Nionavyo mimi: Changamoto za migongano anazokabilili Rais Samia ndani ya CCM ni kubwa kuliko anazokabili toka vyama vya upinzani

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Watu wengi wakisikia maneno ya kina Tundu Lissu , Mbowe na kadhalika, yakionyesha kutoridhishwa na raisi Samia katika majukumu yake kama raisi wa Tanzania, wanapata hisia kwamba watu wa upinzani ndio wanaomnyima raisi Samia usingizi wa usiku. Ukiwaza hivyo uko nje kabisa ya mstari.

Changamoto zinazomnyima raisi Samia usingizi zinatoka ndani ya chama chake CCM, kwa hao hao wanaojiita wana CCM wenzake. Hakuna raisi yeyote wa Tanzania amewahi kupata misukosuko ndani ya CCM kama Raisi Samia. Kuna kila dalili kwamba migongano na tofauti zilizomo ndani CCM zinaanza kumshinda, haelewi ni jinsi gani anaweza kushughulika nazo.

Ishara mojawapo kuhusu Samia kutojua jinsi ya kushughulika na watu wake ndani ya CCM ni kumrudisha Makonda kwenye uongozi wa CCM. Ilifikia mahali Samia ni kama hakumwamini yeyote tena ndani ya CCM, akawa "lonely lady" ndani ya chama na serikali. Kuongeza idadi ya watendaji toka Zanzibar haikumsaidia, kwa sababu huwa hawana influence sana katika matukio ya Tanzania, wapowapo tu. Samia akaona kuna mtu mmoja tu ambaye angeweza kumwamini ndani ya CCM - Makonda.

Lakini je, ilikuwa sahihi kwa raisi Samia kudhani kwamba akimleta Makonda ndani ya CCM atakuwa na mtu anaemuamini wa kumsaidia? Kwa upande mmoja inawezekana imemsaidia kwa kiasi, na inaonyesha kama amemuahidi Makonda kumjenga kuelekea uraisi baada yake, na Makonda anaitumia nafasi hiyo kujijenga mwenyewe pia - bila kujali kuwabomoa wengine ndani ya CCM!

Kwa namna fulani ujio wa Makonda uliwafunga midomo baadhi wa watu ndani ya CCM. Walikuwa wakiimba sifa sana kwa raisi, mpeni maua nk, na wakagundua pamoja na mashairi mengi waliyomwimbia Samia kumbe alikuwa hawaamini kabisa, mtu wake ni Makonda.

Na kuna dalili kwamba Samia ameanza kuwa na woga aliokuwa nao Mkapa alipoamua kumtengenezea njia Kikwete kwa makubaliano kuwa atamlinda, kwamba raisi atakaefuata anaweza kuja kuwaweka kizuizini viongozi wa utawala wa Magufuli na Samia, waliohusika na vitu kama mauaji, utekaji, kuhujumu rasilimali za taifa kama bandari, mbuga za wanyama, ufisadi uliokithiri, nk. Hivyo Makonda akiwa raisi baada ya Samia basi viongozi waliohusika watakuwa salama.

Na labda Samia meharibu zaidi kumrudisha Makonda, kwa kuwa kuna kila dalili kwamba ile migongano anayoikabili ndani ya CCM imeongezeka hata zaidi kwa uwepo wa Makonda. Hili linajionyesha sana kwenye mikutano ya bunge ya sasa na kunapokuwa na matukio kama hili la msiba wa Lowasa.

Ni wazi huko ndani ya CCM kunawaka moto, na raisi Samia ana kibarua kigumu sana kuzuia nyumba yake isiteketee. Ataweza?
 
Mwenzako yuko Oslo sasa hivi, kwenye joto/baridi wa -5C unasema ana changamoto?😂😂😂
 
Kwa kifupi ni kuwa Samia hatakiwi na Watanganyika walio wengi ndani na nje ya CCM.Kama Samia angekuwa ndugu yangu wa karibu,ningemshauri ajiuzuru anakoelekea atakuja kupata kiharusi au ugonjwa wa moyo.Kazungukwa na Wahuni wengi sana na Makonda amekuja kuiweka uchi serikali yake kimkakati!
 
Ninahisi anaweza asigombee 2025. Ila sasa, asipogombea anaweza kumwezesha Makonda awe mteule wa CCM, sio kwa sababu Makonda ana busara na hekima za kuwa raisi, bali tu kuwa na mtu wake wa kumlinda dhidi ya mambo fulani aliyofanya, na kuwakomoa Watanzania bara

Na kama ni kweli Samia hatakiwi huku bara, basi Chadema wanapaswa kutumia hiyo nafasi katika uchaguzi wa 2025, bila kutamka maneno ya kubagua mgombea wa kutoka visiwani. Kwa watu waliosomea communication, ni rahisi sana. Naweza kukutukana bila kukutukana kisheria
 
Back
Top Bottom