MAJIBU YA MAHAKAMA KUHUSU MASHAIDI WA TUNDU LISSU KUFIKA MAHAKAMANI
Majaji na Mshtakiwa wameingia kwa pamoja.
Mawakili wa Serikali wapo tayari.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, kolamu kwa upande wa Jamhuri ipo kama ilivyokuwa awali.
Mshtakiwa yupo na sisi tupo tayari kuendelea, kama Mwenye Kesi yake yupo tayari.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, baada ya maelekezo ya Mahakama, nimeonana na Msajili wa Mahakama hii.
Amekuja kuniona kuniletea taarifa za summons za kuwaita mashahidi wa Mahakama.
Mheshimiwa Msajili amenitaarifu kwamba mashahidi wote walipelekewa summons Dodoma. Hata hivyo, haikuwezekana kuwa-save nakala za summons baada ya kusemekana wapo nje ya nchi.
Mheshimiwa Msajili anasema kati ya hao watatu, mmoja ambaye ni Kamishna wa Polisi, Afande DCI, Mkurugenzi wa Upelelezi katika Jeshi la Polisi, anatarajiwa kurudi nchini leo.
Msajili ameniahidi kuwa siku ya Ijumaa Kamishna wa Polisi atakuwepo Mahakamani kuja kutekeleza wito wa Mahakama.
Wale wengine wawili, ambao ni Generali Jacob Mkunda, ambaye ni Mkuu wa Majeshi, na IGP Camillius Wambura, haijulikani watakuja nchini lini.
Katika haki ya namna hiyo, napendekeza tuahirishe kesi hadi siku ya Ijumaa saa 8:30 mchana.
Ili session ya asubuhi nitumie kushauriana na shahidi, ikiwa ni pamoja na kuchukua maelezo yake.
Baada ya saa 8:30 nitakuwa tayari kuendelea naye.
Kuhusu waliobaki, tusubiri tumalizane na aliyepo. Then tutafanya maamuzi.
La mwisho, Waheshimiwa Majaji, nafahamu jinsi ambavyo ratiba ya shauri hili ilivyo tight, vilevile na mimi nataka sana twende kwenye final submission, ili tupate muda wa kusubiri uamuzi wenu.
Kama watatii wito wa Mahakama na kuja, imani yangu ni kwamba hatutochukua muda mrefu.
Kama mpaka tunamaliza na huyu aliyepo, tukimaliza na hawajaja, nafikiri naweza kuwa na uamuzi kama bado nawahitaji au la.
Wasipokuja kabisa, Waheshimiwa Majaji, hilo litakuwa mikononi mwenu.
Kwa sababu nyie ndiyo mlio-toa summons.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka
Nassoro Katuga Waheshimiwa Majaji kwa masikitiko sina pingamizi la kuhairisha kesi
Waheshimiwa nakumbuka Mahakama ilisema Mwisho tarehe 18
Jaji: Tarehe 26
Nassoro Katuga: Kwa maana hiyo hatupingi kuhairisha kesi
Tunaomba Mahakama hii imsisitize Mshtakiwa Mashahidi wake wafike kwa wakati.
MAHAKA KICHEKO 😀 😀 😀
Jaji Ndunguru: si Mashahidi wake jamani, yeye ndo anatakiwa kuwaleta Mahakamani.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo Waheshimiwa tunaomba tusisitize Mshtakiwa aweze kuwaleta
Tutakuwa tumepoteza siku ya leo nusu na kesho tungeweza kumaliza shauri
Swala la kama Wasipo fika anaiachia mahakama , Mahakama ifanye nini.
Yeye ndiyo anatakiwa Kuiomba Mahakama iwafanye nini Mahakama
Jaji Ndunguru: unaposema anaiachia Mahakama, Mahakama ifanye nini.
Nimekumbuka ule msemo wako Mahakama siyo mama yako.
MAHAKAMA KICHEKO 😀 😀
Nassoro Katuga: ni hayo tuh Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru: kwa hiyo Shauri kwa leo linahairishwa hadi Ijumaa tarehe 18.
Saa 8 kamili badala ya saa 8 na nusu.
TUKUTANE IJUMAA SHAHIDI ALETWE HATA KWA MACHELA.😀
#TUTAKUWEPO
#NoHateNoFear
View attachment 3671955