UPDATES_ZOTE_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 17, 2026
Wanaingia mawakili wa Serikali,
Then kaingia Mhe. Lissu akiwa anasindikizwa na kundi la askari magereza wapo wengi kama kawaida yao.
Mhe. Lissu kaingia na vibe la kutosha na Wanachama na Wananchi waliojitokeza Mahakamani wanapiga makofi mengi ya shangwe.
Imepigwa High Cooooooourt...
Majaji wanaingia, wapo watatu wakiongozwa na Jaji Ndunguru, wanaketi kwenye viti vyao.
Karani anasoma case no . —- Jamhuri Vs Tundu Antipas Lissu
Anasimama Wakili wa serikali anatambulisha jopo la Mawakili wa Serikali na mtuhumiwa Mhe. Lissu
Wakili wa Serikali anasema wana maombi mawili ambayo wanaomba kuyawasilisha;
Jaji anasema tuendelee
Wakili wa Serikali anasema maombi hayo atawasilisha wakili Katuga.
Wakili wa Serikali -Katuga anasema Waheshimiwa majaji upande wa Jamhuri tunamaombi mawili
1.Baada ya kupitia ushahidi ambao umeshatolewa hapa Mahakamani na mashahidi waliobaki, baada ya kuangalia agreed facts, upande wa Jamhuri unaona ni ushahidi toshelezi, hivyo tunaitaarifu Mahakama kuwa Upande wa Jamhuri unafunga ushahidi wake na kwamba tunaomba imark kwamba upande wa Jamhuri unafunga case yake.
2. Ingawa hakuna kifungu kinaonyesha majumuisho ya no case to answer, mimi naliita kuwa ni kosa ambalo siyo kosa zoefu hasa kwajinsi tunavyomtuhumu mtuhumiwa kulicommitt, hivyo tunaomba tufanye submission ya no case to answer.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama anachokusema?
Mhe Lissu: Kwanza kuhusiana na kufunga kesi kwa upande wa mashtaka, hilo sina shida nalo nilisema toka wiki iliyopita tayari wameshakata pumzi.
Watu wanacheka 😂😂😂😂
Kuhusu ombi la pili, Wakili Katuga anasema kuwa japo hakuna kifungu, mimi nasema kifungu kipo pale ambapo ushahidi wa upande wa mashtaka umefungwa, na kwamba pale ambapo Mahakama inaona hakuna kosa ambalo mtuhumiwa ametuhumia nalo then Mahakama husikiliza pande zote mbili kama kuna kesi ya kujibu au la, kifungu cha 312 (1) cha sheria ya mwenendo wa mashtaka, naomba nikisome
(anasoma...)
Hivyo Waheshimiwa Majaji, kwa practice mtuhumiwa ndiye anayeanza kuwasilisha hoja za kama ana kesi ya kujibu au la, mimi niko tayari kuanza Waheshimiwa.
Asante ni hivyo tu.
Wakili wa Serikali - Katuga amewainamia mawakili wa serikali ni kama kuna jambo wanajadili.
Wakili wa Serikali Katuga anainuka anasema Waheshimiwa Majaji, Mtuhumiwa amewalika kwenye kifungu 312(1) hii inahusu no case to answer, mimi nimewaalika kwenye case to answer, Waheshimiwa hicho kifungu alichokitumia inasema statement iliyotumiwa, itatuleta tafsiri tofautitofauti kwa nature ya case hii, halafu kinazungumzia Mawakili wa pande zote mbili hakizungumzii mtuhumiwa ambaye hajawakilishwa, ndo maana nikasema hakuna kifungu mahususi, hii inabaki kuwa discretion ya Mahakama.
Upendeleo wetu tunaichia Mahakama, kuna written submission na kuna oral, ambapo bado Mahakama hii haijaamua.
Waheshimiwa at this instance hatuthibishi guilty ni primacie case to answer.
Anasimama Mhe Lissu anasema Waheshimiwa Majaji hili jambo ni dogo sana, halitaki majadiliano makubwa hivi. Kifungu No. 312(1) inaipa wajibu Mahakama na siyo discretion. Kifungu kinazungumzi no case to answer, hakuna mahali inaonyesha case to answer
Wakili wa Serikali - Katuga anasimama nakusema kuwa Waheshimiwa majaji mimi sijasema hayo naona mtuhumiwa anajielekeza kwenye mambo mengine, labda kama ni off record.
Mhe. Lissu : Waheshimiwa naomba mniache nimalizie.
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema, aah sasa basi mtuache sisi tuamue hilo, uzuri wote mnakubaliana kuwa mnafanya submission.
Wakili wa Serikali - Katuga & Mhe. Lissu: sawa Waheshimiwa majaji.
Wakili wa Serikali - Katuga: Naomba mshtakiwa apewe hii East Africa Law Report aliyopewa na Mawikili wake wa research.
Mhe. Lissu anakabidhiwa.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa rudia ile reference
Mhe. Lissu: Mimi nilikuwa nanukuu tu ile section 312(1) na kwa mujibu wa ile mimi ndiyo nilikuwa napaswa kuanza, hivyo naomba kuanza.
Jaji Ndunguru : eeeh prosecution?
Wakili wa Serikali - Katuga: Sisi hatuna pingamizi waheshimiwa.
Jaji Ndunguru : Case upande wa mashtaka imefungwa, na mnapaswa kusubmitt kwa mdomo.
Mhe Lissu anasema Waheshimiwa Majaji baada ya kusikiliza ushahidi wote wa upande wa mashtaka wa mashahidi wote 17, naomba kutoa hoja kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kabisa kuthibitisha kwamba kuna prima facie case ya kuiwezesha Mahakama hii kumtaka mshtakiwa ajitetee.
Sasa Waheshimiwa majaji prima facie case ni kitu gani?
Waheshimiwa majaji prima facie case/ primafacie evidence ni ushahidi wa mashtaka unaotolewa na upande wa mashtaka ambao usipojibiwa kwa ushahidi wa utetezi mtu anafungwa au analipa fine ambapo kwa case kama ya uhaini mtu ananyongwa.
Kama upande wa mashtaka umetoa ushahidi ambao hata mtuhumiwa hawezi kujibia/ kujitetea then hakuna hatia (prima facie case)
A primafacie evidence siyo ushahidi wa mwisho katika case, ushahidi wa mwisho ni ule unaojumuisha ushahidi wa utetezi, hivyo Prima facie case ni ushahidi wa upande wa Jamhuri.
Msingi wa kisheria wa primafacie case to answer ni kifungu cha 312 (1) ambacho nimeshakisoma, hiki kimefanyiwa maamuzi mengi za Mahakama za juu ambacho kimetengeneza misingi ya kisheria ( Legal principles ) kuhusiana na nini kinapaswa kufanyanyika kuhusiana na hoja ya hakuna case ya kujibu.
Kesi ya East Africa ya Raumanlal Trambaklal Bhatt v Public 332 esp 334-335 hii ina umuhimu ule wa case ya Mkisa Biscuit kwa namna ilivyoweka msingi kisheria Mhe. Lissu
(anasoma citation ya Tramnaklal case)
Mahaka imesema, haitoshelezi tu kuwa ushahidi mwingi umetolewa tu, lazima ushahidi huo mwingi uwe na uzito na credibility.
Waheshimiwa msingi huu Tramnklal ulikubaliwa na Mahakama hiyo ya rufani katika case ya Murini vs Jamhuri 1967 EA 542, Uk 544, Mahakama ilinukuu approval uamuzi wake wa miaka kumi kabla wa case ya Tramnklal.
Mhe. Lissu anasema Katika kifungu cha 546 cha criminal procedure code ambacho kwasasa ni kifungu cha 312 (1).... kwamba masharti ya kifungu cha 246 ambacho saa hizi ni 312 (1) ni cha lazima , wajibu wa kuthibitisha mashtaka upo kwa Upande wa Mashtaka, na sheria yetu imeweka wazi kwamba endapo utashindwa kuthibitisha basi Mahakama itapaswa kumwachia mtuhumiwa.
Maamuzi yote haya yanasema kama Mahakama itamwita mtu ajitetee wakati asipojitetea hakutwi na hatia hii ni makosa kwa mujibu wa case ya Murini vs Republic.
Mahakama ya rufaa Kenya, katika case ya Antony Njuwe Njeru Vs Republic 2006 EKLR, Na yenyewe ilikubali msimamo wa case ya East Africa ya Trambklal
Case ya Republic Vs Benard Ruwangu Ingubu, 2025 KHC 11026 ( KLR) pia imekubali msimamo huo, case nyingine ni case ya Republic Vs James Ogwagwa Nyakina & another, 2025 KEHC 11403 (KLR)
Mahakama ilikuwa ikijadili kifungu ambacho kinaendana na kifungu chetu cha 312 (1)
Waheshimiwa baada ya kuweka huo msingi, naomba nizungumzie kesi ya uhaini inayonikabili, hii siyo kesi ya kwanza katika nchi yetu ni kesi ya tatu, kesi mbili zilizotanguliwa ziliamliwa finally, case ya Grey Likungu Matata na wenzake Vs Jamhuri, (1971) EA496 Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki, na case ya Khatibu Gandi na wenzake TLR.
Katika kesi ya Grey Likungu Matata, Mahakama iliweka masharti matatu ya kuthibitisha uhaini;
i) utiifu kwa Jamhuri/ Raia
ii)Nia ya kutenda kosa
iii)Nia ithibitishwe kwa maandishi au matendo
Waheshimiwa majaji msimamo wa Mahakama wa case ya Grey Likungi Matata ulikubaliwa wote katika kesi ya Tanzania ya Khatibu Gandi katika ukurasa wa 13 wa kesi ya Khatibu Gandi na Wenzake, ambapo iliongeza mengine kwa kujiuliza.... Je maneno matupu yanatengeneza Uhaini? Na majibu yapo ukurasa wa 55, kuwa maneno matupu siyo matendo ya wazi kwenye kosa la uhaini isipokuwa hayo maneno yaelezee kitendo cha uhaini, lakini kusema tu tunataka kuipindua Serikali...hayo ni maneno tu.
Ukurasa wa 67, ijapokuwa ni sahihi kuwa maneno ni maneno matupu, ikiwa ni maneno yanayotumiwa na mtu mmoja, yanaweza kuwa uhaini yakitumiwa na watu zaidi ya mmoja.
Ushahidi unasemaje kuhusiana na nia?
Ushahidi haujathibitisha kama kulikuwa na kosa la kutenda uhaini,
Waheshimiwa majaji kifungu cha 39 (2) (d) kinasema; lazima kuwe na nia ya kuitishia serikali, au bunge au mahakama, shitaka ambalo liko mbele yenu Waheshimiwa majaji linasema maneneno yafuatayo " Tundu Lissu akiwa chini ya utiifu wa Jamhuri ya muungano alionyesha nia ya kutenda kosa uhaini........."
Sheria inasema kosa lazima uitishie Serikali, Bunge au Mahakama, kwa hayo maneno Bunge, Mahakama wala Serikali havijatajwa hata mara moja, swali ni je Serikali imo haimo kwenye hati ya mashtaka? Haimo.
Serikali ni nini Waheshimiwa majaji ? Serikali ni neno la kikatiba siyo maneno ya kuokotwa na Mapolisi mtaani. Serikali imetafsiriwa katika Ibara ya 151 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ooh ooh uchaguzi, ooh Serikali, Serikali haindeshi uchaguzi, uchaguzi unaendeshwa na Tume ya uchaguzi, ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jambo la pili Waheshimiwa majaji, hayo maneno " TUTAZUIA UCHAGUZI" " TUTAKINUKISHA" na mengine yote..... siyo kosa kisheria.
Sheria ya Uchaguzi wa Rais wabunge na Madiwani, 2024 Cap 7 imeanisha makosa kibao ya jinai...ambapo hayo maneno hayamo, sasa hili ni kosa la aina gani? Hakuna.
Infact, hakuna ushahidi wa kutenda kosa lolote la jinai kwa sheria za Tanzania zinazoainisha makosa yanayotokana na hayo maneno waliyoainisha kwenye hati ya mashtaka na kama siyo kosa hakuwezi kukawa na nia ya kosa la uhaini.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji ni muhimu kukumbuka kuwa, mimi ni mshtakiwa pekee katika kesi hii na ikumbukwe katika kesi ya Khatibu Gandi inasema maneno ya mtu mmoja, hayatengenezi uhaini, kwa ushahidi uliotolewa haujathibisha nia ya kutenda kosa la uhaini then on the basis kuwa kusipokuwa na primafacie case nitaitwa nijitetee kwa kipi?
Ni ushahidi gani nisipojitetea utanitia hatiani? Ushihidi ukoje kuhusu publication ya reasonable act?
Lazima kuwe na ushahidi wa machapisho au matendo ya wazi wakati wa pre trial Upande wa Mashtaka wanasema mimi nilichapisha maneno kwenye mtandao wa Jambo TV, hivyo uthibitisho wa haya maneno ulitakiwa uwepo Jambo Tv.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwaelekeze ukurasa wa 185 wa record za Mahakama, upande wa mashtaka ulionyesha ushahidi wa nyaraka 9 na aina 2 za vielelezo ikiwemo Video clips, hawajaleta hata moja.
Shahidi PW 17 ni shahidi pekee wa eye witness aliyenishuhudia kwenye mkutano, testimony ya mashahidi, shahidi PW 17 ndiyo shahidi mwenye ushahidi mzito, alisema yeye na wenzake watano ndiyo waliorecord na kurusha, amesema kwa maneno yake na kwa maandishi kupitia kielelezo D16 na ni shahidi wao, Kwahiyo kama ni tuhuma ya publication siyo yak wangu, aliyepublish ni PW 17 na amesema mpaka leo vipo kwao.
Ushahidi wa nani aliyechapisha hawajaujibu.
Waheshimiwa Majaji, walidai ooh wewe ndiye uliyeitisha Mkutano, shahidi wao PW 17 amesema mwaliko waliupata kwa afisa habari wa Chadema anaitwa Brenda Rupia, na nikamuuliza uliniona mimi nikifanya maandalizi nikipanga viti akasema, hakuna.
Kwenye hili suala la tatu hawajathibitisha kabisa kosa la kuchapisha maneno.
Naomba nimalizie,
Kama hakuna proof ya kucommint treason act, hakuna intention maana yake ni kuwa hakuna primafacie case, na kama hakuna primafacie case mkiruhusu nijitetee mtakuwa mnafanya makosa ya kisheria.
Sasa Waheshimiwa majaji msipokubali mnafanyaje? Mnafanya kile ambacho sheria imewataka mfanye kwa mujibu wa kifungu cha 312 (1) kufanya finding ya kuwa hakuna case ya kujibu.
Waheshimiwa Majaji naomba kama mtatoa huo uamuzi muutoe leo, kama mnaridhika na hoja hii, reason ruling mtatupa baadae, hakuna haja ya mimi kurudishwa Ukonga leo. Hili ni la pili;
La 3 lipo kwenye kifungu cha 367 cha CPA (Sheria ya Makosa ya Mwenendo wa Jina), kama mashtaka ni ya uonevu ya kusingizia mnaweza kuamuru mtuhumiwa alipwe fidia, haya maumivu yangu na familia yangu nani atafidia?? mashahidi wote 17 mmewasikia.
Hivyo naomba iamriwe kuwa sina kosa la kujibu pia ipangwe tarehe nije kuthibitisha madai/ fidia yangu.
Naomba niwape Waraka wa kikosi kazi wa Umoja wa Mataifa, uamuzi wa tarehe 23/2/2026 unaosema niachiwe mara moja na kulipwa fidia. Hivyo Waheshimiwa Majaji msimamo ni kuwa hakuna primafacie case na kwakuwa hakuna Primafacie case, sheria inawataka muandike findings ya NO CASE TO ANSWER
Waheshimiwa majaji ya kwangu ni hayo tu.
Mhe. Lissu anamaliza na kuketi.
Jaji Ndunguru : Ehee Jamhuri ?
Wakili wa serikali Katuga anasimama anasema Upande wetu kwanini tunaona mshatikiwa ana kesi ya kujibu ni kutokana na makosa aliyoshtakiwa nayo kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) (d)
Anasoma kosa kama lilivyoainishwa katika hati ya mashtaka na anaainsha maneno ya uhaini...
"WANASEMA KITU KIMOJA SAHIHI HAPA, WANASEMA TUTAHAMASISHA UASI, NI KWELI TUTAHAMASISHA UASI, TUTAKINUKISHA VIBAYA......"
Waheshimiwa DPP Vs Philipo Joseph Mtonda, 217 Rufaa ya jinai, Tanzlii 2021.... case hii ili cite case Tambaklal na ikarudia maneno ya hiyo Landmark cases ya Tambklal case.
Wakili wa Serikali Katuga anasema pia case ya DPP MorganMalk vs 2013 ambapo ilisema Mahakama ya rufani iliendelea mbele kwa kuifafanua hii principle ya primafacie case kwa kuangalia ushahidi uliotolewa, unajitosheleza kumtia hatiani mshtakiwa kwenye shtaka dogo au kosa analoshtakiwa nalo, ukiangalia kiini cha kosa kwenye mashtaka
Je mshtakiwa ni mwenye utii?
Je mtuhumiwa alitengeneza nia?
Je alidhihirisha nia yake kwa kufanya kitendo?
Waheshimiwa majaji, viini vya kosa ya uhaini vilishaainishwa kwenye case Grey Likungi Matata , elements zilizoainishwa ni kama zile alizoanisha mtuhumiwa tofauti ya viini ni kidogo ukilingqnisha na mazingira ya kosa
Aina ya kwanza, mshtakiwa awe mwenye utii, ya pili mshtakiwa awe ameonyesha nia, ya tatu amedhihirisha nia yake kwa kuchapisha.
Kiini cha tatu cha kudhihirisha kina utofauti kidogo kwakuwa kimechaguliwa kimoja cha kufanya, imebaki na manifestation of deed, kwahiyo upande wa Jamhuri walipaswa kuthibitisha manifestation of deed, siyo overt act siyo kuchapisha. Section 13 ya Interpretation Act inaonyesha kuwa maneno haya hayako similar unless kuwe na neno similar mbele ya hayo maneno.
Mtu hatokuwa sahihi kama mtu ataonyesha neno moja likatumika kati ya hayo, au mtu akatumia neno lingine lisitumike, hakuta kuwa na nyingine litakaloladhimisha Jamhuri lithibitishe overtact na siyo deed.
Upande wa Jamhuri kupitia mashahidi wake 17 unathibisha kuwa umeonyesha viini vya kosa la uhaini, nikianza na kiini cha kwanza; kuhusu kiini kuwa yeye ni mtiifu na raia wa Tanzania ambapo mtuhumiwa alikiri ye ni raia hoja hii tunaiweka pembeni kiini kimekuwa proved.
Ukija kiini cha pili, cha kutengeneza nia, naomba tuangalie maneno yaliyotumika "ALITENGENEZA NIA"
Case ya Mahendra KCV Vs KarmaTaka, 1238/20 (case ya India)
Inasema uchochezi ni kushawishi, kushauri na yaweze kusababisha consequences kwa tafsiri hii maneno yaliyotumika kwenye hati ya mashtaka bila ya kufanya hajitetee yanaonyesha wazi yana suggest consequences, kwahiyo Mahakama kutompa mshtakiwa haki ya kujitetea yanaweza yakamtia hatiani.
Maneno yamethibitishwa na mashahidi wote akiwemo PW17 ambaye yeye alisikia kwa ukaribu kabisa.
Maneno ya kutishia serikali yanaweza kuthibitishwa kwa vyombo mbalimbali; Kutishiwa/ vitisho imetafsiriwa kwenye Oxford dictionary 2nd Edition (anasoma)
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 2 (d) mtu yeyote atakae tengeneza nia kwa nia ya kuitisha Serikali basi utakuwa umetenda kosa.
Hivyo, upande wa Jamhuri kiini cha nia ya kuitishia serikali tunasemq kimethibitishwa na ushahidi wa Pw1, Pw16 & Pw3.
Ambapo Pw1 na Pw16 wamesema maneno yaliyochapishwa yalikuwa na lengo la kuitishia Serikali na wakasema kuitishia Serikali ni kuvunja sheria ambapo serikali ni kwa ajili ya kutimiza majukumu kwa mujibu wa sheria. Pw3 anasema walipanga kupiga watu mawe.
Hoja kuwa Serikali imetajwa au la, serikali imetajwa constructively kupitia hoja ya constructively kilichotajwa ni serikali, halijatishwa Bunge wala Mahakama kwahiyo tunasema primafacie imekuwa established, kupitia hoja hiyo ya to intimidate ambayo imekuwa proved.
Waheshimiwa Majaji, upande wa Jamhuri umeleta mashahidi wengi ambao wanaonyesha walichocheka na uchochezi wa mtuhumiwa.
Kitendo cha kuyatoa na kuchapisha ndo kinaonyesha manifestation with deed, unlike case ya Agrey likungi matata, unlike case ya Khatibu Gandi na hapa ndiyo utaona kila kesi inaamuriwa kutokana na mazingira yake.
Cross examination haikupinga maneno ilijikita kuhoji je maneno yale ni uhaini?
Mashahidi wamethibitisha kuwa mshtakiwa alitoa maneno yale, hivyo upande Jamhuri inaona imethibitisha kwa kuwa haijawa crossexamined.
Waheshimiwa suala la kuchapisha limezungumzwa na mashahidi upande wa Jamhuri, kwamba waliona You tube kwenye account ya Jambo Tv
Anaendelea Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji tuliattempt kuitoa hiyo video lakini by technicalities haikupokelewa,
Kuna aina tatu za ushahidi, ushadi wa maneno wa maandishi na maneno na (nimesahau kidogo mtanikumbusha) in the absence of evidence video that doesn't means all evidence collapse.
😂😂😂😂 Kwahiyo hapa Jamhuri inataka Mahakama iamini maneno tu, halafu Katuga ni mkavu hata aibu haoni, Mawakili wenzake wameinamisha vichwa vyao chini maana submission ya No case to answer aliyofanya Mhe.Lissu imewavuruga sana.
Haya tuendelee
Katuga anasema Ushahidi wa maneno ni sahihi kama unaaminika kutumiwa bila kutumia documentary evidence...haya si maneno yangu yapo Kwenye case ya Abas Kondo Gelbe Vs Jamhuri , CAT 472/2017, Tanzlii 12/08/2020
Kitu kizuri zaidi, kwenye case ya Goodluck Kiyando vs Jamhuri, No. 118/2013 inasema kuwa kila shahidi ana haki ya kuaminiwa, haisemi mpaka uwe na documentary evidence.
Pw1 alisema ni mtuhumiwa aliyechapisha kupitia Jambo Tv, pia Pw17 alisema kupitia sisi wewe ndiyo ulichapisha.
Waheshimiwa majaji kupitia hoja hizi mashahidi wanasema kupitia kitendo cha kuongea na vyombo vya habari, kitendo kilikusudia maneno yako (mtuhumiwa) yaufikie umma ili umma uchocheke.
Umma ni kina nani? Kifungu cha tano cha Kanuni ya Adhabu ya sheria iliyotumika kumshtaki mtuhumiwa
Tumezungumza Publication, Publication ...Publication ni kitu gani? Black Law dictionary inatafsiri nini maana ya kutangaza, taking into account that it was live streaming
Hivyo kupitia viini vyote vya Uhaini Jamhuri imevithibitisha hivyo tunaona mtuhumiwa anapaswa kupewa nafasi ya kujitetea kutokana na mazingira ya kesi yake.
Pw1 anasema Mtuhumiwa wakati anahojiwa alisema maelezo yake/ ushahidi wake atakuja kuutolea Mahakamani,
hivyo kwakuwa Jamhuri imethibitisha viini vya kosa tunaona ni haki ya mshtakiwa kujitetea kwa mujibu wa kifungu cha 312 (1) cha sheria ya makosa ya jinai.
Kwa upande wetu ni hayo tu waheshimiwa majaji tunaomba kuwasilisha.
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema, Hoja zilizotolewa ni nyingi na mashahidi ni wengi hivyo tunaomba tupate muda wa kupitia na kutolea uamuzi, kesi inahairishwa mpaka tarehe 21/08/2026
Saa tatu kamili asubuhi.
Imepigwa High Cooooourt
Majaji wanatoka pamoja,
Mawakili wa serikali wananyanyuka
Mhe Lissu anamalizia kupanga vitabu na sheria zake huku akisemezana na viongozi wenzake wa chama.
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
WEKA EMOJI KAMA UMESOMA.