Tauhida Cassian Gallos ahoji Bungeni mkakati wa Serikali kudhibiti matukio unyanyasaji na ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na watoto

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,038
974

MHE TAUHIDA CASSIAN GALLOS Ahoji Bungeni Mkakati wa Serikali Kudhibiti Matukio Unyanyasaji na Ukatili wa Kingono Dhidi ya Wanawake na Watoto

"Je, kuna mpango gani wa Kudhibiti matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kingono dhidi ya Wanawake na Watoto nchini?" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum

"Wizara inatekelezeka mpango kazi wa Taifa kwa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto uliopelekea kuanzisha Kamati 18,886 za ulinzi na usalama wa Wanawake na watoto zinazotoa elimu na taarifa na Masuala ya ukatili wa kijinsia" - Mhe. Mwanaidi Khamis, Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

"Aidha, Serikali imeunda Madawati 2,405 ya ulinzi wa mtoto katika shule za msingi 1765 na Sekondari 640. Madawati ya kijinsia katika Vyuo Vikuu 296, Madawati 115 katika maeneo ya sokoni na Madawati 420 katika vituo vya polisi yanayoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia."

"Juhudi hizi zimewezesha kupunguza kwa vitendo ukatili wa kimwili kutoka asilimia 40 mwaka 2015 hadi asilimia 27 mwaka 2022 na ukatili wa kingono kutoka asilimia 17 mwaka 2015 hadi asilimia 12 mwaka 2022. Serikali itaendelea na kampeni mbalimbali za ulinzi na usalama wa Wanawake na watoto"

"Vitendo vya unyanyasaji kwa Wanawake bado vipo na vimeshika kasi. Je, Serikali inachukua hatua gani mahususi kuweza kupunguza vitendo vya ukatili kwa Wanawake? - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum

"Wizara imechukua hatua ya kuwajengea uwezo na kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwaunganisha Wanawake katika fursa zilizopo katika jamii zetu, lengo ni kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na ukatili wa Wanawake"

"Serikali imechukua hatua zinazowezesha watoto kupata elimu ya kujitambua, kujieleza na kutoa taarifa zinazohusu ukatili wa kingono, kuanzisha Bunge la watoto, Mabaraza ya watoto na Madawati ya ulinzi na usalama wa watoto katika shule za msingi na sekondari" - Mhe. Mwanaidi Khamis, Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
 

Attachments

  • 44855580-24f6-4c21-ae06-c02c3d0a5dfe-1024x683.jpg
    44855580-24f6-4c21-ae06-c02c3d0a5dfe-1024x683.jpg
    109.6 KB · Views: 1
  • 1oiuyt.JPG
    1oiuyt.JPG
    114.5 KB · Views: 1
Hiyo ni hoja dhaifu mnoo, haihitaji kuanzishiwa thread hapa JF, huyo mbunge nadhani amesimama na kuongea hayo ili tujue tu naye yupo bungeni na huwa anaongeaga!
 
Back
Top Bottom