Mbunge Maryam Azan Mwinyi: Serikali Imejipangaje Kuwasaidia Wahanga Wanaopata Ujauzito Kutokana na Matukio ya Ukatili wa Kijinsia (Ubakaji na Udhalili

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

Mbunge Maryam Azan Mwinyi: Serikali Imejipangaje Kuwasaidia Wahanga Wanaopata Ujauzito Kutokana na Matukio ya Ukatili wa Kijinsia (Ubakaji na Udhalilishaji)

Serikali imesema imeandaa mipango na mikakati ya kuwasaidia waathirika na manusura wa vitendo vya ukatili ili kuhakikisha wanapatiwa huduma muhimu za kukabiliana na athari zitokanazo na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Mwanaidi Ali Khamis ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Maryam Azan Mwinyi lililouliza Serikali imejipangaje kuwasaidia wahanga wanaopata ujauzito kutokana na matukio ya ukatili wa kijinsia kama ubakaji na udhalilishaji.

Amezitaja huduma zinazotolewa na Serikali kuwa ni huduma za afya , afya ya akili, Saikolojia na kijamii.

Nyingine ni za hifadhi, chakula na malazi kupitia nyumba salama na urejeshaji wa Wanafunzi shuleni.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa mikopo ya asilimia kumi kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake (WDF) ili kusaidia Wanawake kujiinua kiuchumi na kutoa mikopo yenye masharti nafuu.
 

Attachments

  • Untitledwqasxz.jpg
    Untitledwqasxz.jpg
    9.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom