Tatizo la kuvimba mwili na matatizo ya ngozi

border

Senior Member
Jun 22, 2017
145
142
Nawasalimu kwa upendo wa dhati.

Nimekuwa nikipata changamoto kwenye mwili wangu hasa KUVIMBA kwa mwili NGOZI kuwashwa kupata viupele na kuacha alama pale ninapojikuna.

Tatizo hili lilianza taratibu na limekuwa likikua siku hadi siku, ilianza nikila matunda hasa matikiti mwili unaniwasha Sana na nikijikuna napata viupele ambavyo baada ya kipindi Cha muda mfupi upotea. Pia ikaja nikinywa soda ya Pepsi au kutumia dawa za antibiotics mwili unavimba kwenye baadhi ya Maeneo nakuwasha Sana.

Ningependa kujua tatizo hili linasababishwa na Nini na Nini tiba yake kwani nimefanya kipimo Cha blood culture na fool blood picture lakini haikuonekana tatizo lolote.

Karibu

IMG_20230831_192318_030.jpg
 
Kapime ini, figo, damu na xray ya kifua. Itakusaidia kujua chanzo ni nini haswa? Ila tatizo lipo hapo kwenye hivyo nilivyoviorodhesha.

Ili upate unafuu jaribu kuogea maji ya uvuguvugu yatakupa nafuu. Alafu usijipake mafuta yoyote mwilini wala kutumia sabuni kuogea.
 
Nenda hospital kubwa mapema ukacheki vipimo alivyoorozesha mdau hapa juu, kuvimba Kwa mwili hasahasa uso vinaendana na kufeli ya Figo. Ila inaweza kuwa hata kuwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini.
 
Kapime ini, figo, damu na xray ya kifua. Itakusaidia kujua chanzo ni nini haswa? Ila tatizo lipo hapo kwenye hivyo nilivyoviorodhesha.

Ili upate unafuu jaribu kuogea maji ya uvuguvugu yatakupa nafuu. Alafu usijipake mafuta yoyote mwilini wala kutumia sabuni kuogea.
Ahsante
 
Back
Top Bottom