Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

Discussion in 'Great Thinkers' started by MwanaFalsafa1, Aug 7, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuna wengine wetu tulikua wadogo mwaka 1995 kuweza kufuatilia kinyanganyiro cha uraisi mwaka huo. Ndiyo maana ningependa kujua zaidi nini kilicho jiri ndani ya CCM mpaka kupelekea kumteua raisi mstaafu Benjamin WIilliam Mkapa kuwa mgombea wa CCM kwa mwaka huo.

  Machache ninayo jua ni kwamba final three ya CCM ilikua Kikwete, Mkapa na Msuya. Nasikia Kikwete alishinda round ya kwanza ila hakupata zile asilimia 51 zinazo hitajika kupata ushindi wa moja kwa moja. Round ya pili ikawa yeye na Mkapa na Nyerere kwa kutumia ushawishi wake ndani ya chama aka hakikisha ushindi unaenda kwa Mkapa.

  Kwa nijuavyo mimi (naweza kusahihishwa) ni kwamba Nyerere hakudhani Kikwete kakomaa kiuongozi kuweza kuwa raisi mpaka akadiriki kusema "hatuendi kutoa posa tunaenda kuchagua raisi. Kama mtu anampenda mtu kwa sababu ya sura akanywe nae chai."

  Sasa kwa wanaokumbuka zaidi (najua wapo wengi) naomba mnisaidie kunipa somo la historia hapa ya nchi yetu kwa sababu kinyanganyiro cha 1995 ndicho kilicho toa raisi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  maneno hayo aliyasema kumzungumzia lowwasa
  lowassa jina lake lilikatwa na nec,
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nyerere aliijua tabia mbovu ya Kikwete na kwamba hafai kuwa rais. Pia wakiwa hapo Dod6a alijulishwa namna ambavyo Lowasa alihamishia majeshi kumsupport Kikwete. Ni baada ya Lowasa kupigwa nyundo na JK wa ukweli (yaani Mwalimu).
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Asante kwa kunisahihisha mkuu.
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,598
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka baadhi ya mambo licha ya kwamba nilikuwa bwana mdogo.Gari ya Mrema nilisukuma.Wengi tuliamini angeingia ikulu kama si mwalimu.Mwalimu angemchagua JK maybe ingekuwa bora zaidi kwasababu angekuwa chini ya uangalizi wake.Mkapa ni mnafiki mkubwa,mwalimu alifanya kosa hapo.Kama alikjuwa kin EL wanamipesa,basi angemshurutisha Mkapa awawajibishe.Ama angetilia msisitizo kuwa wawajibishwe na si kuwanyima nafasi za kisiasa.Sasa alipotutoka tunaona tatizo bado lipo,na this time mafisadi ndo wenye nguvu because mwalimu was an one army man.
  Ntarudi.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kikwete alifika top three by accident mno

  Ilipofika 1995 idadi kubwa ya waliojitokeza kugombea kwa CCM walikuwa wakristo na kulikuwa na uvumi kuwa CCM wana utaratibu wa kubadilishana kwamba amemaliza mwinyi Muislam, anaekuja atakuwa mkristo.

  Nyerere alisikia hiyo habari akaikemea mno,akasema rais hata akiwa muislam tena na tena na tena ili mradi anafaa

  But waislam wa CCM wengi hawakuchukua fomu za urais. Siku ya mwisho ya kuchukua fomu, ikawa muislam ni mmoja tu Kighoma Malima na kwa kuwa Malima alikuwa na kashfa za kodi asingefika mbali..

  So Nyerere alienda kumwambia Kikwete achukue fomu za uraisi ili chama kisionekane kimewatenga waislam au kuna mfumo wa kubadilisha uongozi kidini...

  So Kikwete kwa kuwa muislam pekee, akaachiwa jina lake mpaka top three ingawa wote walikuwa wanajua hatapewa urais....na kuna taarifa kuwa alishinda kura mara ya pili pia... sababu kubwa alionekana ni too inexperienced
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa kama form two hivi na nakumbuka nilifatilia kwa makini walipobaki watatu wa mwisho...kama sikosei mshindi alitangazwa usiku ambaye alikuwa Mkapa.

  Duh ccm niliichukia tokea zamani, nakumbuka nilikuwa sijafikisha miaka kumi na nane lakini nilifoji hadi nikampigia kura Mrema.... i should have known... Mrema godamit...traitor
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nini kilipelekea EL kuhamishia majeshi kwa JK?
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280

  Kaka umejuaje yote hayo? Au ulishiriki kwenye mchakato mzima?
   
 10. majata

  majata JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Dogo kulikuwa na mtu alikuwa anaitwa Tuntemeke sanga huyu aliishia kwenye 5bora lakn huyu alikuwa na uwezo mkubwa kwani alikuwa anafanya maamuzi mazuri hata akiwa bungeni, lakini alikuwa haivi na nyerere hivyo akatoswa.
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nini kilipelekea Kikwete achukue form akijua fika hatoshinda? What incentive did he have? Aliahidiwa nini?
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Je unaweza kuniambia alikuwa anafanya nini kabla ya kugombea urais? Yani alishawahi kushika nyadhifa zipi. Na baada ya kushindwa uraisi akaishia wapi?
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sikusema alijua hatashinda
  nilichosema ni kuwa ilionekana hivyo
  kwa kuwa alikuwa very inexperienced na alichukua fomu kwa kuambiwa na nyerere
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Oh ok samahani ni mimi ambae sikuelewa vizuri mkuu.
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  nina ndugu ni ccm insiders
  hata la kikwete kuhamia chadema 2005 ni la ukweli na mbowe alipewa bilioni tatu za kuandaa mazingira
  but leo ukilisema hilo utaoonekana unazusha
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mh mkuu can you tell as more about this? JK alipanga kuhamia kama akishindwa au?
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  huo ulikuwa mpango wa wanamtandao
  haijulikani kama angekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo
  mostly walimhofia mkapa kuweka mtu wake,
  but walifanikiwa kum neutralize mkapa
  na ndo maana jk hawezi kuruhusu mkapa ashitakiwe
  mkapa alikuwa na nguvu ya kumzuia asiwe rais,but alimuachia
  ingawa kwa shingo upande
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh ama kweli Faizal ana kila haki ya kuwashangaa watu.. Hivi kweli mtu unafikia kusema ati waislaam walikuwa hawakujiandikisha hivyo ndio JK akaingia? Je, kweli watu mnasahau kwamba Salim A Salim ndiye alikuwa chaguo la mwalimu na candidate ambaye Watanzania wote walimtegemea!.. na kaja kukataliwa na Wazanzibar kwa sababu ya chuki ya kisiasa baina ya ASP na Umma Party! wakamzulia kuwa ktk mipango ya kumuua Karume kesi ikarudi upya..Na hata habari za Kighoma Malima inaonyesha watu hamna kubmukumbu wala ukweli wa kilichotokea zaidi ya hizi hadithi za zimulizi..Kighoma Malima, na watu kibao wamekolimbwa kwa sababu ya kutaka au kukihama chama....
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mkandara unachanganya madawa hapa
  sali alizushiwa hayo mambo kwa uchaguzi wa 2005
  muanzisha mada anazungumzia uchaguzi wa 1995
  na uchaguzi huo salim hakuwepo kabisa katika wagombea,alisema bado ana majukumu oau
  ni kweli mwalimu alimtaka achukue fomu,but hakuchukua
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuhusu kigoma malima
  hebu tazama kumbukumbu zako vizuri
  alichukua fomu za kugombea urais ccm
  alipotemwa akaenda kujiunga na nra na kuibadilisha kuwa narea
   
Loading...