Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

Kwenye nyekundu kuna uzi mmoja ulikuwa ukiendelea wiki kadha zilizopita waweza tafuta ukapata ilikuwa kuwaje na kwanini ilivuma maramoja kisha baadaye kupotezewa kwa Mzee JSM kuitwa Jumanne.

Kwenye bluu, wako wanaosema Kighoma Ali Malima, alikuwa na back-up ya kundi fulani la waislamu ambao walitaka rais atakayefuata baada ya Mzee Mwinyi awe muislamu. Huyu jamaa alikuwa ni mdini kwelikweli. Anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakishadidia kichini-chini suala la Zanzibar kujiunga na OIC. Baada ya Kibona kama Waziri wa fedha kufariki, yeye ndiye aliyepewa nafasi hiyo.

Akiwa madarakani akaanaza kukomba pesa kidogo-kidogo lakini kikubwa akawa anaficha ughaibuni. Strategically, kwamba atazitumia kwa kampeni. Alipokosa nafasi CCM akachomokea NRA. Akazikumbuka ngawila zake ughaibuni. Alipokwenda zifuata, the perfect thing was done, account ikawa imefungwa na Serikali ya Tanzania. Jamaaa akapata mfadhaiko/mshituko basi akafa. Miongoni mwa waliom-support ni Kitwana Kondo nao wakakumbwa na mfadhaiko, lakini hakufa aliendelea kuishi.

Ni kwa uchache wa kile nachoweza kumbuka na kuandika, wapo wenye mengi ya kueleza. I stand to be corrected.
Mkuu hizi ni hadithi za kusadikika... Huna ushahidi zaidi ya simulizi.. unaposema Kighoma Malima alikuwa akikomba fedha kwani Hazina kuna cash money gani ambayo ilimfanya asikombe wizara ya Elimu..Na tuache hivyo kuna waziri gani ambaye alikuwa hakombi (kufisadi) wakati wa Mwinyi? Wameiba woote lakini aliyeonekana ni Malima tu - muislaam mwenye siasa kali!

Je unakumbuka kwamba hata Lowassa alikuwepo na aliziiba waziwazi mbona hatukusikia yeye kuondolewa nafasi ya uongozi!

Na samahani ni watu kama wewe ndio mimi nawazungumza.. Kila kitu udini udini wakati hukuwa karibu na Malima na kibaya zaidi upo dini nyingine tofauti na Malima hivyo huwezi kuwa na info za ndani isipokuwa unasukumwa na hofu.. Na kuna ubaya gani leo hii mimi nikiunga mkono OIC! ndio inanifanya mimi kuwa extremist?.
 
juu ya kikwete Nyerere alsema hivi :'' mimi sio kuku sitagi mayai lakini ukinipa yai bovu nitalitambua'' kisha akaongeza tena kikwete hujakomaa bado na kura zako hazijatosha.....
 
........Na tuache hivyo kuna waziri gani ambaye alikuwa hakombi (kufisadi) wakati wa Mwinyi? Wameiba woote lakini aliyeonekana ni Malima tu - muislaam mwenye siasa kali! .............

Tatizo sio malima kuwa muislam wa siasa kali au za wastani au baridi , Tatizo ni kwamba alichomoka CCM. Hata Chenge Leo Hii akisema aondoke CCM aingie UDP vile vijisenti vyake vitapigwa stop then itatafutwa sababu za kweli na uwongo........ Tusiende huko lakini silaha kubwa iliyotumika kummaliza na kuzuia account yake nje ndio hiyo.. wether sababu zilikuwa ni kweli au sio ndivyo system zinavyofanya kazi.

Kama unavysema wengi wameiba na wamepona . Wamepona sabbau hawajaasi chama.........
 
Kikwete alifika top three by accident mno

Ilipofika 1995 idadi kubwa ya waliojitokeza kugombea kwa CCM walikuwa wakristo na kulikuwa na uvumi kuwa CCM wana utaratibu wa kubadilishana kwamba amemaliza mwinyi Muislam, anaekuja atakuwa mkristo.

Nyerere alisikia hiyo habari akaikemea mno,akasema rais hata akiwa muislam tena na tena na tena ili mradi anafaa

But waislam wa CCM wengi hawakuchukua fomu za urais. Siku ya mwisho ya kuchukua fomu, ikawa muislam ni mmoja tu Kighoma Malima na kwa kuwa Malima alikuwa na kashfa za kodi asingefika mbali..

So Nyerere alienda kumwambia Kikwete achukue fomu za uraisi ili chama kisionekane kimewatenga waislam au kuna mfumo wa kubadilisha uongozi kidini...

So Kikwete kwa kuwa muislam pekee, akaachiwa jina lake mpaka top three ingawa wote walikuwa wanajua hatapewa urais....na kuna taarifa kuwa alishinda kura mara ya pili pia... sababu kubwa alionekana ni too inexperienced

Penye nyekundu, si kweli. Ni uongo ambao watu wa kundi la Kikwete waliutengeneza/kuuzusha na kuueneza. Makusudi tu ionekane Nyerere alikuwa anamkubali Kikwete. Uvumi huu nilianza kuusikia 2003 toka kwa mwana-CCM fundi wa kujipendekeza, ambaye 2005 alijiweka wazi ni mwanamtandao akimpigia kampeni Kikwete Dar na Moro.

Nyerere alikuwa amekwishalishwa taarifa muhimu na watu wake wa Usalama wa Taifa, na mengine alikuwa anayajua, juu ya wagombea wote wa urais kwa tiketi ya CCM kabla hajaenda Dom na akiwa Dom nini wengine wanafanya.

Kikwete has nothing to boast that JK wa ukweli was pleased with his leadership character at any point. JK wa ukweli was ashamed of him since that day when he set a " failed conspiracy snare" against his boss at Monduli.
 
Nawarudisha nyuma kwenye ndege waliyokodi kina JK na EL 1995. Baada ya kushindwa wakati wanarudi group pamoja na wengine ni Mama Makinda, Samwel Sitta, sikumbuki wengine, slogan ya ari mpya ni utunzi wa mzee Sitta. Hili group liliishi miaka pamoja likisubiri kuingia ikulu.

Naombeni ufafanuzi zaidi uadui wa Sitta na Lowassa ni kwasababu aliukosa u PM TU? NA KAMA NDIO KWANINI AMCHUKIE EL na si JK ALIYE NA POWERS ZA KUTEUA?
 
Mkuu umesema Malima alihusishwa na NRA chama chenye msimamo mkali cha kiislaam. Hivi kweli unaweza kunipa mahusiano ya NRA na Uislaam? na vitu gani walivyokuwa wakipigania (sera na Ilani) na kadhalika. Binafsi nimeyasikia sana haya madai na ningependa sana kupewa historia ama picha nzima ya chama cha NRA, uongozi wake sera za na mwisho uhusiano baina ya Malima na hicho chama cha kidini...Na labda mtu anipe investigative report inayoonyesha Kighoma Malima alikuwa both Muislaam mwenye siasa kali pia aliharibu wizara ya elimu na fedha..

Mkuu wangu hivi huoni kama kila kitu kinajirudia rudia - dejavu..
Dr.Slaa hadi kufikia mwaka 2009 alikuwa hero wa kila mtu, Sii waislaam wala wakristu lakini siku aloonesha nia yake ya kugombea Urais ndipo Upadre wake ulipotangazwa na nia mbaya ya Chadema katika kuupiga vita Uislaam simply 'because JK ni Muislaam.. Sasa habari kama hizi zitakwenda hadi kwa vijana watoto zenu ambao watakuja hadithia jinsi Dr.Slaa alivyokuwa mdini pamoja na kwamba hakuna hata siku moja amezungumzia Uislaam na Ukristu ila kosa lake ni kuikosoa serikali ya CCM..Malima pia alikuwa one of the best of ministers hadi siku alipozungumzia hali ya elimu nchini kukikosoa chama tawala.
Na mchezo huu umechezwa kwa viongozi woote walijaribu kukikosoa chama tawala toka Malecela ambaye alizushiwa hadi kuhama dini kuingia Uislaam na ati anaitwa Jumanne.. kila alojaribu kukisaliti chama au kuweka upinzani mkubwa na chama tawala Udini ulitumika kumdhoofisha...

Na lazima mkuu wangutukubali kwamba marais huandaliwa, hizi habari za kufikiria kwamba mtu unaweza tu kuibuka mshindi na kuwa rais wa nchi kwa kupitia demokrasia ni kuzidanganya nafsi zetu. Na wote hawa toka kina Kolimba, Malima, Mwaikambo na wengineo wameondolewa kwa sababu they knew too much of the system na siku walipojaribu kuhama ndio walijichimbia kaburi lao.. Na nitasema tena hakuna mtu anaweza kushika madaraka ya Urais kama hayupo ktk system. Viongozi huandaliwa na mara zote lazima kuna mahusiano mkubwa na vyombo vya usalama. Nani huwaandaa kwa tanzania kusema kweli sijui ila nafahamu kwamba lazima rais aandaliwe na akubalike na system.

Nitaendelea kusema tu kwamba, habari zoote zinazohusiana na udini ni habari ya kutunga ili kuogopesha wananchi. Tanzania hatuna hofu ya Ukabila na hakuna dalili za machafuko ya kijamii isipokuwa kwa kupitia DINI..Hapa ndipo pekee siasa za majitaka zinaweza kupata nguvu ya kuwajaza hofu (fear) wananchi..Nothing scares us most kama vita, na hakuna sababu nyingine tunayohofia zaidi ya Udini. Na CCM are masters wa kupandikiza mbegu za Udini kwa sababu haiwezekani NRA wakawa waislaam wenye siasa kali, CUF ni chama cha waislaam halafu Chadema leo ndio chama cha Wakristu - What a coincidence!
Mnyamahodzo said:
Kwenye nyekundu kuna uzi mmoja ulikuwa ukiendelea wiki kadha zilizopita waweza tafuta ukapata ilikuwa kuwaje na kwanini ilivuma maramoja kisha baadaye kupotezewa kwa Mzee JSM kuitwa Jumanne.Kwenye bluu, wako wanaosema Kighoma Ali Malima, alikuwa na back-up ya kundi fulani la waislamu ambao walitaka rais atakayefuata baada ya Mzee Mwinyi awe muislamu. Huyu jamaa alikuwa ni mdini kwelikweli. Anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakishadidia kichini-chini suala la Zanzibar kujiunga na OIC. Baada ya Kibona kama Waziri wa fedha kufariki, yeye ndiye aliyepewa nafasi hiyo. Akiwa madarakani akaanaza kukomba pesa kidogo-kidogo lakini kikubwa akawa anaficha ughaibuni. Strategically, kwamba atazitumia kwa kampeni. Alipokosa nafasi CCM akachomokea NRA. Akazikumbuka ngawila zake ughaibuni. Alipokwenda zifuata, the perfect thing was done, account ikawa imefungwa na Serikali ya Tanzania. Jamaaa akapata mfadhaiko/mshituko basi akafa. Miongoni mwa waliom-support ni Kitwana Kondo nao wakakumbwa na mfadhaiko, lakini hakufa aliendelea kuishi.Ni kwa uchache wa kile nachoweza kumbuka na kuandika, wapo wenye mengi ya kueleza. I stand to be corrected.
Nawashukuru kwa insight waungwana.Inavyoonekana tumegawanyika makundi mawili,moja likiamini kuhusiana na hayo ya kina Malima,najingine lisiloamini.Ndugu Mkandara,ni kweli habari hizi zilikuwepo kwenye magazeti tena yanayoheshimika enzi hizo.
 
The Boss,
Nimemtafuta Jenerali nimeambiwa yuko Botswana for 2 months. Simu yake ya Dar ambayo ni roaming naona ama kaizima au mitambo ya Botswana haikubali. Nitaendelea kumtafuta na kama unayo simu nyingine ni PM tafadhali.
 
Mkuu Mkandara,

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba raisi huandaliwa. Kwa kawaida raisi mmoja tu akisha ingia madarakani basi kuna kundi limepanga kutoa raisi ajae. Kwa hiyo ni process inayoenda mbali zaidi na siku tu form za chama zinapo tangazwa. Kama ni hivyo basi JK tunabidi tukubali kuwa ni mwanasiasa hodari (kuwa mwanasiasa mzuri siyo lazima uwe kiongozi mzuri). kwa sababu 1995 yeye ndiyo alikua favorite na 2005 akachukua ushindi.

Ukweli ni kwamba JK kajiandaa tokea ni mdogo kuja kuwa raisi tokea mahusiano aliyo tengeneza UDSM, jeshini na kwenye chama. Tokea mwanzo alikua na nia ya uraisi na akajiwekea mazingira ya kuuchukua na ukweli ni kapata. Mimi naamini system nzima siyo inayo panga nani awe raisi bali hata system yenyewe ina vikundi mbali mbali. Kundi la JK lilijipanga vizuri na nilitambua kuwa kati ya JK ndiye electable kwa hiyo yeye atashinda na wengine kuchukua nafasi zilizo baki. Hata ukiangalia watu wenye cheo sasa ni watu wamefahamiana at a personal level na JK muda mrefu.

Swali langu lakini ni je nani alimuandaa JK kuja kuwa raisi? What was the force behind him? Who were the people behind him? Na kama tokea 1995 ilijulikana JK ana nia na uraisi makundi mengine yalishindwaje kudhibiti kundi la JK? Na hii ni nje ya topic kidogo lakini nani alikua mtu wa Mkapa 2005?
 
Mkuu DSN,

Nashukuru sana kwa uchambuzi wako. Hivyo unavyo sema vina shababiana sana na mtiririko wa matokeo. Nina swali moja. Kwa uelewa wangu (naweza nika sahihishwa) ni kwamba Mkapa alikua na mtu wake 2005. Je kitendo cha Mkapa kumuachia JK apite ni kutambua kwamba JK ndiyo alilkua mshindi halali wa 1995?

Ila JK namkubali kwa uwanasiasa na namsifu kwa kitendo cha kusubiria patiently kwa miaka kumi. He knows the political game. He knew what he wanted and he worked for years to get it. Sidhani kama JK kawa raisi kibahati. It was a sequence of calculated moves.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mkuu Jasusi,

Hili ni swali tu. Je unafikiri Mkapa alikua accidental president? Kwa maana inaelekea majority 1995 walimtaka JK ila Mkapa kwa kupendwa na mtu mmoja tu ndiyo akapata uraisi. Did JK deserve to win the 1995 presidency? Na je unadhani sasa kundi la JK linamuandaa nani kuwa raisi?
 
Ndio hapo nilipopataka kwani wengi wanaamini EL ndie aliyemjenga JK,kumbe JK ndie bibi arusi wengine wasindikizaji wasio jua msindikizwaji.Kwenye msafala wa kenge mamba nao wamo.Hakika Jk alijua kuna siku atakuwa huko aliko taka.
 
Mkuu Jasusi,

Hili ni swali tu. Je unafikiri Mkapa alikua accidental president? Kwa maana inaelekea majority 1995 walimtaka JK ila Mkapa kwa kupendwa na mtu mmoja tu ndiyo akapata uraisi. Did JK deserve to win the 1995 presidency? Na je unadhani sasa kundi la JK linamuandaa nani kuwa raisi?
Mkuu,wakati hata mimi nasubiri Jasusi akujibu.Naamini pia kuwa Mkapa was single handedly been chosen by mwalimu.Kama si mwalimu,Mkapa asingechukua nchi.
 
Mkuu,wakati hata mimi nasubiri Jasusi akujibu.Naamini pia kuwa Mkapa was single handedly been chosen by mwalimu.Kama si mwalimu,Mkapa asingechukua nchi.

Mimi kuna kitu kimoja kina nitatiza kuhusu Mkapa. Mimi naamini Nyerere hakua mtu wa kukurupuka. Kama alimchagua Mkapa naamini kabisa Nyerere alidhani anafaa. Je Mkapa ni alikua anaficha makucha yake au kweli alikuwa "Clean" akaja kubadilika baadae?
 
Alibadilika baada ya mwalimu kufa mkuu.Yaani ndo mnafiki wa kwanza.Kina Jasusi,Joka Kuu na Mkandara watatueleza vizuri yale wanayokumbuka kama wanaweza.

Unafiki na uadilifu ni vitu viwili tofauti vinavyoweza kuwa confused.Mwalimu alikuwa na ideas ambazo alidhani amepata mtu wa kuziendeleza,especially zile positive.Na alikuwa na msimamo sana kuhusu kuheshimu mali za watanzania pamoja na heshma ya kuwaongoza watanzania.He was very strict when it came to leadership principles,morals and ethics.

Kama alivyosema mmoja wetu hapo nyuma.Mkapa was not even projected to become the candidate for CCM.Mwalimu alikuwa na ile falsafa yake ya "Wanaokimbilia Ikulu ni wa kuwaogopa kama ukoma" kwa hiyo akaenda na yule underdog ambaye alijidai kuwa hakimbilii ikulu.(Mkapa)Ni mnafiki ila good for him,alimsoma mwalimu na akajua namna ya kubehave.Aka lay low na kujidai so humble,mwadilifu and so forth....kwamba hana tamaa ya madraka na ni mwadilifu.Na yeye alijipanga kivyake kwa namna ya tofauti kwenye harakati za kuutaka urais.Yote aliyoyafanya baada ya mwalimu kufa hakuna hata moja linaloonyesha kuwa alikuwa mwanafunzi mwema wa Mwalimu.
 
A wonderfully educating thread! Powerful JF. worthy of being a member!

Nikiwa sifahamu mengi ya mwaka 1995 nafurahi sana kufuatilia thread hii. Niliwahi kuambiwa kuwa Mkapa mwaka 2005 was not for JK. Alikuwa na mtu wake (ambaye simfahamu) akiwa na support ya kina Kigoda na Simba. Upepo wa kura za maoni ulimbadilisha mkuu mawazo hata kumsupport JK laivu dakika za mwisho. Upepo huu ulisababishwa na Nguvu ya Rostam na EL ambao kwa moyo walimsupport JK. However the long time dream of JK was to be a president. Baada ya hapo amekuwa akiendeleza siasa ambazo ndo kama vile tena. Kama kwamba kulipiza kisasi ile system ya Mkapa iliwekwa nje (for large percent) unless kwa wale ambao hawakufukuzika! Haya ni yale niliyoyaskia, sina ushahidi wowote. Wenye data endeleeni kutujuza. Longlive JF
 
Mkuu DSN,

Nashukuru sana kwa uchambuzi wako. Hivyo unavyo sema vina shababiana sana na mtiririko wa matokeo. Nina swali moja. Kwa uelewa wangu (naweza nika sahihishwa) ni kwamba Mkapa alikua na mtu wake 2005. Je kitendo cha Mkapa kumuachia JK apite ni kutambua kwamba JK ndiyo alilkua mshindi halali wa 1995?

Ila JK namkubali kwa uwanasiasa na namsifu kwa kitendo cha kusubiria patiently kwa miaka kumi. He knows the political game. He knew what he wanted and he worked for years to get it. Sidhani kama JK kawa raisi kibahati. It was a sequence of calculated moves.

Wasimuliaji wanasema ni kweli BWM alikuwa na turufu zake kwa watu wake,ila ambae inesemekana alikuwa mlengwa sana alikuwaa Profesa Mac M ,lakini pia mwingine alikuwa DK A K.

Ingawa wadau wengine walikuwa ndani ya game nao kivyao ingawa wakiwa viongozi kama PM wa zama hizo FTS.Acha kambi ya mlengo wa Mwalimu,ikiwa na Mwenyekiti SAS, nayo wakichanganya kujaribu turufu yao.Huku nako huku JK chini ya uratibuu wa EL,SS na opportunist ambae aljiunga ghafla baada ya upepo kusoma kuwa hali ni nyingine na kuwa piga uwa huyu bwana JK ndio inaonekana mlengwa akawai kuja kuweka dalaja la kulinda maslahi ya miradi ya wazito nae kama kawaida si mwingine ila ni RA kambini akakubalika nae kuunda timu.

Dakika za mwisho dodoma mzee BMW anajaribu kucheza turufu yake lakini mpaka masaa machache kumaliza mchakato Mzee anaambiwa hakuna jinsi haitowezekana bila huyu JK. Taarifa zikimimika kuwa bila huyo Jamaa Nchi kwishney,kwa kuwa BWM ndiye aliyekuwa mtu mwenye ufunguo wa hatima na kwa kuwa keshapewa ultimatum hivyo pasipo hiana hakuna jinsi ila kuibuka na sifa kumi na tatu za mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Ila ni kweli wahenga walisema subila yavuta heri,ukitaka kujua subira yavuta heri kweli muulize JK
 
Nawashukuru kwa insight waungwana.Inavyoonekana tumegawanyika makundi mawili,moja likiamini kuhusiana na hayo ya kina Malima,najingine lisiloamini.Ndugu Mkandara,ni kweli habari hizi zilikuwepo kwenye magazeti tena yanayoheshimika enzi hizo.
Unafikiri na doubt unachosema wewe? hapana mkuu ndio uandishi wangu kupinga hizi tuhuma na uvumi ambao huenezwa na mtandao wa CCM... wakati ule wa Nyerere walimtumia sana Paul Sozigwa na kama sikosei magazeti yote na radio zilikuwa chini ya serikali...

Nachosema tu ni kwamba hapakuwepo na ukweli wowote kuhusiana na Malima, kama ilivyo leo kwa Dr.Slaa. Ni mchezo wa kisiasa na kama Dr.Slaa angekuwa chaguo la system basi JK ndiye ungemsikia akilaumiwa kwa udini na kadhalika... Truth remains - hakuna kiongozi yeyote aliyetaka kugombea urais kwa kutumia tiketi ya dini hata huyo mchungaji Mtikila hakufanya hivyo!
 
Mimi kuna kitu kimoja kina nitatiza kuhusu Mkapa. Mimi naamini Nyerere hakua mtu wa kukurupuka. Kama alimchagua Mkapa naamini kabisa Nyerere alidhani anafaa. Je Mkapa ni alikua anaficha makucha yake au kweli alikuwa "Clean" akaja kubadilika baadae?

Hili swali la msingi sana .
 
Mkuu Mkandara,

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba raisi huandaliwa. Kwa kawaida raisi mmoja tu akisha ingia madarakani basi kuna kundi limepanga kutoa raisi ajae. Kwa hiyo ni process inayoenda mbali zaidi na siku tu form za chama zinapo tangazwa. Kama ni hivyo basi JK tunabidi tukubali kuwa ni mwanasiasa hodari (kuwa mwanasiasa mzuri siyo lazima uwe kiongozi mzuri). kwa sababu 1995 yeye ndiyo alikua favorite na 2005 akachukua ushindi.

Ukweli ni kwamba JK kajiandaa tokea ni mdogo kuja kuwa raisi tokea mahusiano aliyo tengeneza UDSM, jeshini na kwenye chama. Tokea mwanzo alikua na nia ya uraisi na akajiwekea mazingira ya kuuchukua na ukweli ni kapata. Mimi naamini system nzima siyo inayo panga nani awe raisi bali hata system yenyewe ina vikundi mbali mbali. Kundi la JK lilijipanga vizuri na nilitambua kuwa kati ya JK ndiye electable kwa hiyo yeye atashinda na wengine kuchukua nafasi zilizo baki. Hata ukiangalia watu wenye cheo sasa ni watu wamefahamiana at a personal level na JK muda mrefu.

Swali langu lakini ni je nani alimuandaa JK kuja kuwa raisi? What was the force behind him? Who were the people behind him? Na kama tokea 1995 ilijulikana JK ana nia na uraisi makundi mengine yalishindwaje kudhibiti kundi la JK? Na hii ni nje ya topic kidogo lakini nani alikua mtu wa Mkapa 2005?
Hapo sasa!... Na kama Demokrasia ingekuwa inafanya kazi kihaki 2010 Dr.Slaa angechukua ushindi kiulaini lakini tazama nguvu iliyowekwa kuzuia matokeo.

Kwa kufikiri tu mwaka 1985, Nassoro Moyo angekuwa mbele ya Mwinyi ambaye alikuwa na scandal ya kiutawala, au Warioba na Malecela mbele ya Mkapa, Salim, Sumaye na Kigoda mbele ya JK..Wote hawa wakiwa nafasi za juu kabisa kuwashinda marais hao, lakini walipigwa chini bila wao kujijua tena na chombo ambacho wao wenyewe wamekitumikia CC...Kama ilivyo miujiza ya kidunia tumefikia kuamini lazima Mungu yupo basi hata ktk chaguzi za marais nchini nina hakika ipo nguvu fulani ambayo huandaa mtu kuchukua madaraka laa sivyo Dr.Slaa angeshinda 2010.

Lakini angalia uchawi ulofanyika..
1. Kwanza kura za Urais kujumlishwa makao Dar na sio ktk vituo vya uchaguzi tofauti na kura za madiwani na Ubunge.
2. Matokeo hayakutangazwa mara tu hesabu zilipokamilika na nadhani kuna baadhi ya sehemu kama sii majimbo hatukuwahi kupewa hesabu yake hadi leo hii!.(!??!!!). Noone is questioning.
3. Pamoja na kupinga kwa Chadema hakuna uchunguzi wowote ulofanyika wala kutaka kufanyika isipokuwa kuwalaumu CDM na kuwaomba wakubali matokeo kinyume cha hapo wanataka kuanzisha fujo..
4. Walipotoka Bungeni kwa kutomtambua JK, kosa jingine walizomewa na ikasemekana wafungiwe kwa kutomheshimu rais..
5. The aftermath ya Uchaguzi wa Meya na Maandamano yote ya Mwanza, Tarime na Arusha..Ni mazingaombwe matupu
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom