Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

kinachoendelea leo ni dhambi ya kumnyima uongozi JK nchi isingefika katika hali hii tuliyonayo ss ya watu kujiuzia wao na kusahau ,mamilioni ya wenzao

Mh mkuu kwa hiyo kunyimwa uraisi JK mwaka 1995 kunahalalisha wizi wa sasa unaotokea wakati kapewa uraisi??? SIjakuelewa mkuu.
 
Yeah, inategemea wewe unautazama vipi Udini kwa sababu Malima alichoandika wala sio kusema ni kuonyesha imbalance ktk elimu na jinsi Waislaam na wanawake walivyokuwa hawapewi nafasi sawa na vijanwa kikristu kuendelea na masomo hata kama wanatoka shule moja.. Na kibaya zaidi yeye alikuwa waziri wa Elimu lakini sisi wote tulimpiga vita pamoja na kwamba alikuwa na report kamili yenye ushahidi wa kuonyesha kutokuwepo uuwiano huo...

Sasa nambie kwa nini hatukufanya hata uchunguzi kuitazama report yake badala yake alikuwa akihojiwa tu ili kuonyesha jionsi gani alivyokuwa mdini ktk kutetea report yake ambayo iliwahusu both waislaam na wanawake..Halafu utawasikia watu kama Boss wanasema nakuja na malalamiko hali It is a report for Christ sake na ndio tunaizungumzia na ndio ilikuwa kazi alopewa Malima kuifanya akiwa kama waziri wa elimu.. Sasa kasema hakuna uuwiano na utafiti anao tayari akapachikwa Udini ipi habari kamili ama malalamiko, besides no one could prove him wrong hadi leo hii tunazungumza hapa JF!
Mkuu Mkandara heshma mbele,
Issue ya malima si pia alihusishwa na kile chama cha NRA ambacho kilikuwa cha msimamo mkali cha kiislam?Pia zile habari za kuagizwa kwa majambia kutoka Iran zilikuwa za kweli?Naomba kusahihishwa.
Nakubaliana na utafiti alioufanya,however naamini alikuwa radical.
 
Mwaka 1995,Mrema alikwenda kumtembelea mwalimu.Sikumbuki kama ni butiama ama Msasani.Alikwenda kumwomba ridhaa ya kugombea kupitia NCCR Mageuzi.Alidai anafanya hivyo kwasababu aliamini mwalimu kama baba wa Taifa atakuwa upande wake given the fact kuwa alikuwa akipingana na ufisadi(at least kwa wakati huo)
Mwalimu alimwambia akagombee ubunge.Mrema akabisha,mwishowe mwalimu akamwambia "I cant let my country go to the dogs"
Naomba kusahihishwa.
 
Kama wengine tulivyosema tulikuwa wadogo lakini tumekua na kuyasikia kupitia simulizi na kuona,ukitizama kwa kutumia akili ya kawaida ya uelewa mdogo kuna mambo fulani ya kuona na kutathmini kupitia safari zao JK na EL.

Kwangu mimi binafsi kwa muono wangu na kupitia simulizi hawa mpaka kufikia jamaa kuwa wamoja.Moja nafikili ni msukumo wa rika inasemekana wamesoma wote UDSM mmoja akisoma Uchumi na mmoja akisoma Sanaa na wakiwa wanachama wa Umoja wa Vijana wa TANU.

Kwanye siasa za ujanani kupitia chuo kikuu JK anonekana mapema hata pale kwenye machapisho ya Komredi Jenerali Ulimwengu anapomzungumzia JK katika ujumbe wake wa barua kwa Rais walikutana na kwenye makongamano Nje ya Nchi JK akiwakilisha jumuhiya ya vijana wa chama nafikili TANU kutoka UDSM, JU anamzungumzia JK kama kijana mmoja machachali kwenye mijadala ya maswala ya ukombozi wa Afrika,lakini ambae akusahau stori za kinazi za mpira wa Simba na Yanga za Dar es Salaam.

Kwangu mimi kidogo na kaufahamu ka kifamilia nyumbani yanakuja magazeti yote ya aina mbili kiswahili na kingereza nimesoma kumuona kama naibu waziri,waziri na haswa nikivutwa kumuona kama waziri kijana mwenye muonekano wa kiujana mpaka mavazi.Hii kwa watu wazima wanaweza kujifunza kiongozi yoyote kijana akiwa na muonekano mzuri wa uvaaji na tabasamu lenye mvuto utengeneza kundi kubwa la vijana wadogo wengi wa kike na wakiume pasipo kujali content haswa akiwa makini kwenye mpangilio wa mambo yake basi ukusanya kundi la wafuasi wengi watoto na vijana ambao ndio baadae wapiga kura wake hii ni kweli unaweza kuona kinachoendelea kwa wabunge vijana wa sasa.

Mimi nilimkubali sana JK,japo EL alikuwepo nae kama mbunge na baadae naibu waziri.Ila simulizi zinasema hawa watu ni marafiki toka miaka hiyo.Kwa walio wengi hasa wasomi kuna wakati mnakuwa marafiki japo kihaiba amfanani.Kwa waliofanya SIASA ZA CHUO HILI WANALIJUA. Mnaunganishwa na msukumo wa kikundi zaidi kuleta mageuzi chuoni.

Mfano kwenye chaguzi za vyuo unapofika wakati wa Serikali iliyoko madarakani inamaliza muda wake wale wanachuo wa mwaka wa kwanza,wapili na kidogo baadhi wa mwaka wa Tatu,wanaanza kutengeneza kambi zao za kuanza kuona nani anastahiki na hata wengine kujikuta si wao waliochagua nafsi yao kugombe uongozi bali kambi kikundi ilitumika kuwashawishi kugombea nao kambi kikundi kuwahakikishia ushindi na kuwa itaunda kikosi kazi [Taskforce] na kuharakati na kuratibu mbinu na mikakati kufanikisha kuchaguliwa kwake na kuunda Serikali ya chuo ijayo katika chuo husika.

Vivyo hivyo ukilejea JK na EL,urafiki wao nalazimika kuona kupitia mahusianao yaliyoanzia siasa za Chuo kiuu pale UDSM.Na kama ndio hivyo wanakuwa na ule ule mtizamo ambao lengo linakuwa ni kuleta mabadiliko katika Serikali ya Wanafunzi Chuoni.Siasa za chuo zinasukumwa na rika la kuona matokeo zaidi kuliko uhalisia wa maisha halisi,lakini sio kosa kwa kuwa wengi linakuwa ni swala la umri.Lakini kinachozaliwa ndani ya kambi hizo ni mshikamano pamoja na kuwa mna haiba [Personality] tofauti ila kupitia uchaguzi huo kwa wakati mmoja mmeweza kuungana kutetea aina moja ya uhitaji.Na hakuna kipindi kigumu kama kuwashawishi wasomi kuwa unastahiki kuwa kiongozi wa wao,basi wahusika wa tukio zima la kambi kikundi [taskforce] pindi wafanikiwapo kuunda Serikali ya Wanafunzi hakika huwa ni bonge ya mafanikio na sherehe kwa kuwa wanaamini wamefanikisha jambo kubwa sana [make it happen] kwani wanaamini ukiweza kuwashawishi wasomi basi uraiani ni ubwete tu.

Nilipata kuwa mjumbe na mwenyekiti wa kamati ya kuchuja viongozi wa Chuo [Screening committee] ya viongozi watarajiwa [candidates] kwa kipindi fulani kuna vitu unajifunza ni jinsi gani,tunatayarisha viongozi wa kesho na makusidio na malengo yao nini, wakati mwingine safari tuliyonayo ni ndefu kwelikweli.Kuna walio makini [serious], kunawale ambao hawaeleki wao wanataka nini, na kuna wanaotaka maslahi [privilege] kupitia uongozi huo, wote hawa wanakuwa ndani ya jahazi moja kuunda kambi kikundi kwa kusudio kuunda Serikali ya Wanafunzi.Kwa kuwa aliye makini awezi kuunda Serikali pekee yake kila mmoja anajiunga na mwenzie ila kupata jumuiko la wataka madaraka hayo ya chuo.Wakati mwingine walio makini utumika zaidi kwa kuwa wengine walioko katika kusanyiko hilo wanajua umuhimu wa mtu makini, yaani kwa lugha ya vijana wa sasa wanasema YU KICHWA ama KIFAA.

Hivyo JK na EL,kwa mtizamo wangu watakuwa wameanza kufahamiana na kujijenga kupitia siasa za kujuana kuanzia chuo na ndani yake pia kupitia siasa za umoja wa Vijana wa TANU. Na harakati zote hizo ni kupitia kwenye korido na mabweni ya chuo enzi hizo za kupita chumba hadi chumba saa nane usiku kutoa ushawishi wa maneno na kuuza maneno kwa warembo wa chuo ili kupata support ya kura zao.Ndio ndoto zao zilipoanzia na ndio ndoto hata za Zitto na Riz 1 zilipoanzia chuo kikuu cha UDSM.Ndio maana jamaa anasema "hatukukutana mitaani", hakika kwa sentensi hiyo na ukapimia harakati za siasa za Serikali za Wanafunzi zilivyo hakika hawakukutana mitaani.Manake kwenye kinyanganyiro hicho Serikali za wanafunzi mambo mengi sana ya yanatokea kuhakikisha kikundi fulani kinawazidi kete wengine ili azima yao ya kuchukua madaraka itimie.Tena afadhari sana enzi zao hizo siku hizi mpaka rushwa inafanyika kwenye chaguzi hizo na kuingia kwa siasa za vyama vingi ndani ya Serikali za Wanafunzi.

Baada ya chuo kila mmoja hakika uwa anachukua mwelekeo wake lakini sio kuwa mawasiliano yanakwisha bali ndio mwanzo wa kitabu halisia cha maisha.JK inasemekana yeye alienda kwenye chama [Hapa ndio uwa naona kidogo katika uongozi huyu alijua anafanya nini].Lakini mwenzie nafikilia alikamata ajira Serikalini ukiziangatia wakati huo ajira ni kedekede.

Kuna wengine wanasema walikuwa jeshini wote wakiwa katika mkakati wa siasa jeshini sijui kama ni intake moja au la,ila naambiwa watu kama Mzee Makamba,Jaka Mwambi na JK ni watu ambao inathibitika walikuwa pamoja jeshini, ila sijapata kusikia kwa hakika EL naye alikuwemo,ingawa nimeona kutajwa na baadhi ya magazeti.Ilo sijui wengiine watusaidia kusasahisha.

Jeshin nako kambi ikatengenezwa tena lakini sasa huku ikawa kisiasa na mshikamano wa mfumo halisi [system].Wadau hawa wanafahamiana kila mmoja yukoje lakini kwa kuwa mmoja uwa na umakini kuliko mwenzie na mwingine anajua fulani uwa anakubalika basi anajua atatumia HAIBA yake kama walikotoka kufikia dhamila yake ambayo anaijua mwenyewe.Mwingine naye anafikilia anauwezo anajua uwezo wa mwenzie katika kusimamia na kuratibu mikakati na mwenendo mzima wa nani awe wapi kuleta ushindi hivyo atamtumia kufika anakwokwenda lakini akisahau kuwa kuna wanajamii ambao nao ni binadamu wenye utashi na ufahamu kujua yupi ni yupi wanachuja ili kupata kitu halisi wanachotaka.

Walitumiana mpaka kwenye uchaguzi kwa kuwa mteule anajulikana JK akawa Rais,nasikia wakuu wengine walimsii asimchukue EL lakini kwa kuwa na historia isiyokubalika ukizaingatia maneno ya Mwalimu. Lakini JK akasimamia historia waliko toka, EL akawa Waziri Mkuu,na kwa kuwa dhamila yake inamchanganyiko wa mambo mengi basi yakamkuta ya kumkuta akaitimisha kwa kusema tatizo ni uwaziri mkuu there is a wish am going to grant.

Hakika huu ni mtizamo wangu na simulizi.
 
Kilichojitokeza ni kwamba wale wafuasi wa Msuya walimwunga mkono Che Nkapa na wale Wazenj walikuwa wamepewa maelekezo na Komandoo Salimin (alikuwa bado anakipindi kimoja cha kukaa madarakani) kwamba wasithubutu kumchagua "Play Boy - Kikwete". Kwa hiyo hata Komandoo hakutaka kuwa chini ya Kikwete
wenzako wanapost point wewe unapost pumba. Toa kinyesi chako hapa.
 
Ninachokumbuka Uchaguzi wa 1995
1.Toka ndani ya CCM, Umoja wa Vijana wa CCM Ulimuunga mkono waziwazi mmoja wa wagombea, na kusema kuwa anafaa kuwa Rais Mwenyekiti wa UVCCM Wakati huo John John Guninita alilalamikiwa sana na Che Nkapa, wakati anachukua form akasema kuwa pamoja na kwamba UVCCM Haikumtaja lakini yeye anafaa kuwa Rais.

2.Kwenye Uteuzi wa Mgombea toka CCM Katika raundi ya mwisho yalibaki majina matatu, ambapo Kura zilipopigwa JK akawa mshindi wa raundi ya kwanza, lakini Warioba akanukuu kwenye katiba ya Chama kwamba mshindi lazima apate zaidi ya 50% ya kura zote.Debate ikawa katika watu watatu nusu ni ngapi? Jawabu likawa kurudia kura kwa washindi wawili wa mwanzo ambapo JK na BWM Wakapambanishwa, Komandoo na wagombea wa zenji wakaja na uzushi kuwa kundi la JK Limeandaa mkesha wa Bia kwa ajili ya kusherekea ushindi wa Mgombea wao, Inasemekana kuwa wale wazee wa Zenji wakalaani wanywa pombe na kukataa kumpigia mgombea wao, Hivyo kura za CDM zikaenda kwa BWM. Na akawa Presidaa.

3.JKN akihutubia Morogoro aliwaambia wananchi wamchague Mkapa, Maana Huku Makongoro Nyerere na NCCR kulke Julius na CCM yake, Alisema, nanukuu "Huyu Makongoro ni Mwanagu huyu ni muhuni huyu, Nilimuuliza umeacha lini uhuni akasema Babaaa nimeachaaaa, Ni muhuni huyu na wenzie",Akimaanisha NCCR Mageuzi, My take bila Kampeni kubwa ya JKN, NCCR ilikuwa tishio.

4.Kwenye mdahalo wa Wagombea Bwana Mapesa alikuja na Slogan ya kuwajaza manoti Watanzania.
 
Nashukuru sana wakuu. Baadhi ya post inanipa somo kweli na nashukuru nimeanzisha hii thread maana kuna mengi nilikua siya fahamu ila sasa hivi nimefumbuliwa macho.
 
Je Benjamin Mkapa alipo shinda uraisi alimpa JK kama compromise ili wafuasi wa JK wasikatae kuisaidia CCM wakati wa kampeni? Kwa maana naamini JK kupewa uwaziri na Mkapa haikuwa bahati mbaya.
 
Wakuu JMushi1 na Ngwendu....potezea jamani mjadala uendelee.
samahani wakuu sio lengo langu ila kuna watu wengine wanaleta michango isio na maana. unajikuta unafuata mtiririko halafu mtu anapost pumba btn, inaudhi sana. Ila all in all nimejua mengi sana ambayo nilikuwa siyajui. Unajua kwenye thread kama hii tunahitaji fact na mtu mwenye data za uhakika na sio kuweka mawazo ya kile mtu anachojisikia tu.Thanks for your constructive thread.
 
Je Benjamin Mkapa alipo shinda uraisi alimpa JK kama compromise ili wafuasi wa JK wasikatae kuisaidia CCM wakati wa kampeni? Kwa maana naamini JK kupewa uwaziri na Mkapa haikuwa bahati mbaya.

Sure ndio alimpa kamacompromise wakati mwingine ni vyema kukubali huwa kuna makosa ya kibinadamu na kuwa daima wanasema ukitaka kumjua binadamu mpe pesa.Lakini wakati mwingine ukivishwa viatu vya JK kuona unajua kabisa hiki kiti kilikua changu kisha kinakuponyoka basi yataka moyo.Kwa hilo JK anastahiki hongera hivyo kwa kuingia kusubilia miaka kumi [10].

Wanasema alimuweke Nje kwa sababu za kumweka sawa,hapa kuna aina mbili ushindwe kujipanga au ndio ujipange vyema,kwa kuwa kuna watu wamekuwa huko kwenye diplomasia wameshindwa kujipanga.Hivyo mdau huyu kukaa uko alikutumia vizuri vizuri japohuku nyumbani chini ya mratibishaji wake mambo yaliendelea sawa.

Lakini nasikitika kuwa wanafika hapo juu wanabadilika manake wakati BWM anaingia madarakani alikua maalufu na safi akiwa na jina la MR CLEAN lakini kaondoka akiwa hakumbuki ilo jina kaliacha wapi.Jk nae wanasema hata Mwalimu alikua anamtumia kwenye maswala muhimu ndio maana hata uchaguzi wa 1995 wasimulizi walisema Mwalimu kasema huyu bado mdogo [Unexperinded],hivyo ni hakika misemo inayosemwa kuwa hata ushiriki wake kwenye mchakato hu ni kuwa Mwalimu alimwambia achukue form yaweza kuwa kweli.

Ila nampa pole kwani unapokuwa na kaka yako ukitegemea akuongoze kisha ukute anafanya madudu nyie wadogo nao mtaangukia kutenda yale yale ya brother.Nahakika hata HAIBA ya JK kwa haya yote yaliyojili ya RICHMOND,DOWANS na mengineyo ni urithi wa kuona walionitangulia wako hivi why not me.
 
Mkandara,The Boss,Jasusi na Joka Kuu,
Inaonekana mna kumbukumbu nzuri sana ya uchaguzi wa 1995.Nakumbuka kwa mbali kuhusiana na issue ya NRA na Malima.Is there anyhting you guys remember on that issue?Pamoja na issue nyingine za Iran,pamoja na ile ya kudai Mzee Malecela kubadili dini na kuwa sasa jina lake ni jumanne nk.
Je haya yalikuwa propaganda za magazeti na kupakana matope ama kuna ukweli ndani yake?
Natanguliza shukrani.
Angalizo:Kwa ambaye hajapenda maswali yangu na ikiwa sijayaelekeza kwake,basi naomba apotezee ama aniweke kwenye ignore list yake badala ya kuharibu thread kwa maneno machafu.
 
Asante kwa kunisahihisha mkuu.
Mkuu heshima kwako, sikuwa na maana ya kukusahihisha ila nilikuwa naongezea maarifa kama si kukumbushana baadhi ya mambo. Naheshimu mawazo yako na kusudio lako la kutaka tujikumbushe ni nini kilichochijiri wakati ule ili tuwe na la kujifunza kama si kuwafundisha watoto na vijukuu vyetu vitakavyozaliwa Tanzania kama si Tanganyika (ikiwa vita ya kuirudisha itashinda).
 
Je Benjamin Mkapa alipo shinda uraisi alimpa JK kama compromise ili wafuasi wa JK wasikatae kuisaidia CCM wakati wa kampeni? Kwa maana naamini JK kupewa uwaziri na Mkapa haikuwa bahati mbaya.

Mkapa aliposhinda alimpa JK waziri ya wa nje sio kwa kupenda bali kwa maelekezo tena inawezekana ni ya mwalimu. Inawezekana yeye angempa wizara kama ya Kilimo. Unajua kuna wazara nyingine Tanzania japo ni za muhimu lakini inaonekana kama ni kukomolewa. Si unajua nchi yetu haina dira. Tuna sera ya kilimo kwanza lakini MOFA ni wizara kubwa kiprotocol kiliko ya wizara kilimo. Anyway nisiende huko ......

Ni inasemakana MKapa aliagizwa na Mwalimu kuwa kwa wakati huo anaona akimaliza mkapa atayefuata ni JK. Na katika maelekezo hayo inasemekana shahidi aliyekuweopo ni Mkapa, Nyerere na Kingunge. Ni kwa sabau ya maagiz hayo Mkapa alilazimika kumuweka JK wizara ya mambo ya nje. hayakuwa mapenzi yake........

Kuna wakati Mkapa alitaka kumtosa JK sababu aliona ameshikamana na watu ambao kwa mtazamo wake kama nyerere angekuwepo basi angemtosa lakini kingunge ndiye alikaa kidete kumumbusha maelekezo waliyopewa na mwalimu. Na ndio Maana JK anamuheshimu sana Kingune ........

Lakini nadhani wasi wasi wa Mkapa nao umedhihirika kuwa una hoja sababu matatizo ya ushkaji wa JK na Lowasa.

Lakini hayo yote niliyooleza ni Inasemekana
 
Nami nichangie kidogo. Mwaka huo pia alikuwepo mwana mama aliyechukua fomu, naye alikuwa ni Bi. Rose Lugendo. Ila alipata wakati mgumu alipoingia kwa usaili mbele ya Nyerere.

Kama alivyosema Mkandala, Nyerere alimuomba Dk. Salim aje agombee, wakati huo Salim alikuwa Katibu Mkuu wa OAU. Salim alikubali na kuja Tanzania. Lakini jungu lilianzishwa na Mama Getrude Mongella kuwa nchi hii haiwezi kutawaliwa na Mwarabu. Na hili alilizungumza mpaka kwa Nyerere, akiungana na baadhi ya watu mashuhuri wa CCM toka Bara na waliowengi toka Visiwani. Salim ikabidi asichukue fomu na kurudi Addis Ababa.

Kuhusu Malima, alipoenguliwa CCM alihamia NRA (National Reconstructive Alliance), habari za kujitoa CCM zilisikika kwa Nyerere. Aliitwa na Nyerere na aliombwa kuwa kujitoa kwake CCM kunaweza kukitingisha chama (kumbuka alikuwa nguzo muhimu wakati wa kupigania uhuru). Alikataa na akapanga kujitoa CCM akiwa Tabora, alikata tiketi ya ATC, na alipofika Airport, akaambiwa ndege imejaa, ikabidi asafiri na gari lake hadi Tabora. Akajitoa CCM na kujiunga na NRA, na kubadilisha kifupi cha jina la chama toka NRA kuwa NAREA. Alifariki katika mzingira ya kutatanisha London kabla ya uchaguzi.
 
...........
4.Kwenye mdahalo wa Wagombea Bwana Mapesa alikuja na Slogan ya kuwajaza manoti Watanzania.

Katika wafanyabiahsaa waliokuwa wanamsuport huyu bwana Mapesa ni jamaa mmoja anaitwa Kishimba wa Kanda ya ziwa . Baada ya uchaguzi kuisha TRA walimjia na mahesabu ya kodi zote alizokwepa miaka kadhaa ya nyuma kwa bidhaa alizokuwa akitoa kenya. Jamaa aliteteraka kiasi nadhani toka kipindi hicho akaachana kabisa kukaa karibu na wanasiasa wa upinzani.

Kodi hizo kweli alikuwa anakwepa na alikuwa anawahonga hao hao TRA lakini nadhani ni adhabu alipewa na serikali kwa kumuunga mkono bwana mapesa.

Ndio maana mimi nikiwaona wafanyabiashara walio upinzani nawashimu sana.
 
Nami nichangie kidogo. Mwaka huo pia alikuwepo mwana mama aliyechukua fomu, naye alikuwa ni Bi. Rose Lugendo. Ila alipata wakati mgumu alipoingia kwa usaili mbele ya Nyerere.

Kama alivyosema Mkandala, Nyerere alimuomba Dk. Salim aje agombee, wakati huo Salim alikuwa Katibu Mkuu wa OAU. Salim alikubali na kuja Tanzania. Lakini jungu lilianzishwa na Mama Getrude Mongella kuwa nchi hii haiwezi kutawaliwa na Mwarabu. Na hili alilizungumza mpaka kwa Nyerere, akiungana na baadhi ya watu mashuhuri wa CCM toka Bara na waliowengi toka Visiwani. Salim ikabidi asichukue fomu na kurudi Addis Ababa.

Kuhusu Malima, alipoenguliwa CCM alihamia NRA (National Reconstructive Alliance), habari za kujitoa CCM zilisikika kwa Nyerere. Aliitwa na Nyerere na aliombwa kuwa kujitoa kwake CCM kunaweza kukitingisha chama (kumbuka alikuwa nguzo muhimu wakati wa kupigania uhuru). Alikataa na akapanga kujitoa CCM akiwa Tabora, alikata tiketi ya ATC, na alipofika Airport, akaambiwa ndege imejaa, ikabidi asafiri na gari lake hadi Tabora. Akajitoa CCM na kujiunga na NRA, na kubadilisha kifupi cha jina la chama toka NRA kuwa NAREA. Alifariki katika mzingira ya kutatanisha London kabla ya uchaguzi.
Mfumwa,shukrani sana.

Kwenye bold, umejibu swali langu, nashukuru.
 
Mkuu Mkandara heshma mbele,
Issue ya malima si pia alihusishwa na kile chama cha NRA ambacho kilikuwa cha msimamo mkali cha kiislam?Pia zile habari za kuagizwa kwa majambia kutoka Iran zilikuwa za kweli?Naomba kusahihishwa.
Nakubaliana na utafiti alioufanya,however naamini alikuwa radical.
Mkuu umesema Malima alihusishwa na NRA chama chenye msimamo mkali cha kiislaam. Hivi kweli unaweza kunipa mahusiano ya NRA na Uislaam? na vitu gani walivyokuwa wakipigania (sera na Ilani) na kadhalika. Binafsi nimeyasikia sana haya madai na ningependa sana kupewa historia ama picha nzima ya chama cha NRA, uongozi wake sera za na mwisho uhusiano baina ya Malima na hicho chama cha kidini...Na labda mtu anipe investigative report inayoonyesha Kighoma Malima alikuwa both Muislaam mwenye siasa kali pia aliharibu wizara ya elimu na fedha..

Mkuu wangu hivi huoni kama kila kitu kinajirudia rudia - dejavu..
Dr.Slaa hadi kufikia mwaka 2009 alikuwa hero wa kila mtu, Sii waislaam wala wakristu lakini siku aloonesha nia yake ya kugombea Urais ndipo Upadre wake ulipotangazwa na nia mbaya ya Chadema katika kuupiga vita Uislaam simply 'because JK ni Muislaam.. Sasa habari kama hizi zitakwenda hadi kwa vijana watoto zenu ambao watakuja hadithia jinsi Dr.Slaa alivyokuwa mdini pamoja na kwamba hakuna hata siku moja amezungumzia Uislaam na Ukristu ila kosa lake ni kuikosoa serikali ya CCM..Malima pia alikuwa one of the best of ministers hadi siku alipozungumzia hali ya elimu nchini kukikosoa chama tawala.
Na mchezo huu umechezwa kwa viongozi woote walijaribu kukikosoa chama tawala toka Malecela ambaye alizushiwa hadi kuhama dini kuingia Uislaam na ati anaitwa Jumanne.. kila alojaribu kukisaliti chama au kuweka upinzani mkubwa na chama tawala Udini ulitumika kumdhoofisha...

Na lazima mkuu wangutukubali kwamba marais huandaliwa, hizi habari za kufikiria kwamba mtu unaweza tu kuibuka mshindi na kuwa rais wa nchi kwa kupitia demokrasia ni kuzidanganya nafsi zetu. Na wote hawa toka kina Kolimba, Malima, Mwaikambo na wengineo wameondolewa kwa sababu they knew too much of the system na siku walipojaribu kuhama ndio walijichimbia kaburi lao.. Na nitasema tena hakuna mtu anaweza kushika madaraka ya Urais kama hayupo ktk system. Viongozi huandaliwa na mara zote lazima kuna mahusiano mkubwa na vyombo vya usalama. Nani huwaandaa kwa tanzania kusema kweli sijui ila nafahamu kwamba lazima rais aandaliwe na akubalike na system.

Nitaendelea kusema tu kwamba, habari zoote zinazohusiana na udini ni habari ya kutunga ili kuogopesha wananchi. Tanzania hatuna hofu ya Ukabila na hakuna dalili za machafuko ya kijamii isipokuwa kwa kupitia DINI..Hapa ndipo pekee siasa za majitaka zinaweza kupata nguvu ya kuwajaza hofu (fear) wananchi..Nothing scares us most kama vita, na hakuna sababu nyingine tunayohofia zaidi ya Udini. Na CCM are masters wa kupandikiza mbegu za Udini kwa sababu haiwezekani NRA wakawa waislaam wenye siasa kali, CUF ni chama cha waislaam halafu Chadema leo ndio chama cha Wakristu - What a coincidence!
 
Mkandara, The Boss, Jasusi na Joka Kuu,Inaonekana mna kumbukumbu nzuri sana ya uchaguzi wa 1995. Nakumbuka kwa mbali kuhusiana na issue ya NRA na Malima. Is there anyhting you guys remember on that issue? Pamoja na issue nyingine za Iran,pamoja na ile ya kudai Mzee Malecela kubadili dini na kuwa sasa jina lake ni jumanne nk.Je haya yalikuwa propaganda za magazeti na kupakana matope ama kuna ukweli ndani yake?Natanguliza shukrani.Angalizo:Kwa ambaye hajapenda maswali yangu na ikiwa sijayaelekeza kwake,basi naomba apotezee ama aniweke kwenye ignore list yake badala ya kuharibu thread kwa maneno machafu.
Kwenye nyekundu kuna uzi mmoja ulikuwa ukiendelea wiki kadha zilizopita waweza tafuta ukapata ilikuwa kuwaje na kwanini ilivuma maramoja kisha baadaye kupotezewa kwa Mzee JSM kuitwa Jumanne.

Kwenye bluu, wako wanaosema Kighoma Ali Malima, alikuwa na back-up ya kundi fulani la waislamu ambao walitaka rais atakayefuata baada ya Mzee Mwinyi awe muislamu. Huyu jamaa alikuwa ni mdini kwelikweli. Anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakishadidia kichini-chini suala la Zanzibar kujiunga na OIC. Baada ya Kibona kama Waziri wa fedha kufariki, yeye ndiye aliyepewa nafasi hiyo.

Akiwa madarakani akaanaza kukomba pesa kidogo-kidogo lakini kikubwa akawa anaficha ughaibuni. Strategically, kwamba atazitumia kwa kampeni. Alipokosa nafasi CCM akachomokea NRA. Akazikumbuka ngawila zake ughaibuni. Alipokwenda zifuata, the perfect thing was done, account ikawa imefungwa na Serikali ya Tanzania. Jamaaa akapata mfadhaiko/mshituko basi akafa. Miongoni mwa waliom-support ni Kitwana Kondo nao wakakumbwa na mfadhaiko, lakini hakufa aliendelea kuishi.

Ni kwa uchache wa kile nachoweza kumbuka na kuandika, wapo wenye mengi ya kueleza. I stand to be corrected.
 
Alifariki katika mzingira ya kutatanisha London kabla ya uchaguzi.

Haya mazingira ni mshtuko. kwamba Alienda london kuchukua mshiko wa kuja kujenga chama chake kipya. Na huko alikuwa na mkewe mpya aliyemtumia ndugu yake amuoe kwa niaba yake jijini mwanza.

Baada ya kuwa london na my wife wake mpya alipata mshtuko kwa kushindwa kutoa mapesa yake kwenye account sababu yalikuwa blocked. sababu chanzo chake zilionekana nyingi zimetoka kwenye extrimist group. So ombi la tanzania kuziblock lilikubalika kirahisi.

Basi wale wenye imani za upande mwingine wanasema kifo chake kina mkono wa bi mkubwa....

We fikiria unaeda london unajua una mamia ya mamilioni kadhaaa . unataka kuchomoa unaambiwa huweziiiii.....
 
Mkuu umesema Malima alihusishwa na NRA chama chenye msimamo mkali cha kiislaam. Hivi kweli unaweza kunipa mahusiano ya NRA na Uislaam? na vitu gani walivyokuwa wakipigania (sera na Ilani) na kadhalika. Binafsi nimeyasikia sana haya madai na ningependa sana kupewa historia ama picha nzima ya chama cha NRA, uongozi wake sera za na mwisho uhusiano baina ya Malima na hicho chama cha kidini...Na labda mtu anipe investigative report inayoonyesha Kighoma Malima alikuwa both Muislaam mwenye siasa kali pia aliharibu wizara ya elimu na fedha..

Mkuu wangu hivi huoni kama kila kitu kinajirudia rudia - dejavu..
Dr.Slaa hadi kufikia mwaka 2009 alikuwa hero wa kila mtu, Sii waislaam wala wakristu lakini siku aloonesha nia yake ya kugombea Urais ndipo Upadre wake ulipotangazwa na nia mbaya ya Chadema katika kuupiga vita Uislaam simply 'because JK ni Muislaam.. Sasa habari kama hizi zitakwenda hadi kwa vijana watoto zenu ambao watakuja hadithia jinsi Dr.Slaa alivyokuwa mdini pamoja na kwamba hakuna hata siku moja amezungumzia Uislaam na Ukristu ila kosa lake ni kuikosoa serikali ya CCM..Malima pia alikuwa one of the best of ministers hadi siku alipozungumzia hali ya elimu nchini kukikosoa chama tawala.
Na mchezo huu umechezwa kwa viongozi woote walijaribu kukikosoa chama tawala toka Malecela ambaye alizushiwa hadi kuhama dini kuingia Uislaam na ati anaitwa Jumanne.. kila alojaribu kukisaliti chama au kuweka upinzani mkubwa na chama tawala Udini ulitumika kumdhoofisha...

Na lazima mkuu wangutukubali kwamba marais huandaliwa, hizi habari za kufikiria kwamba mtu unaweza tu kuibuka mshindi na kuwa rais wa nchi kwa kupitia demokrasia ni kuzidanganya nafsi zetu. Na wote hawa toka kina Kolimba, Malima, Mwaikambo na wengineo wameondolewa kwa sababu they knew too much of the system na siku walipojaribu kuhama ndio walijichimbia kaburi lao.. Na nitasema tena hakuna mtu anaweza kushika madaraka ya Urais kama hayupo ktk system. Viongozi huandaliwa na mara zote lazima kuna mahusiano mkubwa na vyombo vya usalama. Nani huwaandaa kwa tanzania kusema kweli sijui ila nafahamu kwamba lazima rais aandaliwe na akubalike na system.

Nitaendelea kusema tu kwamba, habari zoote zinazohusiana na udini ni habari ya kutunga ili kuogopesha wananchi. Tanzania hatuna hofu ya Ukabila na hakuna dalili za machafuko ya kijamii isipokuwa kwa kupitia DINI..Hapa ndipo pekee siasa za majitaka zinaweza kupata nguvu ya kuwajaza hofu (fear) wananchi..Nothing scares us most kama vita, na hakuna sababu nyingine tunayohofia zaidi ya Udini. Na CCM are masters wa kupandikiza mbegu za Udini kwa sababu haiwezekani NRA wakawa waislaam wenye siasa kali, CUF ni chama cha waislaam halafu Chadema leo ndio chama cha Wakristu - What a coincidence!

Mkuu, kama what you are insinuating(in red) holds true then the next president of URT is MIZENGO KAYANZA PETER PINDA.
 
Back
Top Bottom