Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,229
- 17,986
Shahidi wa nne katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia, leo Septemba 8, 2026 ataendelea kutoa ushahidi wake wa utetezi dhidi ya Tundu Lissu.
Jana Septemba 7, 2026, shahidi huyo alianza kutoa utetezi wake, ambapo Lissu alianza kwa kumuongoza kujibu maswali kwamba mkutano wa tarehe 3 Aprili ulihusu nini na nani aliyeuandaa. Katika majibu yake, shahidi alieleza kuwa mkutano huo ulilenga kuwakutanisha watia nia wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ili kuzungumzia msimamo wa chama wa "No Reforms No Election".
Alisema kwamba uamuzi wa kufanyika kwa mkutano huo ulifanywa na Katibu Mkuu wa chama, John Mnyika, pamoja na Sekretarieti, wala haukuandaliwa na Tundu Lissu kama inavyodaiwa.
Shahidi huyo aliongeza kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano iliyopo chini yake (Brenda Rupia) ndiyo iliyoandaa taarifa kwa umma na kuwaalika waandishi wa habari bila kuwapa maelekezo yoyote ya kikazi au ya kurusha matangazo moja kwa moja kuhusu mkutano huo wa mwezi Aprili 2025.
Katika ushahidi wake, Brenda Rupia alisisitiza kuwa Lissu alihudhuria mkutano huo kama mzungumzaji mkuu kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taifa na hakuwa na uhusika na ualikaji wa vyombo vya habari.
Rupia alieleza zaidi kwamba hata umiliki wa maudhui yote ya habari yaliyorekodiwa siku hiyo ulikuwa chini ya vyombo husika vilivyohudhuria na sio Chama wala viongozi wake.
Update kutoka Mahakamani
Shahidi no 4 na Mkurugenzi wa mawasiliano, Brenda Rupia pamoja na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Mzee na Mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema katika ukumbi wa Mahakama Septemba 8, 2026.
Tundu Lissu amefikishwa mahakamani muda huu.
Mwenyekiti wa kanda ya Pwani Mh Boniface Jacob akiwasili mahakamani
Mwenendo wa Kesi, Septemba 8, 2026 tuliishia sehemu ya 364 sasa leo tunaendelea na sehemu ya 365 ambapo Shahidi wa 4, Brenda Rupia anaendelea kutoa ushahidi wake kutokea alipoishia jana.
Mahakama inaanza.
Majaji wameshaingia Mahakamani muda huu.
Mwenyekiti Tundu Lissu pia ameshaingia.
Jaji anasema tuendelee
Anasimama Karani anasema Criminal session No. 19605 kati ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Ajuaye kama kawaida Wakili wa Serikali anatambulisha wenzake na kusema tuko tayari kuendelea.
Brenda anapanda kwenye kizimba ambacho kinatumika kwa ajili ya Ushahidi.
Jaji Ndunguru anamwambia nakukumbusha kwamba upo chini ya kiapo.
Lissu: Naomba waeleze Majaji uwepo wako katika mkutano huo wote.
Brenda: Waheshimiwa Majaji nilikuwepo katika mkutano huo wote
Lissu: Waeleze Majaji watu waliokuwa wazungumzaji katika Mkutano huo.
Brenda: Wazungumzaji walikuwa ni wale viongozi 6 wakuu niliowataja jana.
Lissu: Mzungumzaji mkuu katika mkutano huo alikuwa nani?
Brenda: Mzungumzaji mkuu wa mkutano huo alikuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Tundu Lissu
Lissu: Mkutano huo ulichukua muda gani?
Brenda: Masaa matatu hadi matatu na nusu
Lissu: Mzungumzaji mkuu unakumbuka alizungumza kwa muda gani?
Brenda: Mzungumzaji mkuu ndio aliongea kwa muda mrefu kuliko wote masaa mawili hadi mawili na nusu
Lissu: Nashtakiwa kwa maneno yasemayo (Lissu anasoma maneno ya kwenye hati ya mashtaka yanayodaiwa ya uhaini). Waeleze majaji haya maneno niliyoyasoma nimetumia muda gani kuyasoma
Brenda: Sio zaidi ya dakika mbili
Lissu: Waeleze majaji hotuba yangu ilichukua muda gani katika mkutano huu?
Brenda: Masaa mawili mpaka mawili na nusu
Lissu: Shtaka dhidi yangu linasema haya maneno niliyoyasema Jamhuri wanasema nilikuwa na lengo la kuitishia serikali, waeleze majaji uwepo wa maneno Serikali ya JMT
Brenda: Hakuna neno Serikali ya JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa neno Rais wa JMT
Brenda: Hakuna uwepo wa neno Rais wa JMT
Lissu: waeleze Majaji katika maneno niliyokusomea uwepo wa maneno Makamu wa Rais wa JMT
Brenda: Hakuna maneno Makamu wa Rais JMT
Lissu: Waeleze Majaji uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa JMT
Brenda: Hakuna maneno Waziri Mkuu wa JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Baraza la Mawaziri wa JMT
Brenda: Hakuna uwepo wa maneno Baraza la Mawaziri wa JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT
Brenda: Hakuna maneno Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya JMT
Brenda: Hakuna maneno Mkurugenzi wa Mashtaka wa serikali JMT
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno Halmashauri, Manispaa au Serikali ya Mtaa
Brenda: Hayo maneno yote hayapo
Lissu: waeleze majaji uwepo wa maneno Mkuu wa Mkoa, au kiongozi mwingine yeyote wa serikali
Brenda: Hayo maneno hayapo
Lissu: Mtu akikuambia haya maneno niliyokusomea yanaitishia Serikali ya JMT wewe unasemaje?
Brenda: Mimi naona sio kweli hayaitishii serikali ya JMT
Lissu: Katika hayo maneno niliyokusomea waeleze majaji uwepo wa maneno yoyote yanayohusu jeshi lolote nchi hii
Brenda: Hayo maneno hayapo
Lissu: Nikisema Jeshi lolote nina maana ya Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Magereza, Jeshi la akiba, Jeshi la Mgambo, Mgambo wa Jiji, Idara ya Usalama wa Taifa
Brenda: Yote hayo hayapo.
Sehemu ya 366
Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake ambae ni Mkurungenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA, Brenda Rupia.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa majaji hayo maneno niliyokusomea yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, kuna maneno tutakwenda kuvunja sheria za nchi
Brenda: Hayo maneno hayapo
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno tutaenda kupiga watu wanaoenda kupiga kura au kuwakata vidole
Brenda: Hayo maneno hayapo
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno mkachome vituo vya mwendokasi, daladala au mabasi yenyewe
Brenda: Hayapo kabisa
Lissu: Waeleze majaji uwepo wa maneno tutawapiga wasimamizi wa uchaguzi na kuchoma vituo hivyo
Brenda: Hayo maneno hayapo
Lissu: Kuna maneno yamesemwa kwamba polisi 16 waliuwawa wakati wa uchaguzi wa Okt 29, 2025, waeleze majaji uwepo wa maneno tutakwenda kuua polisi wakati wa uchaguzi
Brenda: Maneno hayo hayapo
Lissu: Kwa ufahamu wako shahidi, mtu akisema msimamo huu unaashiria uasi anakuwa ametenda kosa gani?
Brenda: Mtu akisema msimamo huu unaashiria uasi sio kosa kwasababu uasi ni kupinga pamoja na kukataa jambo
Lissu: Mtu akisema tutazuia uchaguzi anakuwa ametenda kosa gani kwa ufahamu wako?
Brenda: Sio Kosa mtu akisema tutazuia uchaguzi
Lissu: Kwa ufahamu wako mtu akisema tutavuruga uchaguzi anakuwa ametenda kosa gani ?
Brenda: Kwa ufahamu wangu sio kosa
Lissu: Kwa ufahamu wako mtu akisema tutahamasisha uasi anakuwa ametenda kosa gani katika nchi hii?
Brenda: Anakuwa hajatenda kosa lolote
Lissu: kwa ufahamu wako mtu akisema tutakinukisha, anakuwa ana maana gani?
Brenda: kwa ufahamu wangu tutakifanya kinukie, tukipika pilau inanukia pia
Watu kicheko😂😂😂😂
Lissu: Kufanya kitu kinukie ni kosa gani kwa sheria za nchi hii?
Brenda: Sio Kosa
Lissu: Kufanya kitu kinuke ni kosa gani kwa mujibu wa sheria za nchi hii?
Brenda: Sio Kosa
Lissu: Waeleze majaji usahihi wa maneno kukinukisha ni maneno ya mtaani / slang yaani sio neno rasmi
Brenda: Ni neno la mtaani sio neno rasmi hivyo ni slang
Lissu: Nimekuuliza juu ya maana ya neno mojamoja kwenye yote yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, sasa nakuuliza kwa ujumla wake, haya maneno yanaonyesha kosa gani?
Brenda: Hayo maneno hayaonyeshi kosa lolote
Lissu: ushahidi umetolewa hapa mahakamani kuwa haya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, yalichapishwa kwenye YouTube ya Jambo TV
Brenda: Niliona hiyo video kwenye mtandao wa Jambo TV
Lissu: Hiyo video uliyoiona kwenye mtandao wa jambo TV ina urefu kiasi gani?
Brenda: Masaa mawili na nusu hadi masaa matatu
Lissu: waeleze majaji katika hayo masaa mawili na nusu hadi matatu, haya maneno ndio pekee yaliyopo kwenye hiyo video?
Brenda: Sio hayo maneno pekee kwasababu Mwenyekiti alizungumza kwa masaa mawili na nusu hadi matatu
Lissu: Waeleze majaji uwepo wako wakati mashahidi wa Jamhuri wakitoa ushahidi
Brenda: Nimekuwepo kwa sehemu kubwa wakati mashahidi wa upande wa mashtaka wakitoa ushahidi wao
Lissu: Waeleze majaji kama uliona hiyo video ikionyeshwa mahamamani
Brenda: Hapana sijaiona.
Mhe. Lissu: waeleze majaji, uwepo wa ushahidi mwingine wowote zaidi ya maneno yao tu matupu hawa Jamhuri
Brenda: Hakuna zaidi ya maneno matupu tu
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wa Jamhuri wamesema hiyo video uliyoiona Jambo TV mimi ndio niliichapisha kwenye mtandao wa Jambo TV
Brenda: That is impossible kwasababu Tundu Lissu sio mfanyakazi wa Jambo TV
Mhe. Lissu: ushahidi umetolewa kwenye Mahakama hii kuwa baada ya mimi kufunguliwa mashtaka, kulikuwa na kamatakamata sana juu ya viongozi wa chama, waeleze majaji ufahamu wako juu ya hii kamatakamata
Katuga: Tunapinga hilo swali kwasababu ni leading, tunaomba lisiulizwe
Sehemu ya 367
Lissu anaendelea kumuongoza shahidi wake ambae ni Mkurungenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA Hq, Brenda Rupia.
Mhe. Lissu: Swali langu sio leading kwasababu a leading question attracts a yes or no answer. Suala la whether kumekuwa na kamatakamata limejitokeza kwa pande zote, extensively defense witnesses wamezungumza extensively na Jamhuri waliuliza maswali mengi ya dodoso.
Katuga: hakuna sheria inayosema a leading question ni lile swali ambalo lina suggest answer. Ingawa kifungu cha 160 cha Sheria ya Ushahidi kinasema Mahakama inawezs kuruhusu leading question lakini leading question imekuwa defined under section 159 of the Evidence Act.
Jaji Ndunguru: Kanuni za ushahidi in chief, ni kuwa shahidi anapaswa kusimulia anachokifahamu. Hivyo tuongozwe na msingi huo. Twendelee.
Mhe. Lissu: Shahidi nini kilitokea baada ya mimi kukamatwa?
Brenda: Chama kilifungiwa tarehe 10/06/2025 na viongozi walianza kukamatwa na mimi nilikamatwa tarehe 12/07/2025 Namanga Border Stop nikiwa naelekea Nairobi kwaajili ya kutembelea ndugu na baadae nianze safari kuelekea Ujerumani lakini sikufanikiwa kuvuka border.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji ulikuwa unaenda Ujerumani kufanya nini?
Brenda: Nilikuwa naenda kwaajili ya training ya communication skills
Mhe. Lissu: Ielezee hiyo training
Brenda: Kabla ya chama hakijafungiwa Katibu Mkuu aliniappoint Mkurugenzi wa Mawasiliano kwenda Ujerumani kwenye training lakini sikufanikiwa baada ya kukamatwa na nilisafirishwa kwenye gari aina ya probox kwa speed ya 120 na kuendelea na stop ya kwanza ilikuwa Longido ambapo niliingizwa kituo cha polisi bila kuandikisha, hawakuniambia kwanini tulisimama pale hata nilipouliza hawakuniambia chochote na kulikuwa na confusion na kelele baina yangu na hao majamaa ambao walinipeleka pale.
Mhe. Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya hapo?
Brenda: Baada ya kupiga kelele nyingi sana wakaniambia sasa tunakupeleka Central Police Arusha na wakaniambia niko salama niko mikononi mwa polisi. Nilikuwa na hofu kubwa sana kwasababu gari ilikuwa inatembea speed isiyo ya kawaida kuelekea Arusha.
Mhe. Lissu: Ilikuwaje mlipofika Arusha?
Brenda: RPC wa Arusha alikuja kuonana na mimi parking. RPC alitukabidhi gari nyingine aina ya VX yenye plate number ya Zanzibar. Wakaongezeka pia wanaume wawili na wakasema tunaenda Dar es Salaam kuanzia saa nne usiku. Hii gari ilitembea kwa speed kubwa sana na kila tuliposimamishwa walikuwa wakisema ni kazi maalumu na tunaruhusuwa kupita.
Mhe. Lissu: Mliposimamishwa na wakina nani?
Brenda: Traffic wa barabarani.
Mhe. Lissu: Mlifika Dar es Salaam saa ngapi ?
Brenda: Tulifika Dar es Salaam saa kumi alfajiri na tulifika Oysterbay. Wakawa wanamtafuta mtu niliyepaswa kuonana nae wakaambiwa nendeni Central Police, baada ya kwenda Central na kufika. Walimpigia simu George Bagyemu na aliwaambia anakuja na alikuja majira ya saa kumi na moja na nusu
Mhe. Lissu: Baada ya George Bagyemu kufika kitu gani kilitokea?
Brenda: Neno lake la kwanza alisema nilikuwa nakusubili nitakuweka ndani zaidi ya wiki mbili. Na wakaniambia walikuwa wananitafuta kwasababu ya taarifa kwa umma niliyoitoa kwa umma 2/7/2025
Mhe. Lissu: Waeleze majaji hiyo taarifa ilikuwa inahusu kitu gani?
Brenda: Inahusiana na Mbunge wa Bunge la Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje kwenye Bunge la EU anaitwa David McAllister, kuhusiana na ripoti kuwa kuna mpango wa Mwenyekiti kupewa sumu akiwa kizuizini gerezani. George Bagyemu akakabidhiwa passport yangu yenye namba TAE481364 ambayo mpaka leo hii sijawahi kurudishiwa passport yangu wala simu yangu.
Mhe. Lissu: Baada ya hapo kilitokea kitu gani?
Brenda: Waliniambia wanaenda kunipekua nyumbani na tulielekea nyumbani Basihaya nikiwa kwenye karandinga la polisi.
Sehemu ya 368

Mhe. Lissu: waeleze majaji mlipofika nyumbani nini kilitokea?
Brenda: Walipekua kila chumba, nguo zote, hawakuniambia wanatafuta nini lakini nadhani hawakukikuta walichokuwa wanakitafuta
Mhe. Lissu: Waeleze majaji Mapolisi waliokupekuwa walikuwa na search warranty or search order.
Brenda: Sikumbuki maana nilikuwa na stress nyingi sana.
Mhe. Lissu: Baada ya hapo nini kilitokea?
Brenda: Tulirudi central polisi na nilikaa central siku nne na nusu lakini sikufikishwa mahakamani wala sikupewa mashtaka yoyote.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji ulikuwa under police custody kwa siku ngapi kuanzia Namanga hadi central?
Brenda: Siku nne na nusu
Mhe. Lissu: Waeleze majaji tangu siku hiyo mpaka leo ulipelekwa mahakamani?
Brenda: Sijawahi kupelekwa mahakamani mpaka leo
Mhe. Lissu: Waeleze majaji wewe kutoa taarifa kwa umma kuhusu chapisho la David McAllister Mbunge wa EU na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la EU alilochapisha kuwa Mwenyekiti anampango wa kuwekewa sumu gerezani, ulitenda kosa gani wewe?
Brenda: Sikutenda Kosa lolote
Mhe. Lissu: Nini kilitokea baada ya wewe kuachiwa?
Brenda niliendelea na maisha yangu kama kawaida.
Mhe. Lissu: waeleze majaji nini kilitokea kwa viongozi wenzako wengine wa chama
Brenda: Wakati siku hiyo nakamatwa Namanga usiku wa Tarehe 12/7/2025 Mtaalamu wa Rasilimali za Chama Leonard Magere nae alikamatwa Julius Nyerere Airport alipokuwa anaelekea London.
Mhe. Lissu: Alishikiliwa kwa muda gani?
Brenda: Sikumbuki ila nilikutana nae Mahabusu Central Police Dar es Salaam. Nakumbuka Amani Golugwa nae alikamatwa Airport akiwa anaelekea Belgium na pia kulikuwa na mwendelezo wa ukamataji maana Makamu nae alikamatwa na kukaa mahabusu muda mrefu.
Mhe. Lissu: Wewe ulikamatwa, Magere alikamatwa, Makamu alikamatwa , waeleze majaji nani alifunguliwa kesi mahakamani?
Brenda: Hakuna aliyefunguliwa kesi mahakamani
Mhe. Lissu: Nataka nikuulize maswali machache nimalizie
Jaji Ndunguru: Amechomekea Machache mangapi?
Watu kicheko: 😂😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Hayatafika kumi.
Mhe. Lissu: Hotuba yangu ya tarehe 3/4/2025 ilihusu mambo gani makuu?
Brenda: Waheshimiwa Majaji Mwenyekiti Lissu alieleza matatizo ya mifumo ya uchaguzi, sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho, matatizo yaliyotokea chaguzi zilizopita, kwanini Nchi inahitaji electrol reforms, kwanini tunapaswa kuwaelimisha wananchi kuhusu msimamo wa No Reforms, No Elections. Alisema, bila reforms ni ngumu kupatikana kwa democratic elections. Hayo maneno ya uasi yalitokana na msimamo wa G-55.
Mhe. Lissu: G-55 ni watu gani?
Brenda: G-55 ilikuwa ni kikundi cha watu ndani ya chama waliotaka kushiriki uchaguzi. G-55 waliandika kwenye social media kuwa msimamo wa no reforms no election unaashiria uasi kwahiyo Mwenyekiti alikuwa anaelezea huo uasi kuwa ni kupinga uchaguzi ambao sio huru na sio wa haki.
Hapa Brenda ameleta ushahidi mzuri wa hii G-55 ambao mashahidi waliopita hawakuusema.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji uwepo wa nia ya kuitishia serikali katika hotuba yote hiyo ya masaa mawili na nusu hadi matatu
Brenda: Sioni nia ya kuitishia Serikali katika hotuba ile.
Mhe. Lissu: waeleze majaji umenifahamu kwa muda gani na unanifahamu kuwa mimi ni mtu wa aina gani?
Brenda: waheshimiwa majaji namfahamu Mwenyekiti kwa miaka 13 kama kiongozi anayepigania demokrasia, anayepigania haki haki, kama mgombea wa Urasi 2020, Mwenyekiti wa chama na kama mpiganaji aliyeumizwa na serikali ya Tanzania kwa kutokupewa mafao yake ya kibunge kwa kuwa harassed na kukamatwa mara kadhaa na kuwekwa mahabusu na kutolewa kwasababu ya misimamo yake ya kupigania haki na pia namfahamu kama Mwenyekiti wa Chama Kikuu Tanzania CHADEMA.
Sehemu ya 369

Mhe. Lissu: Waambie majaji mtu akikuambia kwamba huyo mtu uliyemuelezea hivyo ni mhaini wewe utasemaje?
Brenda: Kwa maneno yangu inaonyesha ni mzalendo, very patriotic mwenye mapenzi makubwa na nchi yake na mtu ambaye anapenda haki ni ngumu kuwa mhaini
Mhe. Lissu: nimemaliza waheshimiwa majaji.
Sasa ni zamu ya mawakili wa Serikali kuuliza maswali ya Dodoso.
Baada ya Mheshimiwa Tundu Lissu kumaliza Examination in Chief sasa yanaanza maswali ya Dodoso na anasimama Ajuaye anasema ataanza Wakili Winniwa Kuuliza maswali.
Anasimama Winniwa.
Winniwa: Habari ya asubuhi na pole kwa ushahidi mrefu
Brenda: Ahsante.
Winniwa: Ni sahihi nikisema kwamba hujaelezea kuhusu elimu ya uandishi wa habari?
Brenda: Sijaeleza.
Winniwa: Ni sahihi nikisema katika utendaji wako kama Mkurugenzi wa Habari unafanya kazi kimazoea?
Brenda: Hapana.
Winniwa: Ni sahihi hujasema una uzoefu wa muda gani?
Brenda: Nina uzoefu wa mwaka mmoja na miezi mitano. Nilisema kuwa nilichaguliwa Mwezi March 2025.
Winniwa: Ni sahihi hujasema kuwa majukumu yako ni yapi kama Mkurugenzi?
Brenda: Ni sahihi
Winniwa: Ni sahihi ulisema uliandaa matangazo kwa ajili ya kualika watia nia?
Brenda: Sahihi
Winniwa: Hujataja hizo pages ni sahihi ulikopost?
Brenda: Ni sahihi.
Winniwa: Unaelewa maana ya live streaming?
Brenda: Is to show something by live broadcast.
Winniwa: Ni sahihi Chama chenu kinafanya kazi bega kwa bega na Jambo TV.
Brenda: Sijui kuhusu kufanya kazi nao Bega kwa Bega. Sisi tunafanya kazi na vyombo vya habari vyote.
Winniwa: Siku ya Mkutano wa Tar. 03/04 Msemaji Mkuu alikuwa ni Mwenyekiti Tundu Lissu?
Brenda: Ni sahihi
Winniwa: Siku ya Mkutano huo kuna muda mlikuwa hamna control yoyote ya waandishi ni sahihi?
Brenda: Sio sahihi. Tulisema tumewaalika waje kufanya coverage ya tukio la Chama.
Winniwa: Kuna muda mliwaondoa watu watoke nje ya ukumbi wa mkutano?
Brenda: Kuna muda tuliwaondoa ndio.
Winniwa: Kuna maneno umetajiwa sana kuwa yalikuwa quoted. Sasa ni kweli ulikuwepo na ulisikia maneno kama kukinukisha na kuvuruga uchaguzi.
Brenda: Yapo kwenye hati ya mashitaka na yapo kwenye maneno aliyoyazungumza Mwenyekiti.
Winniwa: Nina uhakika nikisema Chama kilisusia uchaguzi?
Brenda: Hatukususia uchaguzi. Ingawa fomu hatukuchukua.
Winniwa: Unaelewa nini ukisema No Reforms: No Election
Brenda: HAKUNA MABADILIKO HAKUNA UCHAGUZI.
Winniwa: Mabadiliko gani mlikuwa mnataka?
Brenda: Electoral Reforms yaani Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asiwe mtu wa kuchagua mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi.
The President should not be able appoint delegate of the commission of the electoral committee, wasimamizi wa Uchaguzi wa Kata wasiwe watendaji wa Kata.
Winniwa: Kwa hayo uliyosema ndio uliona ndio njia ya kuwafanya msusie uchaguzi?
Brenda: Sisi tulikuwa huru Serikali ya wakati huo iendelee hata miaka 3 ili tuwe na mabadiliko ya sheria ndio tufanye a democratic election.
Winniwa: Nchi yoyote chaguzi zipo kisheria?
Brenda: Ndio ziko kisheria lakini chaguzi huru na haki lazima ziwe hivyo.
Winniwa: Kwahiyo mtu akitaka kuvuruga uchaguzi atakuwa anatenda kosa?
Brenda: Sio kweli.
Winniwa: Umesema scenario ndefu kuhusu kukamatwa kwako na ulikuwa unaenda safari ya German. Umeleta uthibitisho wowote kuhusu mwaliko wako wa kwenda German?
Brenda: Sijaleta uthibitisho.
Winniwa: Umesema kama umewahi kupeleka malalamiko yako yoyote kuhusu wewe kukamatwa na kuzuiwa kufanya safari?
Brenda: Sijawahi kufanya hivyo.
Sehemu ya 371
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia Cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu, Brenda Rupia ambae ni Mkurungenzi wa Mawasaliano wa CHADEMA HQ.
Thawabu: Huyo mwamba hapo Ameshitakiwa kwa kukiuka kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu. Hiyo ni sheria na Mahakama imepewa mamlaka ya kutafsiri sheria na ibara ya 107 ya Katiba ndio inasema hivyo isome.
Anaisoma Brenda. Sasa Swali langu ulipokuwa unasema hayo kwamba hajafanya kosa una hayo mamlaka?
Brenda: Ibara ya 107 inasema mwenye mamlaka ya mwisho. Mimi nina mamlaka ya kusema ila mahakama wanayo mamlaka ya mwisho.
Thawabu: Uhaini ni nini?
Brenda: ku betray your country kutaka kupindua Serikali huo ndio uhaini.
Thawabu: Kuhusu kuhamasisha uasi kamusi ya kiswahili inasemaje kuhusu neno uasi?
Brenda: Ni kitendo cha uvunjaji wa sheria lakini B inasema kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka
Thawabu: Kwahiyo tafsiri mojawapo ni kuvunja sheria?
Brenda: Tafsiri mojawapo ni hiyo pia.
Thawabu: Nchi yetu ni nchi ya utawala wa ki imla?
Brenda: Kwa sasa ni nchi ya ki imla inavyoendeshwa.
Thawabu: Yanayofanyika hapa Mahakamani ni mambo ya kiimla?
Brenda: Hapa ni mambo ya kisheria.
Thawabu: Ulisema unaweza kufanya miujiza?
Brenda: Hapana.
Thawabu: Uliwezaje kupanda kwenye gari ambalo halina milango
Brenda: Magari ya polisi yanaeleweka yalivyo.
Thawabu: Walikutesa sana kwenye ile Probox?
Brenda: Hawakunitesa.
Thawabu: Ulikuwa upande wa kulia au kushoto nyuma ya Probox?
Brenda: Upande wa kushoto.
Thawabu: Watu wangapi walikuwepo kwenye gari?
Brenda: Ni watu wawili na mimi watatu.
Thawabu: Nitakuwa sawasawa nikasema ushahidi ulioutoa hauhusiani kabisa na hii kesi?
Brenda: Sijui.
Thawabu: Ile hati yako ya kusafiria ilikuwa inahusiana nini na yeye kukamatwa?
Brenda: Ulikuwa ni mwendelezo wa ukandamizaji wa viongozi wa Chadema. Vyombo vya dola kuendelea kukandamiza watanzania.
Thawabu: Hicho kifungu cha 39 cha Penal Code kinahusiana nini?
Brenda: Huo ni mwendelezo wa kukandamiza viongozi wa upinzani na shitaka hilo ni la uongo. Mwenyekiti sio muhaini. Anamsomea Kamusi hapa Brenda.
Thawabu: Unaweza kusoma kingereza au kiswahili?
Brenda: Anasoma hapa kifungu cha 39. A person who being allegiance to the united republic
Thawabu: Maana yake nini hiyo
Brenda: Mtu mwenye utii kwa Jamhuri ya Muungano
Thawabu: endelea
Brenda: In the united or elsewhere murders or attempt to murder na haya yote Mwenyekiti hajafanya hata moja.
Watu wanacheka😂😂😂
Thawabu: Sijakuuliza useme amefanya au hajafanya.
Brenda: Umesema nisome na kutafsiri. Tulia nifanye hivyo Mwenyekiti hajaua Rais.
Anasimama Mheshimiwa Lissu muda umeisha tayari.
Kesi imehairishwa kwa muda wa saa moja na nusu, Tunaenda break.
Sehemu ya 372
Mahakama imerejea muda huu. Saa tisa kasoro 5 alasiri.
Mhe. Lissu yupo,
Upande wa Jamhuri wanasema wapo kama walivokuwa asubuhi.
Shahidi anaelekea kwenye kizimba.
Jaji Ndunguru anamkumbusha Shahidi kwamba yupo chini ya kiapo.
Wakili wa Jamhuri Thawabu ameanza kumfanyia Cross examination Shahidi no. 4 wa Mhe. Lissu
Thawabu: Mshitakiwa anasema anashitakiwa kwa kurusha matangazo Jambo TV. Amekupitisha kuhusu mashitaka anayokabiliwa nayo?
Brenda: Amenipitisha nikiwa hapa kizimbani.
Thawabu: alichapisha kupitia jambo TV hapa ipo au haipo?
Brenda: Jambo TV haijatajwa hapa na mimi nilikuwa natetea hiyo hiyo hati ya mashitaka.
Thawabu: Umemtaja John Heche kwenye sekretarieti?
Brenda: Huyo sio sekretarieti.
Thawabu: John Pambalu, John Kitoka, John Mnyika ili uwe sekretarieti ni lazima uitwe John?
Brenda: Mimi naitwa Brenda.
Thawabu: Jibu swali sasa
Brenda: Nimeshajibu. Obvious kwa vile naitwa Brenda mimi sio John. Unasemaje wajumbe wa sekretarieti.
Thawabu: Unamjua Diamond, Mboso, Harmonize?
Brenda: Nawasikia.
Thawabu: Wanachoimba kikichezwa kwenye chombo kinakuwa sio chakwao?
Brenda: Kawaulize wao sasa.
Thawabu: Anachosema Lissu kikirushwa na Jambo kinakuwa cha nani?
Brenda: Kinakuwa cha kwao. Ndio wamiliki wa hiyo content waliyoipandisha.
Thawabu: Kipimo cha kuyasema maneno hayo sio kosa ni kipi? Angeyasema kwa muda mrefu ingeathiri nini?
Brenda: Sio kosa hata angesema muda mrefu.
Thawabu: Kuna maneno Rais wa Jamhuri ya Muu gan, Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mashitaka. Ukasema hakuwataja. Wewe ni nani kati ya hao?
Brenda: Mimi sio Rais, sio Mkurugenzi wa Mashitaka. Sio Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Thawabu: Unajuaje kutishika kwa Serikali ya Jamhuri
Brenda: Mimi sijasema hayo mambo. Nashangaa ukisema mambo ya serikali kutishika.
Thawabu: Tusomee tena kuhusu maana ya neno uasi?
Brenda: Kitendo cha kupinga au kuwa kinyume na mambo yanayofanywa na serikali
Thawabu: Soma maana ya kwanza
Brenda: Ni kitendo cha kutaka kuiondoa serikali iliyoko madarakani......
Thawabu: Kufanya kitu kitoe halafu mbaya ni kosa au sio kosa?
Brenda: Sio kosa
Thawabu: Kufuga kuku halafu zikatoa harufu ni kosa au sio kosa?
Brenda: Inategemea utakuwa unafugia wapi?
Jaji Hebu tuendelee mambo ya kufuga Kuku hayo.
Thawabu: Unajua kuhusu Baraza la Kutunza mazingira?
Brenda: Najua NEMC sasa inahusiana nini na kesi hii.
Thawabu: Wewe ni mtaalamu wa hesabu?
Brenda: Mimi nimesoma Accounting.
Thawabu: Tar. 10/06 Tar. 17/06 ulikuwa unatumia calendar gani?
Brenda: Nilikuwa nasema tarehe hadi mwaka na aina za Calendar sijui kabisa.
Thawabu: Hapa Tanzania kuna vyama vingine?
Brenda: Najua Chadema, ACT Wazalendo, Chaumma.
Thawabu: Uliposema Mwenyekiti wa Chama ulisema ulikuwa unasema Mwenyekiti wa Chama ulikuwa unamaanisha Chaumma?
Brenda: Nilipokuwa nasema nilisema mimi ni mkurugenzi wa Chadema. Niliposema hivyo ni Chadema.
Thawabu: Unapokuwa Mkurugenzi unaweza kujua Mwenyekiti analipwa na nani?
Brenda: Sijui
Thawabu: Kwahiyo huwezi kujua analipwa na jambo ndio asiwe mfanyakazi wa jambo tv?
Brenda: Hilo siwezi kujua na nyie mmeleta ushahidi wowote kuwa Mwenyekiti ni mfanyakazi wa Jambo Tv.
Thawabu: Kwenye mkutano wenu G55 waliongea saa ngapi?
Brenda: Hawakuongea na tusingewalazimisha kuongea pia.
Thawabu: Hii sio mahakama ya hisia?
Brenda: Ndio.
Thawabu: Ukimaliza kesi hii wakiona wanataka kukupeleka Mahakamani kwenye ile kesi yako uko tayari?
Brenda: Niko tayari.
Thawabu: Nimemaliza naomba aendelee mwenzangu.
Anasimama Job Mrema nae kuuliza maswali.
Sehemu ya 373
Upande wa Jamhuri wanaendeleaje kumfanyia Cross examination Brenda Rupia
Job: Ni sahihi ulishiriki kwenye mkutano wa Tarehe 03/04?
Brenda: Nilishiriki
Job: Mwenyekiti wa CHADEMA wakati anaongea na wajumbe alipotamka haya maneno aliungwa mkono au hakuungwa mkono?
Brenda: Hakukuwa na hilo swali kwenye mkutano.
Jaji jibu tu swali sasa.
Brenda: sasa sijui.
Job: Majukumu yako ni yapi?
Brenda: Kusimamia itifaki asipokuwepo Naibu Katibu Mkuu
Job: Sehemu ya mawasiliano unafanya nini?
Brenda: Mimi nakuwa incharge wa kuwaalika waandishi wa habari kuja kufanya coverage kwenye matukio ya Chama. Na kupitia hao waandishi wa habari Chama kinawasiliana na Umma. Mimi pia nina oversee utendaji wa kazi ambazo zinafanywa na watu waliopo chini yangu.
Job: kwahiyo wewe ni afisa mualikaji na sio afisa mawasiliano?
Brenda: Hauko sahihi, I have people work under me, on behalf.
Job: Hao watu walioko chini yake wanatekeleza majukumu yangu?
Brenda: Wanawasiliana na watu kupitia mitandao, wanaalika waandishi wa Habari pia. Wanawasiliana na umma kupitia vyombo vya habari, wanatoa pia taarifa.
Job: Wewe kama Mkurugenzi wa habari unaitumia?
Brenda: Naitumia.
Job: Wewe una elimu gani?
Brenda: Accounting
Job: Wewe una taaluma ya habari?
Brenda: Sina.
Job: Umewahi kusikia neno Kishoka?
Brenda: Hiyo Kishoka kingereza maana yake ni nini?
Job: Hatuongei Kingereza hapa.
Job: Mtu yeyote ambae anatoa huduma ya habari na sio mwanahabari kwa sheria za Tanzania
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Wakili anapiga sana kelele hapa Mahakamani, nuisance. Hayo sio maswali kabisa.
Job Mrema: Wewe unayefanya kazi katika idara unafanya kimakosa na uko pale kimakosa?
Brenda: Idara sio mtu mmoja.
Job Mrema: Kumbe hukupaswa kwahiyo kuwa kwenye hiyo kurugenzi hebu fafanua?
Brenda: Kwani Katibu wa Itikadi wa CCM nae amesomea habari wapi?
Jaji: Hayo sasa yaache kwanza.
Brenda: Sasa asiniambie nifafanue.
Job: kwahiyo mtu anayefanya hizo kazi za habari bila sheria ni Kanjanja?
Brenda: Kwa kingereza hiyo maana yake nini?
Job: Huko usiende
Lissu: Anasimama anasema Mh. Jaji hilo neno Kanjanja amelitoa kwao huko anakuja kuuliza. Maana kwenye Kamusi halipo. Asilete maneno ya kikabila chao ayalete hapa.
Job: Sasa shahidi umeelewa
Brenda: Sijaelewa.
Job: Mtu yeyote anayetoa habari kinyume na sheria ambae hana sifa hapaswi kutoa hiyo huduma.
Brenda: Sijui.
Job Mrema: Umekuwa mwanachama wa Chadema toka lini?
Brenda: 2013
Job: Miaka mingapi uko nayo Chadema.
Brenda: Ndio uhesabu.
Job: Falsafa ya Chama ni nini?
Brenda: Ni nguvu ya umma
Job: maana yake nini hiyo falsafa ya umma
Brenda: Kushirikisha umma katika maamuzi ya vikao vya Chama, Kushirikisha umma kuhusiana na Uchaguzi kuchagua viongozi ambao umma unataka, kushirkisha umma katika matumizi ya rasilimali za nchi na kushirikisha umma kwenye jambo linalohusu nchi yao na Chama chao.
Job: Kwahiyo hiyo ndio tafsiri ya Katiba?
Brenda: Hiyo ndio tafsiri yangu.
Job: Soma hiyo ibara ya 3.3
Brenda: anasoma kuhusu Nguvu ya Umma na wananchi kuwa ndio msingi huo wa nguvu ya umma katika kila kitu.
Job: Wakati mshitakiwa anatamka maneno yale Tar. 03/04 ulimuunga mkono?
Brenda: Nilimuunga mkono na Mpaka leo nakubaliana nae kwa hayo maneno.
Job: Tunakubaliana kuwa nchi hii ina Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Brenda: Sahihi
Job: Ibara ya 3.1 ya Katiba ua Chadema inakielekeza Chama kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya 374 ya Kesi itaendelea.....
Part 374
Job: Ibara ya 3.1 ya Katiba ya CHADEMA inakielekeza Chama kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Jaji, wakili anazungumza kama yuko mnadani. Atumie lugha ya kawaida. Napata sana shida mimi.
Job: Ni sahihi kwamba Ibara ya 3.1.3 inalinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Brenda: Ni sahihi.
Job: Ni sahihi Katiba ndiyo inaweka msingi wa utungwaji wa sheria zote nchini?
Brenda: Sahihi.
Job: Sheria ya uchaguzi ni sheria iliyotungwa kwenye msingi wa Katiba hii?
Brenda: Sahihi.
Job Mrema: Suala la kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni ukiukwaji wa Katiba hii?
Brenda: Sio sahihi.
Job Mrema: Hujui kama Katiba inaruhusu kuvuruga uchaguzi?
Brenda: Sijui, ndiyo.
Kwa kifupi, wataalamu wanasema ili umuelewe Brenda, unapaswa kuwa na fikra tunduizi (Critical Discourse Analysis), anapenda sana kuielezea Dkt. Azaveli Lwaitama.
Job: Anaendelea. Ni sahihi ili ushiriki uchaguzi lazima usaini Kanuni za Maadili za Uchaguzi mwaka 2020?
Brenda: Sikumbuki.
Job: Utakubaliana na mimi kuwa mwaka 2020 CHADEMA ilisaini Kanuni za Maadili?
Brenda: Nilishakujibu hata hilo.
Job: Jibu swali sasa.
Brenda: Don't panic, just relax. Nilishakujibu, sijui.
Job: Unaunga mkono maneno yaliyoandikwa kwenye hati ya mashitaka. Sasa, kitendo hicho cha kuunga mkono maneno ya Ibara ya 3.1.3 ya Katiba ya CHADEMA?
Brenda: Huwezi kuwa sahihi.
Job Mrema: Kwa lugha nyingine, suala la kuvuruga uchaguzi, kukinukisha, msingi wake unatokana na Ibara ya 3.1.3 ya Katiba.
Brenda: Ndiyo, unatoka na msimamo wa Chama kuamini katika nguvu ya umma.
Job: Wakati shauri hili linaendelea, wewe umewahi kutoa tamko lolote kuhusu kesi hii?
Brenda: Sikumbuki.
Job: Ulisema kama una matatizo ya kumbukumbu...
Brenda: Niko vizuri sana. Nimetoa matamko mengi sana. Kuhusiana na kumshitaki Mwenyekiti kwa kesi ya uongo, nimesema nia mbovu ya Serikali kumshitaki Mwenyekiti. Nimesema kuhusu nia mbaya ya Serikali kwa viongozi wa CHADEMA na Chama kwa ujumla. Hayo nimesema.
Job: Ulitoa kupitia nini?
Brenda: Simu yangu, kule TikTok.
Job: Ulikuwa unaongea na nani?
Brenda: Niko na simu yangu, naongeaje na mtu? Nilikuwa TikTok, nimesema.
Job: Kutokujua sheria sio kinga?
Brenda: Nafahamu.
Job: Na jinai haiozi?
Brenda: Ndiyo.
Job: Utakubaliana na mimi kuwa tamko hilo ulilolitoa ni kinyume na sheria za nchi hii?
Brenda: Sifahamu.
Job Mrema: Mheshimiwa Jaji, naomba kumalizia hapa. Niwaache wenzangu.
Akiwa amesimama, Katuga anasema:
Katuga: Naomba mshitakiwa apatiwe nyaraka zake, amezishika.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji, nyaraka zangu zimefikaje kwao hawa? Hawatakiwi kushika nyaraka zangu kabisa. Hawa ni maadui zangu, wanapewaje wao?
Jaji: Kwani nani kawapa tena?
Katuga: Wewe ni Mnyamwezi mwenzangu?
Brenda: Mimi ni Mnyamwezi.
Katuga: Sisi ni kaka na dada.
Brenda: Hilo hapana. Siwezi kuwa kaka na dada na mtu anayetaka Mwenyekiti wangu anyongwe.
Katuga: No Reform ililenga nyanja gani?
Brenda: Nyanja ya kisiasa.
Katuga: Kama kwenye hotuba ya Mwenyekiti, baada ya hotuba uliiona hiyo video?
Brenda: Nimeiona kwenye Jambo TV pia.
Katuga: Neno “kukinkinukisha” sio Kiswahili fasaha, ni slang?
Brenda: Nilisema ni slang.
Katuga: Kwa hiyo ni lugha inayotumika na kikundi fulani cha watu?
Brenda: Inaweza kuwa ni sahihi.
Katuga: Ulisema maana yake na inatumika na watu gani?
Brenda: Nilisema maana yake; hilo la kutumika na kikundi gani?
Katuga: “Kukinukisha” uliposema ni kukifanya kinuke au kunukia.
Brenda: Both ni Kiswahili na ni slang.
Katuga: Nikisema sisi watoto wa mjini, nikisema “kukinkinukisha” ni slang inayotumika na vijana wengi?
Brenda: Sahihi.
Part 375 itaendelea kwenye post inayofuata.
Part 375
Katuga: Nitakuwa sahihi kuwa “kwenda kukinukisha” ni kufanya kitu kisivyo sahihi?
Brenda: Sijui.
Katuga: Hujui na slang yako?
Brenda: Slang yetu wote.
Katuga: Waambie Majaji, kwa cheo chako, kama nilikusikia ukisema Rais wa Serikali ya Muungano wa Tanzania hakutajwa, waambie Majaji. Serikali ya Muungano iko nchi gani?
Brenda: Tanzania.
Katuga: Serikali ya Muungano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kitu sawa?
Brenda: Nilifanya marekebisho kuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jaji Nduguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi. Shahidi bado hujamaliza kutoa ushahidi, hivyo kesho utaendelea na maswali ya dodoso na maswali ya rejea, kama yatakuwepo.
Inapigwa: High Coooooouuuuurrrrrt!
Majaji wanainuka na kutoka.
Mhe. Lissu anakusanya makabrasha yake huku akiagana na viongozi pamoja na wanachama waliofika Mahakamani.
Tukutane kesho asubuhi.