SoC04 Tufanye nini ili kudhibiti vitendo vya unyanyasaji wa kingono katika jamii?

Tanzania Tuitakayo competition threads
May 19, 2024
13
7
Unyanyasaji wa kingono hii ni aina ya unyanyasaji, unaohusisha matumizi ya matamshi ya ngono ya wazi ama ya siri, ikiwa ni pamoja na ahadi zisizohitajika na zisizofaa za zawadi kwa kubadilishana na faida za ngono.
Wakati mwingine unyanyasaji huu muathirika, anaweza kutendewa kutokana na hali ya mazingira yanayomzunguka.

1. TURUDISHE MFUMO WA NYUMBA 10
Hapo zamani mfumo huu ulisaidia sana, kuifanya Jamii yetu kuwa salama sana, hakuna mgeni ambaye angeingia mtaani, bila ya taarifa zake kujulikana, na hii ilitokana na ufuatiliaji wa mabalozi katika maeneo yao, tukirudisha mfumo huu wa utawala itasaidia pia kudhibiti haya majanga, kwani matukio mengi yanatokea majumbani.

2. MFUMO WA KUOMBA KAZI UFANYIKE KWA NJIA YA MTANDAO TU
Miongoni mwa maeneo ambayo yana waathirika wengi wa unyanyasaji huu, ni katika maeneo ya kazi, Hasa wakati wa kuomba nafasi za kazi (Usahili), endapo tutabadili mifumo yote ya kuomba kazi serikalini na sekta binafsi, hii itasaidia sana kudhibiti janga hili, kwani wale wasimamizi waliokuwa wakitumia kama ndiyo kigezo kikuu cha kutoa nafasi za kazi, hawatapata hiyo nafasi tena, mtu apate kazi kulingana na vigezo vya taasisi husika, kwa kutuma taarifa zake binafsi na taarifa za kitaaluma, hizo ndiyo zikawe kipaumbele au kigezo cha kupata kazi, na si vinginevyo.

3. ADHABU YA MNYANYASAJI IWE NI KIFUNGO CHA MAISHA
Nashauri kuwa adhabu zinazotolewa kwa wanaofanya vitendo hivi, yaani kifungo cha miaka 30 jela, bado imeonekana kuwa si fundisho kwao, nina amini endapo sheria ikitiliwa mkazo na kuwa kifungo cha maisha jela, inaweza sana kusaidia kudhibiti vitendo hivi vya unyanyasaji wa kingono, kwa kuwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, imeonekana kuwa haifanyi kazi sawia, kwani haijasaidia kudhibiti vitendo vya unyanyasaji huu, vitendo vimezidi kushamiri sana, hebu tuweke sheria ngumu kama hii ya kifungo cha maisha jela, itawaogopesha sana watenda maovu haya na hapo itatupatia wepesi wa kudhibiti kabisa unyanyasaji wa kingono.

sexual-abuse-1600x490-dreamstimemedium_40341023.jpg

4. SERIKALI ITANGAZE HILI KAMA JANGA LA KITAIFA
Leo hii matukio ya unyanyasaji wa kijinsia/kingono, hayakauki kwenye vyombo vya habari, mfano utasikia huyu kabaka mara yule amelawiti, tena kibaya zaidi wanaofanya haya ni watu wa karibu kabisa, wa familia zilizoathirika, serikali ikitangaza kama ni janga la taifa, basi tutazungumza lugha moja, kutoka ngazi ya familia mpaka taifa, na hapo ndipo tutapata ufumbuzi wa kudhibiti hili.

5. NGOMA ZA VIGODORO NA KANGAMOKO ZIFUTWE KABISAA
Matukio ya ngoma hizi yameshamiri sana, maeneo ya kanda ya mashariki, mpaka kusini mwa Tanzania, na sasa imeenea kila mahali pa nchi yetu, ngoma hizi zimekuwa zikichezwa bila staha na wakati mwingine, mpaka watoto wadogo wamekuwa wakihusishwa kwenye ngoma hizo kutazama, hii husababisha watoto waanze kujifunza mambo ya kikubwa mapema, na hii kuchangia kwa urahisi sana, kufanyiwa vitendo vya ngono kabla ya umri wa utu uzima.

IMG_1039.jpg

6. MIDOLI INAYOVALISHWA NGUO MADUKANI IPIGWE MARUFUKU KABISAA
Eneo jingine mtambuka ni hili la midoli madukani, Hasa midoli inayoonesha maeneo ya mwili mzima, kuna wakati imekuwa ikiachwa bila kuwekwa nguo, hapa ndipo athari zake huonekana, maana mtazamaji ataanza kuona sehemu za mwili za mdoli Hasa sehemu za siri, kisha akavuta picha halisi, ambapo humpelekea kupandisha hisia, na mara moja huweza kufanya chochote kilicho karibu yake, ili tu kutimiza haja yake, na hapa ndipo matukio ya unyanyasaji wa kingono hutokea zaidi.

93f55cc108c3d7a482e0b74ea52df026.jpg

7. SHULE ZOTE ZA BWENI ZA JINSI MOJA ZIFUTWE, KISHA ZIWE SHULE ZA MCHANGANYIKO
Kwenye maeneo ya shule Hasa zile za kike tu, matukio haya yamekuwa yakiongezeka kila mara, na Hasa wakifanyiwa ama na viongozi,wafanyakazi au waalimu wa maeneo yao ya shule, tena hufanyika bila idhini ya muhusika mwenyewe, ili tu aweze kufanikishiwa jambo fulani, ambalo yawezekana lingeweza kufanyika bila ngono kabisa, zikiwa mchanganyiko itasaidia kudhibiti matukio haya ya unyanyasaji.

TANZANIA NCHI YANGU ninayoitaka mimi, ni ile ambayo ndani ya miaka 5mpaka 20 ijayo, itajenga kizazi imara chenye kujitambua, chenye mtazamo chanya wa kulipeleka taifa letu mbele, baada ya kipindi fulani kupita, hatuwezi kuwa na mtazamo chanya wa kimaendeleo kama bado jamii yetu itaendelea kuliimba jambo hili kila mara, na huku wale tunaowatarajia kwaajili ya kizazi cha kesho, yaani watoto wakiendelea kuwa ndiyo wahanga wakubwa zaidi, wa matukio haya ya unyanyasaji wa kingono.

images_3.jpeg

TANZANIA ITAKAYODHIBITI UNYANYASAJI WA KINGONO IPO KARIBU KUTOKEA.

NB: Picha zote ni kwa msaada wa Google.
 
MIDOLI INAYOVALISHWA NGUO MADUKANI IPIGWE MARUFUKU KABISAA
Eneo jingine mtambuka ni hili la midoli madukani, Hasa midoli inayoonesha maeneo ya mwili mzima, kuna wakati imekuwa ikiachwa bila kuwekwa nguo,
😀😅😅 daaaah! Hii Tanzania nyie mweeeeh!

TANZANIA NCHI YANGU ninayoitaka mimi, ni ile ambayo ndani ya miaka 5mpaka 20 ijayo, itajenga kizazi imara chenye kujitambua, chenye mtazamo chanya wa kulipeleka taifa letu mbele
Hili hapa ndio neno sasa, maana vyote: sheria na vitisho nk haviwezi kumzuia mtu kufanya vitu vya ajabu kwa tamaa ya mwili. Lakini mru aliyejitambua na mwenye mtazamo chanya anajiendesha (self control) kikamilifu na haendeshwi tena na tamaa za ajabuajabu.

Naona kama wabongo wakieeza hiki kitu, kujiendesha hatutahitaji tena insha ndeefu za tanzania tunayoitaka. Tutakuwa tumeshaipata hiyo ya watu wanaojiendesha vema (self control)
 
😀😅😅 daaaah! Hii Tanzania nyie mweeeeh!


Hili hapa ndio neno sasa, maana vyote: sheria na vitisho nk haviwezi kumzuia mtu kufanya vitu vya ajabu kwa tamaa ya mwili. Lakini mru aliyejitambua na mwenye mtazamo chanya anajiendesha (self control) kikamilifu na haendeshwi tena na tamaa za ajabuajabu.

Naona kama wabongo wakieeza hiki kitu, kujiendesha hatutahitaji tena insha ndeefu za tanzania tunayoitaka. Tutakuwa tumeshaipata hiyo ya watu wanaojiende

😀😅😅 daaaah! Hii Tanzania nyie mweeeeh!


Hili hapa ndio neno sasa, maana vyote: sheria na vitisho nk haviwezi kumzuia mtu kufanya vitu vya ajabu kwa tamaa ya mwili. Lakini mru aliyejitambua na mwenye mtazamo chanya anajiendesha (self control) kikamilifu na haendeshwi tena na tamaa za ajabuajabu.

Naona kama wabongo wakieeza hiki kitu, kujiendesha hatutahitaji tena insha ndeefu za tanzania tunayoitaka. Tutakuwa tumeshaipata hiyo ya watu wanaojiendesha vema (self control)
Upo sahihi kabisa kiongozi, hii ndiyo Tanzania tuitakayo
 
Back
Top Bottom