Tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara- Fahamu chanzo, pata ushauri na tiba ya tatizo hili

Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
10,586
2,000
Habari JF Doctor na wana jamii wote.

Mdogo wangu wa kiume (23yrs) ana tatizo la kuwashwa mwili mzima tokea mwaka 2002. Nimezunguka naye takribani hospitali zote kubwa hapa Dar lakini hatujafanikiwa kupata ufumbuzi wa tatizo lake.

Kwa ufupi ni kwamba alianza tu kuwashwa jichoni, macho yakavimba, akaenda hospital (Burhani) akapatiwa dawa za kutuliza allergy (cetrizine) ile hali ikatulia kwa siku mbili tu, ya tatu mwasho ukarudi tena.

Tukaenda Aga Khan akapimwa kuanzia choo, mkojo, damu lakini hakukutwa na minyoo, wala gonjwa lolote la zinaa akapewa tena cetrizine na ndizo anaendelea nazo mpaka leo kutumia, miaka nane sasa ule mwasho bado upo.

Akijikuna pale panapowasha panavimba mithili ya mdudu amekukojolea au mithili ya mtu aliyewashwa na washawasha, na ni mwili mzima unakuwa unawasha, mpaka anywe cetrizine ndo muwasho unatulia, hii dawa hutuliza kwa km siku nne tu baada ya hapo muwasho pale pale. Alishameza dozi za fungus kama mara nne hivi kwa siku kumi na tano lkn tatizo bado lipo pale pale.

Hofu yangu ni kuwa hizi cetrizine zinaweza zikamletea madhara in a long run. Sasa daktari saidia hapo yawezekana ni nini sababu ya huu ugonjwa?
=====
WADAU WENGINE WENYE TATIZO HILI:

Salaam wanabodi.

Nimekuwa nasumbuliwa na tatizo la kuwashwa mwili mara kwa mara nilikwenda hospital wakapima mkojo na damu hawakuona kitu,

Tatizo hilo limenianza muda mrefu kama miaka mitano iliyopita lakini mpaka leo sijapata tiba.mwili unawasha wote kwa vipindi tofauti tofauti hata nikijikuna haisaidii mpaka upoe wenyewe.Je tatizo ni nini na tiba ni ipi? Msaada tafadhali!
===
Jamani wanajamvi,

Nimekua nawashwa kuanzia kiunoni kushuka chini. Miguuni, mapajani na pia kwenye upaja wa mkono upande wa nyuma. Huwa nawashwa zaidi nikitoka kuoga au nikivua nguo ili nilale. Ni muda sasa. Nilishaga tumia dawa za allergy lakini wapi.

Msaada jamani. Specialist wa ngozi Dar au Mbeya anapatikana wapi??
===
Wadau nimepatwa na tatizo ninawashwa mwili mzima wiki ya pili sasa ilianza kama utani kwa kuwashwa sehemu za siri nikaenda kupima nikaambiwa niko ok kwenye damu nikapewa dawa ya kutibu u t i maana ilionekana kuna uchafu kwa mvali kwenye mkojo nimemaliza dozi nimeenda kuchukua vipimo vyote mpaka vya magonjwa ya zinaa nimeambiwa ok sina ila ninawashwa mwili mzima yaani kila sehemu nikiigusa na vipele bado vipo sehemu za siri kwenye uume na makende na baadhi ya sehemu za mwili naombeni msaada wenu
===

Nina matatizo ya kuwashwa mwili halafu nikijikuna kanatokea kakidonda kadogo iv kama kama vile umejikuna kakipele. Inatokana na nini ama nitumie dawa gani kuepukana na janga hili wenu ushauri. Wazo baya kuliacha hp zuri kulitekeleza
===


hata mimi wakuu, nawashwa mwili mzima km mtu aliemwagiwa upupu, sasa nimejikuta kila baada ya siku3 nakunywa kidonge kimoja cha centrizene (kidonge cha aleji), nikishakunywa tu nakaa hizo siku bila kuwashwa, sasa imekuwa ni tabia ya kunywa dawa ili nisiwashwe, nahofia sumu itazidi kujaa mwilini maana miaka 2 sasa nakunywa dawa tu.
===

Naombeni ushauri wenu madaktari wa jukwaa hili,

Mimi nawashwa sana na mwili kila baada ya kuoga,yaani dakika tano baada ya kuoga huwaga ni za shida sana kwangu.

Nakumbuka nilipata tatizo hili kwa mara ya kwanza 2001 wakati huo kijijini alinitambaa mdudu yule anaitwa slug anatembea kama Kono kono ila hana shell.

Nilitoka lenge lenge kama nimeungua moto na mwili uliwasha sana yaani sana nilikimbia straight hospitali na nilipewa dawa pale pale baada ya muda kidogo nilitulia.

Nikapewa dozi nikatumia,ilipita muda kidogo tatizo lilirudi tena sasa ni kila baada ya kuoga.

Nilirudi hospitali nikaambiwa ni fungus sugu na minyoo nikala dawa lakini wapi!

Nikarudi tena Hapa Dar nikapewa tiba ile ile lakini wapi.

Siamini kama haitibiki hii kitu.

Msaada wenu wanajukwaa hili la JF Doctor ni wa muhimu.

Natanguliza shukrani zangu.

=================
Matatizo Mengine
=================
===


BAADHI YA MICHANGO YA WADAU KUHUSU TATIZO HILI:
Unatumia maji ya kisima au bomba? Kama umeshatumia yote na bado tatizo liko pale pale basi jaribu kubadilisha joto la maji unayotumia.

Hiyo ni allergy tu ambayo itaisha baada ya muda fulani.Mi mwenyewe nilikuwa nayo lkn iliisha yenyewe.

If symptoms persist then seek medical advise!
===

Itakua ni dryness. Jaribu kuoga na shower gel yenye moisturizer au kupaka mafuta ya dry skin.

Sababu lingine maybe maji tu yenyewe. cheki tatizo lilianza lini, kama ulihama au kusafiri hivi karibuni jaribu ku-link.

Kula samaki nyingi kuliko nyama (kama 150 to 250g 2 or 3 times a week) inasaidia kupunguza dryness.
Kama kuwasha kunaendelea pata ushahuri wa daktari (maana hapa sio hospitali, tunashahuriana tu kutokana na experiences)
===

Hii inaitwa acquagenic uticaria, naomba Google afu atapata maelezo mazuri. Lakini mara nyingi no specific matibabu, kikubwa unatakiwa upunguze exposure kwa majimaji kwa muda mrefu.

Kuoga tumia short time na tumia cotton towel and cotton cloths hata mashuka ya kutandika. Pale inapozidi meza antihistamine mfano cetirizin tabs 10mg od 5/7. Ila Google hiyo itakusaidia kupata maelezo mazuri.

All the best
===

1.Acha kabisa kuoga maji baridi- mimi nilipoacha kuoga maji baridi nilipata nafuu kubwa sana.

2.Jitahidi sana mwili usitapate baridi wakati bado haujakauka vizuri,jifunike vizuri mara baada ya kutoka kuoga na ninakushauri ununue BATHROBE mimi lilinisaidia sana.

3.Nunua Anti allergy kama CETIRIZINE AU LORATIDINE (mojawapo kati ya hizo) ziwepo karibu muda wote na uzitumie pale unakapoona kuwasha kunazidi na huwezi kuvumilia,naimani ukienda Pharmacy watakuelekeza namna ya kutumia.

kwa bahati mbaya tatizo hili kama zilivyo allergy nyingine halina tiba ila unaweza kupunguza adha unayoipata kwa kiasi kikubwa kama ukichukua tahadhari za kuto expose mwili wako mara baada ya kutoka bafuni (mimi nilikuwa nawashwa hata nikinyeshewa na mvua!) na kama bado ukiona tatizo linaendelea nenda hospitali yoyote iliyo karibu.
===

Dawa ingine ya Muwasho siyo lazima uwe wa mwili tu, bali kuna sehemu mbalimbali za mwili ambazo

zimejificha na fangasi uenda kujihifadhi katika sehemu hizo nazo unaweza kutumia maji ya aloe vera kwa

kutibu . Kwa jinsi gani unaweza kujizuia au kujitibu na muwasho kwa kutumia aloe vera. Jinsi ya kuandaa maji

ya Aloe vera kwa ajili ya kutoa muwasho na bateria.Chukuwa vikwanya vitano vya alovera kisha safisha kwa

maji safi, kata vipande hivyo kwenye sufuria ya kilo moja. Jaza maji kisha uweke jikono kwa ajili ya

kuchemka. Epua na uyaweke pembeni kwa ajili ya kpoa aukuwa na hali ya uvuguvugu. Toa majani ya

aloe vera katika sufuria na kisha weka katika ndoo tayari kwa kuonga.


Angalizo

Baada ya kuoga unatakiwa kukaa na maji hayo mpaka yatakapo kauka mwilini pia ni dawa ya harara na kufanya ngozi kuwa nyororo. Angalia Picha chini ya Aloe Vera.
View attachment 144519
===

Kwenda kupima ni jambo jema zaidi.Ila kwa dalili zako kuna uwezekano mkubwa sana damu yako itakuwa na over acidity(yaani kiwango cha acid/tindikali kwenye damu ni cha juu kuliko kawaida).Hii husababishwa na mambo mengi sana kama vile ulaji wa vyakula vibovu na matumizi ya madawa mara kwa mara;

Vyakula vibovu huweza kuwa vile vya kusindikwa viwandani kama vile juice,soda,tomato source nk,ulaji wa nyama kwa wingi,ulaji vya vyakula vya kukaangwa kwa wingi,unywaji wa pombe,uvutaji wa sigara na mengine ambayo si ya asili.
Madawa yanaweza kuwa ya antibiotic,diclofenac,panadol,dawa za kuongeza nguvu za kiume,uzazi wa mpango na mengine kama hayo.

Ili kuondoa tatizo unahitaji kula vyakula vya asili na kuachana na vile nilivyotaja hapo juu,kunywa maji mengi,mboga za majani zisiive sana kama vile spinach,celery,broccoli, juice za matunda kama vile parachichi pamoja na mbegu yake iliyosagwa,juice ya caroti,juice ya tikiti,juice ya papai na embe.Epuka sukari ya viwandani,epuka chumvi ya viwandani/chumvi ya unga na badala yake tumia ile ya mawe.

Kama utakuwa serious kwa kufuata ninayoeleza,kuanzia mwezi mmoja utakuwa umepona kabisa.

Karibu.
===

Kama upo kanda ya kaskazini kuna daktari bingwa wa allergy ana clinic binafsi pale YMCA, Amepatwa na allergy ya kitu fulani hapo nyumbani, sasa sambamba na kumpeleka kwa daktari bingwa wa allergy, hebu pia jaribu mbinu hii:

Allergy management by elimination: mwanzishie dawa ya minyoo, asipopata nafuu ufuate hatua hizi moja baada ya nyingine. Best wishe kaaaka
1. Safisha chumba anacholala na sebule anapokaa kwa umakini mkubwa.
2: badilisha mashuka na mablanketi yote anayotumia, mnunulie matandiko mapya
3: badilisha mafuta ya chakula mnayotumia au mpe chakula kisicho na mafuta kabisa, ale michemsho ya vyakula organic au vya asili.

4: badilisha sabuni ya kuoga na kufulia pamoja na tooth paste
Hatua hizi zitekelezwe moja baada ya nyingine hata kwa interval ya wiki moja moja ili kutathmini maendeleo.

Dada yangu alipona allergy kwa kubadilisha sabuni ya kuoga, kutokunywa fanta na mafuta ya kupikia, na mtoto wangu jaribio moja tu la kumbadilishia blanketi na sabuni ya kuoga alipona mazima!
===

Vipele vinakutokea ameneo gani hasa?

Kuna kipindi nilikua nawashwa sana na mwili na kutokewa vipele flani vinakua vyekundu, mwanzo nilijua ni maji ya kuogea nayotumia(ya chumvi) ikanibidi niwe nanunua yale ya boza(hayana chumvi) lkn tatizo liliendelea..... nikapima labda ni magonjwa ya zinaa, minyoo lakini wapi.

Kuna jamaa akaniambia jambo ambalo hadi leo lilinisaidia sana.

Kuna wakati upande wa pembeni tumboni huwa panauma.... sikutilia mkazo.... ila akaniambia ni dalili za figo kufeli ndo maana unapata magonjwa ya ngozi..

Dawa yake acha kutumia vinywaji kama soda, energy na pombe kali(kwa wakati huo ndo ilikua vinywaji vyangu, kiroba na redbull au energy)
Kisha nianze dozi ya maji, baada ya kusikia balaa la figo kufeli.... nilianza dozi ya maji kwa nguvu zote, sa1 hadi sa5 nahakikisha lita2 zimekata, napumzika, sa7 hadi sa11 nakata zingine2 kisha napumzika, sa1 hadi muda wa kulala nakata zingine2.

Kwa kweli matokeo yalikua mazuri, upele ulipona, maumivu sikipata tena.

Kwa hiyo ndugu, unaweza jua una magonjwa ya ngozi(vimelea) kumbe ni tatizo la sumu mwilini.

Mimi sina desturi ya kwenda hospitali wala kunywa midawa, napopewa ushauri wa njia za vyakula huwa nazingatia sana, hata malaria naitibu kwa machungwa tu.
===

Hili ni tatizo lililo nisumbua kwa miaka kama sita na hakuna dawa ilio nisaidia lakini nikushauri vtu vchache vlivo nisaidia had now nko fresh

1.Jaribu kubadirisha maji kama unaoga ya baridi jarbu kutumia maji ya moto.
2.Punguza mda unaotumia kuoga ili kupunguza contact na maji kwa mda mrefu
3.Tumia dodoki soft na usijisugue sana
4.Subiri ukauke ndio ujipake mafuta
5.Tambua mazingira yanayo chochea tatizo mfano mimi mikoa ya baridi ndio ilio kua inaniathir zaid.
Ni ayo tu.
===

Poleni sana waungwana!
siku moja nilisikikiza kipindi cha afya radio moja walikuwa wakizungumza juu ya tatizo la kuwachwa mara tu mtu unapotoka kuoga:-
Sababu
Ni allegy inayosababishwa na bacteria ambao aidha wanakuwemo kwenye maji au kwenye kifaa kinachotewa maji hasa magudulia yenye mfuniko mdogo ambayo hutunza uchafu ambao ambao husababisha fungus ambao mwisho wa siku ndio huleta mwasho mwilini. Pia huweza kutokea kwenye mabomba kutokana na mifumo mingi ya maji kutokuwa salama mfano mabomba ya maji safi kupasuka sehemu ambayo ni makutano na bomba la maji taka etc!

Tiba:
Hiyo ni allegy ivo unashauriwa kutumia anti-allegy lakini pia unaweza tumia shower gel ambayo hutengeneza layer laini inayokuwa ni kinga kwako wakati wa kuoga!

Naomba kuwasilisha, mtaniwia radhi hzo ni point chache ambazo nilizidaka siku hiyo sina utalaam wowote wa kiafya kwa hiyo sitegemei swali la kitaluma! Asanteni.
===
Ninafahamu sababu mbili za hili tatizo lakini zote zinahusiana na allergy.

Ya kwanza ni allergy kwenye maji, kitaalamu inaitwa 'aquagenic urticaria'. Kuna baadhi ya watu ambao wakikutana na maji huwashwa sana, wengine hupata hata maumivu ya ngozi na wengine hata wakinywa maji wanapata maumivu kooni. Hii hutokana na miili ya watu hawa kutopatana na maji.Wanaweza wakatumia dawa za allergy (antihistamines) kama chlorpheniramine (piriton) au cetrizine nk, ili kutuliza lakini hazitibu. Matibabu yake ni kuepuka maji, simaanishi usioge lakini oga kwa muda mfupi kadiri utakavyoweza na epuka kunyeshewa na mvua.

Ya pili inahusishwa na uwepo wa kemikali aina ya sodium lauryl sulfate kwenye vitu kama shampoo, sabuni, cream za kunyolea nywele, na hata kwenye shower gel, hii nayo husababisha allergy ikiwa mtu anayeitumia hapatani na hii kemikali, matokeo yake huwashwa baada ya kutumia hivi nilivyovitaja. Matibabu ya hii ni kutumia sabuni au shampoo ambazo ni sodium lauryl sulfate - free. Ukinunua sabuni au shampoo angalia kama haina hiyo kemikali na nunua ukatumie.
===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII:
- Tatizo la kuwashwa mwilini baada ya kuoga: Fahamu chanzo, ushauri na tiba - JamiiForums
 
Consultant

Consultant

JF-Expert Member
8,611
2,000
Mi nadhani kuna kitu huwa anakula ambacho ana allegy nacho. Mwambie ajichunguze vizuri - siku muwasho ukianza tu, akumbuke amekula nini na nini. Na inaonekana ni chakula anachokipenda maana huu muwasho ni wa muda mrefu.

Kuna ndugu yangu alikuwa akila karanga tu, atawashwa na kuvimba sana. Tulipogundua, mpaka leo karanga hagusi na lile tatizo limeisha

Ingawa jibu langu si la kisayansi zaidi, is worth trying, inaweza kumsaidia
 
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
3,395
1,250
Chimunguru,

umezunguka kote kwa imani za kimwili lakini hazijasaidia kitu
nakushauri pia uende kwenye imani roho, yaani kanisani JESUS is only
one can cure that problems
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
10,586
2,000
@Sinyolita,

Thanks kwa mchango wako Sinyolita, itabidi nikae nae nimuulize ni nini anapendelea kula kwa sana ajaribu kuacha tuone responce inakuwaje
 
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
3,395
1,250
Mi nadhani kuna kitu huwa anakula ambacho ana allegy nacho. Mwambie ajichunguxe vizuri - siku muwasho ukianza tu, akumbuke amekula nini na nini. Na inaonekana ni chakula anachokipenda maana huu muwasho ni wa muda mrefu.

Kuna ndugu yangu alikuwa akila karanga tu, atawashwa na kuvimba sana. Tulipogundua, mpaka leo karanga hagusi na lile tatizo limeisha

Ingawa jibu langu si la kisayansi zaidi, is worth trying, inaweza kumsaidia
ndugu hizi imani za kutukaza kula baadhi ya vyakula kwa madai ni areji ni mbaya sana, Mungu alimpa mwanadamu ruhusa ya kula, hata miye nilikuwa sioti nywele kwa mda wa miaka 3 nikiwa mdogo wakadai ati nisile samaki aina ya kambale, na kitimoto yaani n yama ya nguruwe, lakini ilikuwa ni ngumu kidogo, kwenye kitimoto, nikaenda church,
nikaombewa na sasa sina tatizo la namna hiyo, vitu vingine ni roho chafu tu
 
B

Bawa mwamba

JF-Expert Member
350
0
ndugu hizi imani za kutukaza kula baadhi ya vyakula kwa madai ni areji ni mbaya sana, mungu alimpa mwanadamu ruhusa ya kula, hata miye nilikuwa sioti nywele kwa mda wa miaka 3 nikiwa mdogo wakadai ati nisile samaki aina ya kambale, na kitimoto yaani n yama ya nguruwe, lakini ilikuwa ni ngumu kidogo, kwenye kitimoto, nikaenda church,
nikaombewa na sasa sina tatizo la namna hiyo, vitu vingine ni roho chafu tu
Mungu aliumba wanadamu,magonjwa na vifo.vyote hivyo aliviweka ili tusijisahau na tuwe karibu nae pindi vinapotusibu,.akatujalia imani ili tumwangukie na kumwangalia yeye.akatupa akili ya utambuzi toka enzi za adamu na hawa na kutupa ruhusa ya kuvipa majina vile alivyoviumba na pia kivisifu.

Pia aliumba kazi ili binadamu wategemeane na akazibariki ,navile vile kuwaonyeshea kidole wale wazitumiavyo ambavyo sivyo,nakuwaambia hawata uona ufalme wake [mafarisayo,watoza ushuru] na pia kupitia watendaji wake,aliwakumbusha binadamu umuhimu wa kumpa kaiza kwa yaliyo yake kaiza na kumpa mola yaliyo yake.

pia watendaji hao hao walikumbusha umuhimu wa afya na kusema mwenye afya hamuitaji daktari bali ni kwa wale walio wagonjwa.[musa aliinua nyoka wa shaba na kusema uumwapo na hawa basi muangalie huyu nawe utapona,.kuzingatia hilo ndio maana alama yao ni msalaba na nyoka] tafsiri ya imani ya dini inaharibiwa,.bongo nilipata mgonjwa ambaye ndugu zake walikataa asiongezewe damu,kisa ni Shahidi,...,.sitaki mjadala wa kiimani, ila dini inatumiwa vibaya na kugharimu maisha ya watu,.inapaswa kuchanganya elimu zote,.ya dunia na ya kidini[ a.ya mwenzako changanya na yako,.]
 
F

fimbombaya

Member
47
95
ni tatizo ambalo limejitokeza kwangu takribani miaka mitatu iliyopita hadi sasa! mara tu nimalizapo kuoga ninaanza kuwashwa mwili mzima kwa muda usiozidi dakika 15 na wakati mwingine unapojikuna vipele vidogovidogo hutokea. tatizo hili linaninyima raha mno kwa anaefahamu dawa anisaidie na pia si mbaya kama utanieleza chanzo cha tatizo.
 
Zasasule

Zasasule

JF-Expert Member
1,005
1,195
ni tatizo ambalo limejitokeza kwangu takribani miaka mitatu iliyopita hadi sasa! mara tu nimalizapo kuoga ninaanza kuwashwa mwili mzima kwa muda usiozidi dakika 15 na wakati mwingine unapojikuna vipele vidogovidogo hutokea. tatizo hili linaninyima raha mno kwa anaefahamu dawa anisaidie na pia si mbaya kama utanieleza chanzo cha tatizo.
I thought niko peke yangu who have this problem!!mzee am glad that u posted this topic,ngoja tuone wengine wana ujuzi gani juu ya hili
 
B

bitimkongwe

JF-Expert Member
3,055
1,500
Unatumia aina gani ya sabuni? Jaribu kufanya upelelezi ubadilishe sabuni halafu uone jee kuna mabadiliko yo yote?
 
B

bitimkongwe

JF-Expert Member
3,055
1,500
Jaribu sabuni ambazo hazina perfume kama lifebuoy.

Ukiona hakuna mafanikio jaribu hizi medicated (siyo zenye mercury)
 
myhem

myhem

JF-Expert Member
932
195
Unatumia maji ya kisima au bomba? Kama umeshatumia yote na bado tatizo liko pale pale basi jaribu kubadilisha joto la maji unayotumia.Hiyo ni allergy tu ambayo itaisha baada ya muda fulani.Mi mwenyewe nilikuwa nayo lkn iliisha yenyewe.
If symptoms persist then seek medical advise!
 
S

SARAWAT

Member
38
0
Hata mie natatizo kama hili, naona ni reaction ya maji kwa mwili, nina miaka mingi zaidi ya kumi. Ukimaliza kuoga jipake mafuta haraka hutasikia miwasho, imenisaidia sana. Usifadhaike tupo wengi wenye tatizo hilo
 
wende

wende

JF-Expert Member
714
195
ni tatizo ambalo limejitokeza kwangu takribani miaka mitatu iliyopita hadi sasa! mara tu nimalizapo kuoga ninaanza kuwashwa mwili mzima kwa muda usiozidi dakika 15 na wakati mwingine unapojikuna vipele vidogovidogo hutokea. tatizo hili linaninyima raha mno kwa anaefahamu dawa anisaidie na pia si mbaya kama utanieleza chanzo cha tatizo.
I have the same tatizo,nilifanya medical check up ya haja kubwa nikambiwa kuwa nina minyoo na Amoeba pamoja na alergy.......nikapewa dawa! You cant believe, nilipona kabisa but this lasted for only few days na sasa tatizo lipo vilevile na nafirikia sijui sasa nifanyaje!!

Alafu nikienda DSM, Arusha na Moshi maji ya kule hayawashi kabisa but nikioga maji ya huku Shinyanga......wajamani iyo kero ya mwasho ninayopata sisemi!!!! Maji ya huku ni ya bwawani/mvua si unajua huku shy??

Sijajaribu kubadili joto la haya maji kwa kuyachemsha,,,sipendi sana maji ya moto,,,,naoga all the time maji baridi.....embu watalaam tupeni ushauri jamani tupo wengi tunateseka sana na hii hali. Nami nawasilisha!
 

Forum statistics


Threads
1,424,602

Messages
35,068,211

Members
538,026
Top Bottom