Kule Ntwara:Ukisimama nchale,ukitembea nchale,ukichutama nchale,ukilala nchale!TAARIFA JE WAJUA ?
KAMA KESHO MAHAKAMA ITASEMA MHE TUNDU LISSU ANAKESI YA KUJIBU, RAISI ATAPASWA KUFIKA MAHAKAMANI KAMA SHAHIDI WA LISSU?
Na Emily Mwakilembe
Kama mahakama itaona kesi iendelee basi Tundu Lissu anaweza kuistajabisha Dunia kwenye uwanja wa mahakama akiwapitisha Vigogo kwenye flampeni ya Mafuta ya Sheria. Natamani kusikia sauti ya Sheria! Msamiati ya Haki, chenga za Courtroom
Natamani kuona cross examination ya Genius huyu akiwapitisha mashahidi wake kwenye njia ya Sheria kama Safari ya Loliondo kwa babu Ambokile Mwasapile kupata Kikombe cha haki. naogopa lakini ni salama. Na Hawa ndio mashahidi wa Lissu 15 on the stage.
1. Samia Suluhu Hassan – Rais haramu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Dkt. Philip Mpango – Makamu wa Rais Mstaafu
3. Kassim Majaliwa – Waziri Mkuu Mstaafu
4. Jenerali Camillius Wambura – Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania. (IGP)
5. Ramadhani Kingai – Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)
6. Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa
7. Ramadhani Ng’anzi – DCP — Deputy Commissioner of Police Naibu Kamishna wa Polisi
8. Agatha Atuhaire – Mwandishi wa habari/ mwanaharakati kutoka Uganda
9. Boniface Mwangi – Mwanaharakati wa Kenya
10. John Marwa – Mkurugenzi wa Jambo TV
11. Amani Golugwa – Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA
12. John Heche – Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA
13. John Mnyika – Katibu Mkuu wa CHADEMA
14. Jaji mstaafu Willy Mutunga – Kenya
15. Martha Karua – Mwanasiasa na wakili kutoka Kenya.
Ukisikia ukimeza ya moto kutema Hutaki ndio hii, kesi hii ilipofikia ni kidonda kwenye tako, kukaa panauma kulala panauma, anyway ngoja nisubili Ijumaa, nione tunatema au Tunameza.View attachment 3654085
Mambo ya Komoni wethi‼️🚨BREAKING NEWS - TUNDU LISSU FAKE TREASON TRIAL TO RESUME‼️
The High Court in Dar es Salaam has scheduled the hearing of the case of treason no. 19605/2025 facing Tundu Lissu from 10/08/2026 to 07/09/2026.
Note: the Commonwealth deadline of 30 days to resolve Tundu Lissu’s politically motivated trumped up trial expires on August 10,2026 👊🏽
‼️WAMEBANWA‼️
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imepanga kufanya kikao cha kusikiliza
Shauri la Uhaini Na. 19605/2025 linalomkabili Tundu Lissu kuanzia tarehe 10/08/2026 hadi tarehe 07/09/2026.
Zingatia: Siku ya mwisho wameambiwa na Jumuiya ya Madola wapate suluhu ya kumwachia Lissu ni Agosti 10 😁 yaani tunafinya hadi mwisho!
Sasa msitupotezee muda
Mwachieni Lissu #FreeTunduLissuNOW
Sasa inabidi ufanyaje ili usipigwe nchale?Kule Ntwara:Ukisimama nchale,ukitembea nchale,ukichutama nchale,ukilala nchale!
Kumeanza kuchangamka#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 253
Hii nchi ina maajabu sana.🤧
Wakili wa Serikali Katuga amesimama anasema kwa mujibu wa kifungu cha 313 na 381 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai vyote vinasema mashahidi wa mshitakiwa au mtuhumiwa wanapaswa kutajwa kipindi cha committal yaani kule Kisutu.
Watu wanacheka.😂😂😂😂
Watanzania wanakumbuka Mh. Lissu aliwataja mashahidi wake kule Kisutu na wote tulisikia. Leo Katuga anasimama hapa anasema Mshitakiwa au mtuhumiwa hakumtaja Samia, Majaliwa na hao wengine kule Kisutu.
Katuga anasema pia tunaitaka Mahakama iangalie mashahidi wanaoitwa wanahusika na hii kesi?
Jaji: Sasa usiende huko tuambie kwanza mashahidi ambao hutaki waje ni akina nani?
Katuga: Ni mashahidi wote kabisa.
Relevance ya mashahidi lazima aiseme ni ipi?
Lakini kipekee tunapinga mashahidi wanaotoka Serikalini na nitaeleza kwanini?
Watu wanacheka na kushangaaa nini kinatokea? 😂😂😂
Pale Mahakama itakapotoa wito kwa mujibu wa kifungu cha 146 cha kutoa wito basi kinaelekeza mahakama kutoa hati ya UKAMATAJI. Kutokana na mazingira haya Mahakama haiwezi kutoa hati ya wito bila kujiridhisha kama shahidi huyo ni muhimu, compellable na competent.
Mahakama inapaswa kujiridhisha hivyo vitu vyote, haiwezi kumuita mtu ambae yuko aware na fact in issue lazima awe anajua kinachoendelea.
Mahakama haiwezi kutoa wito ambao haiwezi kuenforce sasa Rais hajaja Mahakamani itatoa arrest warrant?
Haya ni maneno ya Katuga.
Anaendelea hapa naomba niende kwa mashahidi watatu wa mwanzo, Samia Suluhu, Philip Mpango na Kassim Majaliwa kama tumemuelewa mshitakiwa kuwa hawa ni Viongozi wa Serikali anaotuhumiwa kuwatishia. Ibara ya 43 ya Katiba. Rais atakuwa Mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu.
Ibara ya 47 ya Katiba inasema Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama hayupo nchini au atakazoagizwa na Rais.
😂😂😂😂 Yaani Jamhuri wamemshtaki Mhe. Lissu kwa Uhaini halafu wanaweka mpira kwapani hawataki kuja kutoa ushahidi
Katuga anaendelea
Mashtaka yetu ni kuwa mshtakiwa ametengeneza nia ya kuitishia Serikali regardless kama serikali imetishika au haijatishika na mashahidi wetu 17 walitoa ushahdi kwaniaba ya serikali, kwa maneno mengine Rais ameshatoa ushahidi
Watu wanacheka😂😂😂😂😂
Kama mshtakiwa anamalengo kuwa mashahidi waje waeleze kama walitishika au hawakutishika ushahidi huo sio wa muhimu hapa kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Ushahidi wa mashahidi anaotaka kuwaita Lissu sio material, pia sio lazima kuwaita mashahidi hawa kwasababu ni descretion ya Mahakama. Kwa namna Lissu alivyosema waitwe, ni kama anataka kuja kuwauliza maswali ya Dodoso dhidi ya ushahidi uliotolewa na mashahidi wa serikali ambao wameshatoa ushahidi kwaniaba yao kinyume na malengo ya kifungu cha 155 na 156 ya Sheria ya Ushahidi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 209 Mshtakiwa anaweza kuomba Mahakama iite shahidi kama ushahidi wake ni wa muhimu kuisaidia Mahakama.
Sisi tunaona kuwa Lissu amekiuka vifungu vya sheria na hawa mashahidi sio material na hivyo mashahidi waliotajwa kuanzia namba moja hadi 7 tunaomba wasiitwe, hao wengine wa CHADEMA hatuna shida nao ila utaratibu ufuatwe. Ni hayo tu naomba kuwaalika wenzangu.
Part 254 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.