Rais wa Ghana awataka Marais wa Afrika kuacha kuwa 'omba omba'

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Akizungumza kwenye Mkutano na Rais Joe Biden wa Marekani na Marais takriban 50 wa Afrika, Rais Nana Akufo-Addo amesema Afrika lazima iache kutegemea nchi za Magharibi ili kubadili mitazamo duni kuhusu bara hilo.

Amesema "Tukiacha kuwa ombaomba na kutumia pesa zetu, Afrika haitakuwa na haja ya kuomba heshima kutoka kwa mtu yeyote, tutapata heshima tunayostahili. Tukiifanikisha inavyopaswa, heshima itafuata,".

Kauli ya Akufo-Addo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Shirika la Fedha la Kimataifa (IFM) kuipa Ghana mkopo wa Tsh. Trilioni 7 ili kuipunguzia mtikisiko wa Kiuchumi.

=================

Ghana's President Nana Akufo-Addo has said that African countries must wean themselves off "begging" the West to earn global respect and change poor perceptions about the continent.

"If we stop being beggars and spend African money inside the continent, Africa will not need to ask for respect from anyone, we will get the respect we deserve. If we make it prosperous as it should be, respect will follow," Mr Akufo-Addo said.

He made the remarks during the opening of the US-Africa Leaders' Summit in Washington DC.

Mr Akufo-Addo urged greater solidarity among Africans to address shared aspirations.

"Africans are more resilient outside the continent than inside. We must bear in mind that to the outside world, [there's] nothing like Nigeria, Ghana or Kenya, we are simply Africans. Our destiny as people depends on each other," he said.

The president said that the continent had skills and manpower but needed concerted political will to make "Africa work".

Mr Akufo-Addo's remarks came on the day that the International Monetary Fund agreed to give Ghana a $3bn (£2.4bn) loan to alleviate an unprecedented economic downturn in the West African country.

Dozens of African leaders are in Washington to discuss cooperation with the US amid growing Chinese and Russian influence on the continent.

BBC
 
N siku Moja tu toka atoke kupewa mkopo (c ndio kuomba ombaa uko) ,lkn leo anasema Africa tuache kuomba ombaa
 
Bongo
FB_IMG_1671011806778.jpg
 
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amesema kuwa mataifa ya Afrika lazima yajiondoe kwenye utaratibu wa "kuomba" nchi za Magharibi ili kupata heshima ya kimataifa na kubadili mitazamo duni kuhusu bara hilo.

"Tukiacha kuwa ombaomba na kutumia pesa za Kiafrika ndani ya bara hili, Afrika haitakuwa na haja ya kuomba heshima kutoka kwa mtu yeyote, tutapata heshima tunayostahili. Tukifanikisha hilo basi, heshima itafuata," Bw Akufo -Ado alisema.

Hayo ameyasema wakati akifungua mkutano wa viongozi wa Marekani na Afrika unaofanyika mjini Washington DC.

Bw Akufo-Addo alihimiza mshikamano zaidi miongoni mwa Waafrika ili kushughulikia malengo ya pamoja.
"Waafrika wanastahimili zaidi nje ya bara kuliko ndani. Lazima tukumbuke kwamba kwa ulimwengu wa nje, hakuna kitu kama Nigeria, Ghana au Kenya, sisi ni Waafrika tu. Hatima yetu inategemea kila mmoja," alisema.

Rais alisema kuwa bara hilo lilikuwa na ujuzi na wafanyakazi lakini lilihitaji utashi wa kisiasa wa kufanya "Afrika ifanye kazi". Matamshi ya Bw Akufo-Addo yalikuja siku ambayo Shirika la Fedha la Kimataifa kukubali kuipa Ghana mkopo wa $3bilioni (£2.4bn) ili kupunguza mtikisiko wa kiuchumi ambao haujawahi kushuhudiwa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Makumi ya viongozi wa Afrika wako mjini Washington kujadili ushirikiano na Marekani huku kukiwa na ongezeko la ushawishi wa China na Urusi katika bara hilo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Fungueni mipaka ya Afrika kwa Waafrika wafanye biashara.

Unataka Waafrika watumie pesa za Africa ndani ya Africa wakati biashara ndani ya Afrika kwa Waafrika zina vikwazo kibao, mitandao ya barabara na ndege kati ya nchi za Kiafrika mibovu, kiasi kwamba mtu anaweza kuhitaji kwenda Ulaya ili kusafiri kutoka nchi moja ya Afrika kwenda nyingine, hata kupata visa tu kwa Muafrika kwenda nchi nyingine ya Afrika ni tabu.

Sasa hivi kuna computer chip war. Nchi gani ya Africa inatengeneza latest computer chips?

Unawezaje kuongeza biashara wakati nchi za Kiafrika zimeua viwanda, mostly zina export raw products tu?

Unaweza vipi kuongeza biashara wakati bara la Afrika halijaweka kipaumbele kwenye research and development?

Utawezaje kuongeza biashara ya ndani Afrika katika hali kama hiyo?
 
Akizungumza kwenye Mkutano na Rais Joe Biden wa Marekani na Marais takriban 50 wa Afrika, Rais Nana Akufo-Addo

14 December 2022

US-AFRICA LEADERS' SUMMIT: PRESIDENT AKUFO-ADDO URGES AFRICA TO STOP 'BEGGING'

Ghana's President Nana Akufo-Addo has said that African countries must wean themselves off "begging" the West to earn global respect and change poor perceptions about the continent.
Source: Kumasi Online TV
 
MJADALA WA BIASHARA YA DHAHABU KWA MAFUTA WAPAMBA MOTO NCHINI GHANA🇬🇭

Mjumbe wa kamati ya migodi na nishati ya Bunge nchini Ghana, Dr. Kwabena Donkor amesema hizi ni sarakasi zinazochezwa na serikali ambazo ni kiini macho kwani haziwezi kutekelezeka.

Kujaribu biashara ya mali-kwa-mali (barter trade) ya kubadilisha dhahabu kwa mafuta ya petroli / dizeli kimataifa ni dalili ya serikali kushindwa kusimamia uchumi anasisitiza mbunge na mjumbe huyo wa kamati ya bunge Dr. Kwabena Donkor ambaye aliwahi kufanya kazi ktk sekta ya petroli.

Dr. Kwabena Donkor akishiriki ndani ya mjadala exclusive wa kituo cha JoyNews amekwenda ndani zaidi kwa kuhoji ni nani anayemiliki migodi hiyo, na inajulikana ni makampuni makubwa ya kigeni hivyo watawalipa nini wenye migodi je ni kwa pesa za madafu yaani sarafu ya cedis ya Ghana au dollars za Kimarekani ambazo serikali ya Ghana haina fedha hizo za kigeni.

Anaongeza hoja Dr. Kwabena Donkor, pia kama serikali italenga kununua kwa wachimbaji wadogo wadogo itaweza kushindana na bei ya dhahabu ya soko la dunia? Maana itapelekea wachimbaji hao wadogo kutorosha dhahabu kupitia njia za panya za mipakani.

Hii ni kutokana na serikali itashindwa kuwalipa bei nzuri wachimbaji wadogo au kuwalipa kwa dollar za marekani wachimbaji wadogo kulingana na bei ya soko la dunia kwani serikali haina hifadhi ya kutosha ya fedha za kigeni.

Kimsingi katika mada hii moto ya kituo cha TV JoyNews pia mtendaji mkuu (CEO) wa chemba ya migodi ya Ghana, Dr. Sulemanu Koney naye ktk mahojiano ametoa kauli juu ya changamoto ya jinsi ya uhalisia wa uwezekano wa sera hiyo mpya ya biashara ya mali-kwa-mali kuweza kutekelezeka, kwani kuna mengi ya kuyafanya kabla ya sera hiyo kuweza kutekelezeka ingawa chemba hiyo milango yake ipo wazi kwa majadiliano na serikali ya Ghana.
Source : JoyNews
Soma zaidi chanzo :
 
Akizungumza kwenye Mkutano na Rais Joe Biden wa Marekani na Marais takriban 50 wa Afrika, Rais Nana Akufo-Addo amesema Afrika lazima iache kutegemea nchi za Magharibi ili kubadili mitazamo duni kuhusu bara hilo.

Amesema "Tukiacha kuwa ombaomba na kutumia pesa zetu, Afrika haitakuwa na haja ya kuomba heshima kutoka kwa mtu yeyote, tutapata heshima tunayostahili. Tukiifanikisha inavyopaswa, heshima itafuata,".

Kauli ya Akufo-Addo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Shirika la Fedha la Kimataifa (IFM) kuipa Ghana mkopo wa Tsh. Trilioni 7 ili kuipunguzia mtikisiko wa Kiuchumi.

=================

Ghana's President Nana Akufo-Addo has said that African countries must wean themselves off "begging" the West to earn global respect and change poor perceptions about the continent.

"If we stop being beggars and spend African money inside the continent, Africa will not need to ask for respect from anyone, we will get the respect we deserve. If we make it prosperous as it should be, respect will follow," Mr Akufo-Addo said.

He made the remarks during the opening of the US-Africa Leaders' Summit in Washington DC.

Mr Akufo-Addo urged greater solidarity among Africans to address shared aspirations.

"Africans are more resilient outside the continent than inside. We must bear in mind that to the outside world, [there's] nothing like Nigeria, Ghana or Kenya, we are simply Africans. Our destiny as people depends on each other," he said.

The president said that the continent had skills and manpower but needed concerted political will to make "Africa work".

Mr Akufo-Addo's remarks came on the day that the International Monetary Fund agreed to give Ghana a $3bn (£2.4bn) loan to alleviate an unprecedented economic downturn in the West African country.

Dozens of African leaders are in Washington to discuss cooperation with the US amid growing Chinese and Russian influence on the continent.

BBC
Africa tulihitaji kuendelea kukaa na wakoloni kwa miaka kazaa ili tupate elimu yao then tuwafukuze. Tulichokifanya sasa tulijikomboa toka utawala wa mabavu na kureplace na watawala wa kiafrica wenye mabavu nonsense kuzidi hata hao wakoloni na mpaka sada ki fikra tulikuwa bado tumetawaliwa, na ushahidi huo ni mfano Tanzania ilikuwa na waziri aliyeitwa Kambona alienda kufunga Ndoa UK, au muasisi wetu na moja wa wapigania uhuru (Mwl Nyerere) alienda kufia nchini Uingereza. Tanzania ili tuendelee tunahitaji ukombozi wa fikra na Elimu. Yaani hata sasa akipita mzungu/au Mzungu akienda kupata huduma sehemu basi utakuta mtoa huduma atampatia nafasi ya upendeleo mzungu badala ya mwenyeji. Hata fikra za viongozi wetu, unakuta Rais Samia anaamini kabisa tulikosea tulipotaka kuanza kutafuta mbinu za kujitegemea na yeye katurudisha mikononi mwa mabeberu kwa kasi ya 5G.
 
Fungueni mipaka ya Afrika kwa Waafrika wafanye biashara.

Unataka Waafrika watumie pesa za Africa ndani ya Africa wakati biashara ndani ya Afrika kwa Waafrika zina vikwazo kibao, mitandao ya barabara na ndege kati ya nchi za Kiafrika mibovu, kiasi kwamba mtu anaweza kuhitaji kwenda Ulaya ili kusafiri kutoka nchi moja ya Afrika kwenda nyingine, hata kupata visa tu kwa Muafrika kwenda nchi nyingine ya Afrika ni tabu.

Sasa hivi kuna computer chip war. Nchi gani ya Africa inatengeneza latest computer chips?

Unawezaje kuongeza biashara wakati nchi za Kiafrika zimeua viwanda, mostly zina export raw products tu?

Unaweza vipi kuongeza biashara wakati bara la Afrika halijaweka kipaumbele kwenye research and development?

Utawezaje kuongeza biashara ya ndani Afrika katika hali kama hiyo?
Hao ni mdomo tuu, mambo ya muhimu ya kuondoa umaskini kama kuondoa kero mipakani na mikodi hawayaoni, jaribu kuuza mahindi tuu hapo Kenya kuna misururu ya vibali na mikodi kama milioni
 
Mkopo sio msaada kila nchi inakopa hata Us ana madeni makubwa kushinda Tz.

Tofautisha mkopo na kuomba msaada
Hii naifananisha na maisha ya wafanyakazi wenye mishahara midogo Tanzania.

Ni bora yule mfanyakazi anayeenda kuchukua mikopo kwenye taasis za fedha na kuiacha ATM kama dhamana, kuliko yule anayehangaika kuwaomba ndugu na jamaa hela, huyu anadharaulika tofauti na yule aliyeenda kukopa taasis za fedha.

Kwanza ukimuomba hela ndugu, jamaa au rafiki anaanza kukuuliza maswali mengi, ukimpa mgongo anaanza kukusengenya. Lakini ukienda kukopa kwenye taasis za fedha ni chap unapata hela kama una vigezo na hakuna anayekutangaza

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom