Wazazi na Walezi wenye Watoto katika Tasnia ya Sanaa Wanapaswa Kuwalinda dhidi ya Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Azimio la Haki za Mtoto la Umoja wa Mataifa la mwaka 1959 lilitambua umuhimu wa kulinda watoto katika maeneo mbalimbali ya maisha, ikiwa ni pamoja na ushiriki wao katika tasnia ya burudani. Watoto ni kundi kubwa linalopitia unyanyasaji na ukatili wa kijinsia katika jamii, na hili linajitokeza kwa kiwango kikubwa pia katika tasnia ya sanaa. Hata hivyo, wasanii watoto bado wanakumbana na hatari mbalimbali leo, kama vile ukatili wa kijinsia, udhalilishaji, na matumizi ya madawa ya kulevya na pombe.

Mazingira haya magumu yanaweza kusababisha athari za kisaikolojia, matatizo ya afya ya akili, na msongo wa mawazo. Ni wajibu wa wazazi na walezi kuchukua jukumu kubwa katika kulinda watoto wao kwa kutoa usimamizi wa mara kwa mara na kushiriki katika kushawishi mabadiliko ya sheria za ulinzi wa wasanii watoto. Hii itachangia kujenga mazingira salama na yenye kuzingatia ustawi wao.

Je, wazazi na walezi wenye watoto kwenye tasnia hii wana uelewe mzuri jinsi ya kuwalinda watoto dhidi ya unyayasaji?
 
Mwenye Sikio Na Asikie Ila Wengi Wanajisahau Katika Kuendelea Kuwapa Nasaha Za Hapa Na Pale Wakiamini Tayari Ni Watu Wazima
 
Mtu ansjinyanyasa mwenyewe kwa kuvaa nusu uchi,anajadili ngono hadharani na anatoa maoni anapenda akiwa mkubwa aolewe na mume wa namna gani.
Sasa anajidhalilisha au anadhalilishwa?
 
Back
Top Bottom