Mkuu hizi ni hadithi za kusadikika... Huna ushahidi zaidi ya simulizi.. unaposema Kighoma Malima alikuwa akikomba fedha kwani Hazina kuna cash money gani ambayo ilimfanya asikombe wizara ya Elimu..Na tuache hivyo kuna waziri gani ambaye alikuwa hakombi (kufisadi) wakati wa Mwinyi? Wameiba woote lakini aliyeonekana ni Malima tu - muislaam mwenye siasa kali!Kwenye nyekundu kuna uzi mmoja ulikuwa ukiendelea wiki kadha zilizopita waweza tafuta ukapata ilikuwa kuwaje na kwanini ilivuma maramoja kisha baadaye kupotezewa kwa Mzee JSM kuitwa Jumanne.
Kwenye bluu, wako wanaosema Kighoma Ali Malima, alikuwa na back-up ya kundi fulani la waislamu ambao walitaka rais atakayefuata baada ya Mzee Mwinyi awe muislamu. Huyu jamaa alikuwa ni mdini kwelikweli. Anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakishadidia kichini-chini suala la Zanzibar kujiunga na OIC. Baada ya Kibona kama Waziri wa fedha kufariki, yeye ndiye aliyepewa nafasi hiyo.
Akiwa madarakani akaanaza kukomba pesa kidogo-kidogo lakini kikubwa akawa anaficha ughaibuni. Strategically, kwamba atazitumia kwa kampeni. Alipokosa nafasi CCM akachomokea NRA. Akazikumbuka ngawila zake ughaibuni. Alipokwenda zifuata, the perfect thing was done, account ikawa imefungwa na Serikali ya Tanzania. Jamaaa akapata mfadhaiko/mshituko basi akafa. Miongoni mwa waliom-support ni Kitwana Kondo nao wakakumbwa na mfadhaiko, lakini hakufa aliendelea kuishi.
Ni kwa uchache wa kile nachoweza kumbuka na kuandika, wapo wenye mengi ya kueleza. I stand to be corrected.
Je unakumbuka kwamba hata Lowassa alikuwepo na aliziiba waziwazi mbona hatukusikia yeye kuondolewa nafasi ya uongozi!
Na samahani ni watu kama wewe ndio mimi nawazungumza.. Kila kitu udini udini wakati hukuwa karibu na Malima na kibaya zaidi upo dini nyingine tofauti na Malima hivyo huwezi kuwa na info za ndani isipokuwa unasukumwa na hofu.. Na kuna ubaya gani leo hii mimi nikiunga mkono OIC! ndio inanifanya mimi kuwa extremist?.