Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

Tatizo kubwa ambalo linaumiza nchi yetu ni mfumo wa kuwapata wale ambao wanasimama katika nafasi mbalimbali. Tunampata raisi si kwa sababu

yeye ni bora bali kwa sababu genge la watu fulani kwa pesa walizowaibia watanzania na kwa nia yakuonekana kwamba matakwa yao yanasimama

wamemtaka awe raisi. Hii inafanya tuwe na kuchagua raisi bora kati ya wengi waliohafifu. Its like trying to make sense out of nonsense! Matokeo yake

tunapata mtu bomu ambaye kwa sera za chama analazimika kutawala kwa miaka kumi! Imagine watu chini ya kumi wanaamua hatima ya Tanzania

for the next ten years! mfumo huu ndio uliopekea Mkapa 1995, JK 2005 and who knows!? (kama hatutakuwa makini) May be EL/Mwinyi/Nahodha

/Membe or Pinda 2015! Disastor!
 
Penye nyekundu, si kweli. Ni uongo ambao watu wa kundi la Kikwete waliutengeneza/kuuzusha na kuueneza. Makusudi tu ionekane Nyerere alikuwa anamkubali Kikwete. Uvumi huu nilianza kuusikia 2003 toka kwa mwana-CCM fundi wa kujipendekeza, ambaye 2005 alijiweka wazi ni mwanamtandao akimpigia kampeni Kikwete Dar na Moro.

Nyerere alikuwa amekwishalishwa taarifa muhimu na watu wake wa Usalama wa Taifa, na mengine alikuwa anayajua, juu ya wagombea wote wa urais kwa tiketi ya CCM kabla hajaenda Dom na akiwa Dom nini wengine wanafanya.

Kikwete has nothing to boast that JK wa ukweli was pleased with his leadership character at any point. JK wa ukweli was ashamed of him since that day when he set a " failed conspiracy snare" against his boss at Monduli.
Mkuu haya ya JK pale Monduli si wengi tunayafahamu mimi nikiwa mojawapo. Nitashukuru sana ukiweza kutuelimisha mimi na wengineo. Ahsante
 
Calnde you are right. Mfumo ni kila kitu katika nchi. Ndiyo ina dictate kila kinacho endelea kwenye nchi.
 
Unafikiri na doubt unachosema wewe? hapana mkuu ndio uandishi wangu kupinga hizi tuhuma na uvumi ambao huenezwa na mtandao wa CCM... wakati ule wa Nyerere walimtumia sana Paul Sozigwa na kama sikosei magazeti yote na radio zilikuwa chini ya serikali...

Nachosema tu ni kwamba hapakuwepo na ukweli wowote kuhusiana na Malima, kama ilivyo leo kwa Dr.Slaa. Ni mchezo wa kisiasa na kama Dr.Slaa angekuwa chaguo la system basi JK ndiye ungemsikia akilaumiwa kwa udini na kadhalika... Truth remains - hakuna kiongozi yeyote aliyetaka kugombea urais kwa kutumia tiketi ya dini hata huyo mchungaji Mtikila hakufanya hivyo!

Nimekupata mkuu, kwamba ilikuwa ni propaganda machine dhidi ya Malima. Kama ni kweli habari hizo zilikuwa za uzushi, basi nasikitika sana kwani niliziamini.

Viva JF kwa kutuweka sawa na kurekebisha baadhi ya flaws kwenye historia ya Taifa letu. JF ni muhimu sana.
 
Dah binafsi nimejifunza mengi sana. Hivi hamna videos na pictures za uchaguzi wa mwaka huo kuanzia chaguzi ndani ya chama na kwenye chaguzi kuu? Wenzetu wana mtindo wa kudocument mambo kama haya. I have been thinking of making a documentary on the office of the presidency kuanzia Nyerere mpaka JK hapo Mungu atakapo mjalia kumaliza salama 2015.
 
Mwalimu alikua anaona mbali sema sis 2005 tukawa na mawazo ya hapa kwa hapa kama kuku
 
Mwalimu alikua anaona mbali sema sis 2005 tukawa na mawazo ya hapa kwa hapa kama kuku

Maneno yakisemwa yakapingwa na yakatokea ndiyo yana nguvu ya kihistoria. Kama tungefuata maneno ya Mwl. Nyerere leo hii wala tusingeona uzito wa maneno yake. Tungechukulia tu kama jambo la kawaida. Kila taifa changa lazima lipite mabonde kwanza kabla ya kufika kileleni. Labda kipindi hiki kitakumbukwa kama kipindi muhimu sana kwenye historia ya nchi yetu maana sasa hivi historia pekee tuliyo nayo ni uhuru wa Tanganyika na mapinduzi ya Zanzibar..
 
Nimekupata mkuu, kwamba ilikuwa ni propaganda machine dhidi ya Malima. Kama ni kweli habari hizo zilikuwa za uzushi, basi nasikitika sana kwani niliziamini.

Viva JF kwa kutuweka sawa na kurekebisha baadhi ya flaws kwenye historia ya Taifa letu. JF ni muhimu sana.
Niamini mkuu wangu, Hata kesho Regia Mrema akija gundua system ina abuse wanawake iwe ktk ajira au elimu na akasimama kulizungumzia ataonekana Mjinsia (sijui ndio hivyo inaitwa) Au mbunge yeyote mwanamme akisimama na kupinga viti maalum muda wote lazima atapachikwa - Ujinsia kwa sababu huwezi kuzungumzia vitu hivi bila watu kuitazama kwanza jinsia yako kisha wanaunganisha utetezi wa hoja nzima.

Labda niseme tu kwamba Mar. Malima kwa kutoelewa WATU na MAZINGIRA alokuwepo alifanya kosa kubwa sana kuandika ile barua kwa rais Mwinyi akiwa muislaam na akishirikisha viongozi wote waliomtangulia kitaifa na ktk wizara hiyo. Kuwashutumu watu kwa kosa la makusudi kutowapeleka waislaam na wanawake elimu ya juu ni shtaka zito sana ambalo pengine alihitaji muda na subira ktk uwasilishaji wa hoja nzima.

Miaka ya Nyerere na Mwinyi sote tunajua ilikuwa njaa kali, nafasi za ku advance zilikuwa za kugombania na kila mzazi alitaka mwanaye aendelee mbele kimasomo. Katika utafiti nilowahi kuufanya ilikuwa kitu kama asilimi 5 tu ya wanafunzi ndio walikuwa wakiendelea na masomo.. Kwa hiyo vijana wengi wa Masaki, O'bay, Sinza, Mbezi yaani kote sehemu za fridge open (happened to be Christians) walikuwa na majibu ya mitihani ama wazazi wao wako madarakani.

Kushinda darasa la saba na form 4 was a big deal wakati ule yaani wazazi wanaweza kutokula wakisikia umeshindwa..Ukweli ni kwamba haikuwa mpango wa serikali bali serikali ilishindwa kuzuia kama tunavyoshindwa leo na Ufisadi..
 
Mkuu Mkandara au mkuu yoyote yule mwingine, mwaka huo kulikua na mgombea yoyote kutoka Zanzibar? Ukiacha of coarse Salim A. Salim aliye kataa. Na je ilifikaje mpaka Omar Ali Juma akapewa ugombea mwenza? Maana huyu kabla hajafa alikua anaonekana ana nafasi kubwa sana ya kushinda 2005 haswa kama angepush "Ni zamu ya Zanzibar".
 
Mkapa aliposhinda alimpa JK waziri ya wa nje sio kwa kupenda bali kwa maelekezo tena inawezekana ni ya mwalimu. Inawezekana yeye angempa wizara kama ya Kilimo. Unajua kuna wazara nyingine Tanzania japo ni za muhimu lakini inaonekana kama ni kukomolewa. Si unajua nchi yetu haina dira. Tuna sera ya kilimo kwanza lakini MOFA ni wizara kubwa kiprotocol kiliko ya wizara kilimo. Anyway nisiende huko ......

Ni inasemakana MKapa aliagizwa na Mwalimu kuwa kwa wakati huo anaona akimaliza mkapa atayefuata ni JK. Na katika maelekezo hayo inasemekana shahidi aliyekuweopo ni Mkapa, Nyerere na Kingunge. Ni kwa sabau ya maagiz hayo Mkapa alilazimika kumuweka JK wizara ya mambo ya nje. hayakuwa mapenzi yake........

Kuna wakati Mkapa alitaka kumtosa JK sababu aliona ameshikamana na watu ambao kwa mtazamo wake kama nyerere angekuwepo basi angemtosa lakini kingunge ndiye alikaa kidete kumumbusha maelekezo waliyopewa na mwalimu. Na ndio Maana JK anamuheshimu sana Kingune ........

Lakini nadhani wasi wasi wa Mkapa nao umedhihirika kuwa una hoja sababu matatizo ya ushkaji wa JK na Lowasa.

Lakini hayo yote niliyooleza ni Inasemekana
Hapana. Hapa nitakataa kabisa. Mkapa mwenyewe kaniambia kwa mdomo wake kwamba alipomfuata Mwalimu kuomba ushauri kuhusu baraza la mawaziri Mwalimu alikataa katakata akimwambia "it is your government. You choose the people you want to work with." Mwalimu hakuwa na usemi wowote hata kidogo katika uchaguzi wa mawaziri ya serikali ya Mkapa. Ila nasikia alishangaa aliposikia Mkapa amempa Lowassa wizara.
 
Mkuu Jasusi,

Hili ni swali tu. Je unafikiri Mkapa alikua accidental president? Kwa maana inaelekea majority 1995 walimtaka JK ila Mkapa kwa kupendwa na mtu mmoja tu ndiyo akapata uraisi. Did JK deserve to win the 1995 presidency? Na je unadhani sasa kundi la JK linamuandaa nani kuwa raisi?
Mkapa alikuwa "lightweight" katika siasa za Tanzania. Pia hakuwa choice ya kwanza ya Mwalimu, na hilo atakumbusha kila anapopata nafasi. Mwalimu alitaka Salim achukue forms za urais 1995, lakini Salim akikumbuka jinsi alivyodhalilishwa na Wazanzibari 1985 alikuwa anasita akitaka "ateuliwe" Mwalimu akasema kuwa Salim anataka apewe kila kitu kwenye sahani. Waliomshawishi Mwalimu kumsapoti Mkapa alikuwa ni Butiku na afisa mmoja wa Kitanzania aliyekuwa benki ya dunia ambaye alikuwa na uhusiano mzuri na Mwalimu. So Mkapa was Mwalimu's second choice.

Lakini ukiangalia cv za Mkapa na Kikwete kufikia 1995 Kikwete was a featherweight. Hakuwa na accomplishment yoyote ya kujivunia wakati Mkapa alishawahi kuwa mhariri wa magazeti ya serikali, press secretary wa Mwalimu, Balozi, Waziri wa mambo ya nje, etc. etc. Kwa hiyo ile kauli kuwa Kikwete alikuwa bado hajakomaa ililenga kuonyesha hilo. Na hata sasa ukilinganisha utawala wa Mkapa na wa Kikwete and their accomplishments, kama Mkapa asingekuwa fisadi, he would be standing tall above them all.
 

Mimi kuna kitu kimoja kina nitatiza kuhusu Mkapa. Mimi naamini Nyerere hakua mtu wa kukurupuka. Kama alimchagua Mkapa naamini kabisa Nyerere alidhani anafaa. Je Mkapa ni alikua anaficha makucha yake au kweli alikuwa "Clean" akaja kubadilika baadae?
Up to the time Mkapa anaingia Ikulu hakuwa na mali. Nakumbuka alikuwa na Mercedes moja chakavu iliyokuwa ya ubalozi wetu Ujerumani.
So at that time the "clean label" suited him. It was after he was in Ikulu that he could not overcome the temptation to get rich.
 
Hapana. Hapa nitakataa kabisa. Mkapa mwenyewe kaniambia kwa mdomo wake kwamba alipomfuata Mwalimu kuomba ushauri kuhusu baraza la mawaziri Mwalimu alikataa katakata akimwambia "it is your government. You choose the people you want to work with." Mwalimu hakuwa na usemi wowote hata kidogo katika uchaguzi wa mawaziri ya serikali ya Mkapa. Ila nasikia alishangaa aliposikia Mkapa amempa Lowassa wizara.

Kwa hiyo mkuu pamoja na kuwa "second option" Nyerere alimuamini sana Mkapa kwa sababu kwa uelewa wangu (naomba kusahihishwa), Nyerere alikua too involved na serikali ya Mwinyi in terms of kuinfluence baraza na decision making. Je ni kweli hakumuamini Mwinyi (kwenye uwezo wa kuongoza) lakini akamuamini Mkapa? Au aliona alikua too involved na serikali ya Mwinyi akajifunza na kuamua kumuachia Mkapa maamuzi yote?

Ila kuna kingine kina nitatiza mkuu. Wengi wanadai Nyerere kumpenda Mkapa ni kwa sababu ya Ukatoliki wao. Sasa hawa watu wanaelezeaje kuwa first choice ya mzee alikua SALIMA AHMED SALIM?
 
Mkuu Mkandara,

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba raisi huandaliwa. Kwa kawaida raisi mmoja tu akisha ingia madarakani basi kuna kundi limepanga kutoa raisi ajae. Kwa hiyo ni process inayoenda mbali zaidi na siku tu form za chama zinapo tangazwa. Kama ni hivyo basi JK tunabidi tukubali kuwa ni mwanasiasa hodari (kuwa mwanasiasa mzuri siyo lazima uwe kiongozi mzuri). kwa sababu 1995 yeye ndiyo alikua favorite na 2005 akachukua ushindi.

Ukweli ni kwamba JK kajiandaa tokea ni mdogo kuja kuwa raisi tokea mahusiano aliyo tengeneza UDSM, jeshini na kwenye chama. Tokea mwanzo alikua na nia ya uraisi na akajiwekea mazingira ya kuuchukua na ukweli ni kapata. Mimi naamini system nzima siyo inayo panga nani awe raisi bali hata system yenyewe ina vikundi mbali mbali. Kundi la JK lilijipanga vizuri na nilitambua kuwa kati ya JK ndiye electable kwa hiyo yeye atashinda na wengine kuchukua nafasi zilizo baki. Hata ukiangalia watu wenye cheo sasa ni watu wamefahamiana at a personal level na JK muda mrefu.

Swali langu lakini ni je nani alimuandaa JK kuja kuwa raisi? What was the force behind him? Who were the people behind him? Na kama tokea 1995 ilijulikana JK ana nia na uraisi makundi mengine yalishindwaje kudhibiti kundi la JK? Na hii ni nje ya topic kidogo lakini nani alikua mtu wa Mkapa 2005?
Mkuu, si kweli kuwa Kikwete alijiandaa kuwa Rais, ila ni mtu mtu anayependa makuu hodari wa kujipendekeza ili apate kitu au aonekane Mr clean/ Mr Perfect. Kuwa juu ya wengine hata kama has nothing great to deliver.

Kwenye post za miaka ya nyuma waliandika hili alipokuwa chuoni tabia yake ilikuwaje. Angalia trend yake alipokuwa Monduli nini alifanya, nini kilichomwondoa huko kwa aibu. Nini kilimfanya agombane na Mwandosya pale Nishati na madini? Alipokuwa rais wa JMT nini alifanya kwa baraza lake na nini alichofanya kimataifa including AU? What about that move towards MO Ibrahim prize? Connect all those things then you can know what a kind of man is this.

Yes! Up to now his character has not fade.
 
Mkuu haya ya JK pale Monduli si wengi tunayafahamu mimi nikiwa mojawapo. Nitashukuru sana ukiweza kutuelimisha mimi na wengineo. Ahsante
Go for the past post /archived about Kikwete include that, Kikwete in Black and White
 
Binafsi sitausahau mchango Dr AL Mrema kwenye uchaguzi huu. Isingekuwa Wachagga kuuonyesha Uchagga wao kwa Mrema nchi ingekuwa nyingine sasa hivi. Hii CCM isiyosafishika tusingekuwa nayo sasa.
 
Mkuu, si kweli kuwa Kikwete alijiandaa kuwa Rais, ila ni mtu mtu anayependa makuu hodari wa kujipendekeza ili apate kitu au aonekane Mr clean/ Mr Perfect. kuwa kuwa juu ya wengine hata kama has nothing great to deliver. Kwenye post za miaka ya nyuma waliandika hili alipokuwa chuoni tabia yake ilikuwaje. Angalia trend yake alipokuwa Monduli nini alifanya, nini kilichomwondoa huko kwa aibu. Nini kilimfanya agombane na Mwandosya pale Nishati na madini? alipokuwa rais wa JMT nini alifanya kwa baraza lake na nini alichofanya kimataifa including AU? What about that move towards MO Ibrahim prize?Connect all those things then you can know what a kind of man is this. Yes! Up to now his character has not fade.

Mkuu unaweza kutupa kisummary ya vitu alivyo fanya chuo, Monduli, Nishati na Madini, hiyo ya Mo Ibrahim price na baraza lake? Ili kidogo tuone trend?
 
Binafsi sitausahau mchango Dr AL Mrema kwenye uchaguzi huu. Isingekuwa Wachagga kuuonyesha Uchagga wao kwa Mrema nchi ingekuwa nyingine sasa hivi. Hii CCM isiyosafishika tusingekuwa nayo sasa.

Naomba utufafanulie mkuu.
 
Naomba utufafanulie mkuu.
Mrema alikubalika Nchi nzima. Wizara ya Mambo ya Ndani ilikuwa imemjenga sana kwa jinsi alivyokuwa akishughulikia kero za Watanzania. Alifahamika na kukubalika zaidi kwa WATANZANIA kuliko wagombea wote wa CCM na vyama vingine. Wakati wa kampeni ndipo yakajitokeza makundi ya ajabu ya Kichagga yakichangishana fedha kwa wingi na kufanya mikutano yao wenyewe utadhani alitakiwa kuwa Rais wao peke yao.
 
Back
Top Bottom