Ujumbe ulisomeka hivi;
"Akishakufa, msimlete Dar es Salaam wala asiagwe popote, mpelekeni haraka kijijini kwao na mazishi yafanyike haraka". Lakini Mungu ni nani? Mungu ni mmoja tu.
Siku kama ya leo, miaka 10 iliyopita yaani Tar. 7 Septemba 2016, Tundu Lissu, akiwa kwenye makazi ya wabunge alishambuliwa kwa risasi na watu waliokusudia kumuua. Lakini hakufa.
Ilikuwa mchana, jua linawaka, hadharani kwenye makazi ya wabunge. Wauaji walirusha risasi 37, ambapo 16 zilimpata mwilini, na bado hata baada ya matibabu ya muda mrefu kuna risasi inaishi katika mwili wake hadi leo, ambayo haijatolewa kwa sababu za kitabibu.
Leo ni miaka 10, hakuna nukta ya uchunguzi uliofanyika. Ukijumlisha kauli na vitendo vya viongozi wa serikali na vyombo vya ulinzi, unapata kuona ishara kuwa wahusika wa tukio hilo na mengine yanayofanana ni watu wenye madaraka ndani ya serikali ya Tanzania.
Jambo la kumshukuru Mungu, leo Tundu Lissu yupo hai na ana furaha tele. Mungu alimponya Lissu asife, alimponya kupitia watu wengi waliotumia nafasi zao, taaluma na vipawa vyao, mali zao na upendo wao.
Freeman Mbowe, akiwa M/kiti wa CHADEMA aliongoza hatua zote za msaada zilizohitajika kutokea Dodoma, hadi kupelekwa Nairobi.
Salim Turkey alisaidia usafiri wa ndege binafsi uliomsafirisha Lissu kutoka Dodoma hadi Nairobi.
Dr. Mpoki Ulisyubisa, akiwa katibu mkuu wa Wizara ya Afya, bingwa wa tiba dharura, alivua suti na kuvaa koti la daktari na kuongoza matibabu ya dharura katika hospitali ya Mkoa ya Dodoma, ili kuokoa maisha ya Lissu kabla ya kumsafirisha Nairobi kwa matibabu zaidi.
Bila kuwasahau wote waliochangia damu, waliokwenda kumpa faraja, na waliojitolea muda na mali zao hadi leo.
Mungu ni mmoja tu, na ndiye aliamua Lissu aishi. Na kwa hakika Lissu anaishi.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.