BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,117
Jumla ya Sh3 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi katika mitihani yao ya kidato cha sita.

Ufadhili huo ambao unaanza mwaka 2022/2023 unafanyika chini ya mpango unaojulikana kama Samia Scholarship.

Akizungumza hayo leo Jumapili Septemba 25,2022, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Septemba 27,2022 wanafungua rasmi tangazo la ufadhili huo ambao utawahusisha wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha juu na kudahiliwa kusoma masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali.

“Baada ya hapo majina yao yatatanangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wamefanya vizuri sana katika masomo ambao wanastahili kupewa Mama Samia Scholarship,”amesema.

Amesema kuwa wanafunzi 640 ndio waliofaulu kwa kiwango cha juu katika masomo ya sayansi, kwa hiyo watafahamu na endapo watadahiliwa katika masomo ya sayansi watakuwa wanufaika wa ufadhili huu.

Aidha, Profesa Mkenda amesema kesho kutakuwa na mkutano wa wadau wa elimu nchini ambapo lengo likiwa ni kupitia sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na mabadiliko ya mtaala wa elimu.

“Majadiliano yatatokana na hatua iliyofikiwa kutokana na mapitio ya sera na mitaala baada ya kukusanya maoni mengi ya wadau ambayo tuliyakusanya kupitia mikutano mbalimbali na wengine wamekuwa wakituletea kimaandishi,”amesema.

Amewataja wadau watakaokutana ni wahadhiri, waajiri na wadau wa maendeleo, taasisi zinazohusihanisha na lugha, wabunge, wajumbe wa kutoka Zanzibar, jumuiya za kielimu, taasisi za tafiti za kisayansi, taasisi za umma, binafsi na dini.

Pia Profesa Mkenda amewataka Watanzania kuwasilisha rasimu za maandiko yao za riwaya na mashahiri katika kuwania tuzo za waandishi bunifu ambazo zinajulikana kama tuzo za Mwalimu Nyerere.
 
Shule nyingi Sana hasa za Kata ambazo Ni shule wanazo Soma watoto wa maskini shule hizi hazina maabara zenye vifaa za kufundishia sayansi.

Pia hazina walimu wakutosha kufundisha masomo ya sayansi .

Shule za Binafsi Tena zinazotoza ada za mamilioni ndio zenye maabara na walimu wa sayansi !
Hivi Ni sawa kumpa scholarship mwanafunzi aliyetoka kwenye shule hizi ambazo mzazi wake alikuwa analipa ada Milioni 5 Hadi 10?

Mtoto wa masikini anayesoma shule za kata zisizo na maabara Wala walimu wa masomo ya sayansi atapata lini kupenya Hadi apate hii scholarship?

Time will Tell.
 
Jumla ya Sh3 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi katika mitihani yao ya kidato cha sita...
Ni suala zuri sana la kutoa "scholarship" kwa wanafunzi wenye ufaulu mzuri, bali isiishie kwa serikalini tu iwe hata kwa makampuni yanayotengeneza faida.

Kama sehemu ya "Corporate Social Responsibility" makampuni yarudishe kwa jamii fedha ili zitumike katika kuwafadhili wanafunzi wengi zaidi.
 
Saidia Zanzibar.
Amewataja wadau watakaokutana ni wahadhiri, waajiri na wadau wa maendeleo, taasisi zinazohusihanisha na lugha, wabunge, wajumbe wa kutoka Zanzibar, jumuiya za kielimu, taasisi za tafiti za kisayansi, taasisi za umma, binafsi na dini.
 
Kodi zetu ziheshimiwe!
HESLB ni kwa ambao hawajafanya vizuri?
Wasitengeneze classes kwa vijana wetu,after all wanaofanya vizuri ni watoto wa viongozi waliosoma shule nzuri, hivyo wanajitengenezea mazingira ya upigaji.
Hatutaki!👊
 
Jumla ya Sh3 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi katika mitihani yao ya kidato cha sita.

Ufadhili huo ambao unaanza mwaka 2022/2023 unafanyika chini ya mpango unaojulikana kama Samia Scholarship.

Akizungumza hayo leo Jumapili Septemba 25,2022, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Septemba 27,2022 wanafungua rasmi tangazo la ufadhili huo ambao utawahusisha wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha juu na kudahiliwa kusoma masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali.

“Baada ya hapo majina yao yatatanangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wamefanya vizuri sana katika masomo ambao wanastahili kupewa Mama Samia Scholarship,”amesema.

Amesema kuwa wanafunzi 640 ndio waliofaulu kwa kiwango cha juu katika masomo ya sayansi, kwa hiyo watafahamu na endapo watadahiliwa katika masomo ya sayansi watakuwa wanufaika wa ufadhili huu.

Aidha, Profesa Mkenda amesema kesho kutakuwa na mkutano wa wadau wa elimu nchini ambapo lengo likiwa ni kupitia sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na mabadiliko ya mtaala wa elimu.

“Majadiliano yatatokana na hatua iliyofikiwa kutokana na mapitio ya sera na mitaala baada ya kukusanya maoni mengi ya wadau ambayo tuliyakusanya kupitia mikutano mbalimbali na wengine wamekuwa wakituletea kimaandishi,”amesema.

Amewataja wadau watakaokutana ni wahadhiri, waajiri na wadau wa maendeleo, taasisi zinazohusihanisha na lugha, wabunge, wajumbe wa kutoka Zanzibar, jumuiya za kielimu, taasisi za tafiti za kisayansi, taasisi za umma, binafsi na dini.

Pia Profesa Mkenda amewataka Watanzania kuwasilisha rasimu za maandiko yao za riwaya na mashahiri katika kuwania tuzo za waandishi bunifu ambazo zinajulikana kama tuzo za Mwalimu Nyerere.

Chief Hangaya atuambie kwanza hiyo hela kaipata wapi. Sio anachukua hela zetu halafu anazitumia kujifanyia campaign kinyemela! Hawa kenge wanaotawala wametuona Watanzania kuwa hatuna akili kabisa!
 
Shule nyingi Sana hasa za Kata ambazo Ni shule wanazo Soma watoto wa maskini shule hizi hazina maabara zenye vifaa za kufundishia sayansi ,
Pia hazina walimu wakutosha kufundisha masomo ya sayansi .
Shule za Binafsi Tena zinazotoza ada za mamilioni ndio zenye maabara na walimu wa sayansi !
Hivi Ni sawa kumpa scholarship mwanafunzi aliyetoka kwenye shule hizi ambazo mzazi wake alikuwa analipa ada Milioni 5 Hadi 10?
Mtoto wa masikini anayesoma shule za kata zisizo na maabara Wala walimu wa masomo ya sayansi atapata lini kupenya Hadi apate hii scholarship !!?
Time will Tell.
Wapo "wachache" kutoka shule hizi na mazingira hayo hupenya na kufaulu vizuri.
Wengine wanaobakia wanatakiwa kuomba mkopo wa bodi (HESLB) kupitia utaratibu wa miaka yote.
Kukosa ufaulu unaotosha kufuzu kunufaika na Samia Scholarship haipaswi kuwa mwisho wa matumaini ya kupata usaidizi wa kusoma elimu ya juu.

Mwanafunzi uliyemzungumzia hapo juu kimsingi anakosa vingi na ndio mfumo wa elimu (na wa ubepari kwa ujumla) unavyofanya kazi. Anakosa nafasi kwenye "vyuo vizuri", anakosa "kozi nzuri" kwa sababu kigezo kikuu cha udahili ni ufaulu mkubwa.
 
Back
Top Bottom