Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Vidonda vya tumbo ni michubuko inayotokea kwenye kuta za mfumo wa chakula, hasa kwenye sehemu ya tumbo au pia sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo.

88070BE7-0F16-4680-A0C0-DEA1D8A66478.jpeg


Ukubwa wa vidonda hivi hutofautiana, kuanzia millimita chache hadi sentimita kadhaa.

Dalili za ugonjwa huu mara nyingi hutegemea umri pamoja na eneo husika vilipo vidonda hivi. Miongoni mwake ni -
  • Maumivu makali ya kuvuta kwa misuli, au kuwaka moto kwa misuli ya tumbo
  • Tumbo kujaa gesi mara kwa mara
  • Kiungulia
  • Kichefuchefu
  • Kujisaidia choo chenye damu, au choo cheusi
  • Kutapika uchafu wenye damu, au wenye rangi ya weusi
  • Kupata maumivu kifuani, kama moto unaochoma
CHANZO
Kuna nadharia nyingi zinazohusishwa na kutokea kwa tatizo la vidonda vya tumbo. Lakini ukweli ni kuwa, tatizo hili kwa kiasi kikubwa hutokana na sababu mbili tu ambazo ni-
  • Maambukizi ya bakteria jamii ya H. pylori
  • Matumizi mabaya ya dawa za kupunguza maumivu mfano aspirin, ibuprofen, mefenamic acid na diclofenac

Kitaalamu, dawa hizi huwekwa kwenye kundi kubwa linaloitwa Non Steroidal Anti Inflammatory Drugs (NSAIDs).

Dawa hizi zinapotumika pasipo kufuata taratibu sahihi huharibu na kuvunja mfumo wa kinga unaolinda kuta za tumbo hivyo kusababisha kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Ni muhimu sana kuepuka matumizi holela ya dawa za kutuliza maumivu pasipo kufuata miongozo ya magonjwa na dozi sahihi kama sehemu ya kujikinga na tatizo hili. Aidha, mtu mwenye vidonda vya tumbo hashauriwi kutumia dawa hizi kwa kuwa huongeza ukubwa wa tatizo.

Dawa kama paracetamol (Panadol) ambayo kimpangilio huwa haipo kwenye kundi la NSAIDs hufaa kama mbadala wake kwa wagonjwa, lakini mtaalamu wa afya anaweza kushauri matumizi ya dawa nyingine kwa kadri atakavyoona inafaa.

Kwa upande mwingine, maambukizi ya bakteria wa H.pylori hutokea baada ya kula chakula au kunywa maji yenye vimelea hivi. Aidha, choo, matapishi na mate ya mtu mwenye bakteria hawa vinaweza kuwa chanzo cha kutokea kwa maambukizi.

VIHATARISHI
Uvutaji wa sigara ni tabia hatarishi inayosaidia kutokea kwa tatizo hili pamoja na kuongeza ukubwa wa athari zake.

Hupoozesha pia kasi ya uponaji wa vidonda kwa wagonjwa, pamoja na kuongeza uwezekano wa kujirudia tena kwa ugonjwa baada ya kupona.

Pombe, stress pamoja na kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya uwepo wa ugonjwa huu huongeza nafasi ya kupatwa na shida hii.

MATIBABU
Msingi wa matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha mambo mawili yanayotegemea asili yake-
  • Kuangamiza bakteria wa H. pylori
  • Dawa za kuweka sawa au kudhibiti uzalishwaji wa asidi
Udhibiti wa asidi na vimelea huhitajika sana. Matumizi ya dawa za antibayotiki hufaa wakati huu, pia dawa za kudhibiti uzalishwaji wa asidi nyingi hupaswa kumezwa.

Ikiwa changamoto hii itaendelea kujirudia, pia ikiwa changamoto zinazosababishwa na ugonjwa huu kama vile kuziba kwa utumbo au kuvuja kwa damu tumboni zitatokea, upasuaji huwa ni chaguo sahihi.

MAZIWA FRESH
Baadhi ya watu hudhani kuwa maziwa fresh husaidia kutibu tatizo hili. Hii siyo kweli.

Maziwa haya huleta ahueni ya muda mfupi kwa kutengeneza utando juu ya kuta za vidonda. Aidha, aina hii ya maziwa huongeza uzalishwaji wa asidi tumboni pamoja na vimeng’enya vingine ambavyo baada ya kuisha kwa utando wa maziwa husababisha maumivu makali zaidi.

Hivyo, Mtu mwenye vidonda vya tumbo hashauriwi kutumia maziwa fresh.

Chanzo: Cleveland Clinic
 
Mzee wangu ana vidonda vya tumbo shida ni kwamba kila akiongezewa damu baada ya siku kadhaa hb inashuka..

Shida ni nin na kipi kifanyike
 
Mzee wangu ana vidonda vya tumbo shida ni kwamba kila akiongezewa damu baada ya siku kadhaa hb inashuka..

Shida ni nin na kipi kifanyike
Huyo ameshafika stage ya mbali (perforation stage) of course hiyo ni consequences ya vidonda visipodhibitiwa mapema kwa matibabu na life sytle especially diet
 
Huyo ameshafika stage ya mbali (perforation stage) of course hiyo ni consequences ya vidonda visipodhibitiwa mapema kwa matibabu na life sytle especially diet
Kipi ambacho atakutana nacho upasuaj ama nin?
 
Ninavidonda vya tumbo lakin sasa iv ges inanisumbua inapanda hadi kwenye koo Napata maumivu sana na pia Kikohozi hakiishi kila asubuhi
 
Mkuu, Kuna mahali nliambiwa na mtu (aliepona vidonda vya tumbo) kwamba Ile konyagi ndogo ni dawa ya ugonjwa huo?.....

Kwamba unachanganya pilipili kiasi kwenye konyagi unapiga glass nzima x3 kwa siku......Hili limekaaje?
 
Jaman vidonda vya tumbo vinatibika tena week Moja unakula maharage Mimi bibi yangu sio mganga wa kutoa majini au kusafusha nyota ila anatibu vidonda magonywa na magonywa mengine nimeshuhudia watu wakipona sio stori
 
Jaman vidonda vya tumbo vinatibika tena week Moja unakula maharage Mimi bibi yangu sio mganga wa kutoa majini au kusafusha nyota ila anatibu vidonda magonywa na magonywa mengine nimeshuhudia watu wakipona sio stori
Elezea hapa, hakuna mtu mwenye interest ya kumuona Bibi yako, towa maelezo Maharage yanatibu Vipi?
 
Jaman vidonda vya tumbo vinatibika tena week Moja unakula maharage Mimi bibi yangu sio mganga wa kutoa majini au kusafusha nyota ila anatibu vidonda magonywa na magonywa mengine nimeshuhudia watu wakipona sio stori
kong77 tueleze kiundani zaidi kuhusu hiyo tiba ya bibi yako. Anaponya kwa kutumia dawa za aina ipi, ni mitishamba au nini
 
Back
Top Bottom