa wakati akiwa DC Hai, alipaswa kufunguliwa mashtaka ya jinai kortini. Kwa TAKUKURU kumweka mahabusu kwa wiki nzima ni kukiuka sheria za nchi yetu & kuendeleza tabia ya ukiukaji wa haki za binadamu ya vyombo vyetu vya usalama!

Lissu-Sabaya.JPG
 
Tundu Lissu ameandika hivi.....

"Ijapokuwa Ole Sabaya anatuhumiwa kufanya uovu mkubwa akiwa DC Hai, alipaswa kufunguliwa mashtaka ya jinai kortini. Kwa TAKUKURU kumweka mahabusu kwa wiki nzima ni kukiuka sheria za nchi yetu & kuendeleza tabia ya ukiukaji wa haki za binadamu ya vyombo vyetu vya usalama!"

Upeo na hekima wa hayo maneno ya Lissu hapo kwenye mambo ya kisheria na utetezi wa haki za binadamu ni darasa tosha kwa kila mwanasiasa na raia wa kawaida katika jamii yetu. Siasa sio uadui na sheria sio hisia binafsi.

Hongera Tundu Lissu.

IMG-20210601-WA0041.jpg
 
Hivi makomda hajatafuta upenyo wa kuchikichia ughaibuni? Maana huwezi jua ya kesho yatakuwaje.

Fikiria sharti namba moja la mabilioni ya shilingi kutoka kwa wahisani liwe.. Afikishwe ktk vyombo vya sheria aliyedhulumu haki ya kuishi wenzake.

Kipi kitakuwa rahisi kukubali sharti hilo na kumtosa makonda au kukataa sharti hilo ili kumlinda makonda?
 
Lissu yuko sahihi kabisa. Haki ya kisheria kwa Olesabaya ni muhimu mno maana haya yanaweza mpata mtu yeyote haijalishi umefanya au haujafanya makosa. Hii trend ya kushikilia watu kwa muda mrefu kwa sababu wanazojua wao si poa. Unaweza kuwa unashangilia leo lakini hauwezi jua kesho ni nini kitakupata.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom