The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Fanya reverse look up ya phone number itakupa some helpful info.

Nimepata mkuu.

Sasa ukienda katika link hii utaona kuna jamaa amejaribu kutupa swali kwa hio law firm lakini limekuwa ignored!

http://www.merchantcircle.com/bulletins/Madorsky.J.Lewis.Lpa.216-371-7600

Na hapa ni moja ya matangazo yao.

Merchant Blog
Welcome to the blog of Madorsky J Lewis Lpa
Hello! Madorsky J Lewis Lpa is in business in University Heights, OH, and is interested in doing business with you. Contact Madorsky J Lewis Lpa to request a deal, get a coupon or to do business.

You can visit Madorsky J Lewis Lpa at:
3934 Washington Blvd
University Heights, OH 44118
Or call at: 216-371-7600

Check out the Madorsky J Lewis Lpa listing on MerchantCircle for business hours and more info.

Subscribe to the blog to stay up-to-date with Madorsky J Lewis Lpa deals, announcements, coupons or other news.

Thanks!

Kwa hio anaonekana ni mwanasheria wa merchantile law!
 
JF Senior Expert Member Join Date: 2007

Chenge

Hii taarifa imenifanya nisome reports zako tu ili angalau nimalize mapema maana inatia hamasa kusikia hilo. Nafurahi sana kuwa member wa JF nafaidi vitu hata kabla havijawa public.


Ndugu wabongo wenzangu, naomba kutoa heshima zangu nzito kwa wale wote tulioshiriki katika huu mjadala, I am humbled na very much at peace, kwamba leo chombo cha JF kwa mara nyingine tena kunaweza kutumika kuwapigisha magoti mafisadi, na kulifanya taifa zima li-freeze na kuja hapa kutafuta dataz,

Wale mliochangia hii topic, regardless ya mawazo au mitizamo yenu, kwa njia moja au nyingine mmesaidia kuelimisha taifa, ninasema ndugu zangu taifa letu liko njia panda, it does not matter uko wapi, popote tulipo tutumie anything kilichokaribu kupigana kulikomboa taifa letu, tumia hiyo key-board ku-make a change, badala ya kuja hapa ku-buz! buz! weka vitu hapa watu wasome wabadilike, Kwa mafisadi ninawaambia kuwa sasa kazi, tunawamulika kila mlipo!

Hakuna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho, ninazo dataz nzito zaidi, lakini upepo umekaa vibaya kwa sasa, upepo utakapotulia tu tutaendelea na dataz anytime sasa msilale maana zinakuja hizoooo!

Ahsanteni Wakuu, na Mungu Aibariki Tanzania!
 
[QUOTE Hakuna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho, ninazo dataz nzito zaidi, lakini upepo umekaa vibaya kwa sasa, upepo utakapotulia tu tutaendelea na dataz anytime sasa msilale maana zinakuja hizoooo!QUOTE]

Mhhhhh, haya mkuu, tunakuaminia.

Zimwage data mda utakaoona unafaa. Twakuamini mzeee
 
yote afanyayo muungwana ni usanii uliotukuka.
Hakuna mali hata moja iliyoshikwa wala hakuna fedha hata sumni iliyorudishwa.
Tunaziona bongo nyumba za mafisadi zilizojengwa kifisadi bado zote wanazo. Ni rahisi kuzishikilia za tanzania kwanza kuliko hizo za nje.

kwani kiwira wameichukua. Je Rukaza si bado yupo kwenye behewa lake.
Yona mahekalu yake si bado anatesa nayo.
mgonja bado wanaye.
tusileteane habari za kufurahisha. hakuna kilichoshikwa wala kuzuiwa vyote visemwavyo ni usanii.
kama kashindwa kushikilia vya dar vya sauzi ataweza wapi.

the greatest fear is fear itself.
 
Kinachoudhi ni kwamba, uchunguzi wa swala la Chenge umechwa mikononi mwa SFO kama vilke sisi hatuna chombo kama hicho. Nilitegemea kuwa wakati SFO wanafanya uchunguzi wao, na sisi (kupitia TAKUKURU) tungefanya uchunguzi wetu wa kina kuhusiana na jinsi alivyoweza kupata pesa nyingi hivyo na kuzihamisha kutoka nje ya nchi bila kujulikana. Vinginevyo mikataba yote iliyosimamiwa na Chenge kwa niaba ya Taifa letu ichunguzwe kwa kina.
 
yote afanyayo muungwana ni usanii uliotukuka.
Hakuna mali hata moja iliyoshikwa wala hakuna fedha hata sumni iliyorudishwa

Amebakiza miaka miwili na kisha anza kutuma vijana mikoani kwenye kampeni....anangojea naye miaka tano ajikusanyie na yeye ma vijisenti na kutayrisha mrithi wake maybe EL or Kawambwa....hana wasiwasi.....

Mmeshasikia akiwataja mafisadi? na wakati ule wa kampeni mbona aliwa accuse jamaa kadhaa kwa kupewa mikop banki ki rahisi?

Mbona watu wale alio wa accuse wako pale na wanazidi kusonga
 
Ajabu kubwa ni kwamba viongozi wote kasoro huyo Lowassa wote wamejiuzuru kutokana na uchunguzi uliotoka nje kama hiyo EPA na sasa hivi hii Radar, lakini zote hizi zilionekana halali chini ya vyombo vyetu vya uchunguzi...
Hii bado kweli inatupa matumaini na vyombo vyetu?...Halka fu basi viongozi hao hao waliofanya makosa mwanzo kutoa taarifa za Uongo bado wamekamata nyadhifa zao kama vile hakuna kibaya kilichotokea.. nakoma na TZ...
Mtandano ama kweli Mafia hatari sana...
 
Kinachoudhi ni kwamba, uchunguzi wa swala la Chenge umechwa mikononi mwa SFO kama vilke sisi hatuna chombo kama hicho. Nilitegemea kuwa wakati SFO wanafanya uchunguzi wao, na sisi (kupitia TAKUKURU) tungefanya uchunguzi wetu wa kina kuhusiana na jinsi alivyoweza kupata pesa nyingi hivyo na kuzihamisha kutoka nje ya nchi bila kujulikana. Vinginevyo mikataba yote iliyosimamiwa na Chenge kwa niaba ya Taifa letu ichunguzwe kwa kina.

Labda uchunguzi ufanywe na chombo kingine lakini sio TAKUKURU ya Hosea. Umesahau taarifa yao ya uchunguzi kuhusu RICHMOND ilivyowasafisha wahusika na kuonyesha kuwa hakukuwa na uchafu wowote kwenye mkataba huo?. Wadanganyika huwa tunadanganywa sana na nafikiri SFO wanaweza wakatoa mwanga pasipo kuwashirikisha akina Hosea na wenzake. Angalia hata issue ya EPA inavyochanganywa na akina Hosea, Mwema na Mwanyika japo Ernst & Young walishafunua na kuweka bayana kila kitu.
 
Ajabu kubwa ni kwamba viongozi wote kasoro huyo Lowassa wote wamejiuzuru kutokana na uchunguzi uliotoka nje kama hiyo EPA na sasa hivi hii Radar, lakini zote hizi zilionekana halali chini ya vyombo vyetu vya uchunguzi...
Hii bado kweli inatupa matumaini na vyombo vyetu?...Halka fu basi viongozi hao hao waliofanya makosa mwanzo kutoa taarifa za Uongo bado wamekamata nyadhifa zao kama vile hakuna kibaya kilichotokea.. nakoma na TZ...
Mtandano ama kweli Mafia hatari sana...

Vyombo gani vya uchunguzi? Usalama wa Taifa wapo pale peacock hotel wanachunguza wapinzania wametembea na mwanamke gani ili wakauze habari kwenye UWAZI.

Police wao mkuu Mwema anaangaika na JF na kina Max baada ya kucontrate kwenye loophole. Hakuna usalama wanaweza kuzamisha swala la EPA, hiki ni kitendawili kitakachoteguliwa na Mungu na si CCM wala JK.
 
According to the dataz ni kwamba sasa hata Lowassa, naye ameingizwa huko London kwa siri, between the last three days..........!

Tunaendelea kuifuatilia kwa karibu stay tuned.....more to come!
 
Jamani, wakati tunaambiwa Chenge amekuja London kwa ajili "Mambo yake" na SFO, Lowassa ana nini London? ama ndio amekuja kumsajilia mshikaji wake (Chenge)? au ndio katika kupumua? Au .......... please help, niko tayari kumpa raha na kumtembeza japo wanasema "RAHA JIPE MWENYEWE" kama kweli amekuja kupumzika au kupumzishwa
 
Tina umeniacha hoi sana mkuu .Hebu mpe raha zake kwa kumsaidia kumpuzisha
 
Duh sasa Tina unatutisha sasa unataka umpe raha gani FISADI huyo??unataka mle wote za RICHMOND?mmh wabongo bwana unakimelea cha ufisadi nini??mfatilie anaweza kukukonyeza.
 
Back
Top Bottom