Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

Futota

Futota

JF-Expert Member
522
195
mimi naona kama una allergy na sabuni unayotumia, kemikali zinazotumika katika sabuni hizo hazipatani na ngozi yako.

hivyo basi jaribu kubadilisha na kutumia hizi sabuni zenye virutubisho vya kiasili (with natural ingredients) kwa mfano asali, avacado, na kadhalika. sabuni hizi hupatika mara nyingi katika maduka ya kina mama wajasiriamali
 
N

Nancy70

Member
67
0
Nami nilikuwa na tatizo kama hilo na haswa ukioga maji ya baridi na yaliyolala yaani ya katika ndoo. Jaribu kuoga maji ya uvuguvugu na epuka kuoga maji yaliyolala ktk tank au ndoo.
 
ThinkPad

ThinkPad

JF-Expert Member
1,851
1,225
Jamani me pia nilishawahi kukutana na hiyo kitu nilipo toka mwanza na kwenda Tanga nilipooga maji ya tanga niliwashwa hvyo hvyo kwa dk 15 nkatumia detol soap sikuona mabadiliko nikawa natumia detol mpaka nkawa siwashi mwili.
 
Donnie Charlie

Donnie Charlie

JF-Expert Member
8,799
2,000
mimi nina tatizo hili kwa miaka kumi na nimepata tiba tofauti kwa madaktari lakini sijafanikiwa isipokuwa tatizo hupungua ninapotumia maji ya moto pia ni kama mwaka hivi natumia sabuni ya MOVIT kweli imenisaidia sana kufikia hata wakati mwingine naoga bila kuwashwa kabisa.
 
drphone

drphone

JF-Expert Member
3,551
1,250
jamani wakuu naombeni dawa ya kuzuia kuwashwa nina muda sasa nasumbuliwa na tatizo hili nimetumia dawa lakini wapi cjajua nini tatizo lake nishaurini nitumie dawa gani jamani
 
Kitty Galore

Kitty Galore

JF-Expert Member
347
195
hujafafanua ni kuwashwa kwa namna gani, kuna aina nyingi za kuwashwa, sasa tukueleweje?
 
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
30,502
2,000
jamani wakuu naombeni dawa ya kuzuia kuwashwa nina mda ss nasumbuliwa na tatizo hili nimetumia dawa lakini wapi cjajua nini tatizo lake nishaurini nitumie dawa gani jamani
Google asali na mdalasini, kwenye mchanganyiko ongeza kitunguu swaumu. Jitahidini kusoma JFdoctor kila kitu utapata humu jamvini.
 
sulphadoxine

sulphadoxine

JF-Expert Member
2,261
1,195
Hili tatizo la kuwashwa hata mimi ninalo,nawashwa usoni hasa muda wa usiku,yaani inakuwa ni kero sana,na bado sijapata tiba.
 
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
4,133
1,250
Una allergy mkuu kama sio maji au mafuta unayotumia!
 
wende

wende

JF-Expert Member
714
195
Embu oga kwa sabuni yoyote ile bila ktumia kitu chochote kinacho-scratch your body kama vile madodoki etc.
 
Vin Diesel

Vin Diesel

JF-Expert Member
9,068
2,000
pole sana mkuuu....tafadhali kamuone daktari
 
Babuu blessed

Babuu blessed

JF-Expert Member
1,371
1,250
Dawa ya minyonyo umetumia siku za hivi karibuni au la!
 
Rubi

Rubi

JF-Expert Member
1,622
1,225
Pole ndugu ila nashindwa kuchangia kwa sababu hujawa specific unawashwaje na wapi.
 
zumbemkuu

zumbemkuu

JF-Expert Member
10,066
2,000
hata mimi wakuu, nawashwa mwili mzima km mtu aliemwagiwa upupu, sasa nimejikuta kila baada ya siku3 nakunywa kidonge kimoja cha centrizene (kidonge cha aleji), nikishakunywa tu nakaa hizo siku bila kuwashwa, sasa imekuwa ni tabia ya kunywa dawa ili nisiwashwe, nahofia sumu itazidi kujaa mwilini maana miaka 2 sasa nakunywa dawa tu.
 

Forum statistics


Threads
1,424,622

Messages
35,068,583

Members
538,026
Top Bottom