Tumpigie kura Rais Magufuli kuwa "Best Political Leader of the Year 2020"

Kama hili shindano ni la kweli, mwenye kustahili ushindi huo itakuwa ni Nana Addo wa Ghana, ktk vigezo vyote vya utawala bora hakuna anayeweza kumfikia. Tuache unafiki kwa kuwa hata madonda ya rafu za uchaguzi uliopita na madhira yake bado hayajapona.
Jamaa ni jembe haswaaa nilikuwa naangakia baadhi ya sera zao aisee jamaa kiukweki anatashinda tu kwa kishindo hili shindano hauwezi mweka ligi moja na washindani wake .
 
RAIS MAGUFULI NI BORA KULIKO RAIS NANA AKUFO-ADDO WA GHANA; TUZO TUIREJESHE KWETU

Na: Suphian Juma

Jarida la African Leadership ambalo husaidia kuinena vema Afrika duniani, linaendesha zoezi la upigaji kura. Katika kipengele cha Kiongozi Bora wa Kisiasa Afrika yaani AFRICAN POLITICAL LEADER OF THE YEAR; Rais wetu Magufuli yumo akiwaacha mbali MaRais wa Senegal, Afrika Kusini, huku akipitwa kura kiduchu na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo katika upigaji kura unaoendelea mtandaoni.

Naona baadhi yetu Watanzania wanampigia chapuo Nana, nadhani hii ni kwa sababu aidha hawajawahi kuishi Ghana ya Nana, hawajazisoma vema siasa za Ghana ama basi tu ni chuki zao binafsi kwa Rais wetu Magufuli.

Wasiojua Nana ndiye Rais wa kwanza wa Ghana kukopa fedha nyingi zaidi kuliko Rais yeyote tangu Ghana ipate Uhuru. Shirika la Fedha duniani (IMF) limetamka kwamba deni la Ghana linakadiriwa kufika 74.7% kufikia mwaka huu wa 2021. Huyu Rais wa madeni ambaye anawaumiza wananchi wake maskini kulipa madeni hayo atafaaje kuwa bora kuliko Rais wetu Magufuli?

Nana anakadiriwa ndiye Rais ambaye hadi sasa ndiye mwenye mawaziri wengi zaidi kuliko Rais yeyote duniani. Yaani Baraza la mawaziri lake lina jumla ya mawaziri 125 achilia mbali Manaibu waziri wake. Fikiria mishahara yao na marupurupu yao katika nchi ndogo kama Ghana yenye jumla ya watu milioni 30. Sisi Tanzania tupo milioni karibia 60 yaani mara mbili ya Ghana ila Rais Magufuli hata mawaziri robo ya mawaziri wake Nana hatujawahi kuwafikisha. Maana hadi sasa Rais Magufuli ana mawaziri 23 tu.

Kingine cha kutia huzuni Ghana ya Nana ni AJIRA. Unaambiwa Ghana kijana kupata kazi Serikalini au hata kwa Taasisi binafsi ni kizungumkuti. Mwandishi wa DW wa Ghana Manasseh Azure Awuni katika uhariri wake uliochapishwa Desemba 10, 2020 anasema
ni rahisi kijana kubebeshwa mfuko wa saruji shingoni mwake na akapita bahari ya Atlantiki ila si kijana huyo kupata kazi Ghana katika utawala wa Nana Akudo-Addo. Sasa tujiulize Nana Serikali yake kukopa kote huko kwanini pasisaidie kutatua janga la ajira? Nana ni msanii.

Huku kwetu tangu Rais Magufuli aingie madarakani tukiweka unafiki pembeni, hakika viongozi wamekuwa na adabu kwa wananchi. Hali haiko hivo kwa Nana. Wachambuzi wa Siasa walioko Ghana wanasema Mghana wa kawaida hana mamlaka ya kummwajibisha Kiongozi isipokuwa tu hadi ifike muda wa uchaguzi kupitia kura yake sandukuni. Ila huku kwa Mzee Magu, mwananchi wa Buza kwa Mpalange alitukanwa tu na M/kiti wake wa Mtaa, mwenyekiti huyo kazi hana.

Mfano wa hili la kukosekana 'accountability' kwa Viongozi huko Ghana; mwaka 2019 Mwandishi wa Habari za Uchaguzi wa Ghana Ahmed Hussein-Suale alipigwa risasi na kufa Accra. Kabla ya kuuawa Ahmed alitishiwa kifo na Mbunge wa Chama cha Nana, na hadi sasa si Polisi wa Nana wala vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama ambavyo vimewahi kutoa matokeo ya uchunguzi wala kumwajibisha huyo Mbunge ambaye alimtishia kifo Ahmed.

Nana si muumini wa Utawala bora wala wa Uhuru wa vyombo vya habari; Imagine Julai mwaka jana Rais Nana aliamuru kuachishwa kazi Mhariri Mkuu wa Chombo cha habari nchini humo aitwaye Daniel Domelevo licha ya kukatazwa na Asasi za Kiraia kisa tu Mhariri huyo aliruhusu habari irushwe iliyohusu ukaguzi wa Mali za kifisadi za Waziri wake aliyemtegemea kwenye Baraza aitwaye Yaw Osafo-Maafo.

Kiufupi Rais Nana Akufo-Addo ana udhaifu mkubwa mno katika maeneo ya utawala bora na katika vita dhidi ya ufisaidi ukimlinganisha na jembe letu Magufuli. Demokrasia ya kweli lazima iambatane na Utawala bora, uwajibishwaji wa Viongozi na Serikali huku matatizo makubwa kama ajira na maisha bora kwa wananchi yakitekelezwa kikamilifu ila haya kwa Nana bado ni mtihani Mkubwa.

Na isitoshe kusema: uchaguzi wa Ghana ambao ulipita mwaka jana bila kumwaga damu, nyumba na mali za watu kuchomwa si kigezo pekee cha kupima ubora wa Kiongozi. Ghana wana vyama viwili ambavyo ni pacha tofauti ni majina tu NPP ya Nana na NDC ambavyo huachiana madaraka kila uchaguzi; kimoja kikiwa upinzani kinaonekana bora kwa kukisema kilichopo madarakani lakini maisha ya raia wa kawaida ni magumu mno. Huku si kukomaa kwa demokrasia bali kudumaa kwa demokrasia tofauti na tunavyoaminishwa na wanaharakati mtandaoni.

Hivyo nawaombeni kura zote tumpigie Rais wetu Magufuli ambaye ni mchapakazi wa kweli, msimamizi makini wa kodi zetu na mwendelezaji wa miradi mikubwa ya wananchi wake, na kinara wa Utawala bora unaompa mwananchi wa kawaida fursa ya kummwajibisha Kiongozi wake muda wowote kuliko kusubiri wakati wa uchaguzi kama huko kwa Nana Akufo-Addo wa Ghana.

Bofya: https://t.co/xhDotKvYzI?amp=1

Mwisho wa kupiga kura ni Januari 8, 2021. Wahi sasa tuing'arishe Tanzania yetu duniani.

Suphian Juma Nkuwi,
Mtanzania Halisi,
Januari 06, 2020
Phone: 0717027973
Email: yessuphian@gmail.com
FB_IMG_1609934981349.jpg
IMG_20210106_144502.jpg
 
Wewe una uwezo wa kumuwajibisha nani? Hata wakati wa uchaguzi uwezo huo hauna, sababu kura yako ni kama referendum tu, haina nguvu wala maamuzi yoyote yale.

Kingine jikite kwenye kufanya kampeni, ili Magufuli ashinde, kama kweli unataka ashinde. unapoanza kumchimba na kumtusi Nana na Ghana yake inakusaidia nini?
 
Huko ghana kuna platform moja ambayo ni kama jamii forum huku. Nao wanasema bora wampe shetani kula kuliko huyo mzee akufoh. So mnayosema hapa wala hayashtui.
 
Back
Top Bottom